Dear Men, kwanini ni vigumu kusema samahani?

Hili tatizo dada angu ni kwa watu wote. mi nina mchumba angu hata anikosee vipi huwa haombi msamahaa. ukimuuliza kwann anakuambia yeye humuomba msamaha mungu tu. Huwa naishia kusikitika tu
Kama huyo ni mchumba na anakujibu ivo....chukua hatua
 
Lady Jay,
Pole kwa kutooombwa samahani, lakini sio wanaume wote wenye tabia ya kutoomba msamaha wanapokosea. Kuomba msamaha ni utamaduni ambao mtu anaujenga polepole kutokana na malezi au mazingira aliyopitia kama nyumbani, mitaani, shuleni, kazini na makundi aliyokulia. Kama alizaliwa na kukulia katika mazingira ambao aliona baba yake au wanaume hawaombi msamaha wake zao, au wanawake kwa ujumla, itakuwa vigumu kwake kuomba msamaha. Au kama baba yake alimuaminisha kwamba, wewe ni mwanaume usijilegeze kwa mwanamke ikiwemo kuomba msamaha, itakuwa ngumu kwake leo kuomba msamaha.

Lakini pia, kwanini kwako wewe kuombwa msamaha ni muhimu sana kwako, ili hali wanawake wengine hawana shida hata wakikosewa bila kuombwa msamaha?. Yawezekana ulishajenga utamaduni kwamba anayekosea ni wajibu wake kuomba msamaha, haijalishi ni mwanaumeau mwanamke. Yawezekana hili wewe umeliona wakati wa malezi na makuzi yako kwamba mfano ulimuona baba alimuomba mama yako (Ni mfano tu), nawe ukaona kwamba ndio mtindo wa maisha. Jifunze kuwa 'open minded' kwamba sio kila kinachofanywa na mwanaume wako sasa basi chaweza kufanywa na wanaume wote wengine. La hasha.
Umeongea mambo mazito sana..yenye hekma na kama hajaelewa basi tena
 
Kuombwa msamaha kwa maneno inakuridhisha? sasa ngoja nikupe elimu usipende wala usitamani kuambiwa samahani mdomoni coz iyo ni mtu anataka kuwini tu amani ya moyo wake kwa yale aliyokukosea. samahani ya kweli huonekana kwa vitendo, bt mtu akisema samahani thn akarudia kosa afu akasema samahani tena ww inakusaidia nini? NEVER SAY SORRY bt DO SORRY.
 
Tatzo yupo wired na mother. Ndugu wote anacheza nao vzr wanampenda sana. tatzo ndo lipo kwenye hicho kipengele na makelele sometimes
Mwenzangu muamuzi wa mwisho ni wewe

Yakikukuta usije sema haujaambiwa
 
mwanaume hapendi kujishusha,ukichukulia yeye ndio rais wa nyumba!ushaona rais anaomba msamaha kwa walio chini yake?!jibu ni hapana na samahani huenda ukaipata kwa mwanaume ikiwa wewe ndo unamgharamia kila kitu huyo mwanaume na tena atakupa samahani ya kinafki
 
Back
Top Bottom