SoC03 Athari za utapeli wa kimapenzi katika malezi na jamii

Stories of Change - 2023 Competition

Ms fighter

Member
Sep 14, 2021
18
6
Utapeli wa kimapenzi kwa sasa umeshamiri katika jamii yetu. Vijana wengine wanachukulia kama imekua fasheni. Katika jamii ya sasa imekuwa ngumu kujua yupi mwenye mapenzi ya kweli au uongo. Yupi mwenye nia ya kweli au uongo

Mapenzi ni kitu cha muhimu katika jamii yoyote. Upendo ndiyo huunganisha watu na kujenga familia. Lakini katika jamii ya sasa mapenzi ya kweli yamejificha. Mojakati ya wakati mgumu kwa baadhi ya vijana ni wakati wanapofanya maamuzi ya kuoa au kuolewa. Kwa kuwa wanapitia mengi kabla ya kumpata mtu sahihi wamelaghaiwa kimapenzi, wamepotezewa muda, fedha, na kufanyiwa matukio mengi ya ajabu mpaka kukata tamaa hawaamini mapenzi ya kweli na kuona waliofanikiwa kujenga familia imara wanabahati. Kuna vijana hata wame za watu wanawalaghai kimapenzi wafanyakazi wa serikalini kama manesi na walimu na kuwaachia mzigo wa madeni baada ya kutimiza utapeli wao

Utapeli wa kimapenzi unaathari nyingi lakini kwenye ili chapisho ningependa kueleza jinsi utapeli wa kimapenzi unavyoweza kuathiri malezi katika jamii.

Utapeli wa kimapenzi ni kutumia uhusiano wa kimapenzi kufanya udanganyifu. Matapeli wa kimapenzi kuanzisha mahusiano na watu wakiwa na nia zao ambazo mara nyingi sio nia njema. Mbali na kujua hawana malengo na watu walionao kwenye mahusiano lakini wengine uhakikisha wamewazalisha watoto au wamezaa nao wakiwa wanajua kabisa hawatawahitaji bila kujali hatma ya hao watoto wanaozaliwa. Mfano mkaka anaingia katika mahusiano ya kimapenzi na msichana akimuaminisha atamuoa au saa ingine akitaka amzalie ndi amuoe lakini kumbe uyo kaka anamke wake ni namna ya kumfanya uyo msichana awe mchepuko wake wa kudumu ni kumzalisha mtoto ambaye hana malengo naye ili kumfanya uyo msichana mtumwa wake na vijana wengine wanaona njia na kuwakomoa wasichana ni kuwazalisha na kuwakimbia, wengine wanawazalisha mabinti kwa kukusudia na kuwaambia kuwa hao watoto ni zawadi wamewapa au wameamua kuwaachia kumbukumbu kwa kuwazalisha watoto wasiowawajibikia huu ni ukatili. Hawamkatili uyo binti aliemzalisha tuu bali anamkatili pia mtoto asiyenahatia.

Kuzalishwa na kuachwa sio jambo dogo linaweza kumuathiri sana mama mwenye mtoto na hata malezi kwa mtoto. Kuna wamama wanawachukia watoto wao kwa sababu walilaghaiwa na kuzalishwa na watu wasio na malengo nao wengine wanaamini watoto nao ni laana ndi maana wanakataliwa na wanaume wengine wanaamini kuwa watoto wanawafungia milango ya kuolewa na wengine hawana vipato vya kuwasaidia kuwalea wanao waliotelekezwa na baba zao. Ni asilimia chache ya wanawake wanaoweza kusimama imara kuwawajibikia watoto wao waliotelekezwa huku wakiuguza majeraha yao ya moyo na kuwa sawa sanasana wanaoweza kujitegemea.

Utapeli wa kimapenzi ndi sababu kubwa kwa kudorora kwa malezi bora katika jamii. Watoto wengi wanakosa malezi bora kutokana na wazazi wao kuwakataa. Kwa kuwa kwa hao wazazi, wao walikuwa zao la starehe na hawako tayari kuwawajibikia. Na hii ndi sababu tuonaona ongezeko la watoto wa mitaani, watoto wachanga wanaotupwa na watoto wadogo wanaokatisha masomo ili kufanya kazi. Imekuwa kawaida tunasikia watoto wachanga wametelekezwa hospitalini. wengine wanatupwa hii ni sababu watu hawaupi uzito chanzo je tatizo linawezaje kupungua.

Nina mfano ambao sote tumeona na kusikia hivi karibuni kwa mwanamziki wa taarabu, kuna kijana alijitokeza akasema uyo mwanamziki ni baba yake mzazi aliambiwa na mamayake lakini uyo mwanamziki akamkataa alipoomba wapime DNA alikataa watu waliposhinikiza akakubali lakini akasema DNA ikionyesha ni baba na mtoto atafikiri kwa kuwa mtoto wa nje ni wamwanamke na DNA alipie uyo mtoto cha kuhuzunisha ni kuwa uyo kijana anafanana na baba yake hata bila DNA mtu anaona ni baba na mwanaye. Uyo mwanamziki ni kioo cha jamii, lakini anamkana mwanae hadharani na hakuchukuliwa hatua yeyote je walio ndani ya jamii wasiojulikana ni wangapi wanaowakana watoto wao wadogo na hata ambao awajazaliwa na hawachukuliwi hatua yoyote nini hatma ya hao watoto kama sio kuongeza watoto wa mtaani. Kama uyo mwanamziki alivyomkataa mwanae hadharani bila kujali sheria inamaanisha sheria haijaipa uzito watu wanaowakataa watoto wao.
Serikali imejitahidi kuwalinda watoto na kupigania haki zao ikiwa ni pamoja na kuwepo ustawi wa jamii ambapo wanahakikisha wazazi wanawahudumia watoto wao. Lakini Ukweli ustawi wa jamii unapunguza tatizo kwa kiasi, wapo watoto wengi wanaokosa malezi ya wazazi wao, wapo watoto wengi ambao ni watoto wa mitaani lakini wazazi wao wanauwezo ya kuwapa mahitaji yao lakini ni waliamua tuu kuwatelekeza.

Japo kuwa sheria haijaipa nguvu sana uhusiano baina ya watu isipokuwa waliofunga ndoa. Lakini sheria inatakiwa isimame imara kuwalinda watoto, serikali inatakiwa isimame imara kuweka sheria itakayolinda watoto na kulazimisha kila mmoja kuwajibika kwamatunda ya kazi yao hata kama upendo wao ulikuwa wa uongo au usio na malengo lakini watoto wanatakiwa kulindwa na kupata malezi bora kutoka kwa wazazi wao wote wawili kwa afya bora ya kiakili na kuunda jamii ambayo watoto wanakua huku wakiamini wanalindwa na kuthaminiwa. Itakuwa ni kitu cha kushangaza mtoto aliekulia kwenye mazingira magumu (mtaani) na kukataliwa na mzazi wake ingawa anajua wanaishi na akalazimika kupambana na walimwengu akiwa mdogo kulazimishwa kuwa kijana mwema au kumuaminisha kuwa analindwa na anathaminiwa angali yeye amekuwa akiamini amekataliwa na hana thamani. Kumlazimisha mtoto aliekuwa na hizo fikra kuwa kijana na wananchi wa kawaida haina tofauti na kumuonea pia ni asilimia chache ya watoto waliokataliwa kuwa vijana wa kawaida na kusahau kuwa wao walikataliwa pia mitaani kuna vitu vingi hatari kwao. Kwa hiyo serikali yetu inaopambana kuwalinda watoto inapaswa kupambana na chanzo kinachosababisha watoto kukosa malezi bora ikiwa ni wazazi wanaowakataa watoto wao kwa makusudi.

Upendo una nguvu sana na ndio unaounganisha watu. Hamna mtu anayeweza kuepuka upendo kwa sababu ndio unaunda familia jamii na taifa. Lakini watu wanatumia vibaya ili kuwalaghai watu bila kujali athari wanazosababisha kwa kuwa sheria haiwabani sana na pia sio kweli kuwa kila binti anaedanganywa na kuzaliwa amejitakia au ni mjinga. Ili kupungua tatizo la watoto wanaotelekezwa jamii inatakiwa ipewe elimu na kuondoa imani kuwa ni makosa ya binti pekee. Kwenye upendo wa watu wawili vitu vingi utokea ahadi nyingi utengenezwa na hapo matapeli wanaokuja kwa gia ya upendo ndi ufanya uharibifu. Serikali inatakiwa iunde sheria kali ambayo itawalazimisha watu kuwajibika linapokuja suala la watoto. Kama sheria inavyopambana na ubakaji basi iwepo sheria inaowalinda watoto ili kupungua vyanzo vya watoto wanaotelekezwa na watoto wa mitaani

WANASEMA MAPENZI UPOFU BASI SHERIA INATAKIWA IWE MACHO NA IMARA KUWALINDA WATOTO na kuhakikisha wanapata malezi ya wazazi wote wawili.

Picha hapo chini inasemekana baba alimtelekeza akiwa na miaka mitatu lakini amefariki anataka wagawane viungo bila kujali kosa la kumtelekeza mtoto alipokuwa mdogo hai kwa kuwa sheria haimbani.
Screenshot_20230728-032333_1690503842586.jpg
 
Janbo hili lilianza kama mchicha ila kwa sasa limefikia hatua ya mbuyu ambapo kuung'oa ni mtihani kwasababu asilimia kubwa yani katika watu 10 basi 7 wametapeliwa na yote hii inasababishwa na tamaa za kimwili umemwona mtu umempenda mpaka mnapendana wote kumbe kuna kitu ulihisi utakikuta kwake hatimae hakuna ulichokua unahitaji unavunja uhusiano.
Hapa ndio mana dini zimeelekeza kuowa kabla ya kufanya kitu
 
Janbo hili lilianza kama mchicha ila kwa sasa limefikia hatua ya mbuyu ambapo kuung'oa ni mtihani kwasababu asilimia kubwa yani katika watu 10 basi 7 wametapeliwa na yote hii inasababishwa na tamaa za kimwili umemwona mtu umempenda mpaka mnapendana wote kumbe kuna kitu ulihisi utakikuta kwake hatimae hakuna ulichokua unahitaji unavunja uhusiano.
Hapa ndio mana dini zimeelekeza kuowa kabla ya kufanya kitu
Kuoa bila kufanya kitu siyo suluhu,unaoa unakuta ina maji kama bahari au haina vigezo unavyotaka bado utapiga chini
 
Jamii imejaa umaskini ndo maana wengi hutumia mahusiano ka sehemu ya kupata ahueni ya maisha, jambo ambalo linalopelekea usaliti na uvunjifu wa uwaminifu kwenye mahusiano sababu ya tamaa.
 
POST OF THE YEAR IWEKWEJUU
MIMI PIA NAPITIA CHANGAMOTO HIYO YA KUPATA MTU SAHIHI WA KUMUOA ILA USHAURI ULIOSEMA NI WATU WAMSHIRIKISHE MUNGU WAO PIA MIMI
 
Andiko zuri Ila mzani wake umeegemea upande mmoja..

Ulaghai wa kimapenzi -Kichwa cha Uzi...

Nilitaraji kuona both ke + me Wanahusishwa katika andiko lako Ila nimeona ke pekee Kama vile ndiyo wahanga wakubwa kwenye chapisho lako.
 
Back
Top Bottom