Chimbuko la kabila la Wakurya

Asili ya Wakurya ni Misri, walifika Congo kati ya 322. KK
Hapo zamani kulikuwa na mtu aliyeitwa monto, huyu ni mzazi wa wabantu wote.

Monto alizaa Range miongoni mwa wanae, Range alizaa Magaiwa, Magaiwa alizaa, alimzaa Mkurya.

Mkurya alizaa watoto watano ambao ni Nyanchage, Wangwe, Mongoso, Nano na Mendi.

Nyanchage aliwazaa Mtimbaru, Mosi, na Mosonga hawa ndio tunawaita inchage.

Wangwe aliwazaa Moracha, Mwirege, Keroba, Mugumbe na Gisiri. Hawa ndio tunaowaita Engwe, kemoramba yagesaka.

Watu walivyozidi kuongezeka ukoo wa Gisiri ulikimbilia umasaini nao huitwa Osiri hadi leo huko umasaini.

Kutokana na kosa alilolifanya Gisiri, (ni stori ndefu), ukoo wa Moracha ulibadili jina ukaitwa abanyamongo (wenye maghala ya chakula)
Ukoo wa Mugumbe ulibadili jina ukaitwa abalenchoka (wala nyoka, waliishi mlima wa nyoka).

Mongoso alimzaa Mkira, mtoto pekee. Huyu ndo mzazi wa abakira na maana ya MongoMongoso leo ni tembo dume.

Nano aliwazaa Mokenye, Musweta na Msimbete. Hawa ndio waitwao inano yaani nyani.
Kutokana na hawa waliibuka watu mbalimbali kama abakine, abarieri, abamera, abanyanccha na abangoreme.

Mendi alizaa mtoto mmoja tu Munchari, hawa hujiitia emendi yaani panya mdogo au irigeki.

Nani hajaona ukoo aliotokea hapo?

KUHUSU MAJINA;

Wakurya wana majina sita ya wazaliwa wa kwanza. Matatu ya kiume na matatu ya kike.

Naanza na ya kiume Mwita, Marwa na Chacha. Nitamaliza na ya kike Ghati, Bhoke na Rhobi

Mwita asili yake ni uguita, yaani kuua/Kifo. Wakurya kitu kinachowashinda kupambana nacho huamua kukienzi. Kifo kiliwashinda wakaamua wakienzi kwa kuwapa wazaliwa wa kwanza jina hilo ie to familiarize with that misfortune!!! Ili wakizoeee

Chacha asili yake zimekuja, ni jina walilopewa watoto wa kiume waliozaliwa wakati ng'ombe zimeibwa au zimeletwa toka umasaini au usukumani. Wakurya huamini ng'ombe wote ni wao, hivyo ni kama waliporwa, kwa hiyo vijana walipoenda kuiba ilikuwa sio kuiba ila kuzifuata na kuzileta. Zimekuja/Chacha.

Marwa ni pombe iliyoandaliwa na kunywewa kusherehekea ng'ombe zilizoletwa.

Kwa wanawake,
Bhoke ni asali, kitamu, kitu kilichopatikana bila jasho na kitakacholeta vitamu. Hupewa mtoto wa kike kwa sababu huleta ng'ombe bila jasho, ni baraka kwa familia. Linganisha ng'ombe anazoleta Bhoke na zile za kuiba, zinazopatikana kwa kumwaga hata damu. Kwa hiyo ni asali /Bhoke.

Rhobi hutokana na neno Erhobilo, hii ni shangwe inayofanywa na wanawake na wanaume kufuatia tukio zuri kama kurudisha ng'ombe zilizoibwa. Shangwe hiyo ikifanywa na wanaume pekee huitwa engoliga. Lkn wafata nyayo wanapofika nyumbani nyimbo zao huimbwa na wote, na hapo huitwa Erhobilo, ndo asili ya jina Rhobi

Ghati, hutokana na neno la kimaumbile yaani umbile la mwanamke (uke). Kilichofanya likastaajabiwa ni kuwa mke na mume hulala pamoja, inakuwaje mwanamke abebe ujauzito lkn sio mwanaume? Hivyo Ghati maana yake oghotia au kupasuka. Kwamba wamepasuka ndo maana wanabeba ujauzito. Hili ni jina la kuenzi umbile la wanawake.

Ndoa za kimila. Kwa Wakurya.

Nyumba nthobhu, mwanamke aliyezaa watoto wa kike tu, ili atakapokufa baadae nyumba yake isitoweke huamua kuoa binti wa kuendeleza uzao wa nyumba yake

Nyumba mboke ni kama mwanamke hakuzaa kabisa iwe binti wala mvulana, huyu huoa ili apate uzao

Nyumba ntune ni kama kijana alizaliwa kwao na vijana wengine au peke yake, lkn bahati mbaya akafa kabla ya kuoa hasa kama alikuwa amepita umri wa utoto (ubhulisia). Hivyo familia hukaa na kupanga kuoa mke wa kufufua jina la kijana huyo aliyekufa

Nyumba nyana ni aina ya ndoa ambayo mwanaume anayeoa ni taahira au kilema au zezeta. Kwa kuwa jina la mwanaume halipotei ukuryani, basi ndugu wa familia huombwa kuoa na kuzaa watoto lkn watoto ni wa huyo kilema ambaye kwa kawaida anakuwa hawezi majukumu ya kutungisha au kulea

Nyumba nguru, inatokea kama familia haikubahatika kupata mtoto wa kiume mapema, lkn baadae akazaliwa wazazi wakiwa wazee na wamekata tamaa. Huyo mtoto huolewa mwanamke ambaye huja kuzaa kuendeleza uzao wa mtoto. Mtoto huyu akikua huchagua aidha kukubali huyo mke au vinginevyo lkn mwisho wa siku ni familia yake.

Eteto ni aina ya ndoa ya kawaida. Mwanaume anaoa mke wake au mke wa pili (okohareka).

Ikumbukwe Kuwa, awali mwanaume wa kuoa aina ya ndoa hapo juu ni yule aliyechaguliwa kutoka kwenye ukoo au familia ya wahusika.

[HASHTAG]#kwa[/HASHTAG] hisani ya watu wa Tarime
Hii nimeipenda sana weito
 
Wewe ni Muongo. Mkurya Sio Kama Mnavyodhani. Mkurya Huwa Hachokozi Mtu na Ni Mtu Mkarimu Sana. Mkurya Hataki Dhuluma, Kuonewa etc - Hucharuka Pindi Anapotetea Haki Yake Ila Kamwe Sio Mchokozi Kama Unavyodai. Mimi ni Mchaga, Nina Marafiki Wakurya na Sijawai Kuona Wako Hivyo Unavyosema
ni kweri mura ,sifa mojawapo ya mkurya ni kusema ukweri hata kama mchungu mura tata
 
Bhoooke wane anthighire umwenee, ichinkwe nu umwene ngothenyaa, amanche numwene ngosoraa, ichinyinyi nu umwene nkohaa, hamwe na abhana ndanyorya inyaanyiiiii

Bhookhe bhooke nakohanchereeee, tohanchane bosweigho mbeee eeeeeh,

mamamaaaa...........
 
Nadhani waafrika himaya yetu kubwa ilikua pale Misri, Ethiopia,Somalia na Sudan. Misri imevamiwa mara nyingi sana toka kaskazini ikafanya hawa waafrika wakimbilie kusini na magharibi. Makabila mengi yanakiri kutokea kaskazini either sudan au Misri.
 
Safi sana. Hv huku Tanganyika hakukuepo na watu maana ukifatilia historia ya kila kabila utasikia wametoka nje.
Ni kukosekana kwa watafiti wazawa na badala yake kutegemea historia iliyoandikwa na watafiti wa kigeni au mashirika ya kikoloni. Na inakuwa ngumu kupinga nazo. Watu wengi tayari wanaamini walichofundishwa na kusikia.
 
Back
Top Bottom