CNN: Tanzania loses $300m World Bank loan amid crackdown concerns

Sio kweli, wanaozungumziwa ni watoto (<18) maisha yao ni ya hali duni. W
Elimu sahihi ndio inayoweza kuja kuwatoa kwenye mzingo wa umasikini. Wengine wanabakwa na wengine ni kukosa uelewa na pia mila kandamizi. Tusiachie kujengeka kwa matabaka ndani ya nchi yetu.
Ni jukumu letu kama taifa kuhakikisha kuwa watoto wetu wanapata HAKI yao ya elimu BORA bila ya ubaguzi, itakayo wawezesha kuja KUJITEGEMEA.
Tusikwepe wajibu wetu kwa vile tunajiona tuna nafuu. Tunaoweza kusaidia kuondoa mimba za utotoni ni sisi tuliobahatika kuwa na maisha mazuri. Tusikimbilie kuwahukumu watoto wetu. Amen.
 
Mkuu Tang Zhou,

Kwa ruhusa yako, naomba kulitumia bandiko lako hili kama mbegu, kupandishia bandiko kuhusu sovereignty ya nchi yetu vs a vs mikopo na misaada ya mabeberu yenye masharti

Hawa WB kama wana yao, nao ikibidi, waende zao tuu, hawawezi kutunyima mkopo wa elimu kwa kisingizio cha kauli ya Rais Magufuli kukataa mimba za utotoni. Tanzania tangu tumepata uhuru, hatujawahi kuruhusu pregnant girls kuendelea na shule, alichokisema rais Magufuli sio kitu kipya, ni kuusisitiza tuu kitu kile kile, sasa iweje hawa WB, wazuie mkopo huo kwa sababu hizo?!, hawa nao wana yao, kama wana yao waseme tuu, vinginevyo nao tuwafungulie tuu milango, ikibidi kuondoka, nao waondoke tuu, kama Nyerere aliwahi kuwagomea, japo tuliteseka, bora tuteseke huru kuliko kulishwa tukashibishwa utumwani, Kwa rais wetu kupangiwa nini aseme na nini asiseme kisa kuogopa kunyimwa misaada

Japo katika hili la pregnant girls kunyimwa fursa za kuendelea na masomo, mimi siliungi mkono, lakini hili la rais wetu kupangiwa nini cha kusema ili asiwaudhi wakubwa hawa, nasimama na Magufuli.

P
 
Inaelekea wewe ndiye una-tend kufikiri the same way. Kwa hiyo hizo million 300 (gharama ya ku-introduce policy ya hovyo) ndizo zitatumika miaka yote wakati Tanzania ikitekeleza sera hiyo wakati watoto wa kike wakiendelea kuolewa na kupata uja uzito, na kuzaliana wakiwa mashuleni? Kutakuwa na haja gani ya kuwa na sheria ya kuwalinda watoto wa kike wasipate ujauzito? Tatizo la waswahili ni kuanza kufkiri pindi mkiona pesa. Wewe umejiunga nao hao wanaofikiri matumizi ya pesa badala ya madhara ya sera mbovu inayonunuliwa kwa pesa nyingi kama hii kwa ajili ya mataifa machanga. WB wanakununulia sera mbovu kwa billion 600 wewe unakubali kisha unaliingiza taifa kwenye mtego wa miaka yote kubeba bakuli la kuomba misaada na mikopo nje ya nchi kwa ajii ya kutunza mama, watoto na waume zao mashuleni!
 
We jamaa unaudhi sana, kwani kosa LA JPM ni nini hapo!, miaka yote hiyo sheria Ipo kuwa mwanafunzi akipata mimba shule ndio basi, sasa hao world bank walikuwa wapi?
 
Hao world bank wanamatatizo hiyo issue ya wanafunzu kupata ujauzito wakiwa shuleni si la leo.toka zamani ilikuwa hivyo mwanafunzi akipata ujauzito hakiwa shuleni hasa za msingi na sekondali za serikali alikuwa haendelei na masomo.
labda aende za binafsi lakini za serikali ilikuwa hawezi kujifungua halafu akarudi kusoma pale tena.
 
ndiyo mkome sasa kuwapa hatamu wahuni wa kijijini.

wahuni wa mujini wana nafuu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…