CHADEMA hamna akili!
Mnaongelea kuhusu Demokrasia nitajieni nchi moja tu ya Kidemokrasia Dunia hii ambayo baada ya uchaguzi kuisha na Raisi kuapishwa wanasiasa wake wanaanza kampeni za uchaguzi ujao!
Kama ni hivyo kuna haja gani sasa ya Tume ya uchaguzi kuweka kipindi cha kampeni za kisiasa? au hata hilo pia hamulielewi? Bunge lina maana gani? Ni kwa nini mna Wabunge wameenda kufanya nini Bungeni?
1. Jazba huwa hazijibu hoja. Hawajasema wanaanza kampeni za uchaguzi, bali mikutano ya hadhara ni fursa ya vyama vya siasa kuongea na wafuasi wao na wananchi na kuweka mikakati ya namna ya kuimarika kichama na kisera. Ukizuia mikutano ya aina hii unataka kuturudisha kwenye utawala wa chama kimoja - ni kuua demokrasia ya vyama vingi - maana waziri mkuu huwa siyo anayetoa ruhusa namna vyama vya upinzani vinavyopaswa kuendesha siasa zake.
2. Vyama vya upinzani vimefanya kazi kubwa sana hata kuwezesha kumpata rais ambaye ameahidi kuwatumikia Watanzania wote bila kuwabagua. Nina imani kama uchaguzi wa mwaka huu usingekuwa na ushindani mkali ulioletwa na vyama vya upinzani (hasa Ukawa) pengine tungekuwa na rais tofauti.
3. Hivyo, si vizuri kudhani hivi vyama havina maana au kazi yake imekwisha kwa vile vimeshindwa maana ili nchi iendelee na serikali ifanye vizuri zaidi ni lazima vyama vya upinzani viendelee kuisukuma bila kuchoka. Ni kama shuleni kama mwalimu wa zamu anahakikisha kila mwanafunzi anafanya 'prep' hakuna mwanafunzi atakaye kacha 'prep'. Lakini kama mwalimu wa zamu hafuatilii wanafunzi wanafanya wanavyotaka na hakuna prep inayofanyika.