Canada and Tanzania to begin negotiations on FIPA

Kwa mwanachama mtiifu nafurahi leo jamii forums imetinga bungeni kupitia swali la Zitto Kabwe kwa Waziri Mkuu Pinda. Kwa kuwa Pinda amehidi kwamba kabla ya kujibu swali hilo atapitia mitandao tajwa. Basi natarajia kwamba pamoja na kupitia mtandao wa Canada, atapitia pia Jamii Forums. Hivyo ni wakati wa kutoa maoni yetu ya kina kuhusu suala hilo ambalo lilishaanza kujadiliwa hapa tayari

JJ

Bits n pieces....
Mnyika nafikiri wewe kama muwakilishi wa vijana katika chama chenu unajua wazi how misinformation inaweza kuleta balaa katika jamii.

Can you please let us know exactly what transpired in the Q & A session huko Dodoma? Swali la Zitto liliuliza nini juu ya JF?
 
MASWALI KWA WAZIRI MKUU

Kabwe Zuberi Zitto, Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji Umma (Public Investments Accounts Committee).

24/07/2008

Mheshimiwa Waziri Mkuu,

Mkataba wa Kulinda Makampuni ya Madini kutoka Kanada (FIPA) yaliyowekeza nchini Tanzania.

Mheshimiwa Spika, wa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu Ripoti ya Kamati Kuhusu suala la Madini imewekwa wazi na itajadiliwa Bungeni.

Taarifa zilizochapwa katika Tovuti ya Idara ya Uwekezaji na Biashara ya Canada ambayo nimeipata kwa msaada wa Tovuti ya JamiiForums.com zinaoneshwa kuwa Tanzania ipo katika majadiliano na Serikali ya Canada ili kuingia Mkataba wa kulinda Makampuni ya Kanada yaliyowekeza Tanzania (Canada’s Foreign Investment Promotion and Protection Agreements - FIPA). Tanzania imekubali kuharakisha mazungumzo hayo kabla Mapendekezo ya Taarifa ya Bomani hayajatungiwa sheria ili makampuni ya Kanada na hasa katika
sekta ya Madini na mengineyo yaendelee kufaidika na Utajiri wetu wa Madini. Serikali ya Tanzania haijatoa Taarifa kuhusu Mkataba huu kwa Umma ingawa majadiliano yanaendelea.

Kwa nini Serikali inakubali ku ‘undermine’ Uhuru wa nchi yetu na kuingilia Mamlaka ya Bunge kwa kufanya majadiliano ya kulinda mikataba mibovu na wageni ilhali Ripoti ya Bomani ni suala la Bunge hivi sasa?

Mwisho.
 
Safi sana Zitto nimekusoma hapo lakini mbona jibu la huyo PM anaye ingia kwenye mkumbo wa usanii hujalitoa??
Sasa tunataka kujua yeye kajibu nini sasa hapo?Blabla kama kawaida au tusahau jamaa watuachie mashimo tuanze kukamatana wenyewe kwa wenyewe?
 
Majibu ya Pinda ni kuwa alikuwa hana taarifa na taarifa hizo hivyo kaomba kwanza aende kutafuta majibu na kupitia mitandao husika.

Kama waziri mkuu anaweza kusema kuwa hajui kitu kikubwa kama hicho kinaendelea sasa ni nani mtendaji wa serikali?

Nani anapaswa kujua?
 
Swali la Mhe. Zitto ni swali la msingi sana ila nivema kweli tukapata na majibu kamili ya PM ili kupata kuelewa amechukulia kwa uzito gani swala hilo
 
Huyu Pinda yupo sana hapa ila anazuga tu, kwa sababu mpaka leo hajabadili wasaidizi wake aliowarithi toka kwa Lowassa,

Mchambuzi, mpaka leo bado yupo huko na nimeongea naye mara ya mwisho Jumammosi akiwa naye Dodoma kwenye bunge, na wasaidizi wote wa Lowassa, walikuwa na mandate na bsoi wao always kuona hapa kuna nini, na mambo yote walikuwa wanaya-File sasa Pinda hakuyakuta hayo?

Kama kweli hapajui hapa mbona siku hizi amepunguza kelele kama tulivyomwambia hapa JF? Kama bosi wake yupo hapa yeye atakosa vipi? Huyo ni mazishi tu anazuga huyo!
 
Nadhani kati ya maswali ya msingi yaliyowahi kuulizwa hili ni mojawapo.
Hongera mkuu Zitto. Ni kumbana mpaka aseme yote na huo mpango wausitishe mara moja mpaka sheria mpya ya madini itakapotengenezwa. Anajifanya kushtuka kwamba hana taarifa..lakini huo ni usanii kama kawaida yao wanafanya mzaha katika masuala mazito kama hili..
 
Mh Zitto tunashukuru kwa kufuatilia kwasababu hilo la FIPA likipita basi tumekwisha.
Shukran pia zimwendee MWAFIZINA kwa kuleta issue hii hapa jamavini.

Mhafidhina
user_offline.gif

Mhafidhina is HIV -VE
Member
Join Date: Wed Feb 2008
Location: Dar es Salaam, Tanzania
Posts: 47
Rep Power: 0
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif

Thanks: 47
Thanked 41 Times in 16 Posts
Credits: 3,686

icon4.gif
Canada and Tanzania to begin negotiations on Foreign Investment Protection
Background on the Canada-Tanzania FIPA Negotiations:

Canada and Tanzania have agreed to begin negotiations towards a Foreign Investment Promotion and Protection Agreement (FIPA). The parties have pledged to work together to conclude an agreement in a timely manner.

A bilateral FIPA will provide greater predictability and certainty for Canadian investors considering investment opportunities in Tanzania, and will underscore Tanzania’s reliability as an investment destination. Canada’s objective in entering these negotiations is to secure a comprehensive, high-quality agreement which will protect investors through the establishment of a framework of legally binding rights and obligations.

Jamani, hii taarifa nimekutana nayo huku Canada jana (tarehe 21/07/2008), wenzetu wako kwenye negotiations za Mkataba wa Investment Promotion and Protection Agreement with the Government of Tanzania.

Wenzetu wao wameamua kuliweka wazi kabisa na kulitangaza hadi kwenye website yao ya serikali, (http://www.international.gc.ca/trade...-tanzanie.aspx) Lakini cha kushangaza ni kwamba sisi huko kwetu najua hakuna mtu yoyote anayejua chochote kuhusu mkataba huu muhimu sana. Sitashangaa tukiona tunaletewa tena mkataba mwingine wa ajabu manake kama ilivyo kawaida mikataba hii serikali yetu huifanya ikawa ya siri sana.

Kama wamediriki kufanya lobbying for the sake of their companies sitashangaa wakatubamiza kwenye mkataba huu, tusipokua makini tunaweza tukawauzia nchi yote kabisa.

Kwa wale wabunge ambao wapo humu ndani ya JF (Dr. Slaa na Zito na wengine) nawaomba mjaribu kulipigia kelele hili swala, tunaomba serikali watoe official statement kuhusu mkataba huu muhimu, wenzetu wao wametoa press statement na huu mkataba sio siri kwao, wananchi wao wametaarifiwa vizuri kabisaa.

Pia tunaomba kujua ni nani wanaoliwakilisha Taifa kwenye hizo negotiations za huu mkataba muhimu sana kwa Taifa. Tusije "tukadanganyika" kama ilivozoeleka.
 
Hongera Zitto. Na nafurahi kuona JF inazidi kuwa kisima cha maarifa cha kuwasaidia waheshimiwa wetu katika kudhihirisha uzito wa hoja wanazotoa bungeni wakitumia ushahidi unaopatikana hapa JF. Yako mengi sana hapa JF, nawashauri wabunge wayatumie, na wawe jasiri kama Zitto, watamke wameyapata hapa ili hata anayetaka details na mawazo ya wananchi wengine aje mwenyewe hapa ayaone.
 
Positive move hata wao wanajua kuwa kuna mhimili wa Tano nao ni JF
 
Last edited by a moderator:
Hili ni jambo jingine la kusikitisha linalo onyesha wazi kuwa dhamira ya mafisadi watanzania msipoangalia itawapeleka kubaya.

Kwani huu mkataba mpya unaonekana ni wa kutufanya tushindwe kuvunja mikataba ya zamani.

KUWENI MAKINI WATANZANIA..!

Mkataba huo ukisainiwa basi HAKI HAITAKUWEPO NA UWEZEKANO WA MACHAFUKO NI MKUBWA.

Kwasababu hizi ni mbinu za kuilinda mikataba mibovu kwa kigezo cha sheria mpya ama mkataba mpya wa kulinda mikataba ya zamani isivunjwe na bunge letu.

Wacanada kupull back kumbe ni kupanga mbinu ya kutumalizia mbali..Kwani mkataba huu ukisainiwa basi nguvu ya jeshi la serikali ya mafisadi na labda kwa kusaidiwa na nguvu za makampuni hayo kuzishawishi serikali zao...itatumika kutunyanyasa wananchi.

Hvyo basi ndugu zetu wabunge...Tunaomba taarifa kuhusiana na hili.

Tunaomba taarifa RASMI kama Wacanada walivyofanya kwa kuwapa taarifa wananchi wao!

Mtindo wa serikali yetu kuendelea kukumbatia system kama ile ya Baath Party ya Saddama Hussein...System ambayo wana chama walishikilia karibia kila kazi muhimu za Taifa ikiwa pia kumilikishana visima vya mafuta kwa wanafamilia,wanachama na wale wote wenye kusikiliza na kukubaliana na sera za chama.
Hilo lilipelekea migawanyiko kwani chama ni kila kitu na hivyo kutosikiliza wananchi hata kwenye negotiations...Kila kitu ni SIRI KUBWA!

Kwasababu ya USALAMA WA SADDAM NA BAATHISTS.

Kama ilivyowekwa wazi na serikali yetu kuwa ni USALAMA WA NEC NA JK.

Ni wazi ccm imeamuwa kuikumbatia system ya BAATHIISM kwani Hamkumbuki makamba akisema NEC sasa inaongoza bunge?

Sasa NEC ni nani hao?

Si ndio hao hao serikali yetu ambao ni MAFISADI?

Kwasababu si ndio hao hao wenye kumiliki mali zetu watanzania na pia hata kumiliki UHURU WETU?

Si ndio hao hao wameturudisha utumwani kwa kugeuka ma lobbysts wa makampuni makubwa ya kimataifa ambayo hayajali utu wa mwafrika zaidi ya pesa?

Na hao wanaongoza Bunge?

Sasa kuna haki itakayotendeka humo bungeni kama bunge hilo halitavunjwa?

Mimi sioni uwezekano wa wabunge hao kufanya lolote...Kwanza Makamba keshapeleka siasa huko Bungeni na yeye mwenyewe amekiri pale aliposema alijisahahu na kudhani yuko kwenye mkutano wa kisiasa.

Sasa kweli tuna watu serious jamani wenye kujali UTU?
Umasikini umetumaliza na sababu kubwa ni wasomi!
Wasomi badadala a kuwasaidia wananchi ndio kwanza wanamalizia mbali.

Uongozi hasa wa Taifa kama la Tanzania ni mzigo mzito sana kama kweli wewe ni mzalendo.

Kwanini?

Simple...Wananchi walio wengi ni wajinga!
Kama asilimia labda hata zaidi ya 80 ya wananchi ni wajinga!

Na hata hiyo asilimia 20 iliyobaki haina maana kuwa ni wote wana opportunities..Hilo liko wazi.

Hivyo ni ka group kadogo sana ka wasomi hao na wengine wasio wasomi bali wale ambao tunasema wamezaliwa with a silver spoon on their mouth.

Taifa letu linahitaji mapinduzi na wala si eti mabadiliko.
Serikali mpya ijayo viongozi wajitahidi sana kupunguza matumizi ya serikali!

Ni makubwa kiasi cha kutisha..Na hata kazi yenyewe haionekani.

Kutaka kusaini mkataba na Wacanada kama inavyoonekana ni Mbinu ya mwisho ya Mafisadi ili kusema kuwa haki za makampuni hayo zimekiukwa kwa kuikatisha mikataba mapema kuliko makubaliano.

Kutaka ku imply kuwa sisi wnanchi ndio tumeinyanyasa kampuni ya BARRICK!

Hivi kweli viongozi wanaowageuka wananchi kwasababu tu ya makampuni jamani huo ni UBINADAMU NA UTU KWELI?

KUNA UZALENDO GANI HAPO?

Uungwana NI VITENDO...ZAIDI YA HAPO...JIUZULU JK.
USITULETEE BALAA!
 
Waziri Mkuu hajui kama kuna mazungumzo kuhusu hili!!! Inabidi aje JF ili kujua undani wa mazungumzo hayo!!!! Kweli hatuna serikali!!!!! Yaani anataka kutwambia serikali inafanya mazungumzo haya bila yeye kuwa na taarifa yoyote!!!
 
waziri mkuu anajibabaisha tu, haiwezikani kufanywa jambo kama hilo na yeye kuwa hajui.

hawa watu wanapenda kuspin, lakini mwaka huu wananchi tupo macho.

hongera zitto, hongera muhafidhina, hongera JF......
 
Tumeshajuwa kuwa Mkataba huo ni wa kuwaprotect Wa Canada...To be more specific ni wa kuwaprotect wawekezaji...Sasa huo ni upande wa Canada kwenye negotiations...UPANDE WA SERIKALI NI WA KUM PROTECT NANI?
Na ujumbe wangu ni kwa serikali zote mbili wakati wa mjdala huo...WOULD YOU GUYS CONSIDER THE INHABITANTS?

Canada's objective in entering these negotiations is to secure a comprehensive, high-quality agreement which will protect investors through the establishment of a framework of legally binding rights and obligations.

Na mkikubali mkataba huo wa FIPA usainiwe...Usijekushangaa kuona majeshi ya CANADA ama NATO yakitinga hapo bongo kulinda hizo zinazoitwa legally binding obligations hizo zitakazosainiwa na mafisadi.

Obligations ambazo zitakuwa binded na sheria kati ya mafisadi na kina SINCLAIR.

Na kama hata wakipigiwa kelele na human rights watawatumia baadhi ya vyombo vya usalama wa Taifa ambavyo vinaongozwa na watu wenye kumiliki rasilimali za Taifa kama vile migodi nk.

Na pia jeshi la polisi ama hata baadhi ya viongozi wao wa juu ni mafisadi ambao nao wamepewa share na kuambiwa wayalinde maslahi ya mafisadi kwa gharama zozote kwani wao na familia zao na baadhi ya wanachama wa ccm wananufaika nazo.

Taifa letu limemilikishwa chini ya watu wachache na msishangae wakapewa silaha zaidi za kuwalinda dhidi ya wananchi.

Kila mara mataifa ya nje yamekuwa yakianzisha vita ya wenyewe kwa wenyewe huku Afrika tena mara nyingi kama chumi zao zikiwa kwenye matatizo na pale wanapojaribu kurekebisha uchumi wao kwa kuja Afrika kupata malighafi, vito na nishati wamekuwa hawataki kuwalipa waafrika kile wanachostahili kwani hawana huruma wala nia nzuri na mwafrika na pia hawataki apate maendeleo wala elimu.

Hivyo narudia tena....Kama ni kweli Taifa letu linataka kubadili mwelekeo kabla ya kupigana wenyewe kwa wenyewe..Ni vizuri MAFISADI wakageuza mioyo yao kwani ni wazi kuwa wameshazidiwa nguvu na kuendelea kubishana na kupinga haki ni kupalilia madhara ambayo yanaweza kuzikumba familia zao na vizazi vyao vijavyo.

Ni bora wakasema YATOSHA...Na kukubali maridhiano na nchi ikabidhiwe kwa wazalendo na tuanze mchakato mpya.

Wakati huu ni muhimu sana na kama tukishindwa kuja pamoja ili tudai haki yetu kwa kulipwa kile tunachostahili...Basi narudia tena kuwa tutaingia kwenye civil war na manufaa yatakuwa kwa watu wa nje kwani wao watatuuzia silaha na sisi tutawapa madini kwa kukubali kupewa VIJISENTI vya kutusaidia sisi na TUJIVITOTO VYETU...Lakini wananchi walio wengi watakufa kwa vita na njaa.

Mimi binafsi nawaambia hivi ndugu zangu wabunge.

Inaelekea hamjui kabisa vugu vugu lililopo..Inaelekea bado mna enjoy life na kusihi kwenye dunia yenu wenyewe!

Ninarudia kuwaomba kuwa msipokuwa makini...Historia itawatoa nishai.
 
Majibu ya Pinda ni kuwa alikuwa hana taarifa na taarifa hizo hivyo kaomba kwanza aende kutafuta majibu na kupitia mitandao husika.

Kama waziri mkuu anaweza kusema kuwa hajui kitu kikubwa kama hicho kinaendelea sasa ni nani mtendaji wa serikali?

Nani anapaswa kujua?

Usishangae kama rais wako akiulizwa swali hilo hilo, naye akatoa jibu kama hilo hilo la kizembe! Sijui.....sina taarifa...!
 
hongera Zitto. Na Nafurahi Kuona Jf Inazidi Kuwa Kisima Cha Maarifa Cha Kuwasaidia Waheshimiwa Wetu Katika Kudhihirisha Uzito Wa Hoja Wanazotoa Bungeni Wakitumia Ushahidi Unaopatikana Hapa Jf. Yako Mengi Sana Hapa Jf, Nawashauri Wabunge Wayatumie, Na Wawe Jasiri Kama Zitto, Watamke Wameyapata Hapa Ili Hata Anayetaka Details Na Mawazo Ya Wananchi Wengine Aje Mwenyewe Hapa Ayaone.

Zitto Kafanya Lipi Kubwa? Badala Ya Yeye Kuishukuru Jf Imekuwa Kinyume Chake?
Na Jf Haijatajwa Ila Zitto Kaipigia Chapuo Kwa Vile Yeye Ni Chadema Na Hii Ndio Source Pekee Ya Habari Kwa Chadema Na Gazeti Lake La Mwanahalisi, Ilitakiwa Yeye Atashukuru Sisi Kwa Kumpa Data Kwake Kama Mbunge Na Gazeti Lake Ambalo Analiendesha Kibiashara.
 
Hili ni jambo jingine la kusikitisha linalo onyesha wazi kuwa dhamira ya mafisadi watanzania msipoangalia itawapeleka kubaya.

Kwani huu mkataba mpya unaonekana ni wa kutufanya tushindwe kuvunja mikataba ya zamani.

KUWENI MAKINI WATANZANIA..!

Mkataba huo ukisainiwa basi HAKI HAITAKUWEPO NA UWEZEKANO WA MACHAFUKO NI MKUBWA.

Kwasababu hizi ni mbinu za kuilinda mikataba mibovu kwa kigezo cha sheria mpya ama mkataba mpya wa kulinda mikataba ya zamani isivunjwe na bunge letu.

Wacanada kupull back kumbe ni kupanga mbinu ya kutumalizia mbali..Kwani mkataba huu ukisainiwa basi nguvu ya jeshi la serikali ya mafisadi na labda kwa kusaidiwa na nguvu za makampuni hayo kuzishawishi serikali zao...itatumika kutunyanyasa wananchi.

Hvyo basi ndugu zetu wabunge...Tunaomba taarifa kuhusiana na hili.

Tunaomba taarifa RASMI kama Wacanada walivyofanya kwa kuwapa taarifa wananchi wao!

Mtindo wa serikali yetu kuendelea kukumbatia system kama ile ya Baath Party ya Saddama Hussein...System ambayo wana chama walishikilia karibia kila kazi muhimu za Taifa ikiwa pia kumilikishana visima vya mafuta kwa wanafamilia,wanachama na wale wote wenye kusikiliza na kukubaliana na sera za chama.
Hilo lilipelekea migawanyiko kwani chama ni kila kitu na hivyo kutosikiliza wananchi hata kwenye negotiations...Kila kitu ni SIRI KUBWA!

Kwasababu ya USALAMA WA SADDAM NA BAATHISTS.

Kama ilivyowekwa wazi na serikali yetu kuwa ni USALAMA WA NEC NA JK.

Ni wazi ccm imeamuwa kuikumbatia system ya BAATHIISM kwani Hamkumbuki makamba akisema NEC sasa inaongoza bunge?

Sasa NEC ni nani hao?

Si ndio hao hao serikali yetu ambao ni MAFISADI?

Kwasababu si ndio hao hao wenye kumiliki mali zetu watanzania na pia hata kumiliki UHURU WETU?

Si ndio hao hao wameturudisha utumwani kwa kugeuka ma lobbysts wa makampuni makubwa ya kimataifa ambayo hayajali utu wa mwafrika zaidi ya pesa?

Na hao wanaongoza Bunge?

Sasa kuna haki itakayotendeka humo bungeni kama bunge hilo halitavunjwa?

Mimi sioni uwezekano wa wabunge hao kufanya lolote...Kwanza Makamba keshapeleka siasa huko Bungeni na yeye mwenyewe amekiri pale aliposema alijisahahu na kudhani yuko kwenye mkutano wa kisiasa.

Sasa kweli tuna watu serious jamani wenye kujali UTU?
Umasikini umetumaliza na sababu kubwa ni wasomi!
Wasomi badadala a kuwasaidia wananchi ndio kwanza wanamalizia mbali.

Uongozi hasa wa Taifa kama la Tanzania ni mzigo mzito sana kama kweli wewe ni mzalendo.

Kwanini?

Simple...Wananchi walio wengi ni wajinga!
Kama asilimia labda hata zaidi ya 80 ya wananchi ni wajinga!

Na hata hiyo asilimia 20 iliyobaki haina maana kuwa ni wote wana opportunities..Hilo liko wazi.

Hivyo ni ka group kadogo sana ka wasomi hao na wengine wasio wasomi bali wale ambao tunasema wamezaliwa with a silver spoon on their mouth.

Taifa letu linahitaji mapinduzi na wala si eti mabadiliko.
Serikali mpya ijayo viongozi wajitahidi sana kupunguza matumizi ya serikali!

Ni makubwa kiasi cha kutisha..Na hata kazi yenyewe haionekani.

Kutaka kusaini mkataba na Wacanada kama inavyoonekana ni Mbinu ya mwisho ya Mafisadi ili kusema kuwa haki za makampuni hayo zimekiukwa kwa kuikatisha mikataba mapema kuliko makubaliano.

Kutaka ku imply kuwa sisi wnanchi ndio tumeinyanyasa kampuni ya BARRICK!

Hivi kweli viongozi wanaowageuka wananchi kwasababu tu ya makampuni jamani huo ni UBINADAMU NA UTU KWELI?

KUNA UZALENDO GANI HAPO?

Uungwana NI VITENDO...ZAIDI YA HAPO...JIUZULU JK.
USITULETEE BALAA!

For this, I salute you JMushi! Thanks!
 
kauli za waziri mkuu pinda zinatia njia panda hatama ya nchi yetu.
kauli ya kuwa meremeta ni suala la usalama wa taifa haliwezi kujadiliwa bungeni wakati kampuni imesajiliwa visiwa vya uingereza na wakurugenzi ni wazungu inatisha. je usalama wa taifa umebinafsishwa? inatisha!!
kauli kuwa waliochota hela za EPA hawawezi kushtakiwa kwa sababu ya uwezo wao kifedha inatisha zaidi. je sheria za jinai ni kwa ajili ya maskini tu?
na hili la zanzibar si nchi sio geni watu walikuwa wanajua lakini kulizungumza kama kiongozi wa ngazi ya juu ya nchi inahitaji umakini kidogo si kuropoka tu. huyu jamaa kweli ni mwanasheria au tunadanganywa?
je tatizo ni hana washauri au ni mkurupukaji?
je kama huyu ndie anaemshauri rais wetu tutegemee nini?
kazi ipo
 
Usishangae kama rais wako akiulizwa swali hilo hilo, naye akatoa jibu kama hilo hilo la kizembe! Sijui.....sina taarifa...!

Majibu wameshapeana yeye na SINCLAIR kitambo tu..Nyie hamjuwi hilo!
Ni kwamba kuwa kiongozi wa Tanzania ni kazi ngumu kwani inahitaji HURUMA!

Ili kweli kuweza kumsaidia Mtanzania ni lazima kumlazimishia kama vile watoto wanavyolazimishiwa dawa.

Na si kuwalazimishia utumwa eti kwasababu tu ni WAJINGA!

Watanzania wengi wao hawajasoma na ni kama watoto wadogo!
Viongozi wasiokuwa na huruma watakuja na maneno kama haya...

Mwinyi:Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu
Mkapa:Watanzania ni wavivu wa kufikiri.
Jakaya Kikwete yeye ndio akaja na MPYA KABISA...Kwani tatizo lake yeye ni kwasababu ya mambo ya technology kama mtandao huu na mengineyo.

Mawasiliano yanakwenda kwa kasi na watanzania wako in touch duniani kote.

Hivyo kuna wale wenye huruma na hawakubali wananchi wapelekwe Utumwani hata kama ni wajinga na hawana elimu...Tuko radhi kufa kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Wale wachache wenye elimu wameona ukweli kuwa watanzania bado ni nyuma sana haswa kwenye kujuwa haki zao.

Na sasa kuna wenye elimu amabao wamejitolea kuwalinda wajinga ili vizazi vya baadaye vinufaike..Vizazi vya wale wajinga na wale wasomi wachache wazalendo na wenye huruma.

Watu unaweza kushangazwa kuwa dini na makabila yanawagawanya kiasi cha kwamba watu hawawezi tena kushirikiana kwenye ujenzi wa Taifa!

Ujinga huo unaochochewa na mkoloni kwa kuwatumia wale wasomi wachache walio ahidiwa pepo na ulinzi wa kila aina na Mkoloni unaelekea kufikia mwisho pale inapokuja kwenye madhara yake kwenye kizazi kijacho kwani kuna wale waliojitolea MUHANGA kwasababu tu ya kizazi kijacho na kamwe SI KWASABABU YA WANANCHI WAJINGA WANAOKUMBATIA TAARAB, MIPASHO, KHANGA, PILAO NA UNAFIKI WA MIGAWANYO YA KIDINI NA KIKABILA!

Wale ambao wako radhi kufa kuliko waambiwe chochote na mkristo,msilam ama mchagga vs kabila lolote lingine!

Na wenye mwisho ni...Mafisadi...Hii ni pamoja na vibaraka wao..

Wale waliomamuwa kuchaguwa kambi za mabwana na kupita pita huko kuomba kila siku itokayo kwa Mungu kama kina Mtikila na wakati wale wanao waomba kina Rostam ndio wanamiliki mali zetu na ni makaburu kwenye ARDHI YETU WANAYOIMILIKI!

Ndugu zangu wabunge...WENGINE TUNAJITAYARISHA KUVIPIGA VITA VINGINE VIPYA DHIDI YA MKOLONI KAMA IKIBIDI.

Na wale mamluki sisiti kusema NDIO TARGET YA KWANZA.
 
Mushi Nimeona Kazi Nzuri Kwani Thread Ya Mziray Na Ripoti Yake Imefutwa Na Hoja Zangu Zimefutwa.lakini Dawa Ya Hoja Ni Kujibiwa Sio Kuzifuta,mkitunyima Nafasi Hapa Wananchi Watahoji Maswali Haya Mtaani. Jf Uongozi Wake Inabidi Ufuatilie Mod Wanaochanganya Mapenzi Kwenye Chama Na Kazi Za Moderator.
 
Back
Top Bottom