Pre GE2025 Baada ya kukamatwa Kisutu, Naibu Katibu Mkuu CHADEMA-Zanzibar apatikana, adai kupelekwa Pori la Mabwepande na kupigwa sana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,780
56,327
Makamu Mwenyekiti Zanzibar Mhe. Said Mzee Said, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Ali Ibrahim Juma na wengine 10 wakiwemo waandishi wanne walikuwa wamekamatwa mapema leo wameachiwa maeneo ya pori la Mabwepande, Kawe wakiwa wamepigwa na kuumizwa sana na Jeshi la Polisi.

Wameumizwa sana na sasa wanapelekwa hospitali ya Mwananyamala.
20250424_101933.jpg
20250424_101930.jpg

IMG-20250424-WA0010.jpg
IMG-20250424-WA0012.jpg

Makamu Mwenyekiti Zanzibar Mhe. Said Mzee Said, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Ali Ibrahim juma na wengine 10 wakiwemo waandishi wanne walikuwa wamekamatwa mapema leo wameachiwa maeneo ya pori la Mabwepande, Kawe wakiwa wamepigwa na kuumizwa sana na Jeshi la Polisi.
View attachment 3313962View attachment 3313963
Kama movie hivi.....kwa hiyo hawakuwa na sababu ya kuwakamata?

Jamaa wanakula Perdiem za bure.
 
Naibu Katibu Mkuu CHADEMA - Zanzibar, Wakili Ally Ibrahim Juma aliyekamatwa asubuhi ya leo katika Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam, amepatikana lakini akiwa na majeraha katika mwili wake na ameeleza kwamba alivyokamatwa alipelekwa katika msitu wa Mabwepande na kupigwa sana.

View attachment 3313975
Kwanjni hawajampeleka Oysterbay kama ana makosa?
 
Naibu Katibu Mkuu CHADEMA - Zanzibar, Wakili Ally Ibrahim Juma aliyekamatwa asubuhi ya leo katika Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam, amepatikana lakini akiwa na majeraha katika mwili wake na ameeleza kwamba alivyokamatwa alipelekwa katika msitu wa Mabwepande na kupigwa sana.

View attachment 3313975
View attachment 3313977
mbona kama kafumaniwa hivi gentleman? :NoGodNo:
 
Back
Top Bottom