CCM imeharibu Elimu yetu. Utumiaje kiingereza miaka 10 kujifunzia halafu usijue kiingereza?

Kingereza ni lugha ya mawasiliano TU kama lugha nyingine TU kikubwa ni kupata maarifa kln pia watanzania walio wengi wanauwezo mkubwa wa kuandika kuliko kuzungumza lugha ya kingereza
hapo kwenye kupata maarifa kama taifa inabidi tuchague lugha rasmi ya kutoka nayo kindergarten mpaka chuo kikuu/vyuo vya kati. mambo ya kuchanganya lugha yanakwamisha vijana kujifunza maarifa kwa usahihi.
 
Ndio maana nasemaga ni upuuzi mtupu kujistress kulipia mamilioni shule ya English Medium ili mtoto akafundishwe kiingereza kwa kiswahili na walimu ambao lugha yao ya mawasiliano sio kiingereza halafu mtoto akirudi nyumbani anaongea na wazazi na marafiki kwa kiswahili
English medium unazijua huzijui ? Nenda kakutane na watoto wa msingi uone wanavyozunguza kingereza kilichonyooka

Kenya hapo lugha ya nyumbani kiswahili kama sisi lakini shule zao zote za Msingi ni English medium Kenya mbona kwao sio issue kingereza

Hata sisi lugha ya nyumbani kiswahili mtoto akitoka shule kama yule wa Kenya anakutana na kiswahili mbona wanamudu kingereza vizuri tu

Labda wewe hujafika Kenya lugha ya nyumbani kiswahili shule ndio kingereza na wako fit.Sababu muda mwingi wa siku watoto wanakuwa shule environment ya kingereza kitupu .Nyumbani wanakuwa na muda kidogo sana ndio maana wana master kingereza upesi

Tofauti na shule ya kayumba siku nzima shule ntoto anasoma kiswahili tu na nyumbani hapo unazalisha mtoto mswahili hasa kingereza kwake itakuwa mtihani mzito kukimudu.
 
Moderator hii ni hoja ya kisiasa msiigeuze ya lugha.

Suala la Elimu ya nchi hii kuwa ya kiwango cha juu ama cha chini ni la mjadala.

Lakini kiwango cha usomi wa wasomi wetu si mjadala unaotakiwa kuahirishwa.

Hivi wasomi wetu tunawapimaje, kwa nini wasomi wetu linapokuja suala la ushindani na wasomi wa nchi nyingine linakuja suala la udhaifu wa wasomi wetu kutokuwa na weledi wa matumizi ya lugha ya kiingereza?

Hivi Elimu yetu ni duni ama wasomi wetu ni weledi ila hawajui lugha ya kiingereza kwa ufasaha?

Kama hawajui kiingereza kwa ufasaha imekuwaje walifaulu mitihani yao kwa kiwango cha juu?

Yaani lugha inayotumiwa kujifunzia kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita (miaka 6) na vyuoni (miaka 3 - 4 au miaka 7) wasomi wetu inakuwaje hawana weledi nayo?

Kuna sehemu CCM wameharibu Elimu yetu ila wanasingizia kiingereza.
Ndiyo maana majangili ya CCM yanasomesha nje
 
Pelekeni watoto English Medium kumaliza hizo kelele za ooh anasoma miaka 10 hajui kingereza

Hilo tatizo kwa watoto waliosoma English medium Primary halipo

Wazazi jiongezeni .Waliosoma English medium mbona wako vizuri mno kwenye kingereza

CCM wameruhusu English Medium ili wazazi wenyewe waakue wanataka watoto wao wasome swahili medium au English Medium huo ni uamuzi wa mzazi sio CCM
Umetisha
 
100% Fact
Kuna mahali elimu yetu haina lengo tunataka mhitimu awe knowledge Gani,.mf nilikuwa na dogo mmoja wiki end hii,ni form v na anachukua combination ya "HKL"nikataka kujua list ya vitabu vyaa kiswahili au kingereza anavyotarajia kuvisoma hakuwa nayo na Wala hajasoma hata kimoja,nikakumbuka miaka yetu enzi za Nyerere historia form III tulisoma mambo ya Warsaw Pact,NATO, Non- alignment,OAU,Vita baridi,Vita ya I ya Dunia na ya Ii,Mambo ya Nyerere,Nkurumah,Nasar,colonialism,wizi na jinzi Africa ilivonyimwa maendeleo nikashangaa dogo huyo alikuwa "totally flabagasted",masikini hajawahi kukutana na hayo,Sasa nafikiria dogo ni kilaza?au wanajifunza nini enzi hizi!
 
English medium unazijua huzijui ? Nenda kakutane na watoto wa msingi uone wanavyozunguza kingereza kilichonyooka

Kenya hapo lugha ya nyumbani kiswahili kama sisi lakini shule zao zote za Msingi ni English medium Kenya mbona kwao sio issue kingereza

Hata sisi lugha ya nyumbani kiswahili mtoto akitoka shule kama yule wa Kenya anakutana na kiswahili mbona wanamudu kingereza vizuri tu

Labda wewe hujafika Kenya lugha ya nyumbani kiswahili shule ndio kingereza na wako fit.Sababu muda mwingi wa siku watoto wanakuwa shule environment ya kingereza kitupu .Nyumbani wanakuwa na muda kidogo sana ndio maana wana master kingereza upesi

Tofauti na shule ya kayumba siku nzima shule ntoto anasoma kiswahili tu na nyumbani hapo unazalisha mtoto mswahili hasa kingereza kwake itakuwa mtihani mzito kukimudu.
wewe ni kichaa kabisa period.
 
Matokeo ya kitu inatokana na source yake, kama walimu wana code mixing na code switching kwenye kingereza je mwanafunzi ataweza kuwa competent kwenye hiyo lugha?
 
Tunamiss critical time ya language learning, science na psychology Inaeleza kwamba binadamu anajifunza lugha naturally anapokuwa kati ya miaka 2-10! Umri huu anaweza kujifunza lugha hata 5 na hutasikia maishani kwake anachanganya hata neno moja kwenye lugha ingine! Sielewi ni mwanaccm gani aliimbia serikali yetu kwamba lugha ya pili inafundishika vizuri kwenye ngazi ya sekondari, na wakabeba Kama kasuku na kubaki nayo. Nchi zote zilizoendelea lugha zinaanza kufundishwa elementary schools na utakuta vijana wanapokua wanaongea vizuri multiple languages. Ukitazama wachina wanaongea kichina vizuri na lugha ingine ya ziada sahihi kbs, warusi. Wajapan, wakenya etc. Sisi kila kitu tunafanya kinyume tukitazamia matokeo yaleyale tunasubiri research za mkumbo za kukariri pia. Mtu mzima hata ajifunze namna gani hawezi kuwa fluent Tazama watu waliohamia Ulaya na Marekani etc miaka hata wakirudi wamestaafu baada ya kuishi maisha yao yote ya utu uzima bado wanaongea na accent zao za kichaga, kinyiramba, kipare, kimatumbi etc wanaongeza vocabulary tu na sio mastery ya language
 
wewe ni kichaa kabisa period.
Jifariji tu

Siku ukienda msimbazi Centre Dar watoto wakifanya mitihani kujiunga form one na mwanao wa kayumba utashangaa

Shule za private sekondari nyingi sasa hivi hutaka mtoto kujiunga form one achague atafanya mtihani wa kujiunga kwa lugha ipi?
Utashangaa ma halll manne yenye watoto hamsini kila Hall yote yamejaa watoto waliochagua kufanya mtihani kwa kingereza .Ila Hall moja halifiki hata watoto 10 ndio pekee wanataka kufanya mtihani kiswahili

Ndipo utajua hujui kuwa wazazi wengi wamehamia English medium utabaki wewe na ujinga wako na kuzalisha mtoto mpumbavu
 
Moderator hii ni hoja ya kisiasa msiigeuze ya lugha.

Suala la Elimu ya nchi hii kuwa ya kiwango cha juu ama cha chini ni la mjadala.

Lakini kiwango cha usomi wa wasomi wetu si mjadala unaotakiwa kuahirishwa.

Hivi wasomi wetu tunawapimaje, kwa nini wasomi wetu linapokuja suala la ushindani na wasomi wa nchi nyingine linakuja suala la udhaifu wa wasomi wetu kutokuwa na weledi wa matumizi ya lugha ya kiingereza?

Hivi Elimu yetu ni duni ama wasomi wetu ni weledi ila hawajui lugha ya kiingereza kwa ufasaha?

Kama hawajui kiingereza kwa ufasaha imekuwaje walifaulu mitihani yao kwa kiwango cha juu?

Yaani lugha inayotumiwa kujifunzia kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita (miaka 6) na vyuoni (miaka 3 - 4 au miaka 7) wasomi wetu inakuwaje hawana weledi nayo?

Kuna sehemu CCM wameharibu Elimu yetu ila wanasingizia kiingereza.
Watakwambia elimu haipmwa kwa lugha huku watoto wao wanawapeleka nje kusoma
 
Back
Top Bottom