ostrichegg
JF-Expert Member
- Jun 30, 2013
- 12,050
- 6,199
Sio kweli, wanaozungumziwa ni watoto (<18) maisha yao ni ya hali duni. WMkuu achana na hawa Wapumbavu wanashabikia kila kitu cha mzungu,wala hawapigi hesabu za mbali, ukiruhusu wenye watoto kurudi shule wanaobeba mimba wataongezeka maana wanajua ruksa kuendelea na masomo na Kama yupo form 1 analipiwa na serikali ada ela ya pampas na kulea atapewa na nani?,siasa zinasababisha watu wengi wawe mataahira.
Elimu sahihi ndio inayoweza kuja kuwatoa kwenye mzingo wa umasikini. Wengine wanabakwa na wengine ni kukosa uelewa na pia mila kandamizi. Tusiachie kujengeka kwa matabaka ndani ya nchi yetu.
Ni jukumu letu kama taifa kuhakikisha kuwa watoto wetu wanapata HAKI yao ya elimu BORA bila ya ubaguzi, itakayo wawezesha kuja KUJITEGEMEA.
Tusikwepe wajibu wetu kwa vile tunajiona tuna nafuu. Tunaoweza kusaidia kuondoa mimba za utotoni ni sisi tuliobahatika kuwa na maisha mazuri. Tusikimbilie kuwahukumu watoto wetu. Amen.