Walitakiwa wasiunganishe saloon, station wagon na pickup, kwa vile bei zao zilikuwa zitatofautiana. Kuna waliokuwa wanalipa 1500, na wanaolipa 2000. Sasa wameunganisha na kuweka bei moja ya 1500. Je tuliokuwa tunalipa 1500 hatustaili punguzo
 
Ningelikuwa na mamlaka nchi hii hilo daraja wa kazi wa kigamboni wangelipita free, Hakuna haja ya kuwa na tozo za kuvuka hapo, Serikali ni wajibu wake kutengeneza miundo mbinu bora kwa wananchi wake ili wawe salama pia kuchochea maendeleo na unafuu wa maisha, Hayo mambo ya tozo naona yangelibaki kwenye Panton tu. Au wana jamvi nakosea?
 
Lingine jingwe lianzie Azania front lipite juu Marine likadondokee stand ya zamani ferry jeshini baada ya chuo cha Mwalimu Nyerere. Meli zipite chini magari watu juu. Pantoni zinachelewesha mawasiliano ya pande mbili.
 
Walitakiwa wasiunganishe saloon, station wagon na pickup, kwa vile bei zao zilikuwa zitatofautiana. Kuna waliokuwa wanalipa 1500, na wanaolipa 2000. Sasa wameunganisha na kuweka bei moja ya 1500. Je tuliokuwa tunalipa 1500 hatustaili punguzo
Kwa siku utalipa 2,500 na kwa mwezi 35,000 mfumo ukikamilka utaratibu huu utaanza.
 
mimi nilikuwa nalipa 2000 sasa hivi 1500 yaani 500 tu punguzo inifanye mimi kufurahia tena nizunguke kupitia kilwa road foleni yake au nipitie mandela road nianze foleni eti kwa ajili ya kupunguziwa 500 ujinga mtupu bora nipitie feri kwa 2000 hakuna foleni barabarani na mafuta ninasave
 
Miaka takribani 10 iliyopita, wananchi wa Kigamboni walisikia kauli ambayo imekuwa ikisumbua masikio na fikra zao kwa muda mrefu sasa. Ndio wakati ule nauli ya kivuko ilikuwa ni Shilingi mia 200 tu na pale wananchi walipolalamikia kuwa ni gharama kubwa waliambiwa "pigeni mbuzi mkishindwa kulipa".
.
.
Nyakati zikasonga wananchi wale wa mitaa ya Wilaya ya Kigamboni wakakumbukwa bana, huku na huku likajengwa daraja linalokatiza baharini, na sasa wananchi wenye magari yao hawakulazimika tena kupanda kivuko kwani walikuwa na "option" ya kutumia daraja jipya. Lakini hapa napo kelele zikawa zilezile, gharama zinazotozwa kwa pikipiki na magari yanayokatiza ni kubwa sana na zinawaumiza wananchi. Bahati mbaya ni kama vile "jamaa" walitia pamba masikioni, hakuna lililofanyika.
.
.
Leo hii, Mei 23 2022 inaingia katika siku za muhimu kwa wale waishio Kigamboni kwani NSSF wametangaza kushusha tozo daraja la Kigamboni kuanzia Mei 20 ambapo waenda kwa miguu/baiskeli ni BURE, pikipiki zimeshuka toka Tsh.600 kwa safari hadi 300, magari yote madogo sasa yatalipa 1500 kwa safari, mabasi ya abiria 15-41 tozo imeshuka toka 5000 hadi 3000 kwa safari. Uzuri ni kuwa kwa watakaolipa kwa wiki watapata unafuu zaidi.
.
.
Pamoja na mengi yanayoendelea sasa nchini, Wana Kigamboni kwa hili wana haki kuishukuru Serikali kwa kufanyia kazi kilio ambacho kimekuwa kikitolewa kwa muda mrefu sasa na matumaini yako wazi kuwa pengine tozo hizo zitafikia KIKOMO "very soon", kutoka kuambiwa wapige mbizi hadi kupunguzwa kwa tozo ni hatua kubwa sana.

Kigamboni.jpg
 
Kwani wananchi wa Kigamboni walitaka tozo ya kuvuka daraja iondolewe kabisa au ipunguzwe?
Sio vizuri kujitekenya mwenyewe halafu kucheka. Tuache usanii.
 
Kwani wananchi wa Kigamboni walitaka tozo ya kuvuka daraja iondolewe kabisa au ipunguzwe?
Sio vizuri kujitekenya mwenyewe halafu kucheka. Tuache usanii.
Kwani kila unachokitaka unapewa. Alafu wewe na jina lako Zanzibar yaonesha unapenda mambo ya kutekenywa maana sielewi yemefikaje kwenye uzi huu
 
Rais Samia Suluhu na Mbunge Faustine Ndugulile wamevunja kikwazo kigumu kabisa Cha maendeleo ya kigamboni.

Sasa tozo zimeshuka na zitalipwa kwa siku badala Kila mtu anapovuka

Hiki kilikuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya kigamboni. Kigamboni ikianza kujengwa itakuwa mji mzuri sana na utaibadilisha Dsm.

Habari zaidi ukurasa wa Instagram wa mbunge..

Ni miaka michache tu iliyopita, wananchi masikini na wanyonge waliambiwa waogelee, lakini mama kaonyesha kwamba yeye kwa hakika ndiye Rais wa wanyonge na masikini

Pia soma;

1). Watu wa Kigamboni tudai haki yetu ya kutumia daraja bila tozo sasa muda ndio huu
View attachment 2235011View attachment 2235012View attachment 2235013
Kinacho nifurahisha kwa hii serikali ya Ccm ni pale wanapo fanya maamuzi ya kuboronga na kuwaumiza raia halafu wakisha kosolewa wakirekebisha bado watajisifu badala ya kuomba radhi.. Funny Ccm.
 
Kongole kwa wana-Kigamboni kwa kupiga kelele na serikali kwa kujaribu kuwapunguzi hadha ya tozo; pressure works.

You win some you loose some; agenda ilikuwa kufutiwa tozo kabisa. Hilo lilishawekwa wazi na serikali aliwezekani.

Review ya tozo inawezekana, charge zilipangwa bila ya data za uhakika on volume za matumizi.

Leo hii wana info za kutosha on amount of traffic na aina zake, so wanaweza kabisa review bei, kuzishusha na bado kurudisha gharama za ujenzi ndani ya muda uliopangwa.

That is not to take away kelele za wana-Kigamboni na hatua za serikali pia kwa kuwasikiliza wananchi wake na kujaribu kuwapunguzia gharama.
 
Back
Top Bottom