Dar: TPA yazuia Makontena 262 yenye Mchanga wa Madini MOFED Kurasini

Nani kawapa ruhusa ya kutangaza bila ziara ya kushtukiza. Bure kabisa!
Wangekuwa waandishi wa habari ili mshitukizo utoke vizuri
 
TPA imebaini makontena mengine 262 yenye mchanga wa dhahabu yaliyokuwa yamehifadhiwa bandari kavu ya MOFED (zamani ZAMCARGO)

Mkurugenzi Mkuu TPA, Deusdedit Kakoko asema makontena yalikuwa hatua za mwisho kukamilisha taratibu za kiforodha kusafirishwa nje ya nchi https://t.co/SRl7wBAwdG

Chanzo: Swahili Times

IMG_20170325_163159.jpg
IMG_20170325_163043.jpg
 
Huu kweli ni mchanga wa kawaida kwenye makontena yote hayo? Kuna motive gani ya kusafirisha mchanga wote huo kwenda huko ughaibuni? Tumezoe dumping kutoka Ulaya kuja Africa lakini sasa inakuwa kama tunaenda kufanya dumping Ulaya!
 
kama hatotueleza vyeti...vya Dab bas lolote litakalofichuliwa litaonekana ni kiin macho
 
Week minded wanataka kutuaminisha kama vile hayo makontena yalikuwa yanatoroshwa ili hali si kweli wale wanatekeleza vipengele vyao vilivyo kwenye mkataba vinacyowaruhusu kisafirisha makontena kwenda nje mwisho wa siku tutaishia kudaiwa mamilionivya dola. kama mi kivunja mkataba zipo taratibu zake na si ubabe waende mahakamani hii itakuwa kama issue ya samaki wa Magufuli waliokamatwa
 
JPM hakuwepo?, au hakuna tukio lingine lililotokea nchini?

Sasa hayo Makontena yamekamatwa kivipi?, kama yametoka Kahama mpaka Bandarini na yanajulikana yana mchanga wa dhahabu wameyakamata kivipi?

Usahihi ni kuwa hayo Makontena YAMEZUILIWA kusafirishwa kwenda nje
Maigizo juu ya maigizo. Unaposema umekamata iwe Na Maana walikuwa wanayatorosha wao Ndio wamezuia. Wanatakiwa waseme ma container yaliyopo bandarini Na bandari kavu ya mchanga kutokana Na zuio la mh RAIS ni idadi Fulani. Sio kutwambia wamekamata.
 
Makontena mengine zaidi ya 200 yenye mchanga kutoka migodini yameshikwa bandarini yakiwa katika yard ya iliyokuwa ZAMCARGO

View attachment 486812
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imebaini makontena mengine 262 yenye mchanga wa dhahabu yaliyokuwa yamehifadhiwa katika bandari kavu ya MOFED (zamani ZAMCARGO) iliyopo Kurasini jijini Dar es salaam yakisubiri taratibu za kiforodha kabla ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi kupitia kitengo cha makontena kinachoendeshwa na kampuni binfasi ya TICTS.

Kubainika kwa makontena hayo kumekuja siku tatu tu baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kutembelea bandari ya Dar es salaam na kukagua makontena 20 yenye shehena ya mchanga wa madini kutoka migodi mbalimbali iliyopo Kanda ya Ziwa.

Mhe. Rais Magufuli alifika bandarini siku hiyo kukagua utekelezaji wa agizo lake la kupiga marufuku usafirishaji wa mchanga wenye madini kutoka migodini.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko, amesema makontena hayo yaliyokuwa katika hatua za mwisho kukamilisha taratibu za kiforodha yamebainika leo tarehe 25 Machi, 2017 katika msako mkali unaoendeshwa na Mamlaka yake.

Mhandisi Kakoko amesema makontena yote hayo yalikuwa na lakiri (seals) za Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), na yalikuwa yanashughulikiwa na kampuni ya usafirishaji wa mizigo ya Freight Forwarders Tanzania Limited iliyopo Dar es salaam.

Mhandisi Kakoko amesema jumla ya makontena 256 yalikuwa katika bandari kavu ya MOFED, wakati makontena mengine sita yalikuwa tayari yameshaingizwa bandarini tayari kwa kusafirishwa.

Ametoa wito kwa makampuni yote ya madini yenye shehena za mchanga yajitokeze yenyewe na kuonesha mizigo yao popote ilipo nchini kabla haijabainika katika msako kabambe unaondeshwa na vyombo vya ulinzi na usalama katika maeneo mbalimbali nchi nzima.

Orodha ya makontena hayo yaliyobainika inaonesha yalifika bandarini hapo katika nyakati tofauti kutoka migodi ya Buzwagi na Pange Mines.

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Bandari Bw. Ramadhani Mungi amesema bandari zote nchini ziko salama na kwamba ulinzi na usalama umeimarishwa kwa kuwekwa askari na vifaa vya kisasa vya ulinzi zikiwemo kamera.

View attachment 486855 View attachment 486856 View attachment 486857 View attachment 486858
Ukisikia usanii ndiyo huu
 
Kwanza mikataba inasemaje maana isije ikawa kama ile meli ya uvuvi aliyoikamata sizonje kisha tukalipa fidia
 
Kwanza mikataba inasemaje maana isije ikawa kama ile meli ya uvuvi aliyoikamata sizonje kisha tukalipa fidia
 
Bavichaa kila mtu mjuaji....e bwana wee haya endeleeni kudadafua tuone
 
Niachane na Bashite na Nape eti nijadili Makontena. Am I Mad?
kick hizo tusihamishane kimawazo.
 
Back
Top Bottom