CCM imeharibu Elimu yetu. Utumiaje kiingereza miaka 10 kujifunzia halafu usijue kiingereza?

Hadi hapa Umeshakiri kuwa kingereza siyo muhimu
Hoja sio kingereza ni mhimu au sio mhimu... Mleta mada anauliza inakuwaje miaka kumi ya kusoma kwa kutumia kingereza na bado mtu hawezi kuongea lugha aliyotumia kusoma... Inaacha maswali juu ya ubora wa elimu yetu... That's the point.
 
Prof. Manji kapata tuzo ya kimataifa katika utabibu; uzi umo humu. Sorry, ninekumbuka Prof. Manji alisoma Harvard, miongoni mwa vyuo bora kabisa duniani.
 
Zamani shule za serikali zilikuwa vizuri sana kwenye kiingereza na masomo mengine yote. Na wengi tuliosoma shule za serikali Kiingereza hakikuwa tatizo kubwa kwetu kama leo (ambapo limekuwa janga kabisa). Tulikuwa tunaongea na wageni tangu sekondari bila tatizo. Hakukuwa na hizi English medium schools ambazo nyingi zinakazania lugha tu kuliko masomo mengine.

Swali la msingi: serikali imekwama wapi? Kuna mahali imelegeza kwenye matumizi (bajeti) na juhudi za kuimarisha elimu na kuacha watu wa chini wajipambanie wenyewe katika umasikini wao. Na sio kiingereza tu. Hata Kiswahili kinakuwa janga taratibu. Wafanya maamuzi hata hawana muda na hizo shule za serikali. Watoto na vijana wao wanasoma kwingine.

Hizi bla bla za kusema kiingereza ni lugha tu haina umuhimu ni kujidanganya kwa Mtanzania. Huwezi kujiendeleza katika fursa na maarifa yanayopatikana dunia nzima kama huna hata lugha moja kubwa ya kimataifa. Hata kupitia internet. Huu uongo wa kudai, Wachina, Wajapani, Warusi, n.k. wanaendelea kwa lugha zao pekee ni porojo za kisiasa. Sio katika dunia ya leo. Ndio maana watu toka Kenya, DR Congo, Burundi wanaongoza kufundisha Kiswahili Duniani wakati Watanzania ni tabu.
 
Halafu nadhani mleta mada hajakutana na watoto wa 2000 waliosoma English medium schools (maana zilichelewa kuanza hapa bongo).

Watoto wanamwaga ngeli hakuna mfano. Hao kina Jenista Mhagama na Ndungulile ngoja waondoke maofisini, watoto wa 2000 wahike dola, ndiyo mtajua hamjui.
 
Zamani zipi hizo? Hao wa zamani si ndiyo hawa akina Jenista Mhagama, ndungulile na Ndalichako? Mbona wanaongea broken?

Wale wanasheria waliokuwa wanaitetea serikali kule nje kwenye zile kesi za uvunjwaji holela wa mikataba, si wazamani wale?

Mfano prof. Mduma na prof. Osolo, si wa zamani wale? Mbona wanaongea kwa shida sana??

Hiyo zamani mlikuwa mnasifiana ujinga tu.
 
Ndugu Kuna vitu unachanganya,,,,,,ipo hivi kufanya mtihani kwa lugha ya kiiingereza haimaanishi kwamba hao watoto Wana umahiri wa kujibu maswali,,,kama mwanafunzi kilaza atabaki kuwa kilaza na kama mwanafunzi ana uwelewa atabaki na uelewa wake.

Wapo waliosoma vijijini shule za msingi, kwa matokeo yao mazuri ya la darasa la 7 Waka nunuliwa na hizo shule za private na Bado walipofika sekondar hawakupoa waliendelea kufanya vizuri,,
 
Kwani kujua kiiingereza ndo kuwa na maarifa,,ufahamu na uchambuzi wa mambo??
 
Kwani kujua kiiingereza ndo kuwa na maarifa,,ufahamu na uchambuzi wa mambo??
Hata uwe na maarifa kiasi gani failure to deliver that maarifa is as good as null and void. Mwalimu aliyejaa maarifa kichwani ila hawezi ku-deliver kwa wanafunzi wake ina faida gani?
 
Kwenye mfumo wa elimu yetu lazma kuna mnufaika ndio maana haibadilishwi.
Wenyewe wanufaika hawawezi kamwe kuwasomesha watoto wao kwenye shule hizi ambazo wao ndio wameiweka. Akili mtu wangu akili
 
Mi nawaza tofauti kidogo. Tunashindwa kujiamini kuongea Kiingereza kwasababu tunataka kumuigilizia Mwingereza anavyoongea bila kukumbuka Lahaja za kiawahili hazifiti kwenye kiingereza.

Watafute wabongo wanaokijua vizuri Kiingereza waambie wasutane. Au wapigane Biti..

Neno ninaloliwaza kiswahili haliyoki kinywani kwa sauti husika.

SULUHISHO.
Tujifunze Kiingereza kwa Lahaja ya Kiswahili hapo tutatusua kama Wahaya maana wanatumia Lahaja yao ya Kihaya kuongelea Kiingereza.

Kwa usienielewa, ni hivi Neno "STREET" tujifunze kulitamka "SITIRITI".. Mwezi mmoja Tuu wabongo wengi Mamton...!

Wengi Tunaona Haya Kuongea Kiingereza Kwahofu ya Kukosea Kumuigiliza Muingereza Anavyoongea. Ila Wengi Lugha hiyo Tunaijua vizuri ndio maana kuiandika na kuisoma si changamoto kama kuisikia na kuiongea.
 
Magufuli alisoma na kufaulu kwa lugha ya Kiingereza kwa zaidi ya miaka 17 na alitoka kappa.
Ahahahahh 🀣 🀣 🀣 🀣
 
Kuongea kingereza siyo usomi china , Japan, Russia hawaongei kingereza ila wanamchango mkubwa kwenye Technology servicescape
Je, kuna Mchina amesoma na kufaulu kwa lugha ya Kiingereza kwa zaidi ya miaka 16 ?
Dr. Magufuli, Dk. Ndalichako wamesoma kwa Kiingereza kwa zaidi ya miaka 16 na wanetoka kappa.
Hao wachina wanasoma kwa lugha zao. Wewe tangu DARASA la 1 umesoma Kiingereza kama lugha mpaka la saba. Form 1 mpaka chuo kikuu unasoma kwa Kiingereza na hujui unakuja kuleta habari za Wajapan mara wachina
 
Vitabu vya kufundishia walimu vyote ni taabu tu.
Wengi walioko vyuo vya walimu ukiwaambia wakupe maudhui ya vitabu kama Things Fall Apart na Grain of Wheat au Mine Boy tuliosoma enzi hizo kidato cha kwanza na pili utadhani unawaambia wazungumze Kiyunani cha kale.
 
Ndo umeandika utumbo gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…