Chalamila: Nasisitiza nikifa nizikwe kama waislamu siyo kiislamu. Tunafanya misiba ya kifahari baada ya miezi 2 watoto wanafukuzwa ada

Cute Wife

JF-Expert Member
Nov 17, 2023
1,476
4,183
Wakuu,

Your browser is not able to display this video.

"Nikifa nizikwe kama Waislamu siyo nizikwe Kiislam, miaka ya leo tumekuwa na misiba yenye mbwembwe nyingi sana bajeti ya mamilioni zinakwenda kuupa ufahari msiba lakini baada ya wiki mbili au miezi mitatu kama ni baba na mama waliowaacha watoto msiba unakuwa ni mzuri na wakifahari halafu baada ya miezi miwili mitatu watoto walioachwa wakiwa yatima wanaanza kufukuzwa ada.

Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Dar es asalaam kwenye hafla ya kutoa misaada kituo cha watoto yatima UMRA Kinondoni.
 
Kumbe Uislamu mnaokubali japo mnaishi kiunafiki
 
Karibuni kwenye uislamu hii ni dini simple sana, watu mnacimplicate maisha bure tu.
Uislamu sio tu kazika hata harusi zetu ni simple tu.
Ni msikitini pekee unaweza kukuta raisi wa nchi anasali safu moja na walala hoi hakuna special reserved seats kwa mheshimiwa yeyote msikitini.
 
Kwani Ukristu unazuia mtu kuzikwa saa hiyo hiyo aliyokufa, au ni maamuzi tu ya wanafamilia?
Yeye hana haja ya kuwaambia watu wengine hadharani, awaambie tu wanafamilia wake au aandike wosia, naamini watauheshimu. Hata serikali huwa inasikia kwanza ratiba ya familia. Awaambie tu wanafamilia kuwa hata akifa kifo chenye utata asicheleweshwe, azikwe saa hiyo hiyo, naamini watamtii, hawatasubiri uchunguzi wa polisi
 
Leo ameongea ukwl ,tupo nae
 
Huyu kuna kitu ameshtuka.
Kauli yake ya kwanza alisema anataka akifa azikwe kiisilamu. Kama kawaida Roman Catholic wakainote down hiyo kauli maana huwa hawapendi kujihusisha kwenye mazishi ya mtu ambaye imani yake katika Kanisa imeondoka waziwazi (kwa kutamka, kuishi wawili bila ndoa, kujiua, kufia maeneo yanayoashiria uwepo wa matendo mabaya).

Sasa hivi amekuja na kauli mpya kwamba azikwe kama waisilamu na sio kiisilamu.

Ngoja msubiri picha siku atakapokufa kweli, bila kitubio Roman Catholic huwa hawaangalii sura ya mtu. Aulizwe Ngombale Mwiru, Ruge Mutahaba na Bilionea wa Arusha
 
Umezungumza hoja ya msingi sana mdau ,,,vipo vitu kaa na familia yako na siyo kuja public havina maana yoyote ni kweli hakuna sehemu waliyoandika mkristo azikwe baada ya siku kadhaa hayo ni maamuzi ya familia yako
 
Ninaweza kumuunga mkono kwa uwezo wake wa kifikra ana hoja nzuri lakini ningekuwa mimi hili jambo lilikuwa halina haja ya kuja public keti na familia yako wape misingi kama hiyo katika msiba wako siku ukifa hakuna atakayekataa lakini kuja mbele za watu na kuzungumza ushuzi kama ule haileti maana yoyote
 
Reactions: apk

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…