Debora Tluway Atembelea Chuo cha Vijana Kaskazini Unguja, Azindua Bananza la Utamaduni

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,687
1,238
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Taifa, Komredi Debora Joseph Tluway tarehe 14 Desemba 2024 ametembelea Chuo cha Vijana Kaskazini Unguja na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Chuo hicho
WhatsApp Image 2024-12-15 at 09.35.02 (1).jpeg

Aidha, Mhandisi Debora Joseph Tluway amezindua Bonanza la Utamaduni Kaskazini Unguja lililojumuisha michezo mbalimbali ikiwemo ngoma za asili, Sanaa ya maigizo, kukuna nazi, kuvuta kamba, nyimbo, kukimbia ndani ya gunia na mpira wa miguu.
WhatsApp Image 2024-12-15 at 09.35.04.jpeg

Vilevile, Debora Joseph Tluway Akiongozana na viongozi mbalimbali waliompokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, wametembelea maeneo ya miradi ya UVCCM ambapo wamejadili namna bora ya kuwa na miradi endelevu kwa lengo la kuinua uchumi wa vijana.
WhatsApp Image 2024-12-15 at 09.35.04 (1).jpeg

Pia, Debora Joseph Tluway ametembelea eneo la uwanja wa ujenzi wa nyumba ya Mtumishi (Katibu) wa UVCCM Mkoa wa Kaskazini Unguja ili kujionea mradi huo umefikia hatua gani ambapo ameahidi kushirikiana na Viongozi UVCCM Kaskazini Unguja kuhakikisha ujenzi unakamilika ili Mtumishi awe na mazingira mazuri ya kufanya kazi kwa ufanisi.
WhatsApp Image 2024-12-15 at 09.35.07.jpeg

Mhandisi Debora Joseph Tluway amepongeza maendeleo mazuri ya mradi wa ujenzi wa Maduka ya Chipukizi ambao ulikuwa hatua ya Msingi katika kipindi cha Matembezi ya Zanzibar na sasa mradi huo umefikia hatua nzuri ya upauaji ambao unategemewa kuwa chanzo cha mapato ya Chipukizi wa CCM
WhatsApp Image 2024-12-15 at 09.35.18 (1).jpeg

Mwisho, akiipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya Rais Hussein Ali Mwinyi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, Debora Joseph Tluway amewasisitiza wananchi wa Zanzibar kushiriki kikamilifu katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura hasa muda wake utakapowadia.
WhatsApp Image 2024-12-15 at 09.35.16.jpeg
WhatsApp Image 2024-12-15 at 09.35.17.jpeg
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-12-15 at 09.35.05 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-15 at 09.35.05 (1).jpeg
    191.7 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-12-15 at 09.34.53.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-15 at 09.34.53.jpeg
    193 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-12-15 at 09.34.57.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-15 at 09.34.57.jpeg
    166 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-12-15 at 09.35.02.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-15 at 09.35.02.jpeg
    176.2 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-12-15 at 09.35.18.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-15 at 09.35.18.jpeg
    334.8 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-12-15 at 09.35.15.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-15 at 09.35.15.jpeg
    246.5 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-12-15 at 09.35.10 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-15 at 09.35.10 (1).jpeg
    199.5 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-12-15 at 09.35.10.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-15 at 09.35.10.jpeg
    198 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-12-15 at 09.35.09.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-15 at 09.35.09.jpeg
    268.3 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-12-15 at 09.35.08.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-15 at 09.35.08.jpeg
    372 KB · Views: 2
Naomba kuuliza,huyu bibie hana uhusiano na familia ya Sumayi waziri mkuu mstaafu
 
Back
Top Bottom