CHADEMA MUST now Reform and Restructure!

Wabz,

We unataka wengine tutafutiwe fatwa zaidi baada ya kudaiwa tumenunuliwa. Sasa angalia yaliyotokea Bagamoyo or wherever walipokuwa wamejificha.

Sasa ukiangalia ule mvutano unaosadikika uko kati wa rafiki yetu Zitto na mwenyekiti na uongozi wa Chadema, uamuzi wa Bagamoyo unampa Zitto point za bure!

Hivi walimpigia kura ya kutokuwa na imani nae kwa kura ngapi vile? SMH
 
sikuwahi kuona uchambuzi huu,..
maoni haya ni mazuri sana ila sidhani kama mbowe
ni mtu wa kusikiliza maoni kama haya,...
yeye ni mtu wa maoni yoyote yatakayo muweka yeye kuwa juu
 
sikuwahi kuona uchambuzi huu,..
maoni haya ni mazuri sana ila sidhani kama mbowe
ni mtu wa kusikiliza maoni kama haya,...
yeye ni mtu wa maoni yoyote yatakayo muweka yeye kuwa juu
 
New era politics, new era JF, wakongwe wa JF rudieni nyuz zenu za 2006 na siasa za wakti huo na context ya time hyo, then mje mdharau siasa za sasa na CDM.
 
Ukweli unaonekana na nimependa Hotuba za Viongozi wa Chadema

MBOWE: TUTAENDELEA KUKOMAA NAO HADI KIELEWEKA
na Edward Kinabo, Songea

BAADA ya kuiteka miji na vijiji vya mikoa ya Mbeya, Rukwa na Katavi, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), jana kiliuteka mji wote wa Songea, mkoani Ruvuma kwa maandamano na mkutano wa hadhara, huku viongozi na wanasiasa kadhaa wa chama hicho wakionya kuwa Rais Jakaya Kikwete anaweza kung’olewa kabla ya mwaka 2015.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, akihutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Songea alisema sasa chama hicho kina uhakika wa kuchukua nchi wakati wowote ikiwa Rais Jakaya Kikwete hatachukua hatua za dharula kupunguza makali ya maisha na kuwapa wananchi uhuru wa kutengeneza katiba yao.

Alisema hatua ya serikali ya CCM kunywea na kuanza kujadili Katiba mpya ambayo waliipinga wakati wa kampeni, ni dalili tosha kuwa umma wa Watanzania chini ya muongozo wa CHADEMA unaweza kujiletea neema muda wowote ukitaka.

Alisema badala ya kusubiria miaka mitano CHADEMA tayari imeanza kazi ya makusudi ya kuishinikiza serikali na mamlaka husika kupunguza makali ya maisha kwa kuondoa kodi kwenye bidhaa na huduma muhimu, huku akionya kuwa serikali itakuwa hatarini kama haitaheshimu matakwa ya umma.

“Utamaduni wa kusubiriana miaka mitano, ni janja yao ya nyani, sasa tumeamua tuwapige mtiti, tunapiga maandamano na mikutano ya nguvu. Tumegundua ukicheka na nyani unavuna mabua. Tumevuna umaskini kwa kuchekacheka na CCM kwa miaka 50. Sasa tunawakomalia hadi kieleweke,” alisema Mbowe na kushangiliwa.

Alisisitiza kuwa CHADEMA inapenda sana amani lakini haiko tayari kuona amani ikitumika kama giza la kukandamiza watu wasidai haki na maslahi yao.

Alibainisha kuwa CCM tayari imeshaonyesha udhaifu wa kisera na kihoja ndio maana imeamua kudandia propaganda za kidini na kikabila ili kujaribu kuigawa na kuidhohofisha CHADEMA, jambo ambalo alisema tayari limeshindwa.

“Tunasema hatutatishwa na propaganda za kutugawa. Walisema CHADEMA ni chama cha Kichaga tukawapiga pembeni, walisema CHADEMA ni cha kidini nayo tumewapiga chini. Mchungaji Msigwa, Sugu, Chiku Abwao, Josephat Nyerere ni Wachagga? Hawana hoja. Hapa tuna Waislamu wengi, kuna Wakristo wengi, lakini tunaunganishwa na dhamira yetu ya kupigania maslahi ya nchi, tusikubali kugawanywa. CCM wanatumia sera ya kikoloni ya wagawe uwatawale, lakini hatutaruhusu hilo litokee. Tutakomaa hadi dakika ya mwisho,” alisema.

Aliwataka wakazi wa Songea kuungana na Watanzania wa mikoa mingine katika kushinikiza kushushwa kwa gharama za maisha na kuhakikisha kunaandikwa katiba mpya.

“Na tunawaambia kule bungeni, CCM wakiendelea kupandisha kodi za mafuta na bidhaa nyingine mbalimbali zinazosababisha maisha yawe magumu, haki ya Mungu nawaambia tutaandamana nchi nzima hadi kieleweke. Na huo ndio ujumbe wangu mkubwa kwenu,” alisema Mbowe na kushangiliwa.

Naye Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Slaa, akiwashukuru wakazi wa Songea kwa kura nyingi walizompa katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, alisema kwa hali ngumu ya maisha ilivyo na jinsi Watanzania wengi wanavyoichukia CCM, uko uwezekano mkubwa kwa wananchi kumng’oa Kikwete kabla ya mwaka 2015.

Akitoa mfano alisema katika nchi nyingine ya Japan, wananchi wakiona kiongozi wao hatimizi ahadi, matakwa na maslahi yao humuondoa kwa kumpigia kura ya maoni kabla ya muda wake kukamilika.

“Mjadala wa Katiba ya nchi hii ndio mwanzo wa kuwaondoa madarakani, Kikwete asipotimiza matakwa ya umma anaweza kung’oka kabla ya mwaka 2015. Walichakachua kura, lakini hawakujua kwamba tuna watu wengi nyuma yetu,” alisema Dk. Slaa.

Alisema tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka jana, Rais Kikwete hajathubutu kufanya ziara hata moja ya kuwashukuru wananchi kwa sababu anajua fika hana wa kumshukuru kwani alichakachua kura.

“Tungetaka wakati ule tungefanya vurugu kama Ivory Coast lakini nilikataa nikasema sitaki kwenda Ikulu kwa kumwaga damu. Leo mwenzangu tangu uchaguzi umalizike hajaja kushukuru wananchi, anajua hamkumchagua kwa hiyo hana wa kumshukuru. Amshukuru nani wakati alichakachua kura?” alihoji Dk.Slaa na kuacha umati mzima ukimshangilia.

Alisema tangu awe Rais kwa kipindi kingine cha pili, Rais Kikwete amekuwa akifanya ziara za mara kwa mara nje ya nchi hususan Ulaya huku akiweka wazi kuwa mpaka sasa ndani ya kipindi cha miezi sita ameshakwenda nje ya nchi takriban mara 12.

“Badala ya kuja kusikiliza matatizo yenu, yeye kila mwezi anakwenda Ulaya. Jana amekwenda tena Afrika Kusini …kule amewaambia kwamba Tanzania inapambana na umaskini. Hayo mambo alipaswa kuja kuwaeleza ninyi na sio watu wasiomhusu. Kwa mwezi anakwenda nje mara mbili na mpaka sasa ndani ya miezi sita ameenda nje mara 12,” alisema Dk. Slaa na kuongeza.

“Akishindwa kuwapa wananchi elimu bure, tutamwondoa. Akishindwa kutupa nyumba bora za bati, tutamwondoa na akishindwa kushusha bei za bidhaa na huduma mbalimbali ili maisha yawe nafuu, tutamwondoa.

Japan, waziri mkuu akishindwa kutekeleza wanayotaka wanamwondoa. Usalama wake wa Kikwete wa kufika miaka 5 ni kutimiza matakwa ya Watanzania,” alisema Dk. Slaa.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe aliendelea kumtuhumu Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo, kuwa ni waziri wa madeni kwani tangu ateuliwe deni la taifa limekuwa likongezeka hadi kufikia trilioni 16 hivi sasa.

Alisema kwa deni hilo sasa kila Mtanzania anadaiwa wastani wa sh laki tatu.

“Mkulo ni Waziri wa Madeni asijaribu kabisa kushindana na mimi, tangu ameingia nchi yetu imekuwa ikikopa tu. Tunakopa kununua mafuta, tunakopa kununua vipuri, karatasi na tunakopa kulipa watu mishahara. Ndio maana tunasema katika bajeti mbadala tutataka waziri huyu awajibike,” alisema Zitto.

Maandamano ya jana sawa na yale yaliyotangulia katika mikoa mingine yaliongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Makamu mwenyekiti Said Issa Mohamed na Katibu Mkuu, Dk. Willbrod Slaa, yakianzia nje kidogo ya mji wa Songea katika eneo la Msamala.

Kutoka eneo hilo maandamano hayo yalitembea kwa umbali wa takribani kilometa tano yakipitia barabara kuu inayopita katikati ya mji huu hadi katika viwanja vya shule ya msingi Kibulang’oma kata ya Lizaboni, kulikofanyika mkutano mkubwa wa hadhara.

Maelfu kwa maelfu ya waandamanaji walijitokeza kuunga mkono maandamano hayo huku wakiimba nyimbo mbalimbali za mshikamano na za kukikejeli Chama cha Mapinduzi (CCM), kama “Kama sio juhudi Mafisadi presha inapanda, presha inashuka, CCM tumewashika pabaya.”
Waandamanaji hao pia walibeba mabango yaliyokuwa na ujumbe wa aina mbalimbali kama “Ameshindwa Luteni Makamba sembuse wewe mgambo Mukama, CHADEMA okoa Ruvuma na ufisadi wa mbolea na CCM someni alama za nyakati, Watanzania hatuwataki.”

http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=30625
 
R.I. P CCM (MAGAMBA)
Kwa ule umati wa Songea , najiamini kusema kuwa ccm tulikupenda, lakini kuzimu na kaburi vimekupenda zaidi!
 
Ccm ilishalaniwa na mungu siku nyingi kwa dhuruma walioifanya kwa watanzania wasio na hatia,hukumu inawasubiri mkama na nape mlopokaji
 
Sasa wamebaki na kuwa na na watu kama wakina Nape ambaye anafafana na babu yake Makamba ila tafauti yake Nape ni Kijana
 
Nimejaribu kurudia kukusoma tena Mheshimiwa mchungaji...

Mzee Mwanakijiji,

What we are witnessing with Chadema today is scary! It seems as if the party is yet to do a self examination of what led to its failure to win the elections and as ex[ected, the focus has been on petty stuff, like trading words with Magamba, Rizwan, VAT and so forth rather than articulating strongly key issues that can open the eyes of Watanzania.

On other hand, Zitto tried to address the issue of Mishahara, but failed to put the Serikali on check on the never ending expenditures!

Now with Malori na mshahara wa Dr. Slaa, one has to wonder if Chadema is really serious ready to re-define itself and take over from CCm which is now facing the biggest infight since the days when Jumbe and others were forced out.

I have said it over and over, it is economic stupid! Ufisadi stories are pennies in a bucket of water! Anyway, may be one day they will wake up and become a true opposition!
 
Mzee Mwanakijiji,

On second thought, Chadema are falling into CCM trap with the speed of light! They are engaging in petty politics of podium exchanges! CCM is using Nape for this and Chadema is the whole leadership engaging to the CCM's ruse!

It will be better of if Chadema will either bring back a second version of Operation Sangara fine tuned and so is their Agro Policy to match Kilimo Kwanza.

However I am still not understanding why Chadema is reluctant to use Azimio la Arusha and Tujisahihishe to knock CCM to its knees!
 
Kwa mwendo huu wa maandamano wala cdm hamtafika popote.

Swali: mkimaliza kufanya maandamano mikoa yote mtafanya nini ukizingatia ccm haitabadilisha msimamo wake wa kutowajibisha mafisadi. Kwa kuwa kuwawajibisha mafisadi sie wananchi wenye kusoma situation tumeishaona haitawezekana.

Fisadi anawajibishwa kwa kufilisiwa na siyo kufanya maandanao kama chadema. Na natumai ni Rais wa nchi tu ndio anaouwezo wa kuwafilisi hao mafisadi.

Hivyo chadema hizi ni mbio za sakafuni. Ni bora kama kweli mnaipenda tz mngeanza juhudi kuwasemea na kuwaanika kwa vidhibiti mafisadi na kufuatilia vijisenti wanavyoweka mabenki ya huko ulaya na america ili msaidie intel ya kushinikiza kuwafilisi vizuri.

Just to advice u.

And don't think you are the most clever pple to talk for this nation, no, you are just pple who have ambition to shout against CCM and doubtly not for the nation's benefit.
 
Kweli sasa CHADEMA imekuwa katuni, watachukua nchi gani jamani hawa walevi wa mawazo? Wamekosa ulaji sasa wanaleta maneno ya vitisho yani ni tabia za kichaga kabisa. Nyie nendeni Tanzania Nzima mkaimbe nyimbo zenu zile zile lakini mwisho wa maneno CCM ndio imeshika nchi na 2015 lazima ipite tena .

Ole wenu mkiendelea kutoa maneno ya kijambazi jambazi....virungu vinapigwa polish.
 
Ndugu,
Kama unaona maandamano ya CDM hayatatufikisha popote, kidogo nina wasi wasi na uwezo wako wa ku-assess situation. Kwanza nikuulize kama kusingekuwa na maandamano wanamagamba wangekwenda Dodoma kutangaza kuvua hayo magamba? Kwa taarifa yako tu usifikiri CDM wakishatembelea mikoa yote watazuiwa kurudi tena huko mara nyingine kuendelea kuamsha mapambano. Haya mapambano si ya msimu yataendelea hadi kieleweke. You also said that CDM people are not clever enough to talk for the nation, but what you forgot to mention, which I think was more important, is who do you think are more clever to do so. Please tell us
 
Kweli sasa CHADEMA imekuwa katuni, watachukua nchi gani jamani hawa walevi wa mawazo? Wamekosa ulaji sasa wanaleta maneno ya vitisho yani ni tabia za kichaga kabisa. Nyie nendeni Tanzania Nzima mkaimbe nyimbo zenu zile zile lakini mwisho wa maneno CCM ndio imeshika nchi na 2015 lazima ipite tena .

Ole wenu mkiendelea kutoa maneno ya kijambazi jambazi....virungu vinapigwa polish.

Elewa kuwa jeshi letu la polisi la sasa ni la kisasa zaidi. Lina wasomi wengi wenye uwezo wa kuchambua hoja na kutafakari kabla hawajafanya jambo. Linao askari wenye elimu duni pia lakini waliochoshwa na udanganyifu wa ccm. Hawa hawahitaji tuition kutoka CDM. Uongo uongo wa ccm na ugumu wa maisha walionao wao na familia zao ni mwalimu tosha kabisa. Sasa usijaribu kudangayika kuwa eti mtaamuru jeshi la watu kama hawa litumie virungu kugandamiza haki ilie ambayo hata lenyewe linahitaji. Pengine labda muunde kikosi cha aina ya mungiki kisimame nanyi kwenye hivyo virungu.

Vinginevyo ndugu yangu kama hujui kusoma nyakati, mtawaa murisha polisi wachukue virungu na hapo ndipo mtakavyojua kuwa siyo kila siku ni boxing day!.
 
Chadema wamechukua ruti ya kuandamana..wewe solution yako ni kushauri Chadema ukiwa umejificha nyuma ya kumpyuta yako. Very clever, sasa ngoja nikuulize swali, kazi ya kuwabana mafisadi ni ya Chadema peke yake? wao ndo wamegeuka polisi na waendesha mashtaka sivyo? Very nice.
 
Halo uwezo wako wa kufikiri ni mdogo sana,Ungetoa ushauri wewe unataka nini kifanyike sio kubeza kitu ambacho watu wengi tunaona kinaleta mabadiliko kwa umma.Hivyo kama huna cha kuchangia ni vema ukae kimya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom