CUF yatoa tamko,yamtaka prof. Lipumba asikivuruge chama

CUF wasimame kidete kupambana na huyo msaliti anaetumiwa na chama tawala, kujaribu kuidhoofisha CUF na hivyo kupelekea Ukawa yote kuwa destabilized.. Siasa chafu toka kwa chama kinachojinadi kina ridhaa ya Watanzania kuendelea kutawala..
 
Huko CCM hujaona yanayoendelea kwenye sarakasi za kukabithi uenyekiti wa CCM?
Sisi wajuzi wa mambo tulishawaambia kuwa upinzani wataongea lugha tofauti tofauti kama vile wale jamaa wa enzi zile za mnara babeli, maana wapinzani hawana hoja wote ni njaaa kali mno. Sasa hata wabunge wao wanalia njaa, wanaomba misaada kila pahala,
 
CCM tunatafuta mwenyekiti, kama anataka tunaomba atume maombi haraka iwezekanavyo.
 
Huyu Lipumba kuna kazi amepewa ndo maana anatumia nguvu nyingi sana huo mpango umeshafeli
Na hiyo tabia ya kutuma vikundi kutoa matamko kana ya jana kutishia chama hapo ndio watoto wa mjini wanaseme "amebugi meeen"
 
Prof Lipumba sasa ajikite ktk taaluma yake ya uchumi awasaidie watanzania. Aachane na CUF. Dhambi ya usaliti huwa haisameheki popote.
Prof Lipumba sasa hataweza kuaminika popote pale ktk siasa, labda sasa anaweza kuaminika ktk masuala ya kiuchumi zaidi. Aachane na siasa. Siasa ni mchezo wa wakati tu, wakati ukishapita ktk siasa haujirudii tena.
 
Ataenda Rwanda lini? Kipindi cha uchaguzi aliondoka usiku sana akiwa anatweta kwa jasho,na alionekana ana mawazo sana,mkulu naye alipoapishwa akaenda rwanda!!



Umemaliza vibaya sana, sasa mkulu kwenda Rwanda imehusika vipi hapa?
 
Lipumba angekuwa mjanja,angeanzisha chama chake,akipambanishe na ACT,walau apate mshindi wa tatu
 
Lipumba awe mvumilivu na mwenye subira. August siyo mbali. Asubiri chama kiamuwe. Ila awe tayari kukubali matokeo.
 
Huko CCM hujaona yanayoendelea kwenye sarakasi za kukabithi uenyekiti wa CCM?
Hakuna cha sarakasi, ninyi si ni wambea wambea hamjui hata kinachoendelea ndani ya CCM, kazi yenu kuropoka ropoka tu.
 
Lipumba awe mvumilivu na mwenye subira. August siyo mbali. Asubiri chama kiamuwe. Ila awe tayari kukubali matokeo.
hili ulilosema ndo la msingi,naomba nikuibie Siri zikipigwa kura lipumba atashinda ,ni bora wamdhibiti kabla hajaingia maana kumezuka ubaguzi dhidi ya waabara na wa visiwani. Halafu huku bara lipumba an a network ya watu kuliko mwanachama yyt . Na hata huko Zanzibar anasapoti ya watu kama akina Duni
 
"Hatutamuonea wala kumuonea haya". huu ni muandiko wa Mtatiro.japo baadhi ya maneno yapo kama ya beni.
 
Back
Top Bottom