Bosi anaisambaratisha familia yangu huku nikiwa sina la kufanya

Wana JamiiForums, nawasalimu,

Note: Nadhani maelezo yangu yatakuwa marefu, lakini kama huwa husomi habari ndefu, hebu leo jisomee, nahisi unaweza kujifunza jambo au ukaona tu jinsi maisha yalivyo kwa baadhi ya watu duniani.

Naamini maneno yangu hayatasikiwa na Bots but Humans ambao ni watanzania wenzangu. Siandiki ili kukutisha au uhuzunike kutokana na hali yangu, kwasababu mimi sio mtu wa kwanza kupitia mazingira niliyonayo sasa.

Juzi nilipokea ujumbe kutoka Benki ya Exim. Ujumbe unaonyesha kuwa salio langu la mshahara kwa mwezi huu ulioisha juzi (Juni 2016) ni Tshs elfu 20 na senti kadhaa. Hii ni kinyume na makubaliano na Bosi wangu kwasababu take-home yangu inapaswa kuwa Tshs laki 9 (baada ya makato yote). Nilipomuuliza akadai kuwa ameamua kukata mkopo wote kwa pamoja (alinikopesha Tshs laki 7 kwa matumizi ya kodi ya nyumba, nauli na uhamiaji maana alinihamisha kutoka mkoani).

Anadai sababu iliyopelekea yeye kukata mkopo huo kwa pamoja kutoka kwenye mshahara wangu ni biashara yake kutoenda vizuri. Nilipomuuliza jambo hilo linahusiana vipi na utendaji kazi wangu, akadai kuwa kwenye utendaji niko vizuri, ila yeye ni msimamizi tu, kwahiyo asilaumiwe kwa maamuzi anayoyachukua.

Ndugu zangu, sikupanic kwenye kikao…lakini baada ya kuondoka (leo ni Jumamosi, tumetoka saa 7 mchana), nilihisi kuchanganyikiwa. Kwasababu ndio mshahara wangu wa kwanza na akiba yangu iliishia kwenye maandalizi ya makazi mapya maana nilijua I will settle here in this town.
Kwenye kikao chetu, nilijenga hoja nyingi kumwonyesha kuwa uamuzi wake sio sahihi maana I just got in the City (mwanza to arusha)…jibu lake ni moja tu, “He’s just doing his job, he can’t be responsible”!

Wana JF, nilipokuwa njiani kurudi kutoka kazini kuelekea nyumbani, nilihisi ni kama ninatembea kwa mguu kutoka Arusha kurudi Mwanza. Muda huu ninavyoandika, nimesimama mbele ya mashamba ya mahindi, nikiyaangalia yalivyostawi, na kulia sana, nikisema ni kheri ningekuwa mmoja wa mahindi yale. Maana tangu niokotwe kwenye mlima wa Kitangiri jijini Mwanza (nikiwa na umri wa miezi miwili tangu mama mzazi anitelekeze pale), na kulelewa kwenye Orphanages kibao ambazo kupitia wafadhili wake, niliweza kufika chuo na kujipatia taaluma, sijawahi kukumbana na mtihani mzito kama huu; nimelala nje, nimekula dampo, nimeomba omba barabarani…lakini sijawahi fikia level hii ya kuwa ugenini, as a father, as a husband, bila kuwa na cha kuwalisha wanangu (mwanangu na mke wangu wote huwa nawaita wanangu).
because, ndani hamna kitu, and there’s no way I will survive by Tshs 20 thousands. Maana kiasi hicho cha fedha huisha dakika moja tu mwanetu akipata homa usiku. Hii baridi ya Arusha ni janga kwa kichanga wetu.

Ikumbukwe kwamba wiki kadhaa zilizopita, nilileta uzi hapa jukwaani kuhusu nia ya kuitelekeza familia yangu ili nianze maisha upya, maana nilidhani pengine wao ndio chanzo cha mimi kukosa maendeleo licha ya kujituma kwa kadri ya uwezo wangu. Mlicomment sana, na wengi mlisema kwamba kuna uwezekano mkubwa kuwa mimi sijalelewa na wazazi ndio maana sina utu, hivyo sioni shida kumwacha mke na mtoto. Ni kweli mimi sikuwa na malezi ya familia, lakini maoni yenu yaliuvunja vunja moyo wangu na kufanya nimpigie magoti Abigael na kumuomba msamaha kuhusu tabia nilizokuwa nimeshaanza kuzionyesha za kutaka kuwatoroka yeye na mwanae.

Nyie niliwapa mrejeshi kwamba ninaprocess taraka, No, kwakweli nilishindwa kuimagine misha bila ya hawa wanangu…nilihisi kupotea kabisa, so nikaghaili mchakato wa taraka). Haikupita muda ndio tukawa tumehamia Arusha kwa h-ii ofa ya kazi.

Ndugu zangu, nina majuto makali, kwamba iweje nipoteze maisha ya utoto wangu kwenye uyatima, nipambane hadi niwe na familia, angalau na mimi niwe na watu wa kuita ndugu zangu…ili tu mwisho wa siku nije nidharirike ugenini, mbele ya macho ya mwanangu, kwamba nimeshindwa kumpa chakula? Mbele ya Abigael wangu, kwamba nimeshindwa kumhudumia kama jinsi nilivyomzoesha? Nina majuto makuu ambayo maneno yamdomo na kalamu hayatoshi kuyaelezea. Kama gharama ya kutua msalaba Calvary ni mauti, mimi nipo tayari kufa. I can’t hold any longer.
Kwa nia njema kama haya unayosema kweli tuwasiliane ili mimi nikupe hizo laki 7,sio kwa kukukopesha ni kukupa zawadi tu na wala sihitaji chochote toka kwako
 
Hii ishu wala sio kubwa kama unavyotaka kujiaminisha. Usipende kulialia utafikiri hii dunia umeumbiwa wewe. Duniani ni sehemu ya kupambana kwa hiyo pambana.
 
Mkuu be a man mwenzio nina miezi miwili sijapata mshahara nimeoa kama wewe na nina survive maisha ni kukomaa
 
Life of a human is of few days and full of troubles.

Wewe usitegemee maisha malaini maisha yako very rough na kama ulipitia jalalani Kweli simama kopa sehemu nyingine endelea na life.

Ina maana ukilia lia mtandaoni unafikiri itakua na tija au ni kujivua nguo?

Face someone you can trust borrow him/her some cash hata serikali inakopa ije kuwa wewe na huyo jamaa yako ameanza kuona impact ya ule wimbo wa marehemu kututahadharisha kuhusu namba.
 
Um
Wana JamiiForums, nawasalimu,

Note: Nadhani maelezo yangu yatakuwa marefu, lakini kama huwa husomi habari ndefu, hebu leo jisomee, nahisi unaweza kujifunza jambo au ukaona tu jinsi maisha yalivyo kwa baadhi ya watu duniani.

Naamini maneno yangu hayatasikiwa na Bots but Humans ambao ni watanzania wenzangu. Siandiki ili kukutisha au uhuzunike kutokana na hali yangu, kwasababu mimi sio mtu wa kwanza kupitia mazingira niliyonayo sasa.

Juzi nilipokea ujumbe kutoka Benki ya Exim. Ujumbe unaonyesha kuwa salio langu la mshahara kwa mwezi huu ulioisha juzi (Juni 2016) ni Tshs elfu 20 na senti kadhaa. Hii ni kinyume na makubaliano na Bosi wangu kwasababu take-home yangu inapaswa kuwa Tshs laki 9 (baada ya makato yote). Nilipomuuliza akadai kuwa ameamua kukata mkopo wote kwa pamoja (alinikopesha Tshs laki 7 kwa matumizi ya kodi ya nyumba, nauli na uhamiaji maana alinihamisha kutoka mkoani).

Anadai sababu iliyopelekea yeye kukata mkopo huo kwa pamoja kutoka kwenye mshahara wangu ni biashara yake kutoenda vizuri. Nilipomuuliza jambo hilo linahusiana vipi na utendaji kazi wangu, akadai kuwa kwenye utendaji niko vizuri, ila yeye ni msimamizi tu, kwahiyo asilaumiwe kwa maamuzi anayoyachukua.

Ndugu zangu, sikupanic kwenye kikao…lakini baada ya kuondoka (leo ni Jumamosi, tumetoka saa 7 mchana), nilihisi kuchanganyikiwa. Kwasababu ndio mshahara wangu wa kwanza na akiba yangu iliishia kwenye maandalizi ya makazi mapya maana nilijua I will settle here in this town.
Kwenye kikao chetu, nilijenga hoja nyingi kumwonyesha kuwa uamuzi wake sio sahihi maana I just got in the City (mwanza to arusha)…jibu lake ni moja tu, “He’s just doing his job, he can’t be responsible”!

Wana JF, nilipokuwa njiani kurudi kutoka kazini kuelekea nyumbani, nilihisi ni kama ninatembea kwa mguu kutoka Arusha kurudi Mwanza. Muda huu ninavyoandika, nimesimama mbele ya mashamba ya mahindi, nikiyaangalia yalivyostawi, na kulia sana, nikisema ni kheri ningekuwa mmoja wa mahindi yale. Maana tangu niokotwe kwenye mlima wa Kitangiri jijini Mwanza (nikiwa na umri wa miezi miwili tangu mama mzazi anitelekeze pale), na kulelewa kwenye Orphanages kibao ambazo kupitia wafadhili wake, niliweza kufika chuo na kujipatia taaluma, sijawahi kukumbana na mtihani mzito kama huu; nimelala nje, nimekula dampo, nimeomba omba barabarani…lakini sijawahi fikia level hii ya kuwa ugenini, as a father, as a husband, bila kuwa na cha kuwalisha wanangu (mwanangu na mke wangu wote huwa nawaita wanangu).
because, ndani hamna kitu, and there’s no way I will survive by Tshs 20 thousands. Maana kiasi hicho cha fedha huisha dakika moja tu mwanetu akipata homa usiku. Hii baridi ya Arusha ni janga kwa kichanga wetu.

Ikumbukwe kwamba wiki kadhaa zilizopita, nilileta uzi hapa jukwaani kuhusu nia ya kuitelekeza familia yangu ili nianze maisha upya, maana nilidhani pengine wao ndio chanzo cha mimi kukosa maendeleo licha ya kujituma kwa kadri ya uwezo wangu. Mlicomment sana, na wengi mlisema kwamba kuna uwezekano mkubwa kuwa mimi sijalelewa na wazazi ndio maana sina utu, hivyo sioni shida kumwacha mke na mtoto. Ni kweli mimi sikuwa na malezi ya familia, lakini maoni yenu yaliuvunja vunja moyo wangu na kufanya nimpigie magoti Abigael na kumuomba msamaha kuhusu tabia nilizokuwa nimeshaanza kuzionyesha za kutaka kuwatoroka yeye na mwanae.

Nyie niliwapa mrejeshi kwamba ninaprocess taraka, No, kwakweli nilishindwa kuimagine misha bila ya hawa wanangu…nilihisi kupotea kabisa, so nikaghaili mchakato wa taraka). Haikupita muda ndio tukawa tumehamia Arusha kwa h-ii ofa ya kazi.

Ndugu zangu, nina majuto makali, kwamba iweje nipoteze maisha ya utoto wangu kwenye uyatima, nipambane hadi niwe na familia, angalau na mimi niwe na watu wa kuita ndugu zangu…ili tu mwisho wa siku nije nidharirike ugenini, mbele ya macho ya mwanangu, kwamba nimeshindwa kumpa chakula? Mbele ya Abigael wangu, kwamba nimeshindwa kumhudumia kama jinsi nilivyomzoesha? Nina majuto makuu ambayo maneno yamdomo na kalamu hayatoshi kuyaelezea. Kama gharama ya kutua msalaba Calvary ni mauti, mimi nipo tayari kufa. I can’t hold any longer.
umebakia na laki mbili? Maana laki 9 toa laki 7 si inabaki laki mbili kama balance?
 
Hata mm hapa nimeshangaa!! Inakuwaje mtu mwenye take home ya 900,000 baada ya boss kukata deni Lake la 700,000 abakiwe na elfu 20 badala ya 200,000??

Kuna uongo fulani hapa
Halaf uzi wake wa nyuma aliandika analipwa vzr kama zaid ya M hivi....huyu mwongo
 
yaani niliposoma heading ya thread yako nikajua boss anatembea na mkeo hadi mke anataka talaka ili aolewe na boss huyo kumbe ni mambo madogo tu.....mwanaume kamwe usitegemee mteremko mkuu hayo mambo ya kuyumba financially mbona ni ya kawaida tu....kuna watu wanakopesha kwa riba ndogo mf. 100,000/ riba yake ni 20,000/ kakope hata laki 3 utoboe mwezi mkuu
 
Hapo juu ni unadanganya au umekosea bahati mbaya au unataka sympathy ya wanaJF ututapeli?

Kama matarajio ya mshahara yalikuwa ni laki 9 na Fedha uliyokopeshwa ni laki 7 inakuwaje ubakiwe na elfu 20 na ushee!?

Simple mathematics ulipaswa ubakiwe na laki 2.
Nina mshahara wa laki Tisa na kiasi makato yote yakifanyika nabakiwa na 720000 so probably amekosea but nimemwelewa.
 
Nikiunganisha story ya mwanzo na hii pamoja na yale maisha yako ya nyuma... Inaonyesha mkuu una VIFUNGO na vinahitaji kufunguliwa.

Vifungo ndivyo vinavyowatesa wengi na wengi wao wametembea navyo wasijue wakifikiri ni hali ya kawaida, Ufahamu na kukosa maarifa ya kutoka kwenye hivyo vifungo ndiyo shida.

Ni lazima urudi ndani kwa kina juu ya background yako sisi tunaita deep sea then mpaka hapo ulipo tukitembea kwenye Toba.

Toba kwa mke wako mtoto wako na wale walezi wako huko unazama ndani zaidi na wewe mwenyewe ukijiombea na huyo bos wako pia.

Roho ya kuzuiliwa inaonekana ndiyo inaingia kazini kwako lakini je kwa wale wakristo huwa wanaonywa juu ya sadaka, zaka, shukrani na fungu la kumi kutoka kwenye jasho lako, mana anasema Bwana Mungu mjaribuni kwa hizo uone kama hajafungua madirisha mbinguni mibaraka ishuke juu yako!..

Mana anasema pia njooni tusemezane nami nitakuonyesha mambo makubwa na magumu usiyoyajua, ikiwa hukufanya hivyo utasemezana nini na Bwana Mungu wako mana utakuwa huna kitu cha kumdai Mungu wala cha kuhojiana naye! Upo hapo.

Wewe kabla ya kuzuiliwa hiyo pesa nataka nikuambie ulishazuiliwa kitambo kwenye ulimwengu wa roho kwenye ulimwengu wa mwili ni matokeo tu na ulishachelewa kuizuia hiyo hali ndugu..

NIKUAMBIE KITU SAA HIZI.

Ezekieli:Mlango22
30 Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu.

Wameibomoa familia yako ama familia yako imeshabomoka, wamebomoa kazi yako, wamebomoa mafanikio yako mwenyewe.

NI WAKATI WA KUSIMAMA MWENYEWE KWA AJILI YA KUJENGA FAMILIA ILIYOBOMOKA, KAZI YAKO, MAFANIKIO YAKO.

Hivi vitu si vya mchezo watu wengi wanaleta dharau kwenye haya mambo... Omba yasikukute.
Asante Sana Osie Shemkunde
 
Nina mshahara wa laki Tisa na kiasi makato yote yakifanyika nabakiwa na 720000 so probably amekosea but nimemwelewa.

Unajua kusoma au unaleta ujuaji tu?

Hebu nenda karudie kusoma uone alichoandika kama kinaendana na ulichoandika wewe
 
Hapo juu ni unadanganya au umekosea bahati mbaya au unataka sympathy ya wanaJF ututapeli?

Kama matarajio ya mshahara yalikuwa ni laki 9 na Fedha uliyokopeshwa ni laki 7 inakuwaje ubakiwe na elfu 20 na ushee!?

Simple mathematics ulipaswa ubakiwe na laki 2.
Sure...hata mi nimenusa utapeli
fulani hivi...

Story yake haiko clear...kichwa cha habari na story haviendani

Je hakuna hata mfanyakazi wa hapo wa kumkopesha? Huko Mwanza alipokuwa hakuwa na rafiki? Wafanyakazi wenzie wa Exim Mwanza wako wapi????
 
Pole sana ndo maisha. Kopa kwa wafanyakazi wenzio, hata robo ya mshahara usukume siku, mwezi ukiisha unasonga mbele.
 
yaani niliposoma heading ya thread yako nikajua boss anatembea na mkeo hadi mke anataka talaka ili aolewe na boss huyo kumbe ni mambo madogo tu.....mwanaume kamwe usitegemee mteremko mkuu hayo mambo ya kuyumba financially mbona ni ya kawaida tu....kuna watu wanakopesha kwa riba ndogo mf. 100,000/ riba yake ni 20,000/ kakope hata laki 3 utoboe mwezi mkuu
Hahahahaha hata mi nilidhani boss amemchukuwa mkewe kisha amemfukuza kazi
 
Back
Top Bottom