Chalamila: Nasisitiza nikifa nizikwe kama waislamu siyo kiislamu. Tunafanya misiba ya kifahari baada ya miezi 2 watoto wanafukuzwa ada

Ninaweza kumuunga mkono kwa uwezo wake wa kifikra ana hoja nzuri lakini ningekuwa mimi hili jambo lilikuwa halina haja ya kuja public keti na familia yako wape misingi kama hiyo katika msiba wako siku ukifa hakuna atakayekataa lakini kuja mbele za watu na kuzungumza ushuzi kama ule haileti maana yoyote
Lazima aliweke Public maana anatafuta kiki kwa Samia
 
Naamini kuna vitu vingi ambavyo uisilamu unakataza lakini baadhi ya waumini wake wanavitaka. Alikufa jirani yetu muisilamu hapa, akatolewa hospitali na kuzikwa juu kwa juu, sisi tukaletewa tu taarifa kuwa jamaa ameshakufa na ameshazikwa huko huko siku hiyo hiyo. Watu wengi wakiwemo waisilamu walisikitika kwa kukosa fursa ya 'kumuaga' marehemu.

Ninachotaka kusema kuchelewesha au kuwahisha mazishi katika Ukristu sio suala la kiimani, ni busara za wanafamilia. Mfano Roman Catholic, akifa muumini nyie toeni tu documents za ubatizo na where applicable ndoa, atakuja Padri/Katekista kuendesha ibada ya mazishi hata siku hiyo (kasoro Jumapili maana ratiba inakuwa imejaa na human resources ndio hao hao wanaohudumia misa ya kawaida).
 
Karibuni kwenye uislamu hii ni dini simple sana, watu mnacimplicate maisha bure tu.
Uislamu sio tu kazika hata harusi zetu ni simple tu.
Ni msikitini pekee unaweza kukuta raisi wa nchi anasali safu moja na walala hoi hakuna special reserved seats kwa mheshimiwa yeyote msikitini.
Thubutu
 
"Nikifa nizikwe kama Waislamu siyo nizikwe Kiislam,
1735185268827.png

Ndumilakuwili at his best
Tunaomba na ile statement ya kule alikoambiwa takbir!!!
 
Karibuni kwenye uislamu hii ni dini simple sana, watu mnacimplicate maisha bure tu.
Uislamu sio tu kazika hata harusi zetu ni simple tu.
Ni msikitini pekee unaweza kukuta raisi wa nchi anasali safu moja na walala hoi hakuna special reserved seats kwa mheshimiwa yeyote msikitini.
Ata ukristo ukiwa huna pesa unafunga harusi simple na mwislam mwenye pesa hufunga harusi ya kifahari
 
Huyu anafanya uchawa kwa Samia hana lolote ,

Uzikwe na sanda,uzikwe kwenye sanduku, uzikwe uchi kama hukujiandaa na Mungu wako haisaidii kitu

Huyu anasema hivo ili Samia asimtumbue

HAKUNA UCHAWA HAPO, HIYO NI FACT AMBAYO WAISLAM PEKEE WANAIFAHAM....
Amesema hivi, watu wanafanya misiba ya kifahari na baada ya msiba familia iliyobaki hata kama ilikuwa na watoto wadogo wanatelekezwa. Badala ya kutumia mahela meeengi kwenye mazishi afahadhali hizo fedha zipewe familia/watoto wake kama wapo (kama Waislam wanavyo wapa familia hela zilizo changwa kwenye msiba).
 
Wakuu,

"Nikifa nizikwe kama Waislamu siyo nizikwe Kiislam, miaka ya leo tumekuwa na misiba yenye mbwembwe nyingi sana bajeti ya mamilioni zinakwenda kuupa ufahari msiba lakini baada ya wiki mbili au miezi mitatu kama ni baba na mama waliowaacha watoto msiba unakuwa ni mzuri na wakifahari halafu baada ya miezi miwili mitatu watoto walioachwa wakiwa yatima wanaanza kufukuzwa ada.

Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Dar es asalaam kwenye hafla ya kutoa misaada kituo cha watoto yatima UMRA Kinondoni.
Sikukuu ziko tatu kwa mwanadamu
Ya kwanza kuzaliwa
Ya pili ndoa
Ya tatu kifo
 
Kufa Kufaana, Wewe Ukishakuwa Public Figure na Umevuta Shuka lazima Kamati za Mazishi Ziundwe ili Watu wavute Mpunga, Watu wataangali Influence yako kwenye Community kama bado una ushawishi basi lazima Fedha zitafutwe kupitia stakeholders mbalimbali Purposely ili Budget iwe Kubwa na watu wapate Kupiga Umo umo
 
Msiba huwa unaratibiwa na family,hata wangetaka uzikwe baada ya mwezi ni sawa tu kikubwa wamekubaliana so kakurupuka uyo kuongea public

Jambo hili angelimaliza na his family ingetosha tu
 
Huyu nae hoja zake ni mfu,hakuna sehemu kwenye biblia inasema mtu azikwe kifahari au kimasikini.
 
Ninaweza kumuunga mkono kwa uwezo wake wa kifikra ana hoja nzuri lakini ningekuwa mimi hili jambo lilikuwa halina haja ya kuja public keti na familia yako wape misingi kama hiyo katika msiba wako siku ukifa hakuna atakayekataa lakini kuja mbele za watu na kuzungumza ushuzi kama ule haileti maana yoyote
kama alishabadili dini
 
Kuna watu wakifika level fulani wanaona wameshajipata sana.. Ishu ya kifo na mazishi ni swala binafsi na la kifamilia zaidi.. Hivyo asitutangazie sisi bali aandike wosia wake aukabidhi kwa familia yake

Yeye anadhani labda atakufa akiwa hapo alipo kwamba itakuwa habari kubwa sana? Amuulize JD aliyewahi kusema msiba wake kutakuwa na kadi maalum za mwaliko
Huyu anaweza kuja kufa na watanganyika wasijue kuwa kafa
 
Chalamila anatafuta umaarufu hata kwa mambo yasiyo na maana wala ulazima.

Hivi kuna mahali imendikwa wakristo wazikwe kwa bajeti fulani?

Tangu kale maziko yalifanyika kwa namna familia inavyoamua.

Bwana Mwokozi wetu alizikwa kwenye kaburi lililoandaliwa na Joseph wa Arimataya, kaburi la kuchongwa ndani ya mwamba, lenye mlango, kaburi alilokuwa ameliandaa kwaajili yake na wanafamilia wake. Hili kwa nyakati hizo lilikuwa ni kaburi la gharama kubwa.

Lakini walikuwepo waliokuwa wakizikwa kwenye makaburi yale ya kuchimba ndani ya saa 1 limekamilika.

Kwa hiyo, vyovyote wanafamilia wanavyoamua ni sahihi, maadam hawamlazimishi mtu.

Kwa taratibu za Kikristo, haijalishi unazikwa kwenye kaburi la namna gani, unazikwa baada ya muda gani, unazikwa kwa bajeti gani, ibada ya maziko ni ile ile. Mambo mengine ni uhuru wa wanafamilia kwa namna ile inayowapa faraja wao.

Kama anapendezwa na taratibu za Kiislam, hatakiwi kusubiri mpaka afe, bali anatakiwa kuslimu kuanzia sasa ili awe na ujakika wa kulazwa kaburini kwa mwongozo wa dini ya kiislam.
 
Kla familia inafanya mazishi kwa uwezo wake! Sijawahi kuona familia inakopa ama inavunja kibubu ili ifanye mazishi.. Pengine kachanganya na harusi huyu
 
Chalamila anatafuta umaarufu hata kwa mambo yasiyo na maana wala ulazima.

Hivi kuna mahali imendikwa wakristo wazikwe kwa bajeti fulani?

Tangu kale maziko yalifanyika kwa namna familia inavyoamua.

Bwana Mwokozi wetu alizikwa kwenye kaburi lililoandaliwa na Joseph wa Arimataya, kaburi la kuchongwa ndani ya mwamba, lenye mlango, kaburi alilokuwa ameliandaa kwaajili yake na wanafamilia wake. Hili kwa nyakati hizo lilikuwa ni kaburi la gharama kubwa.

Lakini walikuwepo waliokuwa wakizikwa kwenye makaburi yale ya kuchimba ndani ya saa 1 limekamilika.

Kwa hiyo, vyovyote wanafamilia wanavyoamua ni sahihi, maadam hawamlazimishi mtu.

Kwa taratibu za Kikristo, haijalishi unazikwa kwenye kaburi la namna gani, unazikwa baada ya muda gani, unazikwa kwa bajeti gani, ibada ya maziko ni ile ile. Mambo mengine ni uhuru wa wanafamilia kwa namna ile inayowapa faraja wao.

Kama anapendezwa na taratibu za Kiislam, hatakiwi kusubiri mpaka afe, bali anatakiwa kuslimu kuanzia sasa ili awe na ujakika wa kulazwa kaburini kwa mwongozo wa dini ya kiislam.
Kama anapendezwa na taratibu za Kiislam, hatakiwi kusubiri mpaka afe, bali anatakiwa kuslimu kuanzia sasa ili awe na ujakika wa kulazwa kaburini kwa mwongozo wa dini ya kiislam.
 
HAKUNA UCHAWA HAPO, HIYO NI FACT AMBAYO WAISLAM PEKEE WANAIFAHAM....
Amesema hivi, watu wanafanya misiba ya kifahari na baada ya msiba familia iliyobaki hata kama ilikuwa na watoto wadogo wanatelekezwa. Badala ya kutumia mahela meeengi kwenye msiba afahadhali hizo fedha zipewe familia/watoto wake kama wapo (kama Waislam wanavyo wapa familia hela zilizo changwa kwenye msiba).
Kwa hiyo waisilamu hufupisha mambo kwa muongozo wa kiimani au ili kupunguza gharama?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom