Caught on Tape: Mkakati wa Mamluki wafichuliwa!

Status
Not open for further replies.
Kuna ubaya gani kwa Tanzania kuwa na uhusiano wa Kibalozi na OIC (kwa mujibu wa Katiba yao) kama vile Tanzania ilivyo na uhusiano na Vatican ambapo hatujalazimishwa kujiunga na Vatikani?

Kwanini kwenye OIC ni LAZIMA tuwe wanachama kwanza?

MKJJ inawezekana JK amegundua kuwa hatadeka tena marekani, jirani kaingia kuonoza nchi hivyo noma kwenda kuomba kwa mweusi mwenzako! hata kama tajiri. (jokes ??)

Kwa kuona hivyo kaona sehemu yakuponea si sisi kubuni mbizu za kutukwamua, bali ni kujiunga OIC, akaona kundi pekee la kutusaidia tupate hela ni Uislamu!, na akajua watang'an'gania sana tuingie, na tukisha ingia, hakuna muislamu atakayequestion fedha za OIC ziko wapi wala hakuna atakayeuliza faida iko wapi, kujiunga tu kwao ni kuridhika asilimia 100!

Maanza TZ inaongoza kupewa misaada , ilibidi tuulizane imeenda wapi, imefanya nini kabla ya kusubiri wazitumbue hizi za OIC

waberoya
 
Kupata msaada ni jambo moja, na jinsi ya kuutumia huo msaada ni jambo jingine. Kuuliza nchi zilizo wanachama wa OIC zimefaidika nini?, ni kama kuuliza kidole kimoja cha mkono kilichukua punje gani ya wali, hizi nchi haziko OIC tu, ziko na katika mashirika mengine. Pia zinakopa WB, IMF nk. Hivyo kupata mkopo na jinsi ya kuutumia ni vitu viwili tofauti. Kutumia vibaya haisababishi wengine wasiende kukopa.

Vile vile kuna tofauti kubwa ya mikopo. Ili kuendelea lazima nchi zitoe mikopo wa wananchi wake, na nchi zikope ili kujiinua kiuchumi, ndio maana mabenki hutoa mikopo. Japo mikopo peke yake sio msingi wa maeneleo. Hivyo mikopo inahitajika ili kuiwezesha nchi kufanya mambo fulani (kama kilimo, uvuvi, afya na elimu). Angalia suala la mikopo ya nyumba Marekani. Katika mfumo wa kimagharibi (western economy) mikopo ni lazima iwe na riba (interest), lakini mfumo wa kiislamu mkopo haurejeshwi kwa riba na ndio ilivyo OIC. OIC imeundwa kwa ajili ya kuzisaidia nchi masikini kuweza kupata mikopo kutoka nchi tajiri wanachama bila ya riba kama wanafanyavyo nchi nyingine tajiri, ama mikopo toka mashirika ya kimataifa kama IFM.

Unapokopa mkopo leo OIC wa dola bilioni 10, hata ukirudisha baada ya miaka 20, utalipa dola bilioni 10. Hakuna riba kabisa, huo ndio mfumo wa uislamu, manake riba hurudisha nyuma kuwakwamua wasio nacho, ili nao wawe nacho waweze kusaidia wasio nacho. Sasa ni kujiuliza wapi kuna faida, hapa ninapokopa bila riba, ama kule ambapo kuna riba inayozaa riba. Ni uoga tu, ama kuamua kujifanya kuna hatari kujiunga na OIC. Sasa badala ya kujadili mada muhimu za OIC, tunaanza kuulizana Uganda baada ya Mbale University ni kipi zaidi wanacho sisi hatuna, ukianza kujilinganisha na Uganda, Msumbiji nk, ili ndio ujione uko juu ama la huo sio mkakati wa kimaendeleo. Siku zote Taifa linatakiwa kuangalia kipi hakijafanyika chenye manufaa na si kipi walichotuzidi jirani zetu.
 
Somalia, Niger, Comoro, Mali n.k ni nchi wanachama wa OIC wamenufaika vipi na hiyo mikopo ili angalau tuwe na mifano hai.

Cha msing nikupata mikopo rahisi, kama Somalia, Comoro hawakuitumia mikopo vizuri haina maana sisi wa TZ tutashindwa kuitumia vizuri, kila nchi inamipango yake na management style yake

Nipe mfano wa nchi mwanacha ambayo imepata faida hiyo kulinganisha na misaada mingine kutoka taasisi au jumuiya nyingine.

Access na Alternative source of fund, badala ya kwenda WB, IMF kuomba mkopo wenye riba kubwa OIC tunaweza ku-save pesa nying zikasaidia miradi mingine

Serikali ya Tanzania iliweza kutoa majengo ya Chuo cha Tanesco pale Morogoro pamoja na kampusi ya wapigania uhuru (nadhani Mazimbu pale) kuwa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Tanzania. Tumefanya hivi bila kuwa wanachama wa OIC. Na kuna vyuo vikuu vingine viko njiani kuanzishwa na taasisi mbalimbali za Waislamu ambazo hazitulazimishi nchi iwe mwanachama kwanza ili zitusaidie. Nadhani ya kujitegemea sisi wenyewe ni bora zaidi.

Bado tunaitaji vyuo karibuni kila mkoa, hakuna ubaya akitokea mtu/chama kujenga vyuo kwa maslai ya wa-TZ wote, sirikali ita-DIVERT BUDGET ya ujenzi wa vyuo na kujenga Hospitali au vitu vingine muhimu pia

Hakuna faida aidha ya kuweza kufanya na sisi "mate yatutoke". Uganda ilijiunga mwaka 1974 imefaidika vipi (ukiondoa chuo cha Mbale)? Msumbiji nayo imejiunga lakini imepata manufaa yapi ambayo Tanzania haiwezi kuwa nayo bila OIC?

Uganda inafaidika na $10bilion(by2010) hizi ni kwa ajili ya nchi za afrika pekeyao, pia, Mbale University na ujenzi wa Masindi-Hoima road nk. OIC ni alternative source of fund na ni cheap
Click hapa uone baadhi ya mambo wenzetu wanafaidikaje

OIC & Islamic Development Bank Initiatives in Sierra Leone (Jul 2007)

AfricaNews - Over 1000 gather in Uganda for OIC Business Forum - Mugira

OIC finalizing action plan for women empowerment :: MENAFN - Middle East North Africa . Financial Network

Mifano yote hiyo inauliza swali; ni lazima tuwe wanachama ili tupate misaada hiyo? Mbona tayari tunapata misaada mingi tu kutoka nchi za Kiislamu (Irani ni mfano mmoja na Misri mwingine) kwa muda mrefu tu lakini hatujalazimika kuwa wanachama? Kwanini hii ya OIC lazima tuwe wanachama kwanza?

Tukiwa wanachama ndio tutaweza kupata access na hizo faida za OIC, we misri atakupa kiasi gani na wako reliable kiasi gani? wacha misri na iran, WM, IMF, OIC na dona countries wote watupoatie huwezi kuongoza nchi kutegemea watu wachache, lazima tuwe na options tutaweza kuwa dependent kiasi Fulani

Kuna ubaya gani kwa Tanzania kuwa na uhusiano wa Kibalozi na OIC (kwa mujibu wa Katiba yao) kama vile Tanzania ilivyo na uhusiano na Vatican ambapo hatujalazimishwa kujiunga na Vatikani?

Hatujaona madhara yoyote yaliyo tokea kwa wanachama/secular countries wa umoja huo zaid ya faida, kwa nini tusijiunge?

Kwanini kwenye OIC ni LAZIMA tuwe wanachama kwanza?[/QUOTE]

Faida nying zimeelezwa sasa eleza wasiwasi wako, thanks

Tembelea hii website itakusaidia:
Supporting Development & Poverty Alleviation in Africa (Mar 2007)
 
Somalia, Niger, Comoro, Mali n.k ni nchi wanachama wa OIC wamenufaika vipi na hiyo mikopo ili angalau tuwe na mifano hai.

Nipe mfano wa nchi mwanacha ambayo imepata faida hiyo kulinganisha na misaada mingine kutoka taasisi au jumuiya nyingine.

Serikali ya Tanzania iliweza kutoa majengo ya Chuo cha Tanesco pale Morogoro pamoja na kampusi ya wapigania uhuru (nadhani Mazimbu pale) kuwa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Tanzania. Tumefanya hivi bila kuwa wanachama wa OIC. Na kuna vyuo vikuu vingine viko njiani kuanzishwa na taasisi mbalimbali za Waislamu ambazo hazitulazimishi nchi iwe mwanachama kwanza ili zitusaidie. Nadhani ya kujitegemea sisi wenyewe ni bora zaidi.

Hakuna faida aidha ya kuweza kufanya na sisi "mate yatutoke". Uganda ilijiunga mwaka 1974 imefaidika vipi (ukiondoa chuo cha Mbale)? Msumbiji nayo imejiunga lakini imepata manufaa yapi ambayo Tanzania haiwezi kuwa nayo bila OIC?

Click hapa uone baadhi ya mambo wenzetu wanafaidikaje

OIC & Islamic Development Bank Initiatives in Sierra Leone (Jul 2007)

AfricaNews - Over 1000 gather in Uganda for OIC Business Forum - Mugira

OIC finalizing action plan for women empowerment :: MENAFN - Middle East North Africa . Financial Network

Mifano yote hiyo inauliza swali; ni lazima tuwe wanachama ili tupate misaada hiyo? Mbona tayari tunapata misaada mingi tu kutoka nchi za Kiislamu (Irani ni mfano mmoja na Misri mwingine) kwa muda mrefu tu lakini hatujalazimika kuwa wanachama? Kwanini hii ya OIC lazima tuwe wanachama kwanza?

Kuna ubaya gani kwa Tanzania kuwa na uhusiano wa Kibalozi na OIC (kwa mujibu wa Katiba yao) kama vile Tanzania ilivyo na uhusiano na Vatican ambapo hatujalazimishwa kujiunga na Vatikani?

Kwanini kwenye OIC ni LAZIMA tuwe wanachama kwanza?[/QUOTE]

Si kawaida yangu kulumbana ila hapa naona kuna kitu kimejificha, hivi ni lazma tuone mfano wa wenzetu ndio nasi tuige?. haiwezi kuwa wenzetu wanachezea manufaa ya OIC sisi tuingine na kuitumia effectively na kunufaika zaidi yao? mimi binafsi siamini sana mambo ya kuiga mwingine, ila kujifunza kutokana na makosa ya wengine. hivyo Muhimu ni kuangalia ni kipi kinachowafanya hao wanachama wengine wasinufaike na manufaa ya OIC kama yanavyotajwa. WaTanzania wenzangu tusiwe watu wa kuiga mambo kama yalivyo, tuige kwa kurekebisha makosa na kuboresha zaidi ili tunufaike zaidi.

Kwa ujumla hakuna hoja ya msingi ama hakuna hasara inayoelezwa itokanayo na kujiunga OIC zaidi watu wanapinga kunufaika, sasa kama ndivyo basi tutizame ni vipi tutaweza kujinufaisha nayo.
 
Kupata msaada ni jambo moja, na jinsi ya kuutumia huo msaada ni jambo jingine. Kuuliza nchi zilizo wanachama wa OIC zimefaidika nini?, ni kama kuuliza kidole kimoja cha mkono kilichukua punje gani ya wali, hizi nchi haziko OIC tu, ziko na katika mashirika mengine. .

Ndugu unapatikana wapi nikupe msaada? usijali sina masharti yoyote yale,

Unachotakiwa ni kunipa your full contacts , wewe na familia yako nitawapa msaada, eleza una watoto wangapi na wake wangapi,na wengine unaofikiri naweza kuwasaidia. Mimi nafanya kazi na nina hela nyingi kidogo, naona nikiwasaidia watu kama wewe nitakuwa nimetoa shukrani kwa Mungu maulana.

Are you ready?

usisite tuma PM na information zako zote, wala usione aibu kuniomba najua sisi sote ni wanaume, lakini tumezidiana uwezo wa kutafuta fedha.

Najua bada ya kukupa msaada wewe na famiia yako mtaishi vizuri, mnaweza kujianzishia biashara na nitakupa ushauri ufanyeje.

Natumaini utatumia vizuri, mikopo ipo pia ukitaka sitozi riba hata baada ya miaka 50 utalipa kiasi kilekile.

Najua una kazi na una kazi na maliasili nyingi, ila nimeona bado unataabika na kuhitaji msaada kama wangu, huu pekee utakuondoa kwenye matatizo yako.

Tangaza habari hizi njema kwa ndugu na majirani wengine.

Kumbuka hamna masharti yeyote yale, kwani nikiyaweka ni magumu inabidi pengine ubadili dini, na dini yangu mimi naabudu vitu usivyoweza kuvifikiria, mwenzangu mmoja yeye anaabudu jua na ana masharti kama hayo sijafurahia anavyofanya.

Najua pengine mtu akiwa na shida ni kumpa tu na siyo kumuwekea masharti , na ndio SADAKA NZURI KWA MIUNGU YAO!!

Nasubiri majibu yako, fedha za kwanza nitaingiza wiki moja baada ya kupata contacts zako, na awamu ya pili utapata baada ya miezi miwili baada ya kufikiria mtafanya biashara gani. Nadhani wewe na familia yako mtapendeza sana.

cheers

waberoya
 
Kupata msaada ni jambo moja, na jinsi ya kuutumia huo msaada ni jambo jingine.

Sasa tujiunge tu ili tupate misaada na tusijali jinsi gani tutaitumia?

Kuuliza nchi zilizo wanachama wa OIC zimefaidika nini?, ni kama kuuliza kidole kimoja cha mkono kilichukua punje gani ya wali, hizi nchi haziko OIC tu, ziko na katika mashirika mengine.

Sasa lazima tulinganishe maana inaonekana misaada ambayo hatuipati ni mingi na mikubwa mno kiasi kwamba hatuwezi kuipata hadi tujiunge nayo. Hivi ni misaada ya kiasi gani hiyo ambayo tunaweza kuipata kutoka OIC? Lakini zaidi ni wapi ambapo OIC inasema nchi ikijiunga ina haki ya kupata misaada x, y, na z?

Pia zinakopa WB, IMF nk. Hivyo kupata mkopo na jinsi ya kuutumia ni vitu viwili tofauti. Kutumia vibaya haisababishi wengine wasiende kukopa.

Kwanini unazungumzia "kutumia vibaya"? Unajuaje kuwa nchi hizo zimetumia misaada vibaya? Je Tanzania ina rekodi nzuri kiasi gani ya kutumia misaada ya kigeni?

OIC imeundwa kwa ajili ya kuzisaidia nchi masikini kuweza kupata mikopo kutoka nchi tajiri wanachama bila ya riba kama wanafanyavyo nchi nyingine tajiri, ama mikopo toka mashirika ya kimataifa kama IFM.

Si kweli, inabidi usome malengo ya kuundwa kwa OIC na misaada kwa nchi maskini si mojawapo?

Unapokopa mkopo leo OIC wa dola bilioni 10, hata ukirudisha baada ya miaka 20, utalipa dola bilioni 10. Hakuna riba kabisa, huo ndio mfumo wa uislamu, manake riba hurudisha nyuma kuwakwamua wasio nacho, ili nao wawe nacho waweze kusaidia wasio nacho. Sasa ni kujiuliza wapi kuna faida, hapa ninapokopa bila riba, ama kule ambapo kuna riba inayozaa riba. Ni uoga tu, ama kuamua kujifanya kuna hatari kujiunga na OIC.

Sasa inaonekana hufahamu biashara inafanywaje katika nchi za kiarabu vinginevyo kungekuwa hakuna faida. Yaani nikupe dola 10 halafu urudishe dola 10 tu wakati tunafanya biashara. Wanaposema kuwa hakuna "riba" haina maana hakuna ada na kodi mbalimbali ambazo mtu au taasisi inalipa. Hivyo kuna gharama nyingine unazolipa ingawa siyo riba ambacho ni kiasi kinachotozwa kwa asilimia fulani ya kiasi kinachotolewa kama adhabu ya kukopa huko.

Sasa badala ya kujadili mada muhimu za OIC, tunaanza kuulizana Uganda baada ya Mbale University ni kipi zaidi wanacho sisi hatuna, ukianza kujilinganisha na Uganda, Msumbiji nk, ili ndio ujione uko juu ama la huo sio mkakati wa kimaendeleo. Siku zote Taifa linatakiwa kuangalia kipi hakijafanyika chenye manufaa na si kipi walichotuzidi jirani zetu.

Ni lazima tulinganishe ili tuweze kuona kuwa kama ni kweli OIC ndiyo suluhisho la matatizo yetu au matatizo ya Waislamu. Wakati watu wengine wanatuambia "mbona Uganda na Msumbiji ni wanachama" tukiamua kuwauliza hebu tuonesheni wamefaidika vipi tunaambiwa tunalinganisha. Sasa tusilipolinganisha na majirani zetu tulinganishe na nani?

Kama OIC in clout hiyo ya kusaidia nchi maskini imesaidia vipi Comoro wakati wa Mohammed Bakari kujitenga? Imesaidia vipi Somalia leo hii miaka zaidi ya kumi haina serikali na Somalia ina Waislamu wengi? Imesaidia vipi kukomesha vita Sudan kule Darfur? Yawezekana OIC haina huo ujiko ambao watu wanafikiria inayo.
 
Tukiwa wanachama ndio tutaweza kupata access na hizo faida za OIC, we misri atakupa kiasi gani na wako reliable kiasi gani? wacha misri na iran, WM, IMF, OIC na dona countries wote watupoatie huwezi kuongoza nchi kutegemea watu wachache, lazima tuwe na options tutaweza kuwa dependent kiasi Fulani[/COLOR]

Hivi huo mfuko unaotakiwa kutoa hiyo misaaada kwa nchi 57 una uwezo gani wa kufanya hivyo?

Hatujaona madhara yoyote yaliyo tokea kwa wanachama/secular countries wa umoja huo zaid ya faida, kwa nini tusijiunge?

HIzo faida ni zipi ukitoa mifano halisi kwa nchi wanachama kama OIC, Niger, Nigeria, Comoro, Msumbiji, Uganda, Mali, New Guinea n.k

Faida nying zimeelezwa sasa eleza wasiwasi wako, thanks

Tembelea hii website itakusaidia:
Supporting Development & Poverty Alleviation in Africa (Mar 2007)

Hizo faida kulinganisha na kitu gani kingine?
 
Kwa ujumla hakuna hoja ya msingi ama hakuna hasara inayoelezwa itokanayo na kujiunga OIC zaidi watu wanapinga kunufaika, sasa kama ndivyo basi tutizame ni vipi tutaweza kujinufaisha nayo.

Hasara kubwa ni kulifanya Taifa zima likubaliane na malengo yote ya OIC ambayo msingi wake ni dini na siyo tu kukubali bali ni kwa nchi kujiunga na taasisi ya kidini kitu ambacho kwa karibu miaka hamsini sasa Tanzania haijawahi kufanya.

Sielewi ni kwanini watu hawataki tuwe na uhusiano rasmi na OIC tena wenye level ya kibalozi kama ilivyo kwa Vatikani lakini wanataka tujiunge na kukubali Katiba ya OIC ili tupate misaada tu. Yaani tuuze haki yetu ya kuwa taifa huru ili tuweze kupokea misaada. Misaada gani hii ambayo lazima tujiunge kwanza ili tuipate?
 
MKJJ inawezekana JK amegundua kuwa hatadeka tena marekani, jirani kaingia kuonoza nchi hivyo noma kwenda kuomba kwa mweusi mwenzako! hata kama tajiri. (jokes ??)

Kwa kuona hivyo kaona sehemu yakuponea si sisi kubuni mbizu za kutukwamua, bali ni kujiunga OIC, akaona kundi pekee la kutusaidia tupate hela ni Uislamu!, na akajua watang'an'gania sana tuingie, na tukisha ingia, hakuna muislamu atakayequestion fedha za OIC ziko wapi wala hakuna atakayeuliza faida iko wapi, kujiunga tu kwao ni kuridhika asilimia 100!

Maanza TZ inaongoza kupewa misaada , ilibidi tuulizane imeenda wapi, imefanya nini kabla ya kusubiri wazitumbue hizi za OIC

waberoya

...unafanya kosa lile lile over and again!!! badilika au bila wewe kujijua una sabotage huu mjadala.

asante.
 
Surely nitabadilika, naomba unipe neno la kusubstitute! nikisema baadhi ya waislamu itakuwa sahihi? au nipe neno unalofikiri linafaa.

Sorry for that.

waberoya
 
naona tumeingia huku OIC kwa hiyo nimeona si vibaya tukakumbushana jamani CHARTER ya oic ni hii.
hebu tusome tuone kama inasisitiza lengo leo KUTOA MIKOPO/MISAADA kwa nchi mwanachama au lengo niKUENEZA UISLAM katika nchi mwanacahama
 
Surely nitabadilika, naomba unipe neno la kusubstitute! nikisema baadhi ya waislamu itakuwa sahihi? au nipe neno unalofikiri linafaa.

Sorry for that.

waberoya

kuwa mbunifu...........kazi kwako!!:(
 
Ndugu unapatikana wapi nikupe msaada? usijali sina masharti yoyote yale,

Unachotakiwa ni kunipa your full contacts , wewe na familia yako nitawapa msaada, eleza una watoto wangapi na wake wangapi,na wengine unaofikiri naweza kuwasaidia. Mimi nafanya kazi na nina hela nyingi kidogo, naona nikiwasaidia watu kama wewe nitakuwa nimetoa shukrani kwa Mungu maulana.

Are you ready?

usisite tuma PM na information zako zote, wala usione aibu kuniomba najua sisi sote ni wanaume, lakini tumezidiana uwezo wa kutafuta fedha.

Najua bada ya kukupa msaada wewe na famiia yako mtaishi vizuri, mnaweza kujianzishia biashara na nitakupa ushauri ufanyeje.

Natumaini utatumia vizuri, mikopo ipo pia ukitaka sitozi riba hata baada ya miaka 50 utalipa kiasi kilekile.

Najua una kazi na una kazi na maliasili nyingi, ila nimeona bado unataabika na kuhitaji msaada kama wangu, huu pekee utakuondoa kwenye matatizo yako.

Tangaza habari hizi njema kwa ndugu na majirani wengine.

Kumbuka hamna masharti yeyote yale, kwani nikiyaweka ni magumu inabidi pengine ubadili dini, na dini yangu mimi naabudu vitu usivyoweza kuvifikiria, mwenzangu mmoja yeye anaabudu jua na ana masharti kama hayo sijafurahia anavyofanya.

Najua pengine mtu akiwa na shida ni kumpa tu na siyo kumuwekea masharti , na ndio SADAKA NZURI KWA MIUNGU YAO!!

Nasubiri majibu yako, fedha za kwanza nitaingiza wiki moja baada ya kupata contacts zako, na awamu ya pili utapata baada ya miezi miwili baada ya kufikiria mtafanya biashara gani. Nadhani wewe na familia yako mtapendeza sana.

cheers

waberoya

Ukitaka kumjua mtu akili yake muangalie wakati anapochangia mada, kinachoongelewa kingine. Anarukia kwingine, kuna watoto wa mitaani kibao TZ, sidhani hata uliwahi kufikiri kuchukua wachache ukae nao, kwa moyo huo wakitokea watu zaidi na zaidi tunaweza kuwapa kwa kiasi fulani msaada. ILA UNAFANYA UTANI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!. By the way, YOU CANT BE SERIOUS. "LETS CHILDRENS GO TO SCHOOL AND MEN GO TO WAR".
 
Sasa tujiunge tu ili tupate misaada na tusijali jinsi gani tutaitumia?

Sasa lazima tulinganishe maana inaonekana misaada ambayo hatuipati ni mingi na mikubwa mno kiasi kwamba hatuwezi kuipata hadi tujiunge nayo. Hivi ni misaada ya kiasi gani hiyo ambayo tunaweza kuipata kutoka OIC? Lakini zaidi ni wapi ambapo OIC inasema nchi ikijiunga ina haki ya kupata misaada x, y, na z?

Kwanini unazungumzia "kutumia vibaya"? Unajuaje kuwa nchi hizo zimetumia misaada vibaya? Je Tanzania ina rekodi nzuri kiasi gani ya kutumia misaada ya kigeni?

Si kweli, inabidi usome malengo ya kuundwa kwa OIC na misaada kwa nchi maskini si mojawapo?

Sasa inaonekana hufahamu biashara inafanywaje katika nchi za kiarabu vinginevyo kungekuwa hakuna faida. Yaani nikupe dola 10 halafu urudishe dola 10 tu wakati tunafanya biashara. Wanaposema kuwa hakuna "riba" haina maana hakuna ada na kodi mbalimbali ambazo mtu au taasisi inalipa. Hivyo kuna gharama nyingine unazolipa ingawa siyo riba ambacho ni kiasi kinachotozwa kwa asilimia fulani ya kiasi kinachotolewa kama adhabu ya kukopa huko.

Ni lazima tulinganishe ili tuweze kuona kuwa kama ni kweli OIC ndiyo suluhisho la matatizo yetu au matatizo ya Waislamu. Wakati watu wengine wanatuambia "mbona Uganda na Msumbiji ni wanachama" tukiamua kuwauliza hebu tuonesheni wamefaidika vipi tunaambiwa tunalinganisha. Sasa tusilipolinganisha na majirani zetu tulinganishe na nani?

Kama OIC in clout hiyo ya kusaidia nchi maskini imesaidia vipi Comoro wakati wa Mohammed Bakari kujitenga? Imesaidia vipi Somalia leo hii miaka zaidi ya kumi haina serikali na Somalia ina Waislamu wengi? Imesaidia vipi kukomesha vita Sudan kule Darfur? Yawezekana OIC haina huo ujiko ambao watu wanafikiria inayo.

Hayo yote yalikuwamaswali yako, kuwa waliojiunga wanatuzidi nini?. Ila baada ya kukuuliza unauiza tena kama mimi ndio niliuliza. Unapozungumzia "Processing fees" kwa misaada ni kitu cha kawaida hata ukienda kukopa pale NMB, CRDB, IFM, nk. Sasa kama kote kuna kulipa fedha za kupata huo mkopo wapi bora, kule ambako utalipia mkopo ili uwe processed na baada ya hapo hakuna RIBA. Ama bado kwenye nafuu ni huku kwenye gharama za kuprocess na RIBA. Utazunguka mbuyu lakini ukweli uko pale pale. Sasa umekuja kuwa mikopo eti haina riba lakini kuna gharama unalipia. Hizo gharama ziko kwa kila mkopo, hujui kuwa kuna watu ndio wanamanage hiyo mikopo na pi gharama za kuendesha hiyo mikopo na ofisi zake ndio hupatikana hapo. Lakini bado mkopo wa OIC utakuwa juu manake hauna RIBA, hata kama unalipiwa gharama kama mikopo mingine. Vizuri sasa umekubali hakuna riba, ila kuzunguka kote unazungumzia fedha ya kuprocess, kweli sikio la kufa halisikii dawa. Manake unazungumza vitu vinavyojulikana kama vile hatujui.
 
hapa tunaongolea mate tu.. tafuta mahali utupe mfano kuwa mkopo fulani wa OIC ulitolewa kwa kiasi fulani na uliporudishwa ulikuwa ni kiasi fulani. Then we can talk.
 
Ukitaka kumjua mtu akili yake muangalie wakati anapochangia mada, kinachoongelewa kingine. Anarukia kwingine, kuna watoto wa mitaani kibao TZ, sidhani hata uliwahi kufikiri kuchukua wachache ukae nao, kwa moyo huo wakitokea watu zaidi na zaidi tunaweza kuwapa kwa kiasi fulani msaada. ILA UNAFANYA UTANI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!. By the way, YOU CANT BE SERIOUS. "LETS CHILDRENS GO TO SCHOOL AND MEN GO TO WAR".

Jinsi ulivyokasirika hapa, ndivyo ambavyo wengine tunavyoona aibu viongozi wetu kutaka misaada kila siku kila mahali ili hali we have every reason ya sisi kuwa kama hao walioendelea! aibu kubwa hata wewe kusisitiza, hii vinaonyesha jinsi fikra mgando ulizonazo kuwa ili tuendelee tunahitaji misaada na sio, siasa safi , uongozi bora na watu wenye maadili.

Aibu inakuja zaidi tunapotaka kutumia dini yetu tukufu ya kiislamu kama ni kiombea hela!

asante thinki that TZ is you na unaomba msaada kwa mwanaume mwenzako!

waberoya
 
Kidogo kidogo tunatoka nje ya mada. Tuliambiwa Mazinge yupo Songea tayari kuanza kumwaga "sumu" any update?
 
Jamani ushahidi toka ITV kuhusu kasheshe hii uko wapi? Mbona siku zinakatika tu hatusikii lolote!!! Kulikoni!!? :confused:
 
...na walisema kwamba tungesikia mashamsham ya hilo grupu tuka Tunduma sijui wapi huko swekeni, lakini mpaka leo kimyaaaaaa!! na yule mtoa mada (mdini na baguzi nambari wani) yupo doro kaa kuku anayekufa kwa mdondo...

MKJJ tuletee updates za hawa mamluki!! ebo!!
 
“Tunatamka kwamba endapo ITV hawatatuomba radhi kwa siku hizo saba… tutahamasisha Waislamu na Wakristo nchi nzima kuacha kutazama taarifa yoyote ndani ya kituo hicho, pia kusitisha ushirikiano wowote wa kibiashara na Kampuni za IPP, na mwisho tutaomba dua na kulaani kituo hicho,” alisema Msopa.

Na hawa wameishia wapi au ITV wameomba radhi, eh ? Tuendelee kusubiri.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom