ATCL: Another Richmond!

Jana nimeions ndege ya kwanza ya Community Airlines (Boeng 737 H800). Kama ATCL bado wanasuasua, watapata ushindani mkubwa na wanaweza kupotea kibiashara.
 
..kwahiyo,umekata tamaa?

Sijakata tamaa. Lakini situmii weakness yangu kama asset yangu katika masuala ya kazi au biashara. Na kama kuna kazi au biashara ambayo najiona na weakness, basi nitajifunza.

Tuna weakness katika uendeshaji wa mashirika ya umma.
 
..kuna shughuli nyingine zenye maslahi au muonekano/hadhi ya taifa sekta binafsi haiwezi kuzifanya vizuri au na kwa manufaa ya taifa!bahati mbaya nyingi ya hizi zina element kubwa ya kibiashara!

Si kweli: shirika la "Morani" Mtanzania linaweza kuwa na mwonekano wa Kitaifa/Kitanzania. Deep inside ni mtanzania bado. Kwa ni taifa ni nani? Ni sisi kwa wingi na uchache wetu, mmoja mmoja na michango yao ndiyo inanafanya au kuunda Tanzania!! Sasa hao mmoja mmoja wanaweza kuchangia kwa njia mbalimbali, kwa kukimbia, biashara, ....

..zipo serikali kadhaa zenye mashirika yanayofanya biashara au kusimamia kampuni za kibiashara!moja ni singapore!yenye holding company[ina makampuni/HISA katika makampuni kadhaa ikiwemo singapore airlines na singapore telecommunications]inayoitwa temasek.and mind you,hizo hisa ni over 50%!

Naam ... Haswa, kwamba hata hao wamegundua kwamba Serikali yenyewe haiwezi kuendesha, TOO RISKY, wana-maintain some shares lakini kampuni inaendeshwa kwa misingi ya kampuni binafsi ...

..sheria hizi ni kwa wajinga kama sisi na si wenye ufahamu wa maslahi na maendeleo ya taifa lao!

Sawa... Labda niliweke vizuri zaidi, kwamba sheria inakuwa mbaya pale ambapo haikidhi maslahi yako... nafikiri ni observation muhimu..

.... kuna kipindi ruzuku ni muhimu,ila si dawa endelevu ya kukwamua mashirika yenye hasara!it's supposed to be a shot in the arm!

Yes but in the case of Tanzania with its history and immaturity, way too risky, in my opinion, for now. I do not believe ATCL can build a company that can compete!
 
Jana nimeions ndege ya kwanza ya Community Airlines (Boeng 737 H800). Kama ATCL bado wanasuasua, watapata ushindani mkubwa na wanaweza kupotea kibiashara.

The way to go ... hongera CA.
Huyu ataanza kutulipa kodi karibuni, ajira n.k.

Mimi sioni haja ya kuwa na mashirika yanayotutia umaskini ..
 
Si kweli: shirika la "Morani" Mtanzania linaweza kuwa na mwonekano wa Kitaifa/Kitanzania. Deep inside ni mtanzania bado. Kwa ni taifa ni nani? Ni sisi kwa wingi na uchache wetu, mmoja mmoja na michango yao ndiyo inanafanya au kuunda Tanzania!! Sasa hao mmoja mmoja wanaweza kuchangia kwa njia mbalimbali, kwa kukimbia, biashara, ....

..si umesikia rites walitaka kufunga reli ya tanga. sasa,we amini usiamini,ukweli uko palepale.

Naam ... Haswa, kwamba hata hao wamegundua kwamba Serikali yenyewe haiwezi kuendesha, TOO RISKY, wana-maintain some shares lakini kampuni inaendeshwa kwa misingi ya kampuni binafsi ...

..wao hawajagundua,wanafahamu. na si wao tu,wako wengi. hamna mtu aliyesema serikali yenyewe inaendesha,na wala haiwi hivyo unavyofikiri.kampuni ndio huwa mali ya serikali. sasa,ni tafsiri tu!

Sawa... Labda niliweke vizuri zaidi, kwamba sheria inakuwa mbaya pale ambapo haikidhi maslahi yako... nafikiri ni observation muhimu..

..sawa.

Yes but in the case of Tanzania with its history and immaturity, way too risky, in my opinion, for now. I do not believe ATCL can build a company that can compete!

..tunatakiwa kuwa jasiri,kujiamini na kusema tunaweza,haya mambo ya bado hatujakomaa tutayaacha lini?kwani kitu hukomaa ghafla au baada ya muda,tena wa misukosuko?
 
Ujumbe kutoka kwaa Makwaiya Wa Kuhenga:

Air Tanzania shall not be for sale

Makwaiya wa kuhenga
Daily News; Thursday,December 13, 2007 @22:03

IN this column a while ago, I reported the jubilant mood of workers of Air Tanzania on the rebirth of the national airline as a state owned enterprise.

My reading of that mood was that that mood was a wider translation of the mood of Tanzanians in general that privatisation was neither a dogma nor a panacea to all economic strategies. There are areas where the state, on behalf of a given people should have a stake in strategic areas of a given economy.

Over the last two decades, the people of this country have experienced the vagaries of private capital. The catchword has been: “Privatis- ation as an engine of economic growth”. What has been the focus?

Investors have invariably chosen sectors that would mean a fast buck for them. They have gone for ‘ready made’ enterprises such as the beer and mining industry. We have yet to see their thrust in agriculture - whose potential is comparatively unmatched to any sector. We have yet to see them investing in airdromes and airports of our country to make them of all weather use.

I landed at Tabora airport the other day and I was shocked to see that 46 years after independence it is still not tarmacked. It is not the only airdrome in this pathetic state across the country. Clearly, this is not an area to make good money for investors. So who steps in?

We have learnt albeit the hard way that private capital has its serious limitations - it is neither in the interest of the majority public nor is it in the interest of the government of the day that has a serious agenda to fulfill man’s basic needs.

Now back to our Air Tanzania. Why are investors not coming now - to provide the seed money for its operations? Why didn’t they show interest before? They will not come and their standard reason will be - airline business is ‘risky’ and fragile!

When the government first flirted with an outside investor who came in as a partial owner, with 49 per cent shares in the airline, there was nothing that happened to make the difference.

There was in fact an attempt at killing the airline altogether or at best convert it into an appendage.

Fortunately the government saw the writing on the wall. It has decided for full ownership of the airline funded by the state.

This is a very commendable move, which has enjoyed the support of both the people and Members of Parliament - including those from the Opposition. This support translates simply that it does not always make economic sense to privatise everything. A country must have its symbols and among these symbols is a national airline.

We have begun very well along this road. There is serious commitment on the part of the government of the day which is providing seed capital for the airline with the prime objective to make the airline commercially viable.

There is no reason why it should not break even in the long run because the market is there both locally and internationally.

One big advantage of having an airline that is state-owned is that problems are easily solved in terms of inter-state contacts in case passengers being stranded as have been widely reported in the media. In fact I am reliably informed that stranded passengers bound for their pilgrimage is the result of the other end abroad (not state owned enterprises!) not keeping their word of the deal to haul pilgrims and not Air Tanzania’s problems per se.

We have seen a whole prime minister and the relevant minister working hand in hand with the management of Air Tanzania to ensure that pilgrims make the trip. I am sure this commitment is as result of the state having a full stake in the ownership of Air Tanzania.

So, what people of goodwill should really do is to wish the national flag carrier well. The state should continue supporting the national airline to achieve viability. And once this objective is realised, and in the event need arises to secure strategic alliances for a better international performance, then the airline should seek a partner.

Of course, seeking a strategic partner is not the same thing as privatising the airline or selling it altogether.

One does not use taxpayers’ money to take off the ground an airline only to sell it to someone who was not there during the initial donkey job - just in the name of privatisation. Privatisation is not a religion!

Makwaia wa Kuhenga is also an author. His current title CCM Na Mustakabali Wa Nchi (CCM and the Destiny of our Country) is now in bookstores across the country.

His website: www.makwaia.com

Source: DailyNews.Com

SteveD.
 
Ujumbe kutoka kwaa Makwaiya Wa Kuhenga:

Source: DailyNews.Com

SteveD.

Tatizo la Makwaiya anaona Airline kama alama ya taifa. Hayo mambo yamepitwa zamani. Tuchague moja kati ya mawili: ATC kiwe chombo cha faida au kitoweke kama mashirika mengine.
 
Huyu Makwaia Si Kibaraka Wa Atcl Hamjui Na Kilamwezi Analipwa Mshahara Pale Sales Ofisi,,sijui Kama Bodi Wanalijua Hili,,
 
The basic reason why we would like to have a strong ATCL is first make us proud of what we collectively call "our thing". It is an extension of our individual egos, a basic human trait. People wants not only to own something, but also to be part of success. I believe our egos would be badly bruised, and God knows that has happened only too often, if we continue seeing Tanzanians companies and resources being plundered, that make us a laughing stalk everywhere. So humiliating ..

So i think its time we recognized that we have failed running state companies and try to use other means thru which we could satisfy our collective egos, by saying for example, that, look, that is a successful Tanzanian company, even if the government owns a minority stake, or doesn't even own a thing but provides us with what we want; jobs, taxes...

When Makwaia says private capital should build runways, it shows how flawed his thinking in this matter is. He should extend the list to include roads. The age old fact is, there are things best done by government, and those best done by private individuals or groups. Governments world over are not competent in running businesses. But they can oil and grease (lubricate) the engine that is private sector, (as well as put some breaks and steer them into the desired direction) to run the economy.

Uganda and Kenya nao wanazo airlines zao ambazo serikali ni minority shareholder. They have realized that its not only capital that matters in starting and running a successful company, its the expertise. Na uzalendo, ambao kwetu sisi nafikiri uko likizo...

Tanzanians have a problem, we often equate private sector with blood suckers. Its part of our upbringing. If only we knew that the mashirika ya ummas are worse. But they cannot be blamed for wanting to collectively own and be proud of a shirika la umma, it provides a psychological satisfaction, of saying that is ours, not his or hers or theirs. That makes some feel they are outside the equation, if they take it in a narrow sense. Broadly speaking though, a company belonging to Morani, who is a Tanzanian, also benefits other Tanzanians.

So I say nationalism yes, but in more constructive, sustainable ways. I do not believe a village need to keep a cow that is constantly fed but do not provide milk just because villagers would feel proud of owning a cow. It would be a bad decision to keep the cow that continue draining their resources. Best option would be to sell it or even slaughter and feast on the meat to rid themselves of the burden!
 
mtukwao nami nakuunga mkono kabisa we should hav a strong ATCL,,ila kuna point umenigusa sana ambayo nafikiri ndio imefanya hili shirika liwe hapa lilipo,,,,Hakuna kiongozi anaekamata hili shirika na kufukiria UZALENDO kwanza,,
kila mmoja amekuwa akijitahidi kuwahi chake mapema kitu ambacho ni kibaya na kinaua kampuni mapema,,bora hata wazungu waliokuwa wanakula lakini polep[ole mpka uje kushtuka kampuni imekufa basi washaanza,,hili indabid tuombe mungu si swala tu la kuandika kwenye maandishi,,ona tulipiga makelele wasouth wanatuibia,,haya ona wameingia hawa nao hawana hata mwaka ,,kila
mmoja anajitahidi kuiba anavyoweza ,,,,embu wale wemye akilii naomba tusaidiane kwahili,,Alipochaguliwa bwana mattaka akaaunda management yake,,baada ya hapo wakaanza kuruka nje mmoja baada ya mwingine,wakirudi tu wanabadilishana,,,inasikitisha kuona ikafikia hadi secretary anpewa madaraka ya kukaimu jamani,,hii ni aibu ya ajbu,,kisa watu wanakula per diem za safari,,
wewe DAVID hivi unafikiri hizo dhambi za kutumia kodi za wananchi unafikiri mungu atawaacha,,ona sasa hilo la HIJJA mungu kawadondoshea kiulaini na atawaacha,,

2)KUNA HILI SWALA LA MAGARI LIMENITATIZA SANA ,,HAWA WATU MANAGEMENT WAMETUMA MAGARI MENGI YA KIFAHARI NA WAMELIPIWA NA HELA ZA AIRTANZANIA JE HII NI HAKI JAMANI,,WATU WANALIA NA SHIIDA YA CHAKULA MAGU UKO NA KWENGINEKO,,HUKU WATU WANAJAZA MA LANDCRUISER,,NAOMBA SERIKALI MULIANGALIE HILI NA MUANGALIE TAKUKURU MKO WAPI JAMANI????

3)MWISHO TUAOMBA MR DAVID SAFARI ZIPUNGUE KIDOGO TUJALI UZALENDO LIKIFA HILI SHIRIKA WENGI WATAKOSA AJIRA,,NA SERIKALI WATAKOSA KODI TUNAOMBA MUELEWE HILI ILI IWE FUNDISHO KWA MANAGEMENT,,MEMBER,,WAKIONA SAFARI ZIMEPUNGUA WATAOGOPA,,,HATA KUOMBA SAFARI MAANA NATUMAINI WEWE NDIE UNAEDHINISHA,,,,KWA KWELI NATAMANI NIRUDI KWENYE KAMPUNI KAMA NINGEKKUWA NARUHUSIWA,,,NATUMAINI MUNGU ATASIKIA VILIO VYETUUU

4)ADDITION TO THAT,,,TUNAOMBA SERIKALI MUANGALIE MATUMIZI YOTE YA KIPINDI CHA MATATIZO YA HIJJA,,NA YAWEKWE WAZI,,KUNA WENGI TU WAMEJITAJIRISHA KWA HILI,,,WANADAI KUFA KUFAANA,,,,,TAFADHALINI TENA TUWE NA UZALENDO HATA UKICHUKIA KAMPUNI PENDA HATA NCHI YAKO UTAIJALI KAMPUNI HII NI YA WOTE JAMANI,,

MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI KAMPUNI
 
Pdidy, maswali yako ni mazito sana na kuanzia kesho tutaanza kujaribu kuyajibu. Tafadhali watu wasikose gazeti la "Raia Mwema". Kwani "Raia Mwema" amekuwa very busy kuwaletea habari ambazo only Rai iliwahi kuwa na ujasiri wa kutoa!!
 
UFISADI ATCL – JK IOKOE KAMPUNI
Sisi wananchi tuliyo ndani na nje ya ATCL tumeona hatuwezi kukaa kimya tukiangalia jinsi kampuni inavyoangamia kwa ufisadi wa kisayansi.

Ufisadi wa kisayansi kwa sababu wanaofanya ufisadi huu ni uongozi wa kampuni kwa kutumia nafasi zao za madaraka na kujifanya huo ndio uongozi.

Tuanze kwa kueleza ni maeneo gani yenye ufisadi halafu tutaje viongozi hao na sifa zao.

Tutataja maeneo yenye ufisadi na matumizi mabaya ya mapato ya kampuni na mikopo toka mabenki mbalimbali.Pia safari zilizo nyingi na za muda mrefu bila kujali gharama na faida za safari hizo.Manunuzi ya magari kwa fedha za mikopo na bila kufuata taratibu. Mwisho ni hila za kuwafukuza ama kuwaondoa katika nafasi nyeti wafanyakazi wa zamani na kuweka wapya ambao huajiriwa kiholela na bila ya sifa zinazolingana na kazi zenyewe au hata na wale waliyoondolewa.

Jopo la viongozi na sifa zao zinazoangamiza kampuni ni:-
1. Mkurugenzi mkuu wa kampuni ni David Mataka. Yeye aliteuliwa na Rais JK baada ya rais aliyemtangulia kumtimua kwa ufisadi. JK alimuonea huruma DM baada ya kukaa ubaoni kwa muda na pia kushindwa kinyang'anyiro cha ubunge kwa tiketi ya chama tawala. Wananchi wa jimbo lake na wa chama chake hawakumpa kura kwa kuwa alikwisha onekana mbele ya rais BM kuwa ni fisadi wa hali ya juu japo yeye rais BM alikuwa anawakumbatia mafisadi kama Balali.

Mkuu huyu wa kampuni ameanzisha uongozi wa dharura(Management by crisis) ambapo kila asubuhi wakurugenzi na mameneja wateule katika ufisadi hukaa vikao vya kuangamiza kampuni. Amepata Benz ya kisasa katika mgao wa magari yaliyotolewa na wauzaji baada ya kununua magari ya kampuni huko Dubai kwa bei ya juu. Magari hayo ni ya mwaka 1998 japo bei yake ni karibu na mara mbili ya yale yanayouzwa na makampuni mengine ya Dubai. Yeye huwa anasuka jambo halafu anamwachia George, Eliasaph au William walichochee katika kikao cha hao viongozi.

2. Mark Manji yeye ni mtu wa Musoma japo jina lake la kihindi. Huyu ni mshauri wa mkurugenzi mkuu. Alikuwa mkurugenzi wa idara ya operations wakati wa makaburu japo idara hii huwa inaongozwa na marubani. Alipewa cheo hiki na makaburu ili kuwaweka marubani katika himaya ya makundi. Makaburu walipoondoka aliomba kuacha kazi kwa hiari na akastaafu akaomba kuendelea na kazi tena kama mshauri wa mkurugenzi mkuu. Kwa kuwa alikuwa na mapenzi na makaburu na kwa kuwa ameshapata mafao yake, hana huruma na kampuni kwa sasa badala yake yeye ni kichocheo na hujifanya analijua shirika. Anatumia utoto wa mjini kufanya kazi kwani hana shahada hata moja japo amepewa nafasi nyeti.

3. Eliasaph Mathew aliajiriwa na makaburu kama meneja wa fedha kwa maana hiyo ni mtu wa makaburu. Baada ya mkurugenzi wa fedha aliyekuwa kaburu kuondoka amekaimu nafasi hiyo hadi leo. Huyu ndie kinara wa kupindisha taratibu za matumizi ya fedha na ununuzi. Ni mfuasi namba moja wa DM kwani kwa sasa pesa za kampuni hutolewa kiholela kulipia gharama kwa ufisadi. Mfano kabla ya kufunga mwaka 2007 shillingi millioni mia mbili hamsini zilichotwa kulipa gharama za kutoa magari nane yaliyokuwa katika yadi ya kuweka mgari iliyo ya watu binafsi. Haishi hapo huchota dola elfu tatu taslimu toka kwa mtunza fedha kila mwezi na kumpa huyu mwenye yadi ya kuhifadhi magari. Huidhinisha malipo kwa ankara tu bila kujali taratibu nyingine. Ndiye aliyejumuika katika jopo lililokwenda Dubai kuchagua magari ya kampuni na kuyanunua kwa bei mbaya bila kufuata taratibu za ununuzi. Magari haya ni ya 1998 japo ATCL ni mali ya serikali,hilo halikutiliwa maanani. Yeye amepata zawadi ya VX Landcruiser ya kisasa kama mgao katika hayo manunuzi na sasa ameweka pembeni Vitara yake. Hutumiwa katika mikakati ya kuwaondoa watu wa zamani na wenye sifa kwa kuwazulia kesi na shutuma za matumizi mabaya ya pesa kitu ambacho si kweli.

Waliyoonja joto hilo ni pamoja na Hassani ambaye aliamua kuacha kazi, Hamisi na Mndeme ambao wamesimamishwa kwa suala la bwana Mohamed Makaratasi ambaye ni rafiki wa George Mazula.

4.George Mazula yeye eti ndiye rubani kiongozi na mshauri wa DM. Huyu aliwahi kuachishwa kazi wakati mwenyekiti wa bodi alikuwa ni Abasi Sykes. George aliwahi kuunguza injini mbili za Fokker kwa mpigo pale Tanga. Amewahi kuangusha ndege aina ya Fokker hapa Dar es salaam. Amewahi kuua mtu pale uwanja mpya wa JK Nyerere kwa kukatwa na pangaboi baada ya yeye kuzembea kuzima injini. George ni kiungo wa mikakati yote ya ufisadi na kuondolewa watu katika nafasi zao. Alikuwa mfadhili wa DM wakati akiwa ubaoni. Ni rubani mwenye makeke na mikosi mingi. Katika dili ya Dubai yeye amepata Volvo na kujidai amekopa.

5. Amin Mziray huyu ni katibu wa kampuni. Yeye ni chapombe. Alipewa gari ya kampuni na makaburu na kulipindua kwa ulevi. Anayo shahada ya sheria lakini haitumii kwa maslahi ya kampuni. Kampuni imeshindwa kesi nyingi kwa kutokuwa makini huyu mwanasheria. Yumo katika hili jopo la ufisadi wa kampuni. Katika mgao wa magari ya Dubai yeye amepata VX Landcruiser la nguvu. Hayupo tayari kutetea hoja mbovu zinazotolewa ndani ya vikao vya hili jopo la ufisadi.

6. William Haji, anakaimu nafasi ya mkaguzi mahesabu wa ndani. Aliajiriwa wakati wa makaburu kama mkaguzi wa mahesabu wa ndani chini ya bwana Yakubu. Baada ya muda bwana YAkubu aliwekwa pembeni na huyu bwana kukaimu nafasi yake. Kwa sasa yeye ndiye anayekagua malipo (Pre-audit) hivyo yumo ndani ya mtandao wa ulaji. Ndiye anayetumiwa kutengeneza taarifa za kuzua kesi na uonevu kwa wafanyakazi wa chini. Huchukua nafasi ya afisa usalama wa kampuni ili kupindisha ukweli na hatimaye kuwadhalilisha ama kuwatimua wafanyakazi wasiyo na hatia. Ni hatari sana kwani yupo karibu na DM na Eliasaph katika kila mpango.

7. Sadiki Muze, Yeye ni mkurugenzi wa idara ya operations kwa sasa. Amepewa nafasi hiyo yeye kwani ndiye aliyekuwa mfadhili mkuu wa DM wakati akiwa ubaoni. Pia ni mshirika wa DM katika vinywaji na mwanachama wa kijiwe kimoja na George. Ni Sadiki na George pekee waliyopewa vyeo na kuenguliwa wengine baada ya DM kuchukuwa uongozi ATCL na ni chapombe. Sadiki na George wamelipwa fadhila.

8. Heho Mbiru ni Mkenya, aliajiriwa kwa nguvu enzi za makaburu kama mkurugenzi wa masoko. Aliajiriwa kwa nguvu na aliyekuwa mwenyekiti wa bodi ya ATCL wakati huo Ali Mufuruki kwa kisingizio kuwa hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kushika nafasi hiyo. Ni mzalendo wa Kenya kweli kweli kwani kazi zinazoweza kufanyika hapa (kama Graphics) huzipeleka kwenye kampuni yake. Anayo mapenzi na makaburu hivyo kuleta mabadiliko tunayotaka yeye ni kikwazo na ndiyo maana ni rahisi kutumiwa katika hujuma. Kumbuka tunaushindani na Kenya Airways huyu atatumaliza.

9. Ajay Gopinath raia wa India. Aliajiriwa kwa nguvu wakati wa makaburu na aliyekuwa mwenyekiti wa bodi Ali Mufuruki. Ajay aliwahi kufukuzwa nchini lakini kwa sababu zake Ali alifanya juu chini na kumrudisha kama mkurugenzi wa mauzo. Anatumiwa katika upatikanaji wa fedha na kutumika vibaya. Hana sauti ndani ya utawala huu kwani ni mgeni.

10. Alphonse Mkinga ni meneja utumishi. Alistaafu na kuchukua mafao yake baada ya makaburu kutimka. Anafanya kazi kwa mkataba na kuzuia ajira kwa waliomaliza vyuo.

Ameidumaza idara ya utumishi kwa kutoweka muundo wa utumishi na taratibu mbalimbali za ajira. Matokeo yake mkurugenzi mkuu huleta watu wake japo wapo waliofanya usaili. Mfano ni ajira ya mhudumu katika ofisi ya mkurugenzi mkuu,ajira ya afisa majengo na mali ambaye ni jamaa yake. Huyu bwana Peter Gosh anachukua nafasi ya bwana Hassan Kikoko alieandamwa na huu mtandao wa ufisadi na hatimaye kuamua kustaafu mapema. Yupo dereva aliajiriwa kwa hila japo wapo waliofanya usaili na hadi sasa hawajapata ajira. Bwana Mkinga hana sauti kwani yupo kulinda maslahi yake baada ya kupata ajira ya pili.

11. Fidelis Tarimo ni mkurugenzi wa uhandisi. Historia yake ni ufisadi mtupu. Aliwahi kusimamishwa kazi na aliyekuwa mwenyekiti wa bodi wakati huo Mzee Abasi Sykes. Tarimo alikwenda kusimamia matengenezo makubwa ya Boeing ya ATC wakati huo (major check) nchini Ireland. Hakuwa anafuatilia gharama halisi za matengenezo na kujali maslahi yake hivyo kusababisha gharama kupanda kwa shilingi bilioni moja na nusu toka ghrama halisi na kulitia shirika hasara na kusimamishwa kazi. Alipata nafasi wakati wa makaburu kwani hakuwa mtetezi wa wazalendo. Kwa sasa wafanyakazi wa idara yake hawamtaki na wameandika barua ya kumkataa na wizara inajua hilo. Ni bingwa wa kuuza ndege za kampuni kwa bei ya kutupwa badala ya ile ya makubaliano ya awali. Ana ukabila na hadi sasa ana jamaa yake anasimamia ujaji wa ndege ya kukodi kwa muda mrefu yuko nje ya nchi. Ni fisadi wa kutupwa kwa ajili ya kutaka pesa za kuendeleza biashara zake.

12. Rajabu Itambo ni meneja Galileo Tanzania kampuni tanzu ya ATCL. Rajabu alipewa kazi ya ushauri katika kitengo cha Galileo na aliyekuwa meneja wakati huo Maalim Ali. Kaburu mmoja aliyekuwa mkurugenzi wa biashara Mike Bond aliamua kumuondoa Maalim Ali katika nafasi hiyo na kumuweka Rajabu kwa maslahi yake kwani walitaka kuuza Galileo kabla ya kuondoka jambo ambalo hawakufanikiwa. Mpaka sasa Rajabu ana uhasidi na wafanyakazi wa zamani kwani anataka awe mkuu wa kitengo cha ITC(Information and Technology Communication) Ni mmoja wa vibaraka wa DM.

Hadi tunakwenda mitamboni ATCL haina bajeti na hili linatokana na Eliasaph kutayarisha bajeti hiyo kwa usiri mkubwa akiweka vipengele hewa ambavyo bodi ina wasiwasi navyo hivyo kuikataa kila wakati. Bajeti huwa inatengenezwa na kitengo maalum katika idara ya fedha lakini safari hii imekuwa na usiri mkubwa. Ilibidi iwekwe hadharani kwa wafanyakazi kupitia workers council ndiyo iifikie bodi jambo ambalo halikufanyika.

Kama tulivyoeleza awali matumizi mabaya ya pesa yanapeleka kampuni kusikoeleweka. Pesa huchotwa kama za mtu binafsi bila kujali taratibu za kihasibu. Viongozi hawa kwa vikundi huenda safari kila wakati kuliko viongozi wote waliopita. Posho wanayolipana ni kubwa mno kwa kila siku hivyo hata safari za watendaji wa chini huenda wao. Mwenyekiti wa bodi Mustapha Nyang'anyi aliliambia Sunday Citizen tarehe 12 januari 2008 kuwa uzembe wa menejimenti ya ATCL kutoingia mkataba na kampuni iliyokuwa ikodishe ndege kwa ajili ya mahujaji ndiyo chanzo cha sakata zima la hasara katika usafirishaji wa mahujaji. Ukweli ni kuwa menejimenti haikutaka kushirikisha wafanyakazi wa kawaida kuratibu safari hii kama ilvyokuwa miaka iliyopita. Hii ni kwasababu walitaka iwe siri yao kwa kutafuta ndege ya bei poa kuliko hiyo iliyopatikana kitu ambacho hakikuzaa matunda na hatimaye kusema ATCL haiwezi kusafirisha mahujaji. Mbona kabla ya makaburu iliwezekana. Hapa pana ufisadi sio uzembe tuu. Wapo wazoefu wa kazi ndani ya kampuni lakini wamekodi mtu wa nje Mtambalike rafiki yake DM kwenda kusimamia kurejea mahujaji. Tunasema hii ni hujuma na kuwadharau watendaji wa ndani.

Magari ya kampuni yamenunuliwa kwa bei kubwa bila kufuata taratibu na viongozi wanne kupata magari kutokana na gharama hiyo kubwa na bila kufuata utaratibu wa ununuzi. Hivi sasa kampuni inamadeni mengi kutokana na ufisadi.

Wafanyakazi wasiotakiwa hasa wale wa zamani hutafutiwa sababu za kuwaondoa ili ajira wapewe watu wa DM. Mifano hai tumetaja hapo juu na mingine mingi tunayo kama ule wa Said Ibrahimu kufanyiwa visa na Mark Manji hadi kuamua kustaafu ili yeye Manji aongeze muda alipoamua kustaafu kwa kisingizio kuwa hakuna wa kuchukua nafasi yake.

Kwa sababu tumezungumza kwa kifupi tunaomba yafanyike yafuatayo:-

1. Kuleta wakaguzi kama vile Enerst and Young kukagua mahesabu ya ATCL tangu DM awe mkurugenzi mkuu. Hapa panatosha kuona ufisadi katika:-

(i) Mikopo na over draft na kutafuta jinsi pesa hizo zilivyotumika kwa ukamilifu.
(ii) Kupata maelezo kutoka kwa DM kwa nini toka achukue uongozi ATCL hakubadilisha muundo na uongozi wa makaburu tukijua fika viongozi hao wana maslahi na makaburu.
(iii) Uchunguzi juu ya ununuzi wa magari bila kufuata kanuni na taratibu za ununuzi nje ya nchi na kulinganisha bei na makampuni mengine ya Dubai
(iv) Wachunguzwe hawa viongozi wanne walipataje magari hayo toka kwa kampuni iliyouza magari kwa ATCL kwa bei ya juu. Kama ni mikopo waoneshe pesa walipata wapi na utaratibu mzima wa kuyalipia na kuingiza na kuyakomboa.
(v) Zipatikane sababu za viongozi kuomba kustaafu na kujiajiri tena.
(vi) Uchunguzi ufanywe kupata uhalali wa wafanyakazi wa zamani kunyanyaswa na wengine kusimamishwa kazi kwa hila ili kuajiri wengine kwa maslahi ya uongozi.
(vii) Uchunguzi ufanywe kuhusu malipo yote kwenye kampuni iliyohifadhi magari toka yatolewe bandarini.
(viii)Uchunguzi ufanywe kuhusu elimu na uwezo wa Peter Gosh kwani aliyeondolewa kwa hila alikuwa Civil Engineer.
(ix) Uchunguzi ufanywe kuhusu safari zote walizosafiri hawa viongozi kama zilileta manufaa. Wamesafiri sana na pesa nyingi zimetumika. Kuna wakati menejimenti yote ilikwenda China kwa pamoja japo waliondoka kwa vikundi.
(x) Mwisho serikali ichukue hatua mapema kabla kampuni haijaangamia. Sisi tuliopo nje na ndani tunaona na tunajua, na kama kutahitajika msaada tupo tayari kutoa ushirikiano.
 
Attachments

  • UFISADI ATCL.doc
    70.5 KB · Views: 145
Mimi ni mmoja kati ya wadau katika sekta hii ya anga. japokuwa sasa hivi siishi Tanzania, lakini nimekuwa karibu na Air Tanzania kwa miaka ishirini na moja (21).

Nimeshuhudia nyakati za uongozi mbalimbali toka kwa Mh. Mwapachu hadi Dumisani Sangweni, takribani CEO wasiopungua kumi (10) kwa idadi yao. Pia nimeshuhudia Wenyeviti mbalimbali kwa kipindi hicho tangu akina Lupembe hadi Ali Mufuruki na huku kukiwa na orodha ndefu ya wakurugenzi kadhaa wa bodi ya Air Tanzania. Pia nimeshuhudia Mawaziri kadhaa tangu akina Mh. Nyang'anyi hadi Mh. Chenge. Kwa kifupi ninachotaka kusema ni kuwa Air Tanzania imepitia katika vipindi vingi vya maamuzi kutoka kwa watu mbalimbali yakiwemo yaliyokuwa mazuri na hata yale ambayo yalikuwa mabaya zaidi kuliko wakati mwingine wowote.

Nimesoma kwa makini yaliyoandikwa hapo juu na Bongoson, inanikumbusha wakati wangu wa mwisho katika kipindi cha Dumisani Sangweni, Ali Mufuruki na Basil Mramba. Kipindi hiki hawa watu watatu muhimu kila mmoja alighubikwa na maslahi binafsi. Dumisani kama 'agent' wa SAA alikuwa na kazi moja kubwa kuhakikisha kuwa ATCL inaondoka katika biashara kabisa. Na alipewa jukumu hili hata kabla ya SAA haijasaini mkataba wa kununua zile hisa 49% za serikali ndani ya ATCL. Yeye ndiye aliyekuwa ATCL Desk Officer kule SAA akishirikiana na mwenzie Mike Bond ambaye baadae alikuja kufanywa Mkurugenzi wa Biashara wa ATCL. Kuhakisha kuwa Dumisani anasimamia vema mauaji ya ATCL ndiye mkurugenzi pekee wa iliyokuwa bodi ya ATCL chini ya makaburu ambaye alitumikia toka mwanzo hadi mwisho. Na akiwa 'agent' wa SAA alijitahidi kujipenyeza kwa watu mbalimbali na hata ilibidi kuoa mtanzania. Aliweza pia kufanya urafiki na David Mataka kabla ya david kuteuliwa kuwa CEO wa Air Tanzania, kuna nyakati David alikuwa akifika ofisini kwa Dumisani kumtembelea.

Kwa hiyo sitashangaa sana kama Dumisani influence kama 'agent' wa SAA imefanya kazi ya kumuingiza David hapo alipo na inaendelea kufanya kazi iliyokusudiwa. Moja kati ya kazi kubwa iliyofanywa na Dumisani tangu SAA iliponunua hisa ATCL ni kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanagawanywa kadri inavyowezekana na ikibidi wawe frustrated kwa kiwango cha wao kuacha kazi. na hili liliweza kufanyika kikamilifu, kwani wale wote ambao walikuwa ni watendaji wazuri waliwekwa katika mazingira ya kuacha kazi wao wenyewe au kuondolewa. Kwa mfano Mama Ngulukulu ambaye alibidi aachie ngazi mwenyewe lakini sasa hivi amerudi Air Tanzania kama mkurugenzi wa Bodi na pia amekuwa na wadhifa huo Katika Mamlaka ya Usimamizi wa shughuli za anga Tanzania TCAA. Huyu ni mmoja kati ya watu ambao anaifahamu sekta ya anga kwa kikamilifu kabisa. Samahani nimemtaja huyu mama kama kielelezo tu, lakini kuna watu wengi wa kada mbalimbali ambao walitengwa kwa makusudi ili waweze kujiondoa ATCL. Kwa hakika Dumisani alifanikiwa katika hili.

Ali Mufuruki, pamoja na kwamba sina sifa ya kuingilia kazi au uteuzi wa Mh. Rais, lakini ninapinga vikali kabisa uteuzi wa Ali Mufuruki katika chombo chochote cha umma. Amekosa kabisa sifa ya uzalendo zaidi ya kutumia nyadhifa anazopewa kama ndiyo kazi yake ya kwanza. Katika vipindi vyote ambavyo nimeona bodi mbalimbali za Air Tanzania, nadiriki kusema kuwa Ali ndiye amekuwa mwenyekiti 'mbovu' zaidi kuliko wabovu wengine. Kama mwenyekiti wa Bodi alikosa vision ya kuliongoza shirika kwa kipindi chote na hatimaye kuingiza serikali kati hasara kubwa juu ya ATCL. Yeye Akiwa kama mwenyekiti wa bodi ya ATCL anayewakilisha maslahi ya mbia serikali, hakuwa anaifahamisha serikali ukweli wa mambo yanayoendelea ndani ya Kampuni kwa sababu tayari alikuwa ameshakumbwa na mdudu maslahi binafsi. Kwa kuanzia, menejimenti ya ATCL walihakikisha kuwa wanampatia safari za kwenda huku na kule hata pale ambapo siyo lazima na ikiwemo kumlipia hata safari za kazi zake binafsi (Ushahidi upo katika nyaraka za ofisi pale ATC House).

Kuipatia kampuni yake binafsi ya M&M kazi ya ATCL Public Relations bila ya kufuata taratibu za kizabuni (Ushahidi juu ya hili upo pia katika nyaraka pale ATC House)

Kana kwamba haitoshi alikuwa na msukumo wa kuanzisha kampuni yao ya ndege kule Uganda ya Victoria International Airlines. hii Kampuni ilianzishwa na Mtendaji wake mkuu akiwa baba mzazi wa mkurugenzi wa biashara wa wakati huo Mike Bond. Ali katika hii kampuni hisa zake ni 9% ambazo kuzipata kwake ilikuwa ni rahisi nayo kuhakisha kuwa ATCL inaingia mikataba migumu na Victoria Airlines kwa manufaa ya Victoria Airlines. Hii kampunia ya Victoria ilianzishwa kule Uganda, lakini hali ya hewa iliyochafuka kati ya SAA na Serikali juu ya mustakabali wa ATCL ilisitisha shughuli za Victoria Airlines na hatimaye kufa kabisa, kwani uhai wa Victoria Airlines ulitegemea sana mikataba yake na ATCL. Hii ni hujuma kubwa sana ambayo ingelikumba Shirika kutokana tamaa ya maslahi binafsi ( na siku hizi tunaambiwa yanafanywa kisayansi zaidi, kwa maana watu wanaangalia sheria zina wakataza wapi kwa hiyo wao wapindishe wapi).

Ali Mufuruki akishirikiana na 'maagent' wa SAA walihakikisha kuwa wanawaondoa wafanyakazi wale wote ambao wanaonyesha uzalendo wa kweli kwa Air Tanzania, aidha aliwatisha hata kwa kuwasimamisha kazi ikibidi. Kwa mfano walimfukuza kazi Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi tawi la ATC House kwa njama ambazo zilisukwa. Walimfukuza kazi Meneja wa ATCL Mwanza Bw. Gideon Kamanga kwa sababu tu alikuwa anapigania ATCL. Naye aliyekuwa katibu wa chama cha wafanyakazi ATC House Bw. Kitogo aliamua kujiondoa ATCL kwa sababu ya kutokukubaliana uozo uliokuwepo. Pia kuondoka kwa katibu huyo kunatokana na kufichua serikalini kwamba Ali Mufuruki na Menejimenti yake vimemuajiri mgeni toka Ajay Gopinath bila ya kufuata taratibu stahili zikiwemo za uhamiaji, matokeo yake ni kuwa mgeni huyo aliondolewa nchini kwa kukiuka taratibu za nchi. Lakini kwa manufaa binafsi Ali Mufuruki aliitisha mkutano wa wafanyakazi wote na kuwaambia kuwa atafanya kila atakaloweza ikiwa ni pamoja na kutumia nafasi yake kama mjumbe wa bodi ya TIC kumrudisha huyo mgeni nchini kwa vile hajaona mtazania yeyote anayefaa kusfanya kazi zake. Baada ya hapo menejimenti ilihakikisha kuwa na yule mtoa taarifa ambaye ni katibu wa wafanyakazi aondoke, na kweli ilibidi aondoke kwa shinikizo.

Usimamizi wa Mapato: Chini ya uongozi wa Ali Mufuruki alishindwa kabisa kusimamia na kulinda mapato ya ATCL, yapo mengi lakini nitatoa mifano mitatu;

Wa kwanza;
Akijua kabisa mkataba kati ya SAA na serikali ulielekeza kuwa tiketi za Air Tanzania zirudishwe ndani ya miezi 36 tangu kuanza kwa mkataba, kwa makusudi kabisa hata baada ya kumazilika miezi 36 mauzo yote ya ATCL yaliendelea kufanyika kwa kutumia tiketi za SAA na hivyo SAA kuendelea kuchukua mapato yote ya ATCL na kuyahamishia Johannesburg. Akiwa mwenyekiti wa Bodi hakuweza kujua mapato halisi ya ATCL katika kipindi chake chote alipokuwa ATCL.

Wa Pili;
Alishindwa kuichukulia menejimenti hatua zipasazo baada ya wafanyakazi kubaini ubadhirifu mkubwa wa mapato katika kitengo cha mizigo. Ubadhirifu huo ulihusisha makampuni ya Elizabeth Consultants na Sunfresh / Freight in time. Fedha hizo za ATCL zilipotea kabisa wakati akiwa na taarifa kwa wakati muafaka.

Wa Tatu,
Ali Mufuruki ameisimamia ATCL kwa kipindi chote hicho bila hata kuwa na bajeti ya uendeshaji wa shughuli za ATCL hata mara moja. Jambo hili lilifanywa makusudi ili kuficha hali halisi ya mambo ndani ya ATCL. Inashangaza kwa zaidi ya miaka minne kampuni haikuendeshwa kwa kufuata maadili na misingi bora ya uwajibikaji.

Mh. Mramba, akiwa waziri wa miundo mbinu, naye alishindwa kuchukua hatua dhidi ya mwenyekiti na watendaji wengine kwa sababu anatajwa kuwa ana maslahi binafsi ndani ya Precision Air. Ikumbukwe kuwa kabla ya kurudi kwenye duru la uwaziri Mh. Mramba alikuwa ni Mwenyekiti wa Precision Air. Mh. Mramba alionekana dhahiri kuipa kisogo ATCL baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Miundo mbinu kwa aliweza kutembelea mashirika yote yaliyochini ya wizara yake isipokuwa ATCL peke yake. Juhudi mbalimbali zilifanywa na wafanyakazi ikiwa ni pamoja na kuwatuma viongozi wake kwenda kumuona lakini mara zote waliishia kwa katibu wake Bw. Martin Ntemo. hali iliendelea hivyo hadi hapo Mh. Mramba alipohamishwa kupelekwa wizara nyingine. Ni imani kwamba Mh. Mramba alikuwa anasukumwa na maslahi binafsi.

MAPUNGUFU YA SASA HIVI NDANI YA ATCL
pamoja na sifa nyingi ambazo alipewa Bw. David Mataka wakati anateuliwa kuwa CEO wa ATCL, lakini sasa ni dhahiri ameonesha udhaifu mkubwa sana. Nina imani pia huenda kumekuwa na KOSA LA MSINGI kabisa katika kumshauri Mh. Rais juu ya uteuzi wa mtendaji mkuu huyu. Kwa sababu tangu amekuwa uongozini hadi sasa alitarajiwa kuwa na timu yenye kuonyesha mafanikio badala ya udhaifu. Na katika uzoefu wangu kama hali iliyofikia ATCL ni kama ilivyodokezwa, basi tusitegemee kama ATCL itakwamuka hapo ilipo, hata ikija miujiza gani.
Vilevile inaonekana kuwa Bw David Mataka anatumia udhaifu wa watendaji waliomzunguka katika kufanikisha maslahi yake binafsi ikiwa ni pamoja kutaka kurudi kwenye 'chati'. Wengi ya waliotajwa hapo ni watendaji dhaifu sana, ambao wako tayari kufanya lolote ili mradi wajipatie chochote kwa mfano:

Amini Mziray huyu ni sehemu ya matatizo yaliyopo sasa hivi ATCL, kwani yeye alitumika sana wakati wa makaburu na huku akijua yanayoendelea ni maovu, alikaa kimyaa ili mradi anapata senti yake ya bia jioni.

Alphonce Mkinga, huyu ni mtu ambaye kwanza hajiamini yeye mwenyewe, wakati wa makaburu alitumika kuwakandamiza wafanyakazi wakati akijua kufanya hivyo ni kosa na ni kinyume na maadili ya kazi yake. Amehusika sana katika kupanga njama dhidi ya wafanyakazi.

Mark Manji, Alitumiwa kubariki mipango mbalimbali ya makusudi dhidi ya ATCL hasa kati upande wa uendeshaji, alifahamu madhila makubwa yaliyokuwa yanaipata ATCL dhidi ya ndege za kukodi hususani Fokker 28, lakini hakusema lolote ili mradi biashara zake zinakwenda vizuri.

Eliasaph, huyu ni opportunist, hayuko hapo kwa ajili ya ATCL, yeye ni 'kikosi cha mizinga' kwa kiswahili cha Dar. Anasuburi tu wakati wake ukifika ataondoka anachokifanya hapo kula atakavyoweza kutokana na timu ya ulaji ilivyo. Watu kama hawa hutumia udhaifu wa walio juu yao.

Rajabu Itambo, huyu ni Mkenya alikuja kutafuta 'rizki' kwa bahati nzuri au mbaya akakutana mazingira yanamruhusu kujipenyeza, alitumia mwanya wa makaburu kuwatenga wazawa na yeye kujitafutia ajira ya kudumu.

Ajay Gopinath, huyu hana sifa ya kuendelea kuishi na kufanya kazi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa vile tayari alishavunja taratibu na sheria za nchi na kuondolewa ndani ya masaa 72.

Heho Mbihu, huyu naye ni mkenya ambaye amepandikizwa na Kenya Airways. Juhudi za Kenya Airways ni kuhakikisha inaibana Air Tanzania ndani ya ardhi yake ili isiweze kufurukuta. Ikumbukwe kwamba hasimu mkubwa yaani South African Airways (SAA) ilipoingiangia Afrika Mashariki kwa kununua hisa ATCL ilibidi Kenya Airways iingie ndani ya nchi yetu kwa kununua Precision Air. Kwa hiyo mbinu mbalimbali zinafanywa na ili kuhakikisha mikakati yote ya kibiashara ya ATCL inajulikana mapema ili kuona kama inaweza kuwa athari au la. Kwa upande wa SAA, hawa watu waliletwa wabaki kama informers wao endapo ndoa kati kati ya SAA na Serikali itavunjika. Na waliwekwa katika nafasi za kufanya maamuzi.

Ushauri:
Kwa vile serikali imeamua kwa dhati kabisa kuiimarisha Air Tanzania, pamoja na mambo mengine haina budi kuhakikisha inaunda Management Team itakayokuwa makini zaidi. Vilevile ni muhimu kwa sasa kukodisha management toka kwenye makampuni yaliyobobea katika utoaji wa huduma airline management kwa kukodi walau kwa miaka miwili. jambo hili ni la kawaida sana na liliwahi kufanywa na Kenya Airways wakati wa walipobinafsisha waliwakodisha Speedwing Brian akiwa CEO.

Hii itasaidia kuwapa uwezo wazalendo kushiriki katika mchakato wa kupata menejimenti iliyo bora baada ya muda wa mkataba kuisha.

Faida nyingine itaondoa wale watendaji 'wapambe' ambao wapo ATCL kwa ajili ya kumpendezesha CEO.
LINALOWEZEKANA LEO LISINGOJE KESHO
 
Guyz haya ni ya ndugu zetu waliopo ndani ya AIR TANZANIA

Sisi wananchi tuliyo ndani na nje ya ATCL tumeona hatuwezi kukaa kimya tukiangalia jinsi kampuni inavyoangamia kwa ufisadi wa kisayansi.

Ufisadi wa kisayansi kwa sababu wanaofanya ufisadi huu ni uongozi wa kampuni kwa kutumia nafasi zao za madaraka na kujifanya huo ndio uongozi.

Tuanze kwa kueleza ni maeneo gani yenye ufisadi halafu tutaje viongozi hao na sifa zao.

Tutataja maeneo yenye ufisadi na matumizi mabaya ya mapato ya kampuni na mikopo toka mabenki mbalimbali.Pia safari zilizo nyingi na za muda mrefu bila kujali gharama na faida za safari hizo.Manunuzi ya magari kwa fedha za mikopo na bila kufuata taratibu. Mwisho ni hila za kuwafukuza ama kuwaondoa katika nafasi nyeti wafanyakazi wa zamani na kuweka wapya ambao huajiriwa kiholela na bila ya sifa zinazolingana na kazi zenyewe au hata na wale waliyoondolewa.
Jopo la viongozi na sifa zao zinazoangamiza kampuni ni:-

1. Mkurugenzi mkuu wa kampuni ni David Mataka. Yeye aliteuliwa na Rais JK baada ya rais aliyemtangulia kumtimua kwa ufisadi. JK alimuonea huruma DM baada ya kukaa ubaoni kwa muda na pia kushindwa kinyang'anyiro cha ubunge kwa tiketi ya chama tawala. Wananchi wa jimbo lake na wa chama chake hawakumpa kura kwa kuwa alikwisha onekana mbele ya rais BM kuwa ni fisadi wa hali ya juu japo yeye rais BM alikuwa anawakumbatia mafisadi kama Balali.
Mkuu huyu wa kampuni ameanzisha uongozi wa dharura(Management by crisis) ambapo kila asubuhi wakurugenzi na mameneja wateule katika ufisadi hukaa vikao vya kuangamiza kampuni. Amepata Benz ya kisasa katika mgao wa magari yaliyotolewa na wauzaji baada ya kununua magari ya kampuni huko Dubai kwa bei ya juu. Magari hayo ni ya mwaka 1998 japo bei yake ni karibu na mara mbili ya yale yanayouzwa na makampuni mengine ya Dubai.
Yeye huwa anasuka jambo halafu anamwachia George, Eliasaph au William walichochee katika kikao cha hao viongozi.

2. Mark Manji yeye ni mtu wa Musoma japo jina lake la kihindi. Huyu ni mshauri wa mkurugenzi mkuu. Alikuwa mkurugenzi wa idara ya operations wakati wa makaburu japo idara hii huwa inaongozwa na marubani. Alipewa cheo hiki na makaburu ili kuwaweka marubani katika himaya ya makundi.
Makaburu walipoondoka aliomba kuacha kazi kwa hiari na akastaafu akaomba kuendelea na kazi tena kama mshauri wa mkurugenzi mkuu. Kwa kuwa alikuwa na mapenzi na makaburu na kwa kuwa ameshapata mafao yake, hana huruma na kampuni kwa sasa badala yake yeye ni kichocheo na hujifanya analijua shirika. Anatumia utoto wa mjini kufanya kazi kwani hana shahada hata moja japo amepewa nafasi nyeti.

3. Eliasaph Mathew aliajiriwa na makaburu kama meneja wa fedha kwa maana hiyo ni mtu wa makaburu. Baada ya mkurugenzi wa fedha aliyekuwa kaburu kuondoka amekaimu nafasi hiyo hadi leo. Huyu ndie kinara wa kupindisha taratibu za matumizi ya fedha na ununuzi. Ni mfuasi namba moja wa DM kwani kwa sasa pesa za kampuni hutolewa kiholela kulipia gharama kwa ufisadi. Mfano kabla ya kufunga mwaka 2007 shillingi millioni mia mbili hamsini zilichotwa kulipa gharama za kutoa magari nane yaliyokuwa katika yadi ya kuweka mgari iliyo ya watu binafsi. Haishi hapo huchota dola elfu tatu taslimu toka kwa mtunza fedha kila mwezi na kumpa huyu mwenye yadi ya kuhifadhi magari. Huidhinisha malipo kwa ankara tu bila kujali taratibu nyingine. Ndiye aliyejumuika katika jopo lililokwenda Dubai kuchagua magari ya kampuni na kuyanunua kwa bei mbaya bila kufuata taratibu za ununuzi. Magari haya ni ya 1998 japo ATCL ni mali ya serikali,hilo halikutiliwa maanani. Yeye amepata zawadi ya VX Landcruiser ya kisasa kama mgao katika hayo manunuzi na sasa ameweka pembeni Vitara yake. Hutumiwa katika mikakati ya kuwaondoa watu wa zamani na wenye sifa kwa kuwazulia kesi na shutuma za matumizi mabaya ya pesa kitu ambacho si kweli.
Waliyoonja joto hilo ni pamoja na Hassani ambaye aliamua kuacha kazi, Hamisi na Mndeme ambao wamesimamishwa kwa suala la bwana Mohamed Makaratasi ambaye ni rafiki wa George Mazula.

4.George Mazula yeye eti ndiye rubani kiongozi na mshauri wa DM. Huyu aliwahi kuachishwa kazi wakati mwenyekiti wa bodi alikuwa ni Abasi Sykes. George aliwahi kuunguza injini mbili za Fokker kwa mpigo pale Tanga. Amewahi kuangusha ndege aina ya Fokker hapa Dar es salaam.
Amewahi kuua mtu pale uwanja mpya wa JK Nyerere kwa kukatwa na pangaboi baada ya yeye kuzembea kuzima injini. George ni kiungo wa mikakati yote ya ufisadi na kuondolewa watu katika nafasi zao. Alikuwa mfadhili wa DM wakati akiwa ubaoni. Ni rubani mwenye makeke na mikosi mingi. Katika dili ya Dubai yeye amepata Volvo na kujidai amekopa.

5. Amin Mziray huyu ni katibu wa kampuni. Yeye ni chapombe. Alipewa gari ya kampuni na makaburu na kulipindua kwa ulevi. Anayo shahada ya sheria lakini haitumii kwa maslahi ya kampuni. Kampuni imeshindwa kesi nyingi kwa kutokuwa makini huyu mwanasheria. Yumo katika hili jopo la ufisadi wa kampuni. Katika mgao wa magari ya Dubai yeye amepata VX Landcruiser la nguvu. Hayupo tayari kutetea hoja mbovu zinazotolewa ndani ya vikao vya hili jopo la ufisadi.

6. William Haji, anakaimu nafasi ya mkaguzi mahesabu wa ndani.
Aliajiriwa wakati wa makaburu kama mkaguzi wa mahesabu wa ndani chini ya bwana Yakubu. Baada ya muda bwana YAkubu aliwekwa pembeni na huyu bwana kukaimu nafasi yake. Kwa sasa yeye ndiye anayekagua malipo (Pre-audit) hivyo yumo ndani ya mtandao wa ulaji. Ndiye anayetumiwa kutengeneza taarifa za kuzua kesi na uonevu kwa wafanyakazi wa chini. Huchukua nafasi ya afisa usalama wa kampuni ili kupindisha ukweli na hatimaye kuwadhalilisha ama kuwatimua wafanyakazi wasiyo na hatia. Ni hatari sana kwani yupo karibu na DM na Eliasaph katika kila mpango.

7. Sadiki Muze, Yeye ni mkurugenzi wa idara ya operations kwa sasa.
Amepewa nafasi hiyo yeye kwani ndiye aliyekuwa mfadhili mkuu wa DM wakati akiwa ubaoni. Pia ni mshirika wa DM katika vinywaji na mwanachama wa kijiwe kimoja na George. Ni Sadiki na George pekee waliyopewa vyeo na kuenguliwa wengine baada ya DM kuchukuwa uongozi ATCL na ni chapombe.
Sadiki na George wamelipwa fadhila.

8. Heho Mbiru ni Mkenya, aliajiriwa kwa nguvu enzi za makaburu kama mkurugenzi wa masoko. Aliajiriwa kwa nguvu na aliyekuwa mwenyekiti wa bodi ya ATCL wakati huo Ali Mufuruki kwa kisingizio kuwa hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kushika nafasi hiyo. Ni mzalendo wa Kenya kweli kweli kwani kazi zinazoweza kufanyika hapa (kama Graphics) huzipeleka kwenye kampuni yake. Anayo mapenzi na makaburu hivyo kuleta mabadiliko tunayotaka yeye ni kikwazo na ndiyo maana ni rahisi kutumiwa katika hujuma. Kumbuka tunaushindani na Kenya Airways huyu atatumaliza.

9. Ajay Gopinath raia wa India. Aliajiriwa kwa nguvu wakati wa makaburu na aliyekuwa mwenyekiti wa bodi Ali Mufuruki. Ajay aliwahi kufukuzwa nchini lakini kwa sababu zake Ali alifanya juu chini na kumrudisha kama mkurugenzi wa mauzo. Anatumiwa katika upatikanaji wa fedha na kutumika vibaya. Hana sauti ndani ya utawala huu kwani ni mgeni.

10. Alphonse Mkinga ni meneja utumishi. Alistaafu na kuchukua mafao yake baada ya makaburu kutimka. Anafanya kazi kwa mkataba na kuzuia ajira kwa waliomaliza vyuo.
Ameidumaza idara ya utumishi kwa kutoweka muundo wa utumishi na taratibu mbalimbali za ajira. Matokeo yake mkurugenzi mkuu huleta watu wake japo wapo waliofanya usaili. Mfano ni ajira ya mhudumu katika ofisi ya mkurugenzi mkuu,ajira ya afisa majengo na mali ambaye ni jamaa yake.
Huyu bwana Peter Gosh anachukua nafasi ya bwana Hassan Kikoko alieandamwa na huu mtandao wa ufisadi na hatimaye kuamua kustaafu mapema. Yupo dereva aliajiriwa kwa hila japo wapo waliofanya usaili na hadi sasa hawajapata ajira. Bwana Mkinga hana sauti kwani yupo kulinda maslahi yake baada ya kupata ajira ya pili.

11. Fidelis Tarimo ni mkurugenzi wa uhandisi. Historia yake ni ufisadi mtupu. Aliwahi kusimamishwa kazi na aliyekuwa mwenyekiti wa bodi wakati huo Mzee Abasi Sykes. Tarimo alikwenda kusimamia matengenezo makubwa ya Boeing ya ATC wakati huo (major check) nchini Ireland. Hakuwa anafuatilia gharama halisi za matengenezo na kujali maslahi yake hivyo kusababisha gharama kupanda kwa shilingi bilioni moja na nusu toka ghrama halisi na kulitia shirika hasara na kusimamishwa kazi. Alipata nafasi wakati wa makaburu kwani hakuwa mtetezi wa wazalendo. Kwa sasa wafanyakazi wa idara yake hawamtaki na wameandika barua ya kumkataa na wizara inajua hilo. Ni bingwa wa kuuza ndege za kampuni kwa bei ya kutupwa badala ya ile ya makubaliano ya awali. Ana ukabila na hadi sasa ana jamaa yake anasimamia ujaji wa ndege ya kukodi kwa muda mrefu yuko nje ya nchi. Ni fisadi wa kutupwa kwa ajili ya kutaka pesa za kuendeleza biashara zake.

12. Rajabu Itambo ni meneja Galileo Tanzania kampuni tanzu ya ATCL.
Rajabu alipewa kazi ya ushauri katika kitengo cha Galileo na aliyekuwa meneja wakati huo Maalim Ali. Kaburu mmoja aliyekuwa mkurugenzi wa biashara Mike Bond aliamua kumuondoa Maalim Ali katika nafasi hiyo na kumuweka Rajabu kwa maslahi yake kwani walitaka kuuza Galileo kabla ya kuondoka jambo ambalo hawakufanikiwa. Mpaka sasa Rajabu ana uhasidi na wafanyakazi wa zamani kwani anataka awe mkuu wa kitengo cha ITC(Information and Technology Communication) Ni mmoja wa vibaraka wa DM.

Hadi tunakwenda mitamboni ATCL haina bajeti na hili linatokana na Eliasaph kutayarisha bajeti hiyo kwa usiri mkubwa akiweka vipengele hewa ambavyo bodi ina wasiwasi navyo hivyo kuikataa kila wakati. Bajeti huwa inatengenezwa na kitengo maalum katika idara ya fedha lakini safari hii imekuwa na usiri mkubwa. Ilibidi iwekwe hadharani kwa wafanyakazi kupitia workers council ndiyo iifikie bodi jambo ambalo halikufanyika.

Kama tulivyoeleza awali matumizi mabaya ya pesa yanapeleka kampuni kusikoeleweka. Pesa huchotwa kama za mtu binafsi bila kujali taratibu za kihasibu. Viongozi hawa kwa vikundi huenda safari kila wakati kuliko viongozi wote waliopita. Posho wanayolipana ni kubwa mno kwa kila siku hivyo hata safari za watendaji wa chini huenda wao. Mwenyekiti wa bodi Mustapha Nyang'anyi aliliambia Sunday Citizen tarehe 12 januari 2008 kuwa uzembe wa menejimenti ya ATCL kutoingia mkataba na kampuni iliyokuwa ikodishe ndege kwa ajili ya mahujaji ndiyo chanzo cha sakata zima la hasara katika usafirishaji wa mahujaji. Ukweli ni kuwa menejimenti haikutaka kushirikisha wafanyakazi wa kawaida kuratibu safari hii kama ilvyokuwa miaka iliyopita. Hii ni kwasababu walitaka iwe siri yao kwa kutafuta ndege ya bei poa kuliko hiyo iliyopatikana kitu ambacho hakikuzaa matunda na hatimaye kusema ATCL haiwezi kusafirisha mahujaji. Mbona kabla ya makaburu iliwezekana. Hapa pana ufisadi sio uzembe tuu. Wapo wazoefu wa kazi ndani ya kampuni lakini wamekodi mtu wa nje Mtambalike rafiki yake DM kwenda kusimamia kurejea mahujaji.
Tunasema hii ni hujuma na kuwadharau watendaji wa ndani.
Magari ya kampuni yamenunuliwa kwa bei kubwa bila kufuata taratibu na viongozi wanne kupata magari kutokana na gharama hiyo kubwa na bila kufuata utaratibu wa ununuzi. Hivi sasa kampuni inamadeni mengi kutokana na ufisadi.
Wafanyakazi wasiotakiwa hasa wale wa zamani hutafutiwa sababu za kuwaondoa ili ajira wapewe watu wa DM. Mifano hai tumetaja hapo juu na mingine mingi tunayo kama ule wa Said Ibrahimu kufanyiwa visa na Mark Manji hadi kuamua kustaafu ili yeye Manji aongeze muda alipoamua kustaafu kwa kisingizio kuwa hakuna wa kuchukua nafasi yake.

Kwa sababu tumezungumza kwa kifupi tunaomba yafanyike yafuatayo:-

1. Kuleta wakaguzi kama vile Enerst and Young kukagua mahesabu ya ATCL tangu DM awe mkurugenzi mkuu. Hapa panatosha kuona ufisadi katika:-

(i) Mikopo na over draft na kutafuta jinsi pesa hizo zilivyotumika kwa ukamilifu.

(ii) Kupata maelezo kutoka kwa DM kwa nini toka achukue uongozi ATCL hakubadilisha muundo na uongozi wa makaburu tukijua fika viongozi hao wana maslahi na makaburu.

(iii) Uchunguzi juu ya ununuzi wa magari bila kufuata kanuni na taratibu za ununuzi nje ya nchi na kulinganisha bei na makampuni mengine ya Dubai

(iv) Wachunguzwe hawa viongozi wanne walipataje magari hayo toka kwa kampuni iliyouza magari kwa ATCL kwa bei ya juu. Kama ni mikopo waoneshe pesa walipata wapi na utaratibu mzima wa kuyalipia na kuingiza na kuyakomboa.

(v) Zipatikane sababu za viongozi kuomba kustaafu na kujiajiri tena.

(vi) Uchunguzi ufanywe kupata uhalali wa wafanyakazi wa zamani kunyanyaswa na wengine kusimamishwa kazi kwa hila ili kuajiri wengine kwa maslahi ya uongozi.

(vii) Uchunguzi ufanywe kuhusu malipo yote kwenye kampuni iliyohifadhi magari toka yatolewe bandarini.

(viii)Uchunguzi ufanywe kuhusu elimu na uwezo wa Peter Gosh kwani aliyeondolewa kwa hila alikuwa Civil Engineer.

(ix) Uchunguzi ufanywe kuhusu safari zote walizosafiri hawa viongozi kama zilileta manufaa. Wamesafiri sana na pesa nyingi zimetumika. Kuna wakati menejimenti yote ilikwenda China kwa pamoja japo waliondoka kwa vikundi.

(x) Mwisho serikali ichukue hatua mapema kabla kampuni haijaangamia.
Sisi tuliopo nje na ndani tunaona na tunajua, na kama kutahitajika msaada tupo tayari kutoa ushirikiano.
 
Kama haya ni ya kweli basi ng'ombe wa masikini hazai.

Yaani kabulu alipoondoka tulifikiri mambo sasa yanajipa tunaanza kutangaza jina ulimwengu mzima kwa kasi mpya kumbe tunapiga maendeleo kwa kwenda nyuma. Huyu mkenya inawezekana kwani na nembo mpya imeigwa toka Kenya airways.

Tatizo la kupeana madaraka kiushikaji
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom