Echolima1
JF-Expert Member
- Nov 2, 2019
- 1,934
- 1,988
Iran imeripotiwa kuwaamuru wanajeshi wake kuondoka Yemen na inapunguza uungaji mkono wake kwa Wahouthi huku kukiwa na mashambulizi makubwa ya anga ya Marekani dhidi ya kundi hilo la waasi.
Gazeti la Telegraph la Uingereza limemnukuu "afisa mkuu wa Iran" akisema kwamba Tehran inapunguza uungaji mkono wake kwa washirika wake wa kikanda ili kuzingatia vitisho vya moja kwa moja vinavyotokana na utawala wa Trump.
Afisa huyo pia anasema kuwa hatua hiyo kutoka Yemen imefikiwa ili kuepusha uwezekano wa kuongezeka msuguano na Marekani ikiwa mwanajeshi wa Iran atauawa katika mashambulizi ya anga ya Marekani huko.
Tehran inaelekeza nguvu zake badala ya jinsi ya kujibu Rais wa Marekani Donald Trump na orodha yake ya vitisho, na "hakuna kundi lolote la kikanda tulilounga mkono ambalo linajadiliwa," afisa huyo amenukuliwa akisema.