CUF yatoa tamko,yamtaka prof. Lipumba asikivuruge chama

kwanza kabisa nawapongeza sana ndugu zetu wa chama cha wananchi cuf, kwa kutambua kwamba bw lipumba hafai na hawa mwitaji kwa sasa kwenye nafasi hiyo tena.

Mtawezaje kumrudisha mtu Ambaye aliwaacha katika mapambano je! Alikuwa na nia njema na mustakabali wa maendeleo ya chama! Au alikuwa anataka chama kife?

Huyu hafai kabisa, tena ikiwezekana cuf wamfukuze na uwanachama kabisa. Hawa na dr slaa hawafai kabisa waende chama cha mapinduzi. BG Up cuf twaha taslima anatosha.
 
Huyu mzee yani anajiaibisha sana..kwa nn yeye kama mwanataaluma asiwaachie CUF chama chao??? Kwa nini aliwasaliti??? Yan hadi namuonea huruma
Kila siku najiuliza kwamba hivi huyu Lipumba ni kweli anafikiri sawasawa kuendana na uprofesa wake au ana ugonjwa sugu uliomharibu akili?
 
Sisi wajuzi wa mambo tulishawaambia kuwa upinzani wataongea lugha tofauti tofauti kama vile wale jamaa wa enzi zile za mnara babeli, maana wapinzani hawana hoja wote ni njaaa kali mno. Sasa hata wabunge wao wanalia njaa, wanaomba misaada kila pahala,

Busara ya mtu huonekana katika kusema na kutafakari mambo. Huyu nae naona kuwa ana BUSARA za Shule na kuzaliwa. Angekuwa hana asinge sema hivyo alivyo sema. POLE yake.
 
Kiongozi wa Muda wa CUF na mwanasheria mkongwe hapa nchini amemkata kilimi prof Lipumba Kwa kudai kuwa hakuna kifungu ktk katiba ya CUF au Chama chochote Duniani kinacho ruhusu mtu kujiudhuru uongozi halafu akabatilisha maamuzi yake mwenyewe. Amesema hicho ni kituko cha ajabu na amemuasa Lipumba kuacha kukiyumbisha Chama.

Aidha amemtaka atulie na kusubiri uchaguzi kama anataka kugombea uongozi ndani ya Chama hicho.
Pia amehoji sababu zilizo mfanya ajiuzuru je ameona hazipo kwa sasa?

Pia amewataka wanachama wa CUF kutulia na kusubiri mchakato wa uchaguzi huo mwezi August.
Mh. Twaha Taslima alikuwa akiongea na waandishi wa habari makao mkuu ya Chama hicho leo buguruni na taarifa hiyo imerushwa ktk kituo cha habari channel ten saa moja usiku huu.
 
Binafsi matamko ya CUF huwa nayakubali. Mpangilio na mtiririko wa lugha, hoja zinazofikia kilele cha maudhui na muktadha wa jambo linalotolewa taarifa/ufafanuzi ni wa kiwango cha weledi usiotiliwa shaka na kila mwenye chembe za uzalendo na ufuatiliaji wa siasa zetu. Lakini sijui kwa nini wanapwaya ktk siasa za majukwaani ambazo wengi wa wananchi wanashabikia na kuziunga mkono hasa ktk kizazi hiki. Badilikeni CUF!
 


Chama cha wananchi CUF kimemtaka aliyekuwa mwenyekiti wao Ibrahim Lipumba asitake kukiyumbisha chama hicho wakati nchi hii ikiwa na matatizo makubwa ambapo wananchi wanatakiwa kuunganishwa na kupewa matumaini.
Wamedai wapo wananaotoa kauli zisizo za kweli kwa lengo la kukidhoofisha chama ambao wanatumiwa na maadui wa CUF, na kauli hizo kuonekana zina baraka za chama.
Amesema katiba yao inataka wale wote wanaotaka kusema chochote kuhusu chama wanaenda kwenye vikao vinavyohusika na vikao hivyo vipo katika ngazi mbalimbali kuanzia kata hadi taifa.
 
1. Katika historia ya nchi hii, hakuna kipindi wananchi wamekuwa na matumaini na serikali kama wakati huu.
2. Nilishasema, na nitasema tena....Lipumba akirudi CUF chama kitapasuka na akikataliwa chama kitapasuka pia...wachague watataka kifo kipi (two ways to die, choose one)
 
Lipumba ni tawi la tawara linalotumiwa kuipasua cuf, awe mwanachama wa kawaida au la ajiunge lumumba.
 
1. Katika historia ya nchi hii, hakuna kipindi wananchi wamekuwa na matumaini na serikali kama wakati huu.
2. Nilishasema, na nitasema tena....Lipumba akirudi CUF chama kitapasuka na akikataliwa chama kitapasuka pia...wachague watataka kifo kipi (two ways to die, choose one)
Matumaini yalikuwepo mwanzo sasa hivi hakuna matumaini tena, tuwe wakweli na tuache ushabiki,
wengi wamepoteza kazi, biashara nyingi kudorora, waliona tu watu wakitumbuliwa wakafurahi lakini maisha yamekaza zaidi kwa walalahoi
 
LIPUMBA katumwa kama ilivyokuwa mwaka jana wakati wa Uchaguzi, lengo kuu ni kuizika CUF katika uso wa Tz bara na visiwani
 
Back
Top Bottom