Waziri mkuu wa Canada alipofanya ziara yake Tanzania, moja ya maoni yake kuhusu uuwekezaji hapa kwetu hususa madini, yalikuwa ni sheria mbovu tulizoweka ambazo hazilindi maslahi ya nchi. Sasa sijui ni nini kinachoifanya serikali yake itake kinga kwa wawekezaji kutoka nchini kwake? Alikuwa akipiga porojo kufurahisha akina Bomani na kamati yake? Ni aibu serikali kwenda kufananya mazungumzo hayo wakati kuna miswada bungeni kuhusu mchango mdogo wa madini katika uchumi wetu. Wakishatia saini, je sheria ya bunge itakuwa na maana gani? Kwa nini serikali ya CCM inatuzunguka hivi? Haya ni maswali ambayo tujiiulize kama CCM ina nia kweli ya maisha bora kwa wote.
WABUNGE WA CCM IDHIBITINI SERIKALI YENU.
WABUNGE WA CCM IDHIBITINI SERIKALI YENU.