CHADEMA kuna Ombwe la Uongozi

Msihangaike naye anataka kuhamisha mawazo ya wapenda mabadiriko Viva Roma mkatoriki kwa wimbo wako Viva Lowassa, Viva UKAWA
Asanteni sana
 
Taratibu kamanda..,umekuja kwa hasira sana..povu linakutoka na spelling unakosea. Taratibu Kamanda.

Kwa tafsir yako Tafiti ni nini..? Kwangu mimi yale majibu ya TWAWEZA, SYNOVATE na LOTUS ni majibu ya kitafiti.,yanatuambia kuwa nani anauelekeo gani katika uchaguzi huu.

Haya hata maoni ya BBC nayo haujishughulishi nayo..? Au nao wamenunuliwa na CCM..?
Utafiti una sifa zake sio kila majibu au maoni uyaite utafiti. Utafiti inabidi uwe NA idadi flan ya waliohusishwa ili uwe na mana.

Ni kweli ninetokwa na povu baada ya kuona wanituchafulia fani. Kama wewe unavyoshiba Ccm NA sisi tunashiba kwenye mautafiti so heshimu fani za watu. Maoni sio utafiti
 
Nyimbo ile ile, zinabadilishwa santuri tu.
Mnaruhusiwa kunibadilishia jina ikiwa hilo litawatosha na kuwachosha, lakini sintoacha kuwanyoosha.

Ccm kwenyewe unakaa benchi dakika zote 90 sasa chadema ungesaidia nini zaid ya kuongeza idadi ya wanachama wasio na mchango mfuate mwenzio slaa marekani
 
AMANI IWE JUU YENU ENYI WAJA WEMA WA BWANA MUNGU WANGU...!!

Katika muendelezo wa kuwafikirisha, nimeona leo niwaandikie kuhusu hali ya Upinzani na kampeni zinavyoendelea hapa nchini, ambapo hali ya sintofahamu ikiendelea kudhirihi kwa CHADEMA na Kambi yote ya Upinzani hapa nchini, wachambuzi mbalimbali, wasomi na waandishi wameendelea kuandika wakijaribu kuonyesha tatizo lililoikumba kambi hiyo, wengi wao wakisema FEDHA, vipande vya rupia vilivyoingia CHADEMA vimewafarakanisha. Nami Binafsi ktk muendelezo huo huo wa kuchambua hali hiyo nitaeleza CHANZO ama SABABU halisi ya SINTOFAHAMU inayoikumba kambi ya Upinzani.

Kwa Muhtasari sana, niseme CHANZO na SABABU HALISI ya Upinzani kukosa muelekeo na kufikia hapa tulipo ni OMBWE la UONGOZI katika kambi hiyo ikiongozwa na CHADEMA..Mimi niliwahi kuwa mwanachama wa CHADEMA, tena Kiongozi Mkubwa katika jumuiya yake ya Vijana, nilipata fursa ya kushiriki, kuhudhuria na kuchangia katika vikao na mikutano mikubwa, muhimu na nyeti ya Chama hicho.

Ilikuwa bayana kwetu kuwa, ilipofikia CHADEMA ilihitaji UONGOZI mpya utakaokuja na dira, maono na tafakuri mpya ambayo ingeki-transform chama hicho kuwa chama kamili cha siasa na kuondoa uongozi wa hamasa na mihemko ya kiuanaharakati..

Nikiwa ndani ya Vikao vya CHADEMA nikaliweka hili BAYANA kuwa tunalo ombwe la uongozi ndani ya CHADEMA, sikueleweka, nikaonekana natishia maslahi ya wakubwa na nafasi zao kwenye Chama, nikaonekana ADUI na nikapewa jina MSALITI.

Ukweli ni kwamba FEDHA ambayo leo imetajwa mara kadhaa kuwa ndio sababu kuu ya mfarakano ndani ya CHADEMA, imepata njia kutokana na Ukweli kuwa CHADEMA kuna Ombwe la Uongozi ambao umekosa Vision na Mission, ndio maana wakadhani FEDHA na UMAARUFU wa mtu ni mtaji wa wao kuingia Ikulu, wakasahau misingi, dhamira, imani na kiu ya Watanzania.

CHADEMA haina tabia ya kujitafakari, haijisahihishi, na wamezoea kuishi kimazoea, wanadhani kila siku ni jumapili na kila walisemalo watanzania watalikubali tu madhari limesemwa na wao, na kwamba kila muongeaji basi anasikilizwa. SIO HIVYO...!!

Leo waongeaji wa CHADEMA na WATETEZI wakuu kwenye mitandao ni YERICKO NYERERE, A man with 0.001 IQ, Anaishi katika uongo na uzushi, mpaka kila mmoja amemmpuuza, Mwanakijiji, Chahali na WATABE wengine wa maandishi yenye adili, wameikacha CHADEMA, bado CDM haijiulizi, inajivunia kuwa na YERICKO. Wasomi, watumishi, na wanataaluma wameikacha CHADEMA, bado CDM haijiulizi, wanajivunia madereva bodaboda.

Moja ya sifa ya Mwerevu, ni yule ambae haumwi na nyoka mara mbili, anayejikwaa akaanguka kisha asiishie kuangalia alipoangukia bali hugeuka kwa umakini na kutazama alipojikwaa, ni nini hasa kimemuangusha..Popularity ya CHADEMA na Upinzani imeshuka na inaendelea kushuka kwa kasi, HAWAJIULIZI.

Viongozi wameacha kuchangia hoja za msingi ndani ya Vikao, wameshikwa na woga na wengine wamesusa, Mwenyekiti Mbowe ambae Mimi binafsi nilishamuita ZERO tukiwa ndani ya Kikao changu cha Mwisho nikiwa KAMANDA wa CDM, ameendelea kwenda Mrama kwa kasi ya ajabu...kila jipya analoliamua ni baya kuliko la jana..


Ombea Chadema isife kwani ikifa na wewe utakufa njaa! Utaingiza tena fedha kwa ''kuwatukana na kuwakashifu kina nani?
 
Mimi ni mtumishi wa serikali na ninakushangaa sana unaposema watumishi wameikacha chadema. Kamwe usitake kuongelea nafsi ya mtu,endelea kujikomba huko CCM ili waje wakufikirie kwenye huo ukuu wa wilaya wa kupeana ila si kuja kutusemea humu JF.Walimu kila siku wanalia wamenyimwa kulipwa madai yao ya msingi unadhani bado wana hamu tena na serikali hii legelege?
Pole sana endelea kuwaburudisha waliokutuma ila wengine tunamshukuru sana Mbowe kwakuwa ndiye mpinzani pekee asiye na njaa ya kununulika na vibaraka ulionao!
HUU MUDA WAKO ULIOPOTEZA BORA HATA UNGENADI SERA ZA CHAMA CHAKO,CHADEMA HAIJAWAHI KUTAWALA NCHI HII SASA ALIYETUFIKISHA HAPA KWENYE MAFISADI NI NANI?CCM MMESHINDWA KUDEAL NA HAO MAFISADI PAPA?KAMA TANGU MIAKA 8 MMEISHI NA MAFISADI NA YAMEWASHINDA BADO MNAENDELEA KUOMBA RIDHAA YA KURUDI IKULU ILI MKAFANYE NINI?
NINA HASIRA SANA NA WATU WENYE AKILI ZA KUENDESHA MAISHA YA KUJIKOMBAKOMBA KAMA WEWE!NENDA KAFUNDISHE SIASA HUIWEZI.
 
BEN SAANANE..unamuita BEN aje kunijibu mimi..? tena kuijibu HOJA ya Ombwe la Uongozi ndani ya CHADEMA..? Labda nisema katika usiyoyajua. BEN ni miongoni mwa watu ambao hawaamini katika Uongozi uliokuwepo sasa ndani ya CHADEMA, nimezungumza nae mengi lakini pia tumeshirikiana kulieleza hili nikiwa ndani ya CHADEMA, ingawa mwenzangu alifanya KIUNAFIKI, alitawaliwa na woga na ubinafsi.

Na kuhusu kuwazungumzia makundi mengine, unaweza kwenda kujiridhisha kwenye tafiti mbalimbali zinazoendelea kuhusu kukubalika kwa vyama vya siasa na makundi mbalimbali ya kijamii..kisha angalia makundi hayo ya Wasomi, Wanataaluma na Watumishi wanaikubali kiasi gani CHADEMA..sio unatokwa na povu tu hapa, jiridhishe kabla haujatetea uozo.

Binafsi si shabiki wa chama chochote cha siasa lakin hua nafatilia sana mienendo ya vyama,wanachama na mashabiki wa hivi vyama na nilichogundua ni kwamba ni vigumu sana watu kukubal kukosolewa hasa cdm eti kwa kigezo kua mpinzani ndo mkosoaji ivo yeye hakosei. Shonza ulichoandika nikikitafakal na kuona mambo yanavoendelea ndan ya vyama vya upinzani nakubaliana na wewe kwa asilimia kubwa mno. Viongozi wa vyama wanapaswa kusimamia misingi,dhamira na itikadi ya vyama vyao ili visiyumbishwe na fedha,nguvu na umaarufu wa watu ndan na nje ya chama na vinginevyo hali inawezakua mbaya kwa vyama hivi hasa visiposhinda uchaguz mkuu huu.
 
Binafsi si shabiki wa chama chochote cha siasa lakin hua nafatilia sana mienendo ya vyama,wanachama na mashabiki wa hivi vyama na nilichogundua ni kwamba ni vigumu sana watu kukubal kukosolewa hasa cdm eti kwa kigezo kua mpinzani ndo mkosoaji ivo yeye hakosei. Shonza ulichoandika nikikitafakal na kuona mambo yanavoendelea ndan ya vyama vya upinzani nakubaliana na wewe kwa asilimia kubwa mno. Viongozi wa vyama wanapaswa kusimamia misingi,dhamira na itikadi ya vyama vyao ili visiyumbishwe na fedha,nguvu na umaarufu wa watu ndan na nje ya chama na vinginevyo hali inawezakua mbaya kwa vyama hivi hasa visiposhinda uchaguz mkuu huu.

ingawa umesema sio shabiki wa chama chochote kwa kubaliana na shonza tumeshafahamu upande wako lakini jambo la msingi hapa ni kwamba sisi wenye mapenzi na hivyi vyama tuna matumaini gani kwa wenzetu wasiona kama sio tunaotumia jicho la tatu kufikikiri tuna nafasi ya kuwajulisha na kupambana na udhalimu wa viongozi kwa kuwaelimisha ndugu zetu hakuna aliye mtakatifu ndani ya hivi vyama ila CHADEMA inaboa...
 
ingawa umesema sio shabiki wa chama chochote kwa kubaliana na shonza tumeshafahamu upande wako lakini jambo la msingi hapa ni kwamba sisi wenye mapenzi na hivyi vyama tuna matumaini gani kwa wenzetu wasiona kama sio tunaotumia jicho la tatu kufikikiri tuna nafasi ya kuwajulisha na kupambana na udhalimu wa viongozi kwa kuwaelimisha ndugu zetu hakuna aliye mtakatifu ndani ya hivi vyama ila CHADEMA inaboa...

Sama ndugu nimekupata
 
Shonza Unajivunia UDINI, UJANGILI, SEMBE, RUSHWA, UFISADI, MIASHA MAGUMU, KUKOSEKANA KWA; UMEME,MAJI AU HUDUMA MBOVU ZA AFYA, ELIMU NA BARABARA? Nini hasa unachojivunia ndani ya CCM ? ...
 
Wewe hautakuwa wa Kwanza kuniona Mimi ni mnafiki, lakini pia hautakuwa wa Mwisho, wapo waliokutangulia na wapo watakaufuata baada yako.lakini HOJA yangu itabaki imara na haitabadilika kuwa CHADEMA kuna OMBWE la UONGOZI..ni hoja ambayo nimeisema na kuisimamia tangu nikiwa CHADEMA na nitaendelea kuisema na kuisimamia hata sasa..

Mimi sio katika wale ambao wanataka UPINZANI ufe kabisa, na wala sio katika wale wanaoamini kuwa salama ya CCM ni Upinzani dhaifu..mimi naamini kuwa NGUVU ya CCM, Uimara wake na UTENDAJI wake utakuwa bora zaidi kukiwepo Upinzani Madhubuti, ambao utawakumbusha CCM wanapojisahau..

Mimi ni MwanaCCM, tena sio tu mwanachama bali ni Mtumishi wa CHAMA, naamini katika CCM lakini kama nilivyotangulia kusema kuwa SIAMINI kuwa salama ya CCM ama ya TANZANIA ni kufa kwa Upinzani...siamini hivyo.


umenena na kukiri kuwa wewe ni mwajiriwa wa CCM. BASI ENDELEA KULINDA KIBARUA CHAKO MAANA CCM IKIANGUKA NA WEWE UPO UWEZEKANO UNAOGOPA KUWA JOBLESS. KWA MAELEZO YAKO NI MALOFA NA WAPUMBAVU TU NDO WANAOWEZA KUPATA TAFSIRI AU MAUDHUI YA MANENO YAKO YOTE. BILA SHAKA KAMA UNGALIKUWA BADO UPO CHADEMA UNGEANDIKA KINYUME CHAKE. ILA UMEJITAIDI KUNYEA KAMBI YAKO YA ZAMINI KAMA MAGUFULI AKIONA MAANDISHI YAKO NA AKISHINDA UNAWEZA PATA ZAWADI KAMA YA DC.MAKONDA, NAJUA UNAIJUA NA BADO KUTUKANA TU HAUJAANZA.MAELEZO YAKO YOTE YAPO BIAS KWA 100%. YAANI UMESHINDWA HATA KUJIFICHA KIAINA KUWA UMETUMWA.
 
CDM ilikuwa kabla ya 2015 ..baada ya hapo tunaona kikundi kidogo kinachojiita CDM tunabaki tunashangaa, hiki kikundi mbona hata rangi na mienendo na ile CDM harisi havifanani tena, hiki ni kitu gani? mbona kimechafuka hivi? kinakimbiwa na wenye maono na fikra, waelevu wamejiweka kando ..jahazi linazama na nahodha kalewa wanzuki za magendo
 
Kila ninaposoma thread za huyu dada kuna kitu huwa kinanisikitisha sana kwa vijana wa Chadema wanashindwa kabisa kumjibu mtu kwa hoja, lakini wakati mwingine sishangai huenda tabia ya kuporomosha matusi wanaiga kutoka kwa viongozi wao!
 
Back
Top Bottom