Dawa za Kulevya: CHADEMA wafungua kesi dhidi ya Makonda

Chadema is this necessary? mna majukumu na kesi nyingi mno tayari, kesi kama hizi za kazi gani tena kama sio kumaliza muda ?
Hii ni sehem moja ya mapambano katika kutafuta haki na usawa.
Wacha waendelee kuburuzana kwa pilato na hatimae haki inaweza kupatkana kama mhimili hautachezewa
 
Chadema is this necessary? mna majukumu na kesi nyingi mno tayari, kesi kama hizi za kazi gani tena kama sio kumaliza muda ?
katika political climate tuliyo nayo sasa hivi hapa nchini ambayo constitution inaonekana kukiukwa with impunity, mahakamani ndiyo mahali pekee pa kukimbilia kwa kila kitu. ukizubaa, utajikuta "shimoni"!

so....naunga mkono raia yeyote au taasisi yoyote nchini ambayo itakimbilia mahakamani kwa kila (pigia mstari kila) aina ya vitendo vinavyokwenda kinyume na katiba na/au kukiuka haki za binadamu.
 
Hii kesi haikupaswa kamwe kufunguliwa na chama

kwani chama kimetuhumiwa kuuza madawa ya kulevya

Mbowe ni mpuuzi na kwa upuuzi wake anakitumia chama kama defensive shield yake

Huyu mtu hafai kabisa hata kuwa mwenyekiti wa Chama...Yuko pale kwa maslahi yake Binafsi

Anakitumia chama na rasilimali zake katika kesi binafsi

Ana turnish Image ya chama kuwa inapinga nia njema ya RC Makonda ingawa approach yake imekosolewa sana

Its high time now ...Watu wanaojielewa kuondoka kwenye this stinking party.....
UNA USHAIDI NA HIKI ULICHOKIANDIKA NDUGU AU ??????
 
semeni tu wazi kwamba mnapinga vita dhidi ya madawa ya kulevya. sio 'ooh sisi tunapinga ila wahusika wasitajwe na wafuatwe kwa heshima usiku na kuwepo tarumbeta and blah blah' unafiki mtupu wa chadema
kwa hyo unaona sawa gwajima na manji kutajwa afu wakakutwa hawana hatia??? je huoni wamewapotezea heshima na muda??? gwajima ataaminika tena hta kma mkemia kamsafisha???je wangekuwa na ushahidi tungelalamika kma mbowe angetajwa??
 
Swali langu ni jepesi lakini linanishinda kupata jibu. Nani ni mkubwa zaidi ya mwenzake, Chadema au Mbowe?
 
Kwani CHADEMA ilitajwa kwenye orodha .? Kwanini wanaweweseka !?
kwahyo chadema ipinge mambo yanayowahusu wao tu....afu katiba mpya nani apiganie?? mikataba ya kifisadi kwa kuwa haiwahusu chadema wakae kimya si ndio?? miswada mibovu kma cyber crime na huduma ya habari kwa kuwa haiwahusu chadema na wenyewe wakae kimya???

u cant be serious...... yaani wakae kimya huku katiba inavunjwa eti kwakuwa tu hawajatajwa kwenye list ya madawa???
 
semeni tu wazi kwamba mnapinga vita dhidi ya madawa ya kulevya. sio 'ooh sisi tunapinga ila wahusika wasitajwe na wafuatwe kwa heshima usiku na kuwepo tarumbeta and blah blah' unafiki mtupu wa chadema
Acheni aburuzwe tu kwa pilato
 
its necessary....indeed ili kuua propaganda maana tukikaa kimya tukaacha lipite itafanywa wimbo hadi kufkia 2020 watanzania wanaweza ona kweli chadema ni chama cha wauza unga hasa uko vijijini ila kwa kufungua kesi tunaonekana tuko serious kuwa mwenyekiti wetu hausiki maana akichafuliwa mbowe ndio umechafua upinzani kumbuka yeye ni KUB
Nakisupport chadema kwa kuwa ni upinzani ila kwa hili hapana..hizo mambo naon ni privacy wasichangnye na chama,wat if kam mbowe akaonekana amehusika au majengo yke yamehusika na issue za madawa..maan ake chama chote ktachafuka,ushauri wang mbowe ajitahid kusolve kusolve ili aje approve mbele ya umma yey alionewa..kwnye ukweli mbona uongo mbna huwa unajitenga mkuu.mm nataka nijue makonda ndo kazingua au mbowe,wasituletee siasa nyingi mbowe na makonda..tunatak ukweli 2
 
Chadema is this necessary? mna majukumu na kesi nyingi mno tayari, kesi kama hizi za kazi gani tena kama sio kumaliza muda ?
Mkuu kesi kama hizi zinawasaidia kula ruzuku.Hela yote ya ruzuku ya chadema sasa hivi imakwenda kwenye kitengo cha sheria,Lissu na Mbowe wanagawana ruzuku kama njugu.
Ukitaka kuona Lissu na Mbowe ni wasanii,siku ya kwanza Makonda alipowataja kina chidi benzi,Lissu na Mbowe walitoka hadharani na kutaka watajwe hadharani Mapapa wa unga sio vidagaa.Leo hii wamewahi mahakamani kisa tu Mbowe katajwa,asingetajwa Mbowe.chadema wangekuwa wanapiga kelele watajwe mapapa hadharani
Sasa hivi ukipigwa kibao tu Chadema wapo mahakamani.Kwa ufupi chadema wameweka mawakili kwa kesi zifuatazo
Kesi 3 za Lema-Arusha
Rufaa-Lijuakali
Kesi 3 za Tundu lissu kisutu
Kesi dhidi ya Makonda
Hapo utaona kabisa chama hakina maslahi na kesi hizo.lakini kwa kuwa ndio mwanya mzuri wa kuchota ruzuku,wazee wameamua chama kiweke mawakili watakaolipwa hela ya ruzuku.
 
Yawezekana wameguswa kwa njia moja hadi nyingine. Makonda mmoja kasababisha tumejua ukubwa wa hili tatizo kumbe sensa ilikuwa inapita tunapata idadi kubwa ya Watanzania kumbe wengine madawa yalishawamaliza. Sasa unga umepotea mtaani mateja wanahangaika wengine kama wagonjwa kabisa, hawajifichi tena maana stimu ya kuwafanya wachangamke haipatikani maana sawambazaji ama wamekamatwa au watakamatwa muda wowote. Nafikiri mahakama ifukuze kesi hii ( strike out) na badala yake iamuru hospitali za rehabu zifunguliwe kila mkoa maana ninavyoshuhudia mtaani ni zaidi ya hatari. Hongera sana Kamanda makonda tuliokoe taifa sasa sio kesho.
 
Mkuu lets be serious..... issue ya mbowe ni kesi aliyopewa na kma akifunguliwa mashtaka itabidi aweke mawakili yeye kma mtu binafsi unless chama kimsaidie tu ila hailazimishwi...... hii kesi imefunguliwa na chama kupinga approach wapi waliposema mbowe kafungua kesi kma mmiliki wa mbowe hotels alafu katumia wanasheria wa chadema???

be objective mkuu.... najua humpendi mbowe na naheshim mawazo yako ila kwa hili sioni kma kuna shida yoyote kma chama kimefungua kesi ya kikatiba irrespective mbowe alitajwa or not.
nimekuelewe na nakuunga mguu na kiwiko mkuu
 
Chadema is this necessary? mna majukumu na kesi nyingi mno tayari, kesi kama hizi za kazi gani tena kama sio kumaliza muda ?

Ukishasingiziwa unauza madawa ndipo utajua kwanini wameamua kufungua hiyo kesi.Anayejua maumivu ya kuumwa na nyoka ni yule aliyeumwa na TANDU,NYOKA au NGE kama hawa wadudu hawajakuuma huwezi jua maumivu yake.
 
Chadema is this necessary? mna majukumu na kesi nyingi mno tayari, kesi kama hizi za kazi gani tena kama sio kumaliza muda ?
Hawana sera sasa wanashuhulikia vitu vidogo to keep themselves busy,mwenyekiti wao anatumia nguvu nyiiiingi kujisafisha kuliko kwenda alipoitwa,central!
 
Kwani CHADEMA ilitajwa kwenye orodha .? Kwanini wanaweweseka !?
Hata kama asingetajwa Mbowe Chadema ina wajibu wa kumtetea mtu yeyote, kutetea haki, kusimamia na kuhakikisha nchi inaendeshwa kwa mujibu wa sheria na kuhakikisha misingi ya utawala bora inatekelezwa.
 
Mbowe amekataa kuitika wito wa Makonda, akamponda Makonda vibaya sana, hivi sasa yupo Dar anaendelea na shughuli zake na hawajamfanya lolote, badala yake tunamuona Rais akiitika wito wa kisheria uliotolewa na Halima Mdee bungeni kwa kuunda na kuteua Commissioner wa Kupambana na Madawa ya kulevya na Makonda akijirekebisha, Mbowe yupo Dar anaendelea na shughuli zake!
 
katika political climate tuliyo nayo sasa hivi hapa nchini ambayo constitution inaonekana kukiukwa with impunity, mahakamani ndiyo mahali pekee pa kukimbilia kwa kila kitu. ukizubaa, utajikuta "shimoni"!

so....naunga mkono raia yeyote au taasisi yoyote nchini ambayo itakimbilia mahakamani kwa kila (pigia mstari kila) aina ya vitendo vinavyokwenda kinyume na katiba na/au kukiuka haki za binadamu.
Mi naona wana rasilimali chache naona wangejikita huko majimboni kwao walikoshinda, na kuimarisha chama, kuhangaika na kesi za watu wakati watu wenu mnabambikiwa tena kesi inakuwa ni kama chama cha kesi sasa
 
Back
Top Bottom