CAG REPORT, upotevu wa hela za Serikali

shinyangakwetu

JF-Expert Member
Jun 25, 2015
2,488
2,385
Naomba niende mbali zaidi kuwa niwe Whistle Blower katika baadhi ya sehemu kulikopotea/kufujwa hela za umma.

Rais wetu ana nia nzuri zana anapofanya teuzi mbalimbali ila wengi wanamwangusha kwani kutokana na kibano walichopewa kipindi cha Jiwe sasa wanataka wavute fasta kwa urefu wa kamba zao pindi mama akiwa syo rais tena wawe wameshafanya yao.

Mheshimiwa Rais na wale wote wenye mamlaka pa kuanzia ili kujua majizi yalipo hebu tafitini kidoogo tu majumba yanayomea maeneo tofauti ya nchi zaidi kabisa Dar es salaam na zaidi kwa kabisaaa maeneo ya Mbweni Na Bunju jijini DSM

Kipindi cha JPM ujenzi ulisimama na viwanja vingi vikawa mapori hali ilopelekea waziri wa Ardhi wakati huo Lukuvi kutishia kupoka maviwanja maeneo hayo. Ila sasahivi majumba makubwa na ya kutisha yamemea kama uyoga.

Maeneo ya mbweni wamejipelekea lami hadi milangoni na sasa cha ajabu kuna mnene flani ameshawishi barabara iwekwe lami kuanzia Moga schools hadi kwenye nyumba inakojengwa(hatujui ya nani-ikichunguzwa atajulikana), barabara hii ingekuwa na manufaa zaidi kama ilotoka Ubungo (mbweni) ingeenda mojakwamoja na kupita kwa katibu mkuu CCM(chogolo) ambaye ameweka mjengo wake huko bunju na moja kwa moja kupitia uliko uwanja wa simba na kutokeza barabara karibu na mto mpiji.Barabara hiyo ingekuwa inapunguza foleni ya bagamoyo road.

Kwa hayo machache Mheshimiwa rais na wengine wenye mapenzi mema na nchi yetu wenye mamlaka anzieni hapo.

Kuna thread humu inamsema kamishna wa TRA amevamia viwanja vya wazi mbweni na vingine Bunju beach na viongozi wengine pia wamevivamia. Huko ndiko majizi yalipo.
 
Wakati inasomwa riport ya CAG, Haya majizi yalishapewa adhabu ya kuitwa "stupid" inatosha sana. 🤣 🤣 🤣
 
Back
Top Bottom