Basi la Falcon latekwa na majambazi ktk mlima sekenke

Magezi

JF-Expert Member
Oct 26, 2008
3,359
701
Kuna taarifa kwenye website ya Ippmedia.com kuwa basi la abiria la Falcon limetekwa ktk mlima sekenke na abiria kuporwa ikiwani pamoja abiria nane kujeruhiwa na dereva kukatwa mkono.

Tunaomba mwenye details zaidi atujuze
 
Kuna taarifa kwenye website ya Ippmedia.com kuwa basi la abiria la Falcon limetekwa ktk mlima sekenke na abiria kuporwa ikiwani pamoja abiria nane kujeruhiwa na dereva kukatwa mkono.

Tunaomba mwenye details zaidi atujuze
Pole kwa majeruhi na WAHANGA wa tukio hilo, pale sekenke ni pabaya mno. Kabla hujapanda pale huwa kuna barrier ya polisi sijui imekuwaje.
 
kwa nini wanashindwa kuzuia iujambazi mkuu.. hapa naongelea generally...au unajua kuwa majambazi wakikuvamia nyumbani kwako na ukawapigia hawa jamaa simu wanakujaga saa ngapi?
Haya Kamanda... Ila upunguze mizaha kwenye mambo sensitive....
 
Vipi kuhusu ule utaratibu wa askari polisi kusindikiza magari ya abiria yanaelekea huo ukanda. Umefutwa?
 
:A S-fire1:poleni wahanga wa mkasa huu...............ule utaratibu wa polisi kusindikiza magari ya abiria sio wa kutegemea sana kwa sababu sehemu nyingine polisi wanakula njama na hawa watekaji..................
 
kwa nini wanashindwa kuzuia iujambazi mkuu.. hapa naongelea generally...au unajua kuwa majambazi wakikuvamia nyumbani kwako na ukawapigia hawa jamaa simu wanakujaga saa ngapi?
Wakipokea simu unabahati na wakishapokea simu watajidai hawajui sehemu ulipo vamiwa na ukiwaelewesha watachukua hata saa mbili ndiyo wanakuja sehemu ya tukio.....lakini wameonyesha usitadi wa kurusha risasi za moto kwawandamaji na wale walio kuwa wanadai haki zao kule mbeya.....sasa miminawaomba huo usitadi wao wakurusha risasi za moto wazielekeze kwa majambazi...
 
poleni jamani hali hii mpaka lini pls jeshi ingilia kati tokomeza karaha hii
 
Badala ya baadhi ya watu kuchangia hoja kwa kuleta faida wao wanaleta utumbo!Kuweni na busara acheni ujinga!
 
kwani hao MAJAMBAZI ndio wanaotaka kutuibia kupitia DOWANS? nadhani hawana tofauti ndio hao hao wamezaana sana mpaka wengine wapo milima ya SEKENKE?
 
Ni kilomita chache tu kuingia jimbo la Rostam, barabara ni nzuri ya lami ila ule mteremko lazima uende taratibu labda hapo ndipo majambazi wanapotumia kukamata magari.

Lakini ile barabara kwa sasa ina magari mengi sana hasa ya mizigo naamini kuletaka gari ndani ya dakika kumi lazima katokee ka songamano fulani ka magari.
 
Back
Top Bottom