Bosi anaisambaratisha familia yangu huku nikiwa sina la kufanya

Tatizo hili Jukwaa drama zimekua nyingi.Nikipitia nyuzi zako na comments kwenye nyuzi zingine sioni connection
 
Mkuu mm sio mwandishi, nimeelezea tatizo langu kwa kadri ya uandishi wangu...na hakuna mahali nimemuomba mtu pesa, I just wanted to take this thing out of my heart...maana nimeshaanza kupata fikra za kujioverdose, nilitegemea mtanitia moyo...Sawa, wacha nisahaurike milele.


Joel can you come here at Christ Church opposite na Mapato house sasa hivi. Utakuta kuna mahema na viti vyeusi
 
Pole sana ndugu yangu Joel Johansen. Nimefurahi sana kuona kwamba you eventually managed to embrace your family baada ya wadau kukushauri hapa JF mimi nikiwa mmoja wapo. Sacred decision that is !! Endelea kupambana kwa ajili ya familia yako. Usikate tamaa hata kidogo. Nikuambie tu kuwa tatizo lako ni dogo sana...tena sana. Wewe hilo unaliona kubwa kwasababu hiyo ni aina ya matatizo ambayo unfortunately huna uzoefu nayo katika maisha yako.

Brother, kuna watu wana matatizo makubwa zaidi ya hilo lako na bado wanahangaika kwa matumaini ili kujikwamua. Utafanikiwa mkuu. Challenges (i normally hate to call them problems) zinamfanya mtu awe more mature...but if and only if zikichukuliwa positively hizo changamoto. Mtegemee Mungu kwa kila kitu.

Njoo PM mkuu tujadiliane ili nione jinsi ya kukusaidia kwa jinsi nitakavyoweza. Sisi wote ni ndugu kaka.
 
Naungangana na ushauri uliopewa hapa. Rudi Mwombe Mungu, Mungu aliyekusaidia ukaokotwa ukiwa hai, ukalelewa na kukapata elimu bado yupo nawe kila uendako. Mungu anayaona haya yote. Piga magoti muombe Mungu ni majaribu na utakuwa unawinda ktk ulimwengu wa roho ili kuiangamiza familia yako. Yaonekana lile kusudi lilolomsukuma mama yako kukutelekeza na Mungu akakuponya bado linakunyemelea. Maisha ni Zaidi ya hayo unayofikiria. Bado wewe ni wa thamani Zaidi ya mahindi na watu unaofikiria ni wa thamani zaidi. Kama ungepata nafasi watu wakakueleza wamepitia au wanapitia nini. Hakika waweza rudi na kushangilia kwa jinsi Mungu anavyokupenda. Mtegemee Mungu. Husiwaze kwa kuangalia uyaonayo. Songa Mbele, jitume, tembea hata ukiona shughuli yoyote ya kufanya hata kumwomba mtu umlimie garden yake, kufanya usafi fanya as extra work hupate pesa kujikimu kwa muda mfupi. Just take this as a challenge na yatapita.

Huwa napenda kuwaeleza watu hili jambo liliwahi kunitokea miaka 20 iliyopita, nikiwa na mtoto wa mwaka na nusu nipo ndani sina kazi sijui nitamlisha nini, hapo nina elimu yangu nzuri ila niliamua kuacha kazi kwa sababu ya hadha ya boss akitaka kuwa na mahusiano nami. Niliacha sikujua nifanye nini, shetani alitaka kunionesha lazima ni Obey the rule of the evil society. likini nilisema hapana na nilikataa.

Nakumbuka siku hiyo ndani nilikuwa na sh. 100 tu na unga kidogo, Bahati nyumba niliyokuwa nakaa ilikuwa na umeme hivyo pa kupikia sikuwa na shida. Nikaamua kutoka niende gengeni kununua nyanya vitunguu na nyanya chungu nitengeneze mboga angalau tule na mwanangu kwa wiki. wakati naenda gengeni nikapita mahali kuna mama anafuga kuku aliponiona na mwanangu akaniita akaniambia Lol una mtoto mzuri sana nimempenda, akamwita kijana wake wa kazi akasema ebu ingia bandani ukatafute jogoo mkubwa ukamchinjie mwanangu akanywe supu. Nilifurahi na kulia ndani kwa furaha sana. Jogoo akachinjwa nikachukua nikaenda nyumbani. Hapo huyo mama akanipa na nyanya vitunguu na viungo vingi akaniambia kachanganye umpikie mkwe supu. Sijui ilitokeaje.

Nilikula huyo kuku na mwanangu na katika hiyo wiki nilitwa kufanya kazi ya utafiti ikaniingizia kama mil 4 kwa kipindi cha miezi mitatu Kwa kweli Baraka ziliendelea nikaitwa kusoma Zaidi nikaajiriwa, nikasoma na nje mara kadhaa na Nimekuwa wa tofauti Zaidi ya nilivyojiwazia, Pia sasa namshukuru hata yule boss kwa tabia zake maana ningebweteka nisingefika nilipofikia. Hilo limebaki ni hadithi. It is not a story. Its real. Husikate tamaa, mtegemee Mungu atafungua njia. We endelee kukaa katika mstari. Husikubali ku-obey the rule of evil in this society. ita ku-cost baadaye.

Quite inspirational! Ndio maana nilimuambia kuwa kuna watu wamepitia/walipitia matatizo makubwa zaidi ya hilo lake
 
Mkuu mm sio mwandishi, nimeelezea tatizo langu kwa kadri ya uandishi wangu...na hakuna mahali nimemuomba mtu pesa, I just wanted to take this thing out of my heart...maana nimeshaanza kupata fikra za kujioverdose, nilitegemea mtanitia moyo...Sawa, wacha nisahaurike milele.


Shida yako nini mkuu?? Calm down!!! Una-react very negatively hata kwenye points za msingi zinazotolewa au kuulizwa na wadau hapa after analysing your writing. Hukutakiwa ku-pay any attention kwenye tone za hoja zao bali ulitakiwa u-respond in accordance with the content ya hoja za wanaJF wenzako. Obviously umeacha vacuum kwenye thread yako. Labda ni kwasababu ya tafsiri yako finyu ya TAKE HOME. Au may be ni kutokana na stress uliyonayo. Bro, watu wana nia nzuri sana lakini you don't seem to be humble na pia hutoi relevant responses. Kiasi kwamba majibu yako yanafanya hoja ya wale wanaodhani unasema uongo ipate nguvu. For this jilaumu mwenyewe...usilaumu reactions za watu. Naona hata sie ambao tuliamua kuwa positive kwenye ishu yako unatuweka in a serious dilemma. Kama ulikosea kitu kwenye maandishi yako it is always a sign of strength and maturity kuomba msamaha na kufafanua vizuri. Wewe ni binadamu!!

Am very ready to help you in any way lakini for now nitasubiri kwanza kusikia your objective clarifications ya issues zilizotolewa na wadau waliotangulia.
 
Mkuu, sina malezi ya upande wowote...ni wengi wameniambia hiyo sababu nimefika mahala naona life is not for me.I really wish to be courageous.
Ndugu yangu usijulaumu sana kuhusu historia yako ya nyuma maana utakufuru Mungu bila kujijua, cha msingi we ni mwanaume jikaze na usijione mnyonge sana chukulia hili tatizo kama changamoto ya wewe kusonga mbele zaidi.

Sent from my TECNO-J5 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu mm sio mwandishi, nimeelezea tatizo langu kwa kadri ya uandishi wangu...na hakuna mahali nimemuomba mtu pesa, I just wanted to take this thing out of my heart...maana nimeshaanza kupata fikra za kujioverdose, nilitegemea mtanitia moyo...Sawa, wacha nisahaurike milele.

Pumbaf kajioverdose tu, kwendraaaa
 
Mkuu mm sio mwandishi, nimeelezea tatizo langu kwa kadri ya uandishi wangu...na hakuna mahali nimemuomba mtu pesa, I just wanted to take this thing out of my heart...maana nimeshaanza kupata fikra za kujioverdose, nilitegemea mtanitia moyo...Sawa, wacha nisahaurike milele.
Ndugu johansen nataka niongeze kitu juu yako, Baada ya ule ushauri wangu wa mwanzo.

Anza kuombea Mungu akusaidie kukisikia kile unachotakiwa kukisikia, ufunguliwe masikio yako ya rohoni.
Mtu awaye yoyote aliyefungwa masikio ya rohoni huwa siku zote ni mgumu mfano hakuna. Wakuu wa giza huwa ni wajanja sana wanaanza na kuziba masikio haya ya kiroho ili usiingize kitu na usipate kufahamu, unabaki kwenye gereza hilo maisha yako yote.

Narudia tena mambo ya rohoni si mepesi, wakishayatia pamba tu hayo masikio yako ya mwilini ni kazi buree, kwani hata ungeshauriwa kwa namna yoyote ile huwezi kusikia wala kusadiki!?

Waswahili huwa wanaishia kusema sikio la kufa halisikii dawa.
Hamjawahi kushangaa hbr ya mtu mwizi aliyeona mwizi mwenzie akichomwa moto lkn baada ya muda anarudia kuiba, mtu huyu hasikii wala haoni, unabaki ukishangaa

KWENYE BIBLIA
yupo mtu mmoja aliyeonywa miaka 55 anaitwa MANASE, Soma hbr zake kwenye kitabu cha HESABU.
Hakusikia mtu huyu miaka yote 55 mpaka hapo....

Ombea Macho yako ya rohoni kuanzia sasa ili ukitazama uone.

Kumbuka wanaadam wanahitajika kubadilika kila siku kwasababu dhambi ni uasi,

Naam,
Ezekieli: Mlango wa 12:2 Mwanadamu, wewe unakaa kati ya nyumba iliyoasi, watu ambao wana macho ya kuona, ila hawaoni, wana masikio ya kusikia, ila hawasikii; kwa maana ni nyumba iliyoasi.

Hayo macho na masikio yanayozungumwa kwa ezekiel si macho ya mwilini..

Kumbuka shetani siku zote ana dili na ufahamu wa mtu huwezi kuamini!!! Rejea chezo alilochezewa Adam.
 
MUNGU akutie nguvu...katika hilo jaribu unalopitia...kikubwa hapo unahitaji kufunguliwa...
 
Back
Top Bottom