Ndugu zangu Watanzania,
Huwezi kuzuia Upendo wa watu kwa CCM,huwezi kuzuia mahaba waliyonayo watanzania kwa CCM,huwezi kuficha hisia za upendo walizonazo watanzania kwa CCM.hiki chama kinapendwa kuliko asali.hiki chama kinakubalika kuliko pesa ya mmarekani, hiki chama kimebeba matumaini ya watanzania.
CCM inapendwa utafikiri watanzania wote wamenyonya na kunywa maji ya bendera ya CCM.ni furaha ,shangwe, tabasamu, nderemo, vifijo,hoihoi , chereko chereko kila viongozi wake watuapo mahali fulani.
Sasa leo ilikuwa ni zamu ya mkoa wa Shinyanga ambapo bingwa na nguli wa Diplomasia na jasusi Mbobevu aliongoza wajumbe wa Secretarieti kukanyaga ardhi ya Mkoa wa shinyanga.ambapo yeye na wajumbe hao akiwepo Mwenezi Taifa Mheshimiwa CPA Amos Gabriel Makalla bingwa wa mahesabu na uhasibu na wenye kufanya siasa za kisayansi walipata mapokezi ya kifalme na mazito sana kuwahi kushuhudiwa mkoani hapo.
Ambapo watu walifurika na kumiminika kwa wingi Utafikiri kama mchanga wa bahari,ambapo hata sisiminzi asingeweza kupata nafasi ya kupenya na kupita.
Hii maana yake nini ndugu zanguni? Hii maana yake ni kuwa watu na watanzania wote wana imani na matumaini Makubwa sana na chama cha Mapinduzi. Wana matarajio makubwa kutoka CCM na wanaamini ndio chama pekee chenye uwezo wa kuwaongoza na kuwakwamua kiuchumi pamoja na kuwaletea maendeleo.ndio maana wana furika kwa wingi kusikiliza nini kimebebwa na viongozi wao kutoka makao makuu ya chama.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.