BBC: Korea Kaskazini kupata tani 700,000 za mchele kwa kupeleka silaha na wanajeshi Urusi

5523

JF-Expert Member
Nov 13, 2014
2,120
2,170
Kwenu wadau njaa mbaya:

pputin.jpg

Gazeti la Korea Kusini la Korea Herald linaripoti, likimnukuu balozi wa zamani wa Korea Kusini nchini Urusi, kwamba badala ya usambazaji wa risasi na kutuma wanajeshi kushiriki katika vita vya Urusi na Ukraine, viongozi wa DPRK watapokea kutoka Moscow takribani tani 600-700 za mchele kwa mwaka na upatikanaji wa teknolojia ya anga.

Balozi wa zamani Wi Song-lak, ambaye alipokea taarifa kutoka kwa kamati ya kijasusi ya Korea Kusini, alisema kwamba siku za nyuma Moscow iliipatia Pyongyang tani 50,000 hadi 100,000 za mchele kwa mwaka, lakini sasa mahitaji yataongezeka hadi 600,000- tani 700,000.

Korea Kaskazini inasema inazalisha takribani tani milioni 4 za nafaka kila mwaka, lakini hiyo ni takribani tani milioni 1 pungufu ya kile inachohitaji, Wi Song-lak alisema.

Kwa hivyo vifaa kutoka Urusi vinaweza kusaidia Pyongyang kujaza upungufu wake wa nafaka kwa zaidi ya nusu. Urusi pia inaisaidia Pyongyang, ambayo inajiandaa kurusha satelaiti mpya ya kijasusi, yenye teknolojia ya hali ya juu ya anga, kulingana na maafisa wa Korea Kaskazini.

Lakini sehemu muhimu zaidi ya makubaliano na Moscow, kulingana na balozi wa zamani, ni ukweli kwamba Pyongyang ilipata msaada wa kijeshi wa Urusi katika tukio la vita kwenye Peninsula ya Korea.

"Korea Kaskazini, ilipigana upande wa Urusi. Ikiwa vita vitatokea kwenye Rasi ya Korea, Korea Kaskazini inaweza kutegemea Urusi kuja kusaidia," Wie alisema.

Kulingana na mamlaka ya Ukraine na Magharibi, DPRK imetuma takribani wanajeshi 10,000 nchini Urusi, ambao hivi karibuni wanaweza kutumwa kwenye vita vya Urusi na Ukraine.

Miji mikuu ya Kyiv na Magharibi pia inasema kwamba Pyongyang imeipatia Urusi kundi kubwa la makombora ya mizinga.

Hivi karibuni, Rais wa Urusi Vladimir Putin hakukanusha kutuma wanajeshi wa Korea Kaskazini nchini Urusi, akisema kuwa pande hizo zitashirikiana ndani ya mfumo wa makubaliano ya ushirikiano uliohitimishwa hivi karibuni kadri watakavyoona inafaa.
 
Hizo ni propaganda!

Jeshi bila uzoefu wa vita halisi bado linakuwa si jeshi kamili.

Kutumia mazoezi na mbinu walizofundishwa kwenye eneo halisi la vita ndipo jeshi linaimarika.

Korea ya Kaskazini mwisho wa kupigana vita halisi na vya kisasa ni kwenye vita vya wakorea wenyewe.

Korea ya kaskazini imeomba wapeleke wanajeshi wake kwenye vita ya Ukraine ili wapate uzoefu wa vita hususani ya kisasa inapigwanaje na kuangalia ubora wa zana zap upoje kwenye vita kamili.

Si Korea bali hata China ilipeleka vijana wake hususani kwenye urban warfare.

Hii hali inamuogopesha Korea ya Kusini ndiyo maana anatapa tapa!
 
Huo ni Ushirikiano Mzuri sana! Kubadilishana silaha kwa Ngano.
Hata hivyo huenda ni propaganda za hasimu wake South Korea.
Russia wana nafaka ya kumwaga! Imeshagawa bure tani nyingi za ngano kwa nchi maskini za Afrika.
North Korea Kuna njaa sana mkuu usikatae
 
Huo ni Ushirikiano Mzuri sana! Kubadilishana silaha kwa Ngano.
Hata hivyo huenda ni propaganda za hasimu wake South Korea.
Russia wana nafaka ya kumwaga! Imeshagawa bure tani nyingi za ngano kwa nchi maskini za Afrika.
Kuna kipindi vijana wa Tz kwenye operation moja walichakazwa kwa urahisi.

Sababu ilikuwa walishindwa kutumia kikamilifu zana walizopatiwa na jambo likarekebishwa na hii ndiyo umuhimu wa operation linalijenga jeshi na kuwa imara zaidi kwenye uwanja wa mapambano.

Ndicho kinachotokea kwa Korea ya Kaskazini. Ni lazima atest ubora wa silaha zake kwenye vita kamili akikabiliana na adui zipoje? Mbinu zake zipoje? Ukizingatia vita ya Ukraine inapiganwa kisasa. Hivyo jeshi la Korea ya Kaskazini lina imarika zaidi.

Hii hali inamuogopesha Korea ya Kusini, kwa sababu mwenzake anapata ubora halisi wa kijeshi na si yeye anayepata ubora wa kwenye training ambao hauna tofauti na mwigizaji.

Kwa kuzingatia hayo naye ameomba kupelekea vijana wao Korea Kusini Ukraine kwa upande wa Nato.

Hali ilivyo mbaya Russia amekuwa akiwafyeka hawa majenerali wa Nato huko Ukraine imma wakiwa kwenye vikao hotelini au kwenye mahandaki.
 
Hizo ni propaganda!

Jeshi bila uzoefu wa vita halisi bado linakuwa si jeshi kamili.

Kutumia mazoezi na mbinu walizofundishwa kwenye eneo halisi la vita ndipo jeshi linaimarika.

Korea ya Kaskazini mwisho wa kupigana vita halisi na vya kisasa ni kwenye vita vya wakorea wenyewe.

Korea ya kaskazini imeomba wapeleke wanajeshi wake kwenye vita ya Ukraine ili wapate uzoefu wa vita hususani ya kisasa inapigwanaje na kuangalia ubora wa zana zap upoje kwenye vita kamili.

Si Korea bali hata China ilipeleka vijana wake hususani kwenye urban warfare.

Hii hali inamuogopesha Korea ya Kusini ndiyo maana anatapa tapa!
Kwanini hukuangazia mambo mawili
1. North korea kukumbwa na balaa la njaa kutokana na uchumi duni wa nchi yao mpaka kufikiria kuuza roho zao ili wapate chakula kwa watu wao.
2. Russia kuishiwa ama kupungukiwa na wanajeshi kuendelea na vita ya Ukraine ambayo inazidi kuwagarimu muda kuliko matarajio.
 
Kuna kipindi vijana wa Tz kwenye operation moja walichakazwa kwa urahisi.

Sababu ilikuwa walishindwa kutumia kikamilifu zana walizopatiwa na jambo likarekebishwa na hii ndiyo umuhimu wa operation linalijenga jeshi na kuwa imara zaidi kwenye uwanja wa mapambano.

Ndicho kinachotokea kwa Korea ya Kaskazini. Ni lazima atest ubora wa silaha zake kwenye vita kamili akikabiliana na adui zipoje? Mbinu zake zipoje? Ukizingatia vita ya Ukraine inapiganwa kisasa. Hivyo jeshi la Korea ya Kaskazini lina imarika zaidi.

Hii hali inamuogopesha Korea ya Kusini, kwa sababu mwenzake anapata ubora halisi wa kijeshi na si yeye anayepata ubora wa kwenye training ambao hauna tofauti na mwigizaji.

Kwa kuzingatia hayo naye ameomba kupelekea vijana wao Korea Kusini Ukraine kwa upande wa Nato.

Hali ilivyo mbaya Russia amekuwa akiwafyeka hawa majenerali wa Nato huko Ukraine imma wakiwa kwenye vikao hotelini au kwenye mahandaki.
Mkuu mada hapo juu inaeleza ilibidi North Korea akauze roho za wanajeshi wake ili apate mchele asitirike kutokana na njaa wewe unazungumza kupata uzoefu na silaha., hao north korea silaha zao zishatumika sana Ukrean lakini Urusi kashindwa kutoboa sasa mwaka 3, North Korea wao wanalia njaa Urusi wao jeshi hawana kuendela na vita, wanapigana kwa hasara
 
Mkuu unaijua njaa?

Tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990 North Korea ilisemwa kuna njaa mpaka sasa hivi mwaka 2024 habari ni zilezile!

Njaa hii hii tunayoijua sisi au njaa nyengine?
Njaa ya msosi mkuu, Kuna kipindi waliomba walegezewe vikwazo ili wasitengeneze silaha za maangamizi kwa msaada wa chakula
 
Mkuu mada hapo juu inaeleza ilibidi North Korea akauze roho za wanajeshi wake ili apate mchele asitirike kutokana na njaa wewe unazungumza kupata uzoefu na silaha., hao north korea silaha zao zishatumika sana Ukrean lakini Urusi kashindwa kutoboa sasa mwaka 3, North Korea wao wanalia njaa Urusi wao jeshi hawana kuendela na vita, wanapigana kwa hasara
Kwa mwonekano wa nje inaonekana hivyo kwa sababu ndicho kitu kinachopendwa kuzungumziwa ila kwa mwonekano wa ndani ndivyo hivyo nilivyoandika.

Itafsirike kuwa wamefanya mabadilishano ya wanajeshi na chakula kwa sababu ya njaa ila dhamira ni tofautu.

Ukitaka kufahamu zaidi tafuta interview za majenerali wastaafu wa Jwtz waliulizwa swali kuna umuhimu gani wa kupeleka wanajeshi wetu kwenye operation ambazo hata hazituhusu, utapata jawabu.
 
Unafahamu kwamba hata China watu wake wapo kule Russia kwenye mgogoro wake na Ukraine?

Hili nalo unalitafsiri vipi?
Mkuu hayo ya China siyajui nilitaka kumweleza mdau aliyeshangaa North Korea kupewa Mchele.
 
Kwanini hukuangazia mambo mawili
1. North korea kukumbwa na balaa la njaa kutokana na uchumi duni wa nchi yao mpaka kufikiria kuuza roho zao ili wapate chakula kwa watu wao.
2. Russia kuishiwa ama kupungukiwa na wanajeshi kuendelea na vita ya Ukraine ambayo inazidi kuwagarimu muda kuliko matarajio.
Kuhusu suala la vita baina ya Ukraine na Russia wasomì tofauti wameshaliongelea vya kutosha na majenerali wa Nato kwa nyakati tofauti wameshaliongelea vya kutosha kuwa Ukraine imeshashindwa na hakuna popote taarifa ya kuonesha Russia kupungukiwa na wanajeshi kwenye mapambano yake na Ukraine na wakatoa na ratio baina ya kuuawa kwa wanajeshi wa Russia na Ukraine.

Juzi kati ama mwezi uliyopita ulifanyika mdahalo wa wasomi Prof Jeffrey Sachs na Prof john mearsheimer wamelizunguzmia hili kwa mapana na conclusion yao na uhakika wa mambo ni tofauti na yako kabisa.

Juzi kati taarifa ya kijasusi ya Ujerumani imesema Russia imejipanga na hii vita mpaka miaka 3 mbele yaani 2027 kitu ambacho wao hawakukitarajia.

Sasa sijui wewe takwimu zako unazitolea wapi?

Nukta namba 1 nimeshakujibu kwenye post nyengine.
 
Kwenye mdahalo Urusi ishashinda vita lakini kwenye uwanja wa vita Russia inakodi askari kutoka North Korea wakivalia uniform za russia na zaid ya elfu10 wametumwa urusi kwenye maeneo ya mpakani na Russia kuikomboa Kurks, haya yote tunaita wamekuja kupata mafunzo eti?

Professor aliekaa kwa kiti na meza ambaye ni pro-russia anakuaminisha ww uliye huko ufipa na umejifungia hujui na hutaki kujua chochote kwenye uwanja wa vita.,

Vita haipimwi kwa maneno matupu mdomoni ata kabla ya vita russia alijiita super power na kwamba atamaliza operation yake na ukrean kwa saa 72 tu.

Sikuizi amebadilisha neno operation anaviita vita, yeye mwenye putin anaviita vita lakini ww unasema sio vita ww na proffesor wako munasema kaz imeisha., ni vile wafuatq mkumbo
 
Back
Top Bottom