Bajeti 2016/2017 imebakiza miezi mitatu muda wake uishe,je imeleta mabadiliko huko kwenu?

Bajeti hii imebakiza miezi mitatu imalizike.

Ilikuwa ni bajeti ya trilioni 29,je katika maeneo mbalimbali nchini kwetu kuna kitu kinachofanana na trilioni 29?

Trilioni 29 zimebadili taifa/mkoa/wilaya/mtaa wako?

Kama imetuachia "hewa" pia sema tu

Tupia jibu lako hapa

[HASHTAG]#achamanenoonyeshaviwanda[/HASHTAG]

!
!
[HASHTAG]#AchaManenoWekaVyeti[/HASHTAG]
 
Uzi unaswali la msingi sana, ila wengi wetu tunajibu mzaha kama tulivyozoea.. nashauritujibu swali na kama hakuna ulichokiona basi toa palipo haribika.
Mi nashukuru kwamba tayari tuna "wings of Kilimanjaro, reli mpaka Moro nasikia inaaza, makutano ya Tazara yanaboreshwa, Njia za umeme zinakwenda kwa kasi ya ajabu, Nyasa washapata meli ya kwanza, mbili ziko njiani.
Kwa viwanda wanaotegemea kuona majengo ya viwanda ndani ya miezi tisa ya budget, tena viwanda vinyomilikiwa na JMT nawaonea huruma kwa "ujinga" walio nao
 
Huu Uzi ni mzuri sana na hapa ndio serikali inakuwa accountable. Trillion 29 ilikuwa ni kujitafutia matatizo tu. Wakati wanapitisha ile budget USA tayari walikuwa wamebana zile pesa za REA. Serikali ikasema itajiweza. Huku napo, Magufuli akiahidi kuweka trillion moja kwa ajili ya ujenzi wa reli. Akaongelea ongezeko la budget ya dawa, nalo likashindwa. Akakurupua issue ya kuhamia Dodoma ambayo imekuwa ni chungu ila amejikaza. Idadi ya waliohama wizara zote, ni kama wafanyakazi wa halmashauri ya wilaya ambayo ni mpya.
Hili la pangaboi ni mpango wa siku nyingi na ulikuwepo kwenye budget.
Kwenye ajira amekwama vibaya mno. Viwanda havionekani. Amebana matumizi lakini pesa hazionekani.
Kwetu husema kukupa yaani Unapata pesa hujui Zinaenda wapi.
Majigambo ya mapato hakuna, benki zimekwama, uhakiki umemuibua Makonda peke yake.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Bajeti hii imebakiza miezi mitatu imalizike.

Ilikuwa ni bajeti ya trilioni 29,je katika maeneo mbalimbali nchini kwetu kuna kitu kinachofanana na trilioni 29?

Trilioni 29 zimebadili taifa/mkoa/wilaya/mtaa wako?

Kama imetuachia "hewa" pia sema tu

Tupia jibu lako hapa

[HASHTAG]#achamanenoonyeshaviwanda[/HASHTAG]
Uhakiki hujauona mkuu?
 
...Mimi niko huku Kijijini kwetu Lunenzi, bado twasubiri zile milioni 50 za kijiji chetu...
 
Bajeti hii imebakiza miezi mitatu imalizike.

Ilikuwa ni bajeti ya trilioni 29,je katika maeneo mbalimbali nchini kwetu kuna kitu kinachofanana na trilioni 29?

Trilioni 29 zimebadili taifa/mkoa/wilaya/mtaa wako?

Kama imetuachia "hewa" pia sema tu

Tupia jibu lako hapa

[HASHTAG]#achamanenoonyeshaviwanda[/HASHTAG]

By the way ruzuku ya Chadomo imeongezeka, wameshajenga ofisi au wanazunguka tu huku wakitoa povu??? Mwenyekiti atapimwa apimwi....? issue iwekwe wazi kama Askofu.
 
Back
Top Bottom