Dar: TPA yazuia Makontena 262 yenye Mchanga wa Madini MOFED Kurasini

Nasikia mgodi ushawatangazia retrenchment wafanyakazi wake kama mkulu hatabadili msimamo.
 
Huu kweli ni mchanga wa kawaida kwenye makontena yote hayo? Kuna motive gani ya kusafirisha mchanga wote huo kwenda huko ughaibuni? Tumezoe dumping kutoka Ulaya kuja Africa lakini sasa inakuwa kama tunaenda kufanya dumping Ulaya!

Sidhani kama kuna mtu yeyote mwenye akili timamu atakayeingia gharama ya kusafirisha kitu kisicho na thamani kutoka kanda ya ziwa mapaka Dar halafu apakie kwenye meli kwenda ng'ambo bila kuwa na vitu vya thamani kubwa vilivyofichwa humo. Lazima tujiulize, kama container linaweza kuwa declared kuwa na nguo za mtumba linakutwa na magari matatu ya kifahari, je hilo la mchanga haliwezi kuwa na kilo angalau ishirini tu za dhahabu??????:confused::confused::eek::eek:
 
Mmmh tuache uongo. Hayo yamekwama kutokana na tamko la Mkuu. Nilifanya kautafiti kidogo kujiridhisha kuhusu hii ishu ya mchanga au dhahabu kwenye makontena.
Kwanza inasemekana kuwa kabla hayajatoka makontena mgodini yanakuwa yamekaguliwa na taasisi husika za madini na kushirikana na TRA. Sampuli huchukuliwa na maafisa wa serikali kujiridhisha kilichomo na kupigiwa bei ya soko kwa siku ya kuyafunga na kuweka lakiri za watu wa madini na TRA. Thamani ya madini yote yaliyo kwa kontena hukokotolewa na pia mrabaha kwa kila kontena (4% of Gross Value) hukokotolewa kulingana na sheria ya madini 2010 na hulipwa mapema kabla hawajapewa Export Permit kutoka ofisi ya wizara ya madini na release oder permit kutoka TRA. Malipo hayo hufanyika mapema kabla mzigo haujatolewa kwenye migodi husika ambayo nchini ni Bulyanhulu na Buzwagi yote ya Kahama. Hivyo taarifa sahihi zipo kwa ofisi zetu za umma za Madini na TRA.
Huo ndio utaratibu.Lakini unakiukwa kinachoandikwa sio kilichomo ndani ya container.
Angalia juzi,zimekutwa Range rover 3 mpya za mwaka 2016 lakini nyaraka zinaonesha kuwa ni viatu vya mtumba.
Subiri siku mbili tatu hizi utapata mstuko baada ya samuli ya kila kontena kupimwa upya upya.
 
hawa wanataka kick. naimn kontna hzo zp kihalal. na naimn wakichngza wataambulia patupu. hao sio wajinga kuziweka hapo acacia n kampn kubwa dunian lnfny kaz kwa wered mkubwa. kwao kashfa ndogo inaweza wadondosha katka masoko yahisa. ko hawafany ujinga hao
 
Ni hatari kumpa mtu awe na kampuni ya usafirishaji makontena bandarini kama ilvo hatar kumpa mtu bandari yan kuibnafisha bandari na uwanja wa ndege ni muhimu sana kwa nchi na sehem hzo n hatar kama ztakuwa hazna ulinz na umakini wa kutosha kujua nn kinaingia na nini kinatoka
 
hilo sio kosa kwa kuwa kwa wakati ule walikua wanaruhusiwa ni sawa na ishu ya viloba tu kukutwa kwenye yard ni swala la kusubiri tu tamko la serikali litasemaje
 
Huo ndio utaratibu.Lakini unakiukwa kinachoandikwa sio kilichomo ndani ya container.
Angalia juzi,zimekutwa Range rover 3 mpya za mwaka 2016 lakini nyaraka zinaonesha kuwa ni viatu vya mtumba.
Subiri siku mbili tatu hizi utapata mstuko baada ya samuli ya kila kontena kupimwa upya upya.
Issue ya container za juzi kukutwa na Gari ndani Yake badala ya mtumba sio jambo LA kushangaza kwa upande Wa bandari, linaweza kuwa kosa LA shipper kutoku declare kilichomo ndani. Na Mara zote adhabu Yake ni fine.

Suala LA thamani ya madini yaliyomo ndani ya mchanga kwenye container ni estimation inaweza kuwa ndogo au zaidi kulingana na sehemu mchanga ulipotoka(mkanda).
 
Maswali machache najiuliza;
Je wanapoyazuia watayafungua na kutafuta kujua kilichopo ndani?
Je hizo seal ziliwekwa baada ya Raisi kupiga marufuku au kabla?
Je kama ziliwekwa kabla kuna utaratibu gani wa kutenda haki?
Je kama ziliwekwa baada ni nani na nani wanahusika na watachukuliwa hatua gani?
Je kama huu usafirishaji wa mchanga upo kwenye mikataba ya uchimbaji kulikuwa na utafiti maalumu uliofanyika kabla ya uamuzi wa kusitisha usafirishaji huo? Na je tunajua ni nini kitafuata? Nchi haitaingizwa kwenye migogoro mingine isiyoisha kama ile ya kufua umeme?
Je nchi ilishatuma wapelelezi wake kwenye hicho kiwanda kinachopokea mchanga na kuthibitisha kuwa tunacholipwa kutokana na mchanga huo kinaendana na thamani yake?
Je ulifanyika uchambuzi yakinifu kuweza kukokotoa hasara itakayotokana na kusitishwa kwa usafirishwaji huo? kwa maana kujua gharama ya kusafirisha container mpaka migodini, kulijaza mchanga, kulisafirisha tena mpaka Dar, kulifanyia clearances, mikataba ya clearance and handling pale bandarini, malipo ya TRA, ukaguzi nk. upakiaji na upakuaji katika sehemu zote hizo, utunzaji wa hayo makontena kwenye yard zote hizo husika, mkataba na wasafirishaji kwa meli nk. nk...?

Tumefika hapa kwa sababu tumesaini mikataba ya madini isiyokuwa na tija kwa Taifa. Ndiyo maana Mwalimu aliwahi kusema kama hatujawa tayari kuyachimba ni afadhali tuyaache huko ardhini kuliko kukubali kudanganywa, unaonyeshwa kipande cha chupa unachekelea kama zuzu ukithania ni almasi.
 
Kwa nimi tuendelee na ndoa ya TICS? hawa viongozi wa zamani bado wanatuibia hadi awamu hii ya 5 na, hadi lini?
 
Huo ndio utaratibu.Lakini unakiukwa kinachoandikwa sio kilichomo ndani ya container.
Angalia juzi,zimekutwa Range rover 3 mpya za mwaka 2016 lakini nyaraka zinaonesha kuwa ni viatu vya mtumba.
Subiri siku mbili tatu hizi utapata mstuko baada ya samuli ya kila kontena kupimwa upya upya.
Uko ajua maana ya kuwepo seal za TMAA na TRA. Kabla ya kufungwa lazima wathibitishe na kama haitoshi wanapewa au wanachukua sample wakapime popote pale wanapotaka. Kuna mingine tunawaonea watu wa migodini.
Zikipimwa upya kitakachokutwa kilipaswa kukutwa muda mrefu maana sample zake watakuwa nazo. Pia kampuni ya kimataifa ya vipimo SGS ishtakiwe kama ikithibitika kilichomo sio Kama wao walivyopima.
 
dah! Kwa mara ya kwanza. Mwenyekigoda atakuita msaliti. Samahani, hivi mgonjwa anatumwa hospitali au anafata matibabu.

Hayajashikwa, tuwe wa kweli.

Hayo yamekwama toka siku ile alipopiga marufuku mchanga kusafirishwa.
 
Back
Top Bottom