Boniface Mwabukusi aapishwa kuwa Rais wa TLS. Aanza kazi rasmi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,637
55,332
Wakili Mwabukusi aapishwa rasmi kuwa Rais wa chama cha Wanasheria Tanganyika.

Wakili Boniface Mwabukusi ataendesha chama cha Wanasheria Tanganyika kwa Miaka mitatu.

Uapisho huo umefanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Wakili Boniface Mwabukusi alitangazwa kuwa Mshindi wa Urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) akiwashinda Wanasheria wengine watano waliokuwa wakiwania nafasi hiyo

Mwabukusi alishinda kwa Kura 1,274 huku Sweetbert Nkuba aliyekuwa akipewa nafasi kubwa ya kushinda akifuatia kwa Kura 807. Kwa matokeo hayo, Mwabukusi anakwenda kukiongoza Chama hicho cha Wanasheria kwa kipindi cha miaka mitatu.

Mawakili wengine waliokuwa wakiwania nafasi hiyo ni Kapt. Ibrahim Bendera aliyepata Kura 58, Paul Kaunda aliyepata Kura 51, Emmanuel Muga aliyepata Kura 18 na Revocatus Kuuli aliyepata Kura 7

HOTUBA YA WAKILI MWABUKUSI

Your browser is not able to display this video.

Pia, soma; Wakili Sweetbert Nkuba kupinga ushinda wa Wakili Boniface Mwabukusi kuwa Rais wa TLS
 
Asante kwa taarifa.
 
KAKAMATA NINI MKONO WA KUSHOTO?
 
Sasa mbona kashika Biblia kwa mkono wa kushoto?
Surat Al-Haqqa (69:25-26):
  • "Na ama yule atakayepewa kitabu chake kwa mkono wake wa kushoto, atasema: ‘Laiti nisingalikuwa nimepewa kitabu changu.’"
  • "‘Wala nisingalijua hesabu yangu.’"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…