Cement ya Dangote kabla ya Uchaguzi 8,000; baada ya Uchaguzi 13,000

mshumbusi

JF-Expert Member
Oct 24, 2011
457
232
Wakati wa kampeni jamaa alikuwa anasema "simenti ya DANGOTE itauzwa kwa tsh 8000".

Lakini baada ya uchaguzi simenti imeanza kuzalishwa na kuuzwa kwa Tsh 13000 kwa watu wa mtwara.

Ilhali dangote anatumia malighafi,nguvu ya umeme wa gesi kutoka hapahapa mtwara lakini wanamtwara wananunua siment kwa bei ya 13000.

Na washikaj wamekaa kimya wanatazama kama hawaoni,utadhani hawakuahidi wakobize na series ya majipu na ziara za kukurupuka zisizo na mafanikio.

We need #DOERS_NOT_TALKATIVES.
Hamkutuahd kufanya ziara za kukurupuka bali kuna vitu mlituahid,hivyo ndo 2nataka vitimizwe na si manenomaneno tu.

 
Hapa Kazi tu! Simenti zina umuhimu au ulazima gani kujengea? Kuna nyumba zimejengwa kwa kutumia udongo na bado zipo zimesimama imara wakati majengo ya madarasa yaliyojengwa kwa matofali ya simenti yana nyufa kibao. Boresheni ujenzi wa kutumia udongo na kuezekea nyasi!! Habari ya mjini ni kutumbua na kutumbua majipu na kawaachia harufu ya usaha!!
 
Waliwahadaa watz nao watz wakakubali kudanganyika, kazi wanayo mwaka huu wakati huo resource nyingi zinapatikana hapa hapa misumenti yao bado bei kubwa hii si hatari
 
Kweli akuna ukombozi mgumu kama wa kifikla!!!

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Lakini Dangote bado hajaanza kuzalisha cement. anasubilia mpaka vinu vyote viwe tayari ndio azalishe. hiyo cement wanaitoa nje ya Tanzania.
 
Anataka arudishe kwanza gharama zake za uwekezaji ndipo ateremshe bei. Mambo ya jukwaani ni jukwaani, kwani mwenyewe Dangote alituahidi bei hiyo?
 
Ndugu unaonekana unaishi kwenyenyumba ya kaka yako maisha no nyumba na kwa wanasiasa waambie izi ni ezi za kuwekana sawa na sio kudanganyana kama watoto
 

Sidhani kama hiyo ndio hoja. Kimsingi kuna viwanda vingine vya cement..kama kodi lazima ziwe sawa kwa wote. What was their base to come up with the price 8,000 tsh per base?
 
Lakini Dangote bado hajaanza kuzalisha cement. anasubilia mpaka vinu vyote viwe tayari ndio azalishe. hiyo cement wanaitoa nje ya Tanzania.
Hapo pia kuna cha kujadili. Mkataba wa serikali na Dangote katika kuingiza hizo simenti kabla ya kiwanda chake kuanza kuzalisha ukoje. Anaingiza simenti hiyo na kulipa kodi ile inayotakiwa au simenti inaingizwa kama moja ya mikakati ya kukuza soko la simenti yake kabla ya kuanza kuzalishwa hapa nchini hivyo halipi kodi?
 
Sidhani kama hiyo ndio hoja. Kimsingi kuna viwanda vingine vya cement..kama kodi lazima ziwe sawa kwa wote. What was their base to come up with the price 8,000 tsh per base?
Kwaiyo kipindi cha uchaguzi iyo kodi haikuwepo be serious
 
Pole sana Watanzania wenzangu...

Wamezoea kutudanganya, Nasi Tumezoea kudanganywa.


Hapa Kazi Tu, Siisomi Namba.
 
Kuna mdau alifafanua kuwa kiwanda kinauza Tsh elfu nane. Ukiweka na VAT inakuwa Tsh 9440. Hiyo ndiyo bei ya kiwandani. Lakini ukiinunua kwa distributa ina maana naye ataongeza faida yake, na huenda akakulipisha na VAT. So in the end bei ndio inakuwa hiyo hapo...
 
Ah hahahahaaaaaaaaaaa kweli hapa kazi tu
 
Hiyo 8000 ilitajwa kuwa ndiyo itakuwa bei ya mnunuzi wa mwisho. Maana yake hayo madudu yote ya kodi yatakuwa yemewekwa humo!!
 
Kwaiyo kipindi cha uchaguzi iyo kodi haikuwepo be serious

Walikupa mchanganuo wa bei zao? Tatizo tunaongea na emotions na sio facts. Mfano bei za mafuta zimeshuka sana Dunia nzima ila sio bongo. Kwanini?
 
Hoja ni kwamba kipindi cha uchaguzi hayo yote yalikuwa hakuna hadi tukapata cement kwa elfu 8
 
Walikupa mchanganuo wa bei zao? Tatizo tunaongea na emotions na sio facts. Mfano bei za mafuta zimeshuka sana Dunia nzima ila sio bongo. Kwanini?
Kodi si ziko "Fixed" kwa kigezo cha asilimia? Kwa hiyo kama mafuta yanashuka kwenye soko la dunia na hapa nchini ni lazima pia yashuke, kwa kuwa asilimia kumi ya Milioni moja ni Laki moja, lakini asilimia kumi ya laki tisa ni elfu tisini. Kwa ivo bei ya mafuta kutokushuka nchini mwetu hakuhusiani hata kidogo na kodi ya ndani bali mauza uza ya watawala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…