Dawa za Kulevya: CHADEMA wafungua kesi dhidi ya Makonda

tukikaa kimya kesho atatajwa lowasa keshokutwa lisu keshokutwa mdee afu chama kitachafuliwa........ lazma tupinge uhuni huu maana ni taswira ya chama ambayo ipo on stake...... ni lazma propaganda hii izimwe mapema sana tukichelewa sana itakula kwetu.
Mbowe si kafungua kesi tayari?
 
Hii kesi haikupaswa kamwe kufunguliwa na chama

kwani chama kimetuhumiwa kuuza madawa ya kulevya

Mbowe ni mpuuzi na kwa upuuzi wake anakitumia chama kama defensive shield yake

Huyu mtu hafai kabisa hata kuwa mwenyekiti wa Chama...Yuko pale kwa maslahi yake Binafsi

Anakitumia chama na rasilimali zake katika kesi binafsi

Ana turnish Image ya chama kuwa inapinga nia njema ya RC Makonda ingawa approach yake imekosolewa sana

Its high time now ...Watu wanaojielewa kuondoka kwenye this stinking party.....
Kwahyo wewe ndo unafaa. .
 
Hapo inatakiwa mahakama itupilie mbali. Hakuna haja ya kesi wakati kuna kesi zingine za msingi za kushughulikia.
 
semeni tu wazi kwamba mnapinga vita dhidi ya madawa ya kulevya. sio 'ooh sisi tunapinga ila wahusika wasitajwe na wafuatwe kwa heshima usiku na kuwepo tarumbeta and blah blah' unafiki mtupu wa chadema
Kwa hiyo kamishna mpya naye anapinga? Hizi buku saba zinawatoa watu ufahamu sana
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimefungua kesi ya kikatiba Mahakama Kuu dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kwa kukiuka sheria na taratibu katika kushughulikia watuhumiwa wa biashara za dawa za kulevya nchini.

Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Mwenyekiti wa Chadema, Freemana Mbowe, pasipo kutaja tarehe ya kesi, alisema majaji waliopangiwa katika kesi hiyo inayokusudiwa kusikilizwa Februari 21 ni pamoja na Jaji Sakiety Kihiyo, Jaji Lugano Mwandambo na Jaji Pellagia Khaday.

Mbowe aliongeza kusema kwamba Chadema inakubaliana kabisa na inaunga mkono mapambano dhidi ya uingizaji na utumiaji wa dawa za kulevya lakini staili anayoitumia Makonda inawafanya watuhumiwa kuukimbia mkono wa sheria.

“Sisi Chadema tunakubaliana na kabisa na mapambano dhidi ya waingizaji na watumiaji wa dawa za kulevya nchini lakini kwa staili ambayo Makonda anaitumia ni kuwaandaa wafanyabiashara wanaotuhumiwa kuukimbia mkono wa sheria”alisema Mbowe

“Kupinga kwetu utaratibu wa kutaja majina ya watu hadharani pasipo vielelezo kutamsaidia Makonda na mamlaka nyingine kufuata sheria katika kushughulikia suala hilo kama ilivyofanyika hivi karibuni,” alisema Mbowe

Akikabidhi ripoti hiyo yenye majina 92 ya watuhumiwa wa dawa za kulevya yakiwemo majina ya watoto wa viongozi kwenye uongozi wa serikali ya Awamu ya Pili, Tatu na Nne, Makonda alisema kwamba yeye (Makonda) na Kamishna wa Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam, Simon Sirro, waliamua kutaja majina hadharani kwa kuwa biashara ilifanyika hadharani.

“Majina 97 yanawahitaji watu wa Interpol (Mtandao wa Kimataifa wa Polisi) waweze kuvuka nje ya mipaka yetu kwa ajili ya kushughulikia baadhi ya watuhumiwa waliopo kwenye orodha,”alisema Makonda.

Vita ya kupambana na uingizwaji na utumiaji wa dawa za kulevya ilitangazwa hivi karibuni na Makonda (Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Dar es Salaam) huku wafanyabiashara, viongozi wa dini na wanasiasa akiwemo Mbowe wakitajwa hadharani kwamba miongoni mwa watuhumiwa.

Chanzo: Raia Mwema
Poleni sana chadema kwa kujikeep busy for nothing...

Hilo shtaka kama ni la kikatiba ibara ya ngapi imevunjwa maana huwezi kushtaki tu kama unaomba maji.
Kwani CHADEMA ilitajwa kwenye orodha .? Kwanini wanaweweseka !?
 
semeni tu wazi kwamba mnapinga vita dhidi ya madawa ya kulevya. sio 'ooh sisi tunapinga ila wahusika wasitajwe na wafuatwe kwa heshima usiku na kuwepo tarumbeta and blah blah' unafiki mtupu wa chadema
Hata mimi nilikuw na sapot makonda aendelee kuwataja ili hata wadogo zetu wawatambuwe kwa sura na wajilingnishe nao km wameathirika na wao na hii itasaidia watu kujitambuwa kuwa km wateja wanaathirika sana kiafya, kifedha na mengne mengi km hayo compared to wauzaji wao maisha safi na kila kitu kiko mwake mpaka familia zao.
 
Inaonkama kabisa hawa jamaa wameishiwa na sera mambo binafsi unahusishama maana nn ss mbona Lisu kwenye kesi zake hahusishi chama?
 
Acheni kutoa povu someni sheria mwenye kumtetea makonda mahakamani sio mambo ya kuleta sheria za makaburu
 
Hakukuwa na umuhimu wowote wa chama kufungua kesi katika hili

Mbona hamjui kusoma upepo nyie?

Mnamtetea nani?

Manji?

Hii ishu kama chama haitakiwi kuchukua upande ambao mbowe analazimisha chama kuuchukua.....

Kuna mambo mangapi ya msingi ya kuyafanyia kazi zaidi ya kuhangaika na makonda katika haya mambo eti mnaita "Approach"

Side mnayochukua sasa kama chama ita turnish image ya chama kuliko kuijenga....

Chama hakijawahi kufungua kesi kupinga ishu ya sharia za vyombo vya habari na sharia ya mtandao inayopingana na haki ya kikatiba ya kujieleza,CHADEMA haijawahi kusimama kidete kupinga fao la kujitoa,CHADEMA haijawahi kusimama kidete kutetea HESLB kupadisha rate ya mikopo hovyo hovyo,CHADEMA haijawahi kufungua kesi ya kikatiba ku challenge mfumo wa tume ya Uchaguzi...Eti leo mnafungua kesi ya "Approach"

Jinga kabisa
mkuu punguza jazba na matusi tupo hapa kuelezana sio kutukanana hivyo tuheshimu kutofautiana mawazo.

Mkuu kma kesi za kikatiba zilishafunguliwa nyingi tu mfano ile ya zuio la mikutano ya kisiasa n.k.... by the way most ya hizo hoja zako zilishaibuliwa bungeni na kambi ya upinzani sasa sijui hufuatiliagi hoja za kambi ya upinzani ama la....

kesi kama hii lazma chama ifungue maana CREDIBILITY ya chama ipo ON STAKE..... je watanzania wakiaminishwa chadema ni chama cha wauza unga tutapata wapi hyo moral authority ya kupinga mambo kma hayo unayoyasema??

tusipomcontent makonda kisheria hyo staili yake anaweza kuitumia kukiua chama je kesho akimtaja lisu na mashinji kuwa ni wauzaji utafanyeje??

chama lazima kiwe safi kabla hakienda kukosoa utendaji mbovu wa serikali hivyo CREDIBILITY ya chama lazma ichukuliwe serious ukitaka kuona umuhimuvwa credibility ya chama kumbuka kesi ya lwakatare na ile ya igunga jinsi chama kilivyowekeza nguvu ili kisichafuke mbele ya umma wa watanzania

Kwahyo tuelewane hapo kinachopiganiwa ni heshima ya chama na mbowe akichafuka ni cha kimechafuka na chama kikichafuka cost yake ni kubwa kuliko unavyofikiri kma unabisha uulize propaganda ya cuf kuwa chama cha kidini na kigaidi huku bara kilivyoififisha hadi leo.

CREDIBILITY IS THE FIRST PRIORITY
 
Mbowe si kafungua kesi tayari?
Chama lazima kicounter attack what if makonda atangaze kesho kuwa ofisi za chadema kunauzwa cocaine chama kitafanyeje?? haitokuaa too late??? hii sio issue ya chadema tuu hta wanaharakati na wapigania haki za binadam na wenyewe wafungue kesi maana yaliyomkuta mbowe au manji au gwajima yanaweza kukukuta hta wwe chinchilla coat je nano atakutetea??? kma kuna watu wamejitolea kuwasaidia kulinda credibility ya wananchi na utu wao kwanni msiwasifie mnaishia kuwavunja moyo??
 
Back
Top Bottom