Elections 2010 Breaking News: CCM wanamuandaa KINANA kuwa spika wa bunge

Bunge hili ni la CCM wao ndio wana majority , na wako zaidi ya 2/3, kwa hiyo wao ndio watakao pitisha miswada pindi watakapo taka ipite hata km wapinzani hawata taka kwani ni wachache hawawezi kukwamisha kitu chochote. Walaumuni wananchi walio wachagua kwa uchache.

Wananchi na TUME kwa kuchakachua matokeo.
 
Habari za ndani kutoka CCM zinasema kada aliyejizolea umaarufu katika uchaguzi wa mwaka huu ndg Kinana anaandaliwa kuwa spika wa bunge.

Wabunge wote wa CCM wanaandaliwa kuwekwa chini ili waelezwe hili na ole wake atakayehujumu.Suala la form ni danganya toto tu......

Jamani tutafika kweli? Kwanza kwanini kumtafuta spika iwe kazi ya chama? Hivi hili ni bunge la CCM ama nini?

WATANZANIA TUSIKUBALI......

Bravooo Hon. Mr Speaker mfikiriwa, Kinana, ulifanya vizuri sana kupanga ushindi wa CCM kwa kuzua hoja ya udini, ndoa na umwagaji damu dhidi ya aliyekuwa Rais mteule Slaa na kuchakachua mchana kweupe. Hakika unastahili ofisi kubwa sana Tanzania. Na kwavile PM haiwezekani, uspika ni logical position. Hata mtu asiyejua somo la takwimu anaelewa kabisa yale majimbo yenye upinzani mkali NEC ya CCM (kama alivyoiita Kiravu) yalicheleweshwa kutangazwa matokeo.

Sasa utakapopewa kazi hii dhambi ya ubaguzi uliyoifanya itakurudia kutoka kwa mahasimu wako wa nafasi ya uspika ndani ya CCM kwa kusema kwamba:-
1- wewe sii Raia halali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
2- umeshiriki kupora nyara za taifa kama pembe za ndovu
3- etc etc nasikia hata utekaji wa m**i
4-
5-
 
Kasi ya bunge linalokuja hakuna spika atakayeweza kulizuia, kila juhudi ya kutaka kulinyamazisha itaonekana live kwenye TV na kusikika redioni.

Natabiri kisayansi kuwa CCM inaenda kupasuka kiasi ambacho hatujawahi kushuhudia since records begun.

Sio kupasuka kwani ilikwisha kufa, sasa ni kuingia kaburini!
 
Habari za ndani kutoka CCM zinasema kada aliyejizolea umaarufu katika uchaguzi wa mwaka huu ndg Kinana anaandaliwa kuwa spika wa bunge.

Wabunge wote wa CCM wanaandaliwa kuwekwa chini ili waelezwe hili na ole wake atakayehujumu.Suala la form ni danganya toto tu......

Jamani tutafika kweli? Kwanza kwanini kumtafuta spika iwe kazi ya chama? Hivi hili ni bunge la CCM ama nini?

WATANZANIA TUSIKUBALI......
Hatujafika bado? from kuvaa makatambuga (matairi)viroba mpaka kupambana na ufisadi hewa?safari gani tunayoitaka?
 
Kasi ya bunge linalokuja hakuna spika atakayeweza kulizuia, kila juhudi ya kutaka kulinyamazisha itaonekana live kwenye TV na kusikika redioni.

Natabiri kisayansi kuwa CCM inaenda kupasuka kiasi ambacho hatujawahi kushuhudia since records begun.

Chesty nakubaliana na wewe kama wabunge wengi wa CCM wataungana na wabunge wasio wa CCM kwa dhamira thabiti ya kuwapigania Watanzania.
Lakini kwa wabunge tunaowajua wa CCM ambao asilimia kubwa wako pale kwa kujaza matumbo yao, hilo wala usilitegemee, wakiona mambo magumu watafanya vile vikao vya chama, baada ya hapo kinachofuata wote tunajua, ni kupiga meza tu, maneno mengi na kumalizia kwa '' Baada ya kusema hivyo ndugu Mheshimiwa Spika , NAUNGA MKONO HOJA''
 
Hakika umepotoka ndugu yangu, lazima ukili ukweli sita aliongoza vizuri bunge kutompa Sita itakuwa ni pigo jingine kwa SSM, lakini watu wenye busara wa CCM kama Jenister, Mwakyembe, Kilango, Lazaro hawatakubali hata kwa vitisho vya radi ya Sumbawanga
 
Siyo Kinana peke yake anayepigiwa upatu na CCM, wapo pia LOWASA, SALMA KIKWETE, RIDHIWANI KIKWETE, ROSTAM AZIZ, MASHA, LEWIS MAKAME, KIRAVU, MARIN HASSAN NA ABDULRAHMAN SHIMBO. HAO NI BAADHI TU YA WANACCM NIMEWATAJA.

WATANZANIA TUSIKUBALI......[/QUOTE]
 
Maadam wameshindwa kuheshimu maoni ya watanzania
basi sintashangaa wakimchagua kinana hata rostam kuwa spika wa bunge.

Sishangai, nasema sishangai kwa sababu hao ndio ccm na wameamua hivyo.

Ila tusiwabeze watanzania wakilalamika hali ngumu za maisha kwa maana wao walichagua ila fulani akapora ushindi wao. tufanye kazi under pressure kuhakikisha tunaelimisha zaidi ya hapa tulipofikia
 
Sasa hivi tuna jicho la kuangalia Seriklai. CCM wabunge wao baada ya kuondoa mawaziri watakuwa kwenye 210 sawa na 64% (bado sijaondoa absentees) hivyo hawana uwezo wowote wa kubadili katiba bila ya ridhaa ya upinzani.
 
habari za ndani kutoka ccm zinasema kada aliyejizolea umaarufu katika uchaguzi wa mwaka huu ndg kinana anaandaliwa kuwa spika wa bunge.

Wabunge wote wa ccm wanaandaliwa kuwekwa chini ili waelezwe hili na ole wake atakayehujumu.suala la form ni danganya toto tu......

Jamani tutafika kweli? Kwanza kwanini kumtafuta spika iwe kazi ya chama? Hivi hili ni bunge la ccm ama nini?

Watanzania tusikubali......
soma katiba na sheria
 
sioni ubaya wa kinana kuwa spika tofauti ya kinana na sita na msekwa ni ipi, ccm wanatoa fomu kwani wao ndo wenye haki kisheria kutoa spika basi nasi chadema tupeleke wetu akapigiwe kura na ccm awe spika ajibu hiyo. Mr ii au mdee wawe ma spika au tozi wetu wa arusha? Mambo hayo
soma katiba na sheria ndio uje kuchangia
 
Huyu Kinen... sorry Kinana ameifanyia kazi kubwa CCM mwaka huu so naona wanataka kulipa fadhila kwa kumpa nafasi hiyo nyeti.
 
Utaratibu wakumpata SPIKA ni kuwa kila chama kinateua mgombea wake na kila chama kinaruhusiwa kuingiza mtu mmoja kwa hiyo CCM hawajafanya kosa kutangaza nafasi ya mgombea uspika kupitia chama chao kwani baada ya kuchukua form watachujana. KUCHAKACHUANA WAO KWA WAO kwanza.
 
Kinana ni fisadi la mafisadi wote...mimi binafsi sitakuwa tayari yeye apewe hicho kiti...iwe itakavyokuwa naomba tusaidiane akose hiyo nafasi
 
sishangai kwani hizi ndizo mbinu za mafisadi. wametumia hela nyingi kwenye uchaguzi hivyo watahakikisha zinarudi kwa kutoruhusu maswali bungeni. dhambi hii inapaswa watanzania tumrudie Mungu atuepushe na kundi hili la mafisi na mbweha na mbwa mwitu
 
kasi ya bunge linalokuja hakuna spika atakayeweza kulizuia, kila juhudi ya kutaka kulinyamazisha itaonekana live kwenye tv na kusikika redioni.

natabiri kisayansi kuwa ccm inaenda kupasuka kiasi ambacho hatujawahi kushuhudia since records begun.

yeah!
 
Kasi ya bunge linalokuja hakuna spika atakayeweza kulizuia, kila juhudi ya kutaka kulinyamazisha itaonekana live kwenye TV na kusikika redioni.

Natabiri kisayansi kuwa CCM inaenda kupasuka kiasi ambacho hatujawahi kushuhudia since records begun.


Chesty !!!!!! Very well said. It is absolutely true, yaani sasa ulee upinzani wa kweli uliotabiriwaga ndio uko njiani.
 
Back
Top Bottom