Baada ya Lissu kuchukua fomu ya Urais, Dr Mwakyembe atishia kuifuta TLS

Status
Not open for further replies.
"Serikali imekiasa Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS) kibaki kuwa chombo cha kitaaluma cha kulinda weledi, viwango na maslahi mapana ya uanasheria na kisikubali kuyumbishwa na mihemko ya uanaharakati wa kisiasa isiyo na tija kitaaluma.

Akiongea na ujumbe wa TLS kwenye ofisini yake ndogo ya Dar es Salaam leo, Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe amesema TLS ibakie njia kuu kama ilivyo kwa vyama vingine vya kitaaluma nchini, isighilibiwe na michepuko.

Amesema uanzishaji na uendeshaji wa TLS kwa sheria ya Bunge umesukumwa miaka yote na dhamira njema ya Serikali ya kutaka kuilinda na kuilea taaluma ya uanasheria ili ikue na ijenge weledi stahili na hivyo itoe mchango bora katika ujenzi na uendeshaji wa utawala wa sheria nchini.

"Ikiwa TLS sasa inajiona imekua kiasi cha kutosha na sasa inataka iingie kwenye majukumu ya ziada ya uanaharakati wa kisiasa, Serikali haitasita kuifuta sheria iliyoanzisha TLS ili chama hicho kijisajili chini ya Sheria ya Vyama kama NGOs zingine nchini au ikiwezekana chini ya Sheria ya Vyama vya Siasa kama vyama vingine vya siasa nchini".

Ameongeza kusema harakati zinazoendelea ndani ya TLS zenye mwelekeo wa kisiasa, zimeifanya ofisi yangu isimame kidogo kukamilisha marekebisho kadhaa ya sheria ya TLS maana hatma ya TLS haieleweki, "it remains in the balance".

Awali, waziri huyo aliueleza ujumbe huo wa TLS ukiongozwa na Mtendaji Mkuu wa TLS, Wakili Lameck Calleb, kuwa Serikali imefarijika sana kwa ushirikiano mkubwa uliotolewa na chama hicho katika maandalizi ya muswada wa sheria ya huduma ya msaada wa kisheria ambayo imepitishwa na Bunge na sasa unasubiri saini ya Rais wa Nchi kuwa sheria.

Aliongeza kuwa Wizara inaitegemea sana ushurikiano wa TLS hata katika utungaji wa Kanuni za sheria hiyo mpya, mchakato wake ambao tayari umeanza."
 
Yaani ametambua mchango wake kwenye muswada tajwa na mambo mengine lakini kale ka woga ka Tundul Lissu kuwa Rais wa TLS bado kamemsukuma kuituhumu kama chombo cha kisiasa...
 
Je! Iko sheria inayo ongelea kumzuia kiongozi katika chama cha siasa kuwa rais TLS? Tafadhalini wanasheria saidieni hapa.
 
Yaani Rais ni Muoga saana hivyo anatumia Defensive Mechanism. Hivyo anaagiza wateule wake wafanya anachowaagiza kufanya. Bungeni yupo Kibaraka yule Bibi Kijana.
 
Hahaha hata jamaa anayeogopa dent wake? Tendeni haki basi
 
Hawa ma Dr wa kibongo huwa hawatumii taaluma yao ipasavyo..hiyo kauli ni zaidi ya udikteta huwezi amini kama ni msomi katamka maneno hayo ya shombo
 
By Kibatala;

Kauli ya Waziri Mwakyembe kwamba Serikali haitasita kuifuta TLS inajibiwa kwa hoja nyepesi sana; nini kimemstua? Mbona hakuongea pale Judge Mkuu Mstaafu alipochukua forms za kugombea Urais kupitia CCM? Alihoji ni lini Judge Agustino Ramadhani alichukua membership card ya CCM? Au kwa Waziri Mwakyembe ni sawa tu kwa Marais wa zamani TLS kugombea Ubunge kupitia CCM muda mfupi baada ya kuachia nafasi;na ku-create kila impression kwamba alikuwa CCM card-carrying member?
Waziri Mwakyembe anafikiri Mawakili (taaluma ambayo yeye amejipumzisha nayo kwa muda na halipii ada full kwa kuwa ni non-practising member) hawana utashi wa kutosha kutofatisha kati ya itikadi za siasa na msingi wa TLS?

Alikuwa wapi yeye kama Wakili (japo ambaye ni non-practising) kutetea tulipotishiwa kuunganishwa katika case iwapo tutatea wateja wetu? Alikuwa wapi kukemea Polisi walipokamata Mawakili wakiwa kazini?

Waziri Mwakyembe anafikiri ni rahisi kiasi hicho kuifuta TLS kwa kuwa tu yeye ni Waziri? Hafahamu kuna Mahakama ambazo yeye hazi-control na kuna tools kama Judicial Review, etc?

Alikuwa wapi kuzumzia maafisa wa Polisi waliostaafu na punde tu wakagombea Ubunge kupitia CCM? Tena hawa walikuwa ni Mawakili na wanachama wa TLS. Mbona hakuzungumzia neutrality ya Jeshi la Police?

Vipi kuhusu Mwanajeshi alyeteuliwa nafasi ya juu CCM?

Watuache TLS tuchague viongozi wetu ili tutimize majukumu yetu ya kisheria.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…