Chadema fanyeni vikao vya ndani kukosoana, kurekebishana, na kusahihishana

Mmemtoa wapi huyu naye? Mbona anaongea si kwa utulivu?
Ndiyo lugha zenu mpya hizo: utulivu, ustaarabu, n.k.; huku mkitumia lugha laini kilaghai kuhadaa watu.
Acha huyo David azungumze kwa lugha yoyote itakayofikisha ujumbe.
 
Yeye mwenyewe kwenye mkutano wa hadhara mjini Iringa anasema aliambiwa asifanye mkutano Iringa mpaka uchaguzi wa chama utakapomalizika.
(Hakumtaja aliyemzuia)

Lakini Je unadhani mwanachama wa kawaida anaweza kumzuia Makamu Mwenyekiti wa chama kufanya mkutano mahali popote ndani ya Tanzania?

Uzi uko humu umetokana na habari iliyoambatana na video iliyonakiliwa toka mtandao wa X.
Na mimi niliuona na kusikia alichosema Lissu. Unasema kweli.

Inafahamika vizuri sana, kwamba ndani ya CHADEMA kuna watu wanaomshabikia sana Samia, kwa sababu zao wenyewe.
Mwenyekiti alipokengeuka watu hawa hawakujificha tena wanafahamika. Sasa kama Mwenyekiti kagundua kwamba aliuziwa mbuzi kwenye gunia, na kutaka kudai pesa yake, hawa wapambe waliokuwa nyuma yake katika mpango huo watakuwa njia panda. Maana ndani ya CHADEMA yenyewe wamekwisha jitambulisha waziwazi kuhusu kuwa karibu kwao na Samia.
Wengine wamo humu humu JF.
 
kuna watu wanajaribu kushupaza shingo na kujipiga kifua kwamba hali ni shwari chadema, but it's obvious kuna taharuki, kuna kuviziana kusiko na afya miongoni mwa waandamizi na mwisho wake ni aibu 🐒
 
Kama Mbowe anataka kuimaliza CHADEMA na kujimaliza mwenyewe kisiasa; hili la kuungana na Samia ndilo litakalowamaliza.
Mbowe kishadanganywa katika "Maridhiano"; hivi kweli atakuwa bado hajagundua ulaghai anaofanyiwa?
Sidhani kuwa ni pesa inayompofusha, kutakuwa na jambo jingine kabisa.
 
Ni vizuri mkafanya vikao vya ndani, kurekebisha na kusahihisha kasoro na dosari zinazoonekana mpaka nje ya chama, ambazo zinaweza kuathiri taswira, umoja na maelewano ya viongozi waandamizi wa chama kwenye jamii....

Sio kwa ubaya lakini, kukosoana hadharani hakutawaacha salama, vinginevyo, aina hii ya kukosoana ni njia ya kusambaratisha chama kwa makusidi, huku tayari kila moja ameshajiandalia na kujihakikishia destination nyingine mpya ya kisiasa humu nchini, kuelekea uchaguzi mkuu ujao....

time will tell....

ama kweli,
fahali wawili hawakai zizi moja :DisGonBGud:
Wakati jiwe maghu anadukua mazungumzo ya kina ngereja, makamba, kinana,wakimponda ulikuwa wapi? Jela?
 
Na mimi niliuona na kusikia alichosema Lissu. Unasema kweli.

Inafahamika vizuri sana, kwamba ndani ya CHADEMA kuna watu wanaomshabikia sana Samia, kwa sababu zao wenyewe.
Mwenyekiti alipokengeuka watu hawa hawakujificha tena wanafahamika. Sasa kama Mwenyekiti kagundua kwamba aliuziwa mbuzi kwenye gunia, na kutaka kudai pesa yake, hawa wapambe waliokuwa nyuma yake katika mpango huo watakuwa njia panda. Maana ndani ya CHADEMA yenyewe wamekwisha jitambulisha waziwazi kuhusu kuwa karibu kwao na Samia.
Wengine wamo humu humu JF.
kwahiyo unataka kusema chadema kuna ambae hakunufaika na utashi na ukomavu wa Dr.Samia Suluhu Hassan ?

kwamba Lisu na Mbowe sio wanufaika?

na kwamba leo hii wangekua wanafanya siasa kama wanavofanya leo isingalikua utashi wa huyu Dr Samia Suluhu Hassan ...🐒

hakuna alieuziwa mbuzi kwenye gunia kwasabb hapakua na biashara yoyote miongoni mwao katika siasa..
 
Kama Mbowe anataka kuimaliza CHADEMA na kujimaliza mwenyewe kisiasa; hili la kuungana na Samia ndilo litakalowamaliza.
Mbowe kishadanganywa katika "Maridhiano"; hivi kweli atakuwa bado hajagundua ulaghai anaofanyiwa?
Sidhani kuwa ni pesa inayompofusha, kutakuwa na jambo jingine kabisa.
si ni maridiano yalimtoa Mbowe jela na yaliwarejesha lema na Lisu nchini ama 🐒
 
Ccm kunawaka moto, karibia watagawana mbao. Sukuma gang wanahoji kwann itolewe fomu moja tu ya kugombea urais kupitia ccm??

View attachment 2980833
bado ni kile kile tu kwenye hoja yangu ya msingi kama ambavyo nimewasihi waandamizi wa Chadema kufanya vikao vya ndani na kuresolve difference zao, kulaumiana kwenye media au majukwaa ya kisiasa hakuna tija 🐒

huyu kijana nae ndio wale wale kama baadhi ya waandamizi wenye agenda zao za siri japo zinafahamika......

kwamba wameshajiandaa mpaka na vyama wanavyokwenda kujiunga navyo, ila sasa eti mpaka wavuruge vyama walivyopo sasa 🐒

hiyo ni siasa duni kabisa 🐒
 
Ni vizuri mkafanya vikao vya ndani, kurekebisha na kusahihisha kasoro na dosari zinazoonekana mpaka nje ya chama, ambazo zinaweza kuathiri taswira, umoja na maelewano ya viongozi waandamizi wa chama kwenye jamii....

Sio kwa ubaya lakini, kukosoana hadharani hakutawaacha salama, vinginevyo, aina hii ya kukosoana ni njia ya kusambaratisha chama kwa makusidi, huku tayari kila moja ameshajiandalia na kujihakikishia destination nyingine mpya ya kisiasa humu nchini, kuelekea uchaguzi mkuu ujao....

time will tell....

ama kweli,
fahali wawili hawakai zizi moja :DisGonBGud:
Makamu Mwenyekiti anakimbelembele sana, hamekosa nidhamu, hajui protocols za chama, hajui mkubwa wala mdogo, akishakunywa konyagi ni shida kweli kweli, wapigane tu, hakuna namna nyingine, lissu aanze kumrukia mbowe vichwa, sugu amkate Msigwa mtama bali alimradi undava undava tu, dadek, 😁😁😁
 
Alitumwa akamkashifu Mwenyekiti na Katibu Mkuu wake?
Umkisikiliza kwa makini kwenye ile video Lissu ameukashifu uongozi wa chama.
Kwamba yeye hapewi pesa za mikutano kwakuwa chama hakina pesa, lakini kuna pesa za kuhonga kwenye chaguzi za ndani za chama.

Na chama kimemuonya asifanye mkutano Iringa mpaka baada ya uchaguzi, lakini amepuuza.

Kwa kifupi hakuna aliyemtuma.
Kwanza Chama ni nani?? Tuanzie hapo...Yaani Makamo Mkiti anaweza kuonywa na Boni Yai?? Hivi Sugu yule mkimpa Umakamo mkiti anaweza kuita kikao / Lindi Mkutano akapata hata watu 6?? Chadema hamtoshi wala hamtakaa mchukue nchi hii nyie.
Mbowe tukubaliane hutaki wanasiasa wengine wajitokeze na wewe ni mzee unasema ooh umewasaidia kwani wewe ulipokua jela wengine si walikua huko nje wanakusaidia?? Mbowe utaua hicho chama kwa tamaa zako unataka hela huku unataka uonekane ni mpinzani wa kweli lazima kimoja uharibu
 
Ni vizuri mkafanya vikao vya ndani, kurekebisha na kusahihisha kasoro na dosari zinazoonekana mpaka nje ya chama, ambazo zinaweza kuathiri taswira, umoja na maelewano ya viongozi waandamizi wa chama kwenye jamii....

Sio kwa ubaya lakini, kukosoana hadharani hakutawaacha salama, vinginevyo, aina hii ya kukosoana ni njia ya kusambaratisha chama kwa makusidi, huku tayari kila moja ameshajiandalia na kujihakikishia destination nyingine mpya ya kisiasa humu nchini, kuelekea uchaguzi mkuu ujao....

time will tell....

ama kweli,
fahali wawili hawakai zizi moja :DisGonBGud:
Hiyo kukosoana huko ndani ndio kumeifanya ccm kimekuwa chama Cha kupuuzi mno, ni bahati tu Bado katiba hii inaipa nafasi ccm kuchezea chaguzi za nchi hii.

Hata wanaotaka kwenda kwenye destinations nyingine wanaruhusiwa kuondoka muda wowote Ili wakawahi nafasi huko waendako. Na kuhusu uchaguzi, hakuna uchaguzi wowote credible hapa nchini wa kufanya mtu aliye serious eti awe anajiandaa. Kinachoendela kwenye chaguzi zetu ni maonyesho ya upuuzi wa mtu mweusi linapokuja suala la uchaguzi. Ingekuwa kura ndio zinatoa mshindi ungekuwa na hoja, lakini sio ule upuuzi unaofanyika kwenye chaguzi zetu.
 
Huenda kweli usemacho, lakini usisahau wao ni binadamu, na kama walivyo binadamu wote hutokea wakati kuna kuhitilafiana.
Hivyo zikitokea hitilafu za namna hiyo wamalize kwenye vikao vya ndani.
Kauli za Tundu Lissu mjini Iringa zimeacha doa kwenye ulingo wa siasa.
Kwa level yake haikupendeza kuwatuhumu viongozi wenzake mbele ya halaiki.
Alichofanya Tundu Lisu ni approach sahihi kabisa. Unapoona upuuzi popote unaukemea hadharani ama ndani. Haya mambo ya kupotezeana muda kwenye vikao vya ndani ndio kulea wapuuzi wanaopewa pesa chafu na ccm.
 
Ni vizuri mkafanya vikao vya ndani, kurekebisha na kusahihisha kasoro na dosari zinazoonekana mpaka nje ya chama, ambazo zinaweza kuathiri taswira, umoja na maelewano ya viongozi waandamizi wa chama kwenye jamii....

Sio kwa ubaya lakini, kukosoana hadharani hakutawaacha salama, vinginevyo, aina hii ya kukosoana ni njia ya kusambaratisha chama kwa makusidi, huku tayari kila moja ameshajiandalia na kujihakikishia destination nyingine mpya ya kisiasa humu nchini, kuelekea uchaguzi mkuu ujao....

time will tell....

ama kweli,
fahali wawili hawakai zizi moja :DisGonBGud:
Naunga mkono hoja, na katika vikao hivyo, wasisitize heshima kwa viongozi, mtu akiishakuwa kiongozi, lazima aheshimiwe. Mfano Mwenyekiti Mbowe, amefanya vikao vya maridhiano na CCM na vikaleta manufaa makubwa Chadema, ikiwemo kupata ruzuku na kukubaliana kitu kinachoitwa kugawana nusu mkate.

Wakati wote wa vikao hivyo Makamo Mwenyekiti yeye alikuwa zake Ubelgiji kwa wazungu wake.

Chadema ilisaidiwa fedha za vikao vya Baraza Kuu, kufanya ziara nje ya nchi, na fedha za nauli kuwarejesha wakimbizi waliokimbilia nje ya nchi akiwemo yeye.

Aliporudi, badala ya kuwa ni mtu wa shukrani, akaanza kubeza maridhiano na kuwatukana viongozi wenzake hadharani kuwa hawana akili!. Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability? hebu msikilize mwenyewe hapa
View: https://youtu.be/Qa59DIQs2yI?si=9oIbwnDXvO-cDzed

Wakati Lissu anaponda maridhiano, angalia JJ Mnyika anasema nini kuhusu maridhiano,
View: https://youtu.be/x5yFws4dc1U

Hivyo naunga mkono hoja, Chadema lazima waitane, wakalishane chini, wasemezane, na kurekebishana.

P.
 
Alichofanya Tundu Lisu ni approach sahihi kabisa. Unapoona upuuzi popote unaukemea hadharani ama ndani. Haya mambo ya kupotezeana muda kwenye vikao vya ndani ndio kulea wapuuzi wanaopewa pesa chafu na ccm.
Mkuu Tindo , hebu msikilize hapa
View: https://youtu.be/Qa59DIQs2yI
Hizi ni lugha za kistaarabu?. Unawajua ni kina nani anaowananga hapo kwa kuuliza kama wanaakili?.
P
 
Mkuu Tindo , hebu msikilize hapa
View: https://youtu.be/Qa59DIQs2yI
Hizi ni lugha za kistaarabu?. Unawajua ni kina nani anaowananga hapo kwa kuuliza kama wanaakili?.
P

Zile chaguzi zetu huwa ni za kistaarabu? Au kwenye kauli tu ndio unataka ustaarabu, lakini kwenye chaguzi sio lazima kuwe na ustaarabu? Honestly Kuna unafiki mkubwa kwenye hii nchi, kama umeamua kusimamia ustaarabu simamia ustaarabu, sio huo ustaarabu wa kuogopa kusema ukweli kwa kufumbia macho uhuni wa chama chako. Inshort kwenye mambo ya ustaarabu ww ni Bora ukae kimya maana huna uthubutu wa kukemea wakosa ustaarabu.
 
Mkuu Tindo , hebu msikilize hapa
View: https://youtu.be/Qa59DIQs2yI
Hizi ni lugha za kistaarabu?. Unawajua ni kina nani anaowananga hapo kwa kuuliza kama wanaakili?.
P

huwa najiuliza kama kuna mtu mzima msomi, mwenye familia, hekima na busara zake anaweza kuvumilia kuishi chini ya huyu muungwana kwa kugha hizo. na kama yupo basi atakua anaona aibu sana, na kabisa hawezi kuona future njema kuongozwa na bwana huyu :whatBlink:
 
Back
Top Bottom