chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
15,937
27,069
Rais Samia Suluhu na Mbunge Faustine Ndugulile wamevunja kikwazo kigumu kabisa Cha maendeleo ya kigamboni.

Sasa tozo zimeshuka na zitalipwa kwa siku badala Kila mtu anapovuka

Hiki kilikuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya kigamboni. Kigamboni ikianza kujengwa itakuwa mji mzuri sana na utaibadilisha Dsm.

Habari zaidi ukurasa wa Instagram wa mbunge..

Ni miaka michache tu iliyopita, wananchi masikini na wanyonge waliambiwa waogelee, lakini mama kaonyesha kwamba yeye kwa hakika ndiye Rais wa wanyonge na masikini

Pia soma;

1). Watu wa Kigamboni tudai haki yetu ya kutumia daraja bila tozo sasa muda ndio huu
IMG-20220523-WA0000.jpg
IMG-20220523-WA0001.jpg
IMG-20220523-WA0002.jpg
 
Ni jambo jema
Hakika, kigamboni ikifunguka, ni moja ya maeneo yaliyopangika vizuri, asilimia kubwa imepimwa, Ina beach nzuri sana.

Nguvu kubwa ielekee kwenye kuioa kilometa za kutosha za lami, ndio wilaya yenye kilomita chache sana za lami kuliko wiaya nyingine ya Dsm.

Mama awape bilioni hata 30 Kila mwaka
 
Ameshusha tu au pia amefidia hilo pengo lililoachwa? Hizo fedha zinazokusanywa zilikuwa na kazi maalumu nafikiri, sasa kama anaondoa ni lazima afidie hilo pengo kule kwingine, vinginevyo ni ujinga tu!
 
Ameshusha tu au pia amefidia hilo pengo lililoachwa ? Hizo fedha zinazokusanywa zilikuwa na kazi maalumu nafikiri, sasa kama anaondoa ni lazima afidie hilo pengo kule kwingine, vinginevyo ni ujinga tu!
Vyovyote vile, the end justifies the means...orrr the means justifies the end
 
Vyovyote vile, the end justifies the means...orrr the means justifies the end

Hakuna cha vyovyote vile, walioweka hiyo tozo hawakuwa wajinga, walikuwa wanakusanya fedha ili ifanye kazi fulani sasa ukiindoa ni lazima uifidie ili wasikwazike, vinginevyo haumsaidii yoyote kwani hilo daraja ni lazima litunzwe na kufanyiwa matengenezo pia!
 
Rais Samia Suluhu na Mbunge Faustine Ndugulile wamevunja kikwazo kigumu kabisa Cha maendeleo ya kigamboni...
Naomba kujua BEI ya Petrol pale Zanzibar, Njoo DSM, niambie SIRARI mpakani inasomekaje Bei Kwa sasa, mtumishi hasifiwi Kwa kutimiza wajibu wake Kwa wananchi ambao ndio WAAJIRI wa viongozi. Amen
 
Hakuna cha vyovyote vile, walioweka hiyo tozo hawakuwa wajinga, walikuwa wanakusanya fedha ili ifanye kazi fulani sasa ukiindoa ni lazima uifidie ili wasikwazike, vinginevyo haumsaidii yoyote kwani hilo daraja ni lazima litunzwe na kufanyiwa matengenezo pia!
Kiongozi daraja lilijengwa kwa pesa ya mkopo toka NSSF nadhani marejesho yanarizisha ndomana Mother ameamua kupunguza tozo
 
Naomba kujua BEI ya Petrol pale Zanzibar, Njoo DSM, niambie SIRARI mpakani inasomekaje Bei Kwa sasa, mtumishi hasifiwi Kwa kutimiza wajibu wake Kwa wananchi ambao ndio WAAJIRI wa viongozi. Amen
Kafanye utafiti, ukitaka kutafuniwa utatafuniwa vingi
 
Kafanye utafiti, ukitaka kutafuniwa utatafuniwa vingi
Nazijua sana! Msijisifie kufuta mia Tano Kigamboni pekee, wakati Nchi nzima tozo ziko Palepale, Bei za petrol IMPACT yake ni kubwa inagusa Kila kitu. Msibweteke kaz Bado kubwa.
 
Zoto zifutwe zote na mzigo wa deni uwe wa taifa zima.

Hata hivyo wanasema shukuru kwa hata kidogo unachopata ndiyo uungwana.
 
Ifutwe kbs sio sawa unawa barua watanzania kwankuamuankuishi kigamboni Wanalipamkodi zingine zote na bado kutoka nankurudi Malawi wanalipia kivuko na daraja hii si sawa
 
Back
Top Bottom