Bajeti 2016/2017 imebakiza miezi mitatu muda wake uishe,je imeleta mabadiliko huko kwenu?

Huwezi ukaendesha nchi kwa makusanyo ya kodi trilioni 12 hadi 15 huku ukidai bajeti ni 29 trillion. Mbaya zaidi hii Serikali ilivyo na usiri mkubwa hatutajua katika bajeti ya 29 trilioni 2016/2017 kiasi halisi cha pesa kilichotolewa ni kipi.

Bajeti ambayo haikuridhiwa na bunge inaonyesha matokeo yake maamuzi ya kupuuzia utawala wa Sheria Ni haya to sana.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Imeleta mabadiliko makubwa sana. Hongera magufuri.
1. Maisha yamekua magumu sana.
2. Biashara zinaendelea kufungwa.
3. Ajira umekua ni msamiati mpya.
 
Na Trump anaongeza bajeti ya ulinzi na kupunguza bajeti ya misaada kwa nchi za nje...ile surplus anaipeleka kwenye ulinzi. Zile ndoto za MCC na madudu.menguine ndo kwaheri
 
Na Trump anaongeza bajeti ya ulinzi na kupunguza bajeti ya misaada kwa nchi za nje...ile surplus anaipeleka kwenye ulinzi. Zile ndoto za MCC na madudu.menguine ndo kwaheri
Ni shida
 
ARUSHA sombetini kabla ya bajeti tulikuwa tunapata maji kwa wiki Mara 2 lakini baada ya bajeti kuidhinishwa mpango Wa maendelezo ya maji Arusha mjini .sasa hivi maji tunapata Mara moja kwa mwezi kwa muda Wa masaa mawili
Na mbaya zaidi mbunge wetu Lema yuko ndani
 
Kule kwetu kolomije hakuna mradi mpya mtoto wa mjomba hajapata mkopo maji hayatoki japo ziwa lipo karibu halizidi km 100 mengine tumuachie daudi bashite
 
watu wanataka vyeti vya bashite ..masuala ya maendeleo hawana muda nayo...
 
Tanzania ya viwanda! Ni nani aliyewadanganya kuja ya sera ya ovyo namna hii???? Miaka ya 1970 - 1980s Tanzania ilikuwa na viwanda vingi kuliko sasa. Lakn serikali ya wakati huo haikuwahi kutamka kama ni ya viwanda. Tena viwanda vyote vilikuwa na base, yaani kulikuwa na kilimo cha mazao makubwa yaliyokuwa yana-support viwanda hivyo. Kuna watu hawajui kwamba Tanzania ilishakuwa nchi ya kwanza kwa zao la Mkonge duniani! Kahama, korosho, chai, pamba nk yalikuwa mazao makuu katika nchi yetu na yalitoa msukumo mkubwa wa kuwepo kwa viwanda wakati huo. Viwanda vya sasa vitachipuka kutoka mbinguni?????
 
Kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ni vigumu sana kuliko kushughulikia vyeti feki vya akina Daudi Bashite. Kwa nini tusianze kwanza na mambo ambayo ni rahisi na yaliyo ndani ya uwezo wetu????
 
Bajeti hii imebakiza miezi mitatu imalizike.

Ilikuwa ni bajeti ya trilioni 29,je katika maeneo mbalimbali nchini kwetu kuna kitu kinachofanana na trilioni 29?

Trilioni 29 zimebadili taifa/mkoa/wilaya/mtaa wako?

Kama imetuachia "hewa" pia sema tu

Tupia jibu lako hapa

[HASHTAG]#achamanenoonyeshaviwanda[/HASHTAG]


Hii budget kiuhalisia haipo na ukijua mambo ya budget yanaanza April shame on it khaaa

mimi sio mchochezi
 
Back
Top Bottom