Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,732
- 13,485
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus anatarajiwa kuzungumza na Wanahabari (Wahariri na Waandishi wa Habari), Ikulu ya Dar es Salaam, leo Alhamisi Februari 22, 2024
Endelea kufuatilia kitakachoendelea...
Zuhura Yunus:
Rais Samia Suluhu Hassan alifanya ziara Vatican ambapo alikutana na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Francis, Mjini Vatican pamoja na Katibu Mkuu wa Vatican.
Ziara ilikuwa nzuri na kikubwa ilikuwa kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia na maendeleo kati ya Tanzania na Vatican.
Sehemu ya mazungumzo mengine yalihusu Elimu, afya na huduma za maji ambayo Vatican wameyapa kipaumbele katika uhusiano wake Nchini Tanzania.
Rais Samia alishukuru ufadhili wa kada mbalimbali unaotolewa na Vatican.
Rais Samia alipendekeza uongezwe wigo wa ushirikiano ikiwemo katika ufundi stadi baina ya pande zote mbili.
Ziara ya Norway
Baada ya kutoka Vatican, Rais Samia na msafara wake walielekea Norway na kupokelewa na Mfalme, hii ilikuwa ziara ya kihistoria kwa kuwa kiongozi wa mwisho wa Tanzania kufanya ziara alikuwa Baba wa Taifa Julius Nyerere.
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Zuhura Yunus akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 22 Februari, 2024.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Vyombo mbalimbali waliohudhuria mkutano ulioandaliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jijini Dar es Salaam, tarehe 22 Februari 2024.
Waziri wa Kilimo, Hussein Mohammed Bashe:
Tunaanza kusajili madalali wa mazao
Ukuaji wa zao la Tumbaku Nchini Tanzania ni tishio kwa nchi jirani, leo tunazidiwa na Nchi moja tu Barani Afrika ambayo ni Zimbabwe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Alexander Mkumbo
Kuhusu umuhimu wa ziara katika suala la uwekezaji, uwekezaji ni mchakato huwezi kutegemea majibu ya papo kwa hapo.
Mfano Rais alifanya ziara Nchini China Mwaka 2021, kutokana na ziara hiyo kutoka China kuna viwanja viwili vikubwa hapa Nchini.
Mfano mwingine Rais alifanya ziara Misri ambayo iliwezesha uanzishwaji wa kiwnada cha Nyaya na transfoma na vifaa vingine vya umeme.
Ziara ya Indonesia imesababisha kuna kampuni kubwa kutoka Indonesia inakuja kufungua kiwand cha mbolea Mtwara ambayo itakuwa inatengenezwa kwa njia ya gesi.
Pia Indonesia tumekubaliana wanakuja kufungua viwanda vya sukari, jambo zuri ni kuwa tunatakiwa kuwa na usambazaji ili hata mambo ya bei elekezi yanakuwa hayapo
Hizo bei elekezi ni mkakati wa muda wa mpito.
Naibu Katibu Mkuu: Sanamu ya Nyerere imefanana naye kwa 92%
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaibu Mussa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba
Kuna tatizo kubwa la wizi wa mafuta ya Transfoma hasa maeneo ya Temeke, Mbagala na Kigamboni, inapotokea hivyo transfoma inaungua na kusababisha watu zaidi ya 100 waliounganishiwa umeme.
Kuhusu uhaba wa sukari Nchini
Waziri wa Kilimo, Hussein Mohammed Bashe anasema: Tuna tatizo la upungufu wa sukari Nchini, hatujawahi kuwa na changamoto kama ilivyo sasa, hii naifananisha na ilivyotokea mwaka 2017/18.
Baada ya mvua za el nino, gape yetu imeshuka kutoka laki mbili hadi 30,000 mwaka 2023, hapa nazungumzia msimu wa kilimo, tulihitaji taki 490,000 tukazalisha Tani 460,000, tukaingiza Tani 30,000
Mwaka huu tulitarajia kuzalisha Tani 550,000, pia tulitoa vibali vya kuingiza Sukari kiwango kisichopungua Tani 100,000.
Mpaka sasa sukari iliyopo Bandarini na iliyoanza kusambazwa ni wastani wa Tani 31,000.
Rais alitoa ruhusha ya kuagiza Tani 100,000 lakini sasa sukari tutakayoingiza ni zaidi ya Tani 300,000 kwa kuwa tumeona hali ya mashamba, tutaendelea kuingiza sukari kutoka nje.
Tunaamini hadi kufika Machi 15, 2024 tutakuwa tumeingiza Sukari Tani 60,000, tunataraji wakati wa Mfungo w Ramadhani kutakuwa na uimara kiasi fulani.
Hadi sasa tumekamata Wafanyabiashara 84, tupo kwenye hatua za mwisho kuwapeleka Mahakamani, sukari inaingia anauziwa 2,500 hadi 2,800, yeye akinunua anaenda kuuza kwa Tsh 4,000.
BASHE: WAFANYABIASHARA WA SUKARI WACHAGUE KUUZA AU KUACHA, TUMEWALINDA VYA KUTOSHA
Akifafanua kuhusu changamoto ya Sukari Nchini, Waziri wa Kilimo, Hussein Mohammed Bashe amegusia kuhusu Serikali kufanya mabadiliko ya biashara ya sukari na kuruhusu ushindani wa biashara hiyo kwa wawekezaji wa ndani na wa nje ya Nchi
BASHE: TUMEKAMATA WAFANYABIASHARA 84 WA SUKARI
Waziri wa Kilimo, Hussein Mohammed Bashe akifafanua kuhusu uhaba wa Sukari Nchini na hatua ambazo Serikali inachukua, akielezea pia kuhusu baadhi ya Wafanyabiashara wanaouza bei tofauti na iliyoelekezwa na Serikali.
Waziri wa Kilimo, Hussein Mohamed Bashe akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Vyombo mbalimbali waliohudhuria mkutano ulioandaliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 22 Februari, 2024.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba Katibu Mkuu akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Vyombo mbalimbali waliohudhuria mkutano ulioandaliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 22 Februari, 2024.
Balozi Shaibu Said Musa - Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza na Wahariri wa Vyombo mbalimbali waliohudhuria mkutano ulioandaliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 22 Februari, 2024.