Bongo Movies wengi ni vilaza, si ajabu wameilaza sanaa ya uigizaji. Wasomi ingieni huko

Niliona sinema moja hivi wanaonyesha mhusika akikumbuka matukio ya mwaka 1990. Kituko ni pale mhusika anapanda Bajaj, gari lina namba hizi za sasa za T...
Nakubaliana na uzi huu.

Watu wanaweza wakadhani unatania Mkuu kumbe ni kweli
 
Kmmk umeongea nondo tupu ki uhalisia hii industry imejaa misukule na vibuyu ina watu wa ajabu sana.Hii industry ningetamani ivamiwe na wasomi wanaolalamikia ajira kuna fursa ya kufa mtu.MI NIMEPIGA MARUFUKU KWANGU KWENYE SMART TV YANGU HAPA SEBULENI KUANGALIA USHUZI UNAOITWA BONGO MOVIES...eti utasikia wanasema HAKIKA NI ZA KWETU mama.eeee

Unajua uigizaji unahitaji akili iliyochangamka, uwezo wa kumficha mtazamaji nini kinafuata, lakini bongo movies wao picha likianza tuu ukishaona baadhi ya wahusika tayari ushajua mwisho wa filamu
 
Halafu usiombe muigizaji wa bongo muvi aanze kuwaza utashangaa anawaza halafu ndani ya mawazo anaanza kuwaza tena.

Lakini mi hii tasnia nafikiri haiwalipi ndiyo maana wanaboronga. Kazi zao zinaibwa sana. Wizara husika inatakiwa kuangalia namna ya kuinua hii tasnia sababu kama tukifanya vizuri tutaishika vizuri East Africa na DRC.

:D:D:D

Zinaibiwa kwa sababu wengi uwezo mdogo
 
Mtoa mada umeongea Jambo la mbolea Sana , nilifatilia CV ya Michael Scofield kwenye series ya Prison Break ,aisee jamaa mpak ana master's ya uigizaji , yaani kiufupi Tu Holywood huwez kupewa script kama shule ni zero kichwani.

Bongo movie hawana jipya Kwa sababu ni poor in education , hebu niambie kama kuna kipande cha kuiendesha ndege au meli nani atacheza ?.? Hata masuala ya ku-crack code za Mawasiliano hcho kipengele Nani atacheza ?? Wanabaki Tu na vitu normal kama Mapenzi , kuendesha vigali basi.

Wewe mpaka sasa hakuna aliyeigiza filamu kisiasa, na hii ni kutokana hawana Idea na hayo mambo.

Hakuan filamu za migomo na maandamano,
Hakuna filamu za chuoni zaidi ya kudhani kuwa chuoni ni sehemu ya starehe kazi kuvaa nguo za uchi, ajabu sana hii
 
Umeongea vizuri..chuo cha sanaa Bagamoyo kinao na kinatoa wataalamu. Naunga mkono hoja ya faza nelly ya ukosefu wa mitaji.
Angalia sinema zile za miradi mfano malaria au uzazi ambazo zinakuwa na ufadhili mzuri zinakuwa bora kwa kuwatumia waigizaji wale wale lakini wanakuwa kwenye uangalizi na waongozaji waliosomea. Ukitaka kuthibitisha hili angalia sinema ya CHUMO.

Mitaji sio shida mkuu.

Hizo hizo filamu wanazoigiza mbona wanaigiza utumbo mtupu?

Shida ni shule Mkuu,
Mtunzi hana shule
Muongozaji hana shule
Mtayarishaji hana shule
Mchukua kamera hana shule
Waigizaji hawana shule unategemea nini hapo?

Hizo filamu zingine kama Siri ya Mtungi, Chumo zimeongozwa na watu wenye shule,
 
Ni kweli kabisa mambo mengi ambayo hata si ya kibajeti kiviile wanakuwa hawako makini nayo kama vile subtitle kwa lugha ya kiingereza wanachapia sana.

Embu angalia Series nyingi za Kikorea au Kifilipino Bajeti ni yakawaida, mazingira ni ya dailojia tuu lakini filamu zao zinakuwa nzuri, embu angalia Wanaijeria halikadhalika
 
Mkuu jinsi ulivyo tukandia sisi vilaza ni wazi kuwa unachuki nasisi na sio filamu. Kwa hiyo tulipokimbia shule na kuwaacha nyie majinias iliwauma eee? mlitegemea maisha yatuchape siyo?
 
Acheni kuwasakama bongo movies. Sababu ni zile zile;

1.Lack of capital. Stori inahitaji props zinazoendana na script lakini Bajeti ni Tsh. 400,000. Unategemea nini ?

2. Lack of/No Government support. Serikali inataka wasanii wasajili Drones kila unaposhoot hata scene moja kwa sababu za kisiasa. Ukienda kuomba location ya kituo cha Polisi unanyimwa, mahakamani unanyimwa, ofisi ya umma unanyimwa na stori inahitaji uhalisia. Kuvaa sare za askari ni tatizo, mlolongo ni mrefu na hauna matumaini. Unategemea ubora?

3. Poor tools and equipments. Vifaa vya wenzetu ni professional zaidi. Camera na Lens ni cinematic, vifaa vya kuongeza effects CGI etc.

etc. etc.

Mkuu hizo hizo wanazoigiza zenye bajeti ndogo mbona hakuna wanachofanya.
Hivi unafuatilia filamu za kikorea au kifilipino?
Yaani kuna filamu ukiiangalia tuu ukiikadiria bajeti yake sio kubwa haina mambo mengi, lakini filamu inakuwa nzuri,

Haya niambie Kanumba aliwezaje?
 
..Yule jamaa Idrisa Sultan alianza kujitahidi kuweka mambo sawa.....hakuna kitu inakera na wakati huo huo kuumiza kama kuangalia bongo movie...hakuna uhalisia hata kidogo.....kwa Bongo movie siku zote Gateman lazima awe kama taahira fulani hivi..sijui wamejifunza wapi?

Yaani mambo ya ajabu sana, yaani wale walinzi wa Suma Jkt ndio wapo hivyo?

Mtu na akili yake anawezaje muajiri mlinzi tahahira au comedy, sijui waliipata wapi hiyo
 
Tatizo la wasanii wa bong fleva nililelile linalo kumba wachugaji wa kilokole born again christians wengi ni vilaza school drop-out wa form 2 form 4 na dalasa 7 ... eti mtu anakupa baraka anakemea mapepo nk.

Hao watu wameharibu sana dini za watu na familia za watu kwasabab hawana uwezo wa kuchambua na kuelewa bibilia vizuru wanapotosha wengi na wanawatumia wengi.........

Shida ndio ilipo hapa,
 
Wasomi tunatamani sana kuingia humo tatizo wenyeji wana majungu, fitna, roho mbaya, chuki, husda na zaidi ulozi,

Tunaogopaaaa.

Soko lao litakuwa mashakani,

Embu angalia ile Movie ya The Dance aliyoigiza Irene Uwoya, Idea ilikuwa nzuri lakini Uwoya ile movie aliyumba hasa kwenye kipengele cha mawasiliano kwa kutumia kingereza
 
Back
Top Bottom