Askofu Gwajima apekuliwa na Polisi nyumbani kwake, bado anashikiliwa kituoni

Kwani we unayajua matunda aliyoyalenga yeye? Hii vita ngumu sana kwa asiyeianzisha, maana hatujui nini matarajio ya muanzishaji ikiwa wanaochunguzwa wanataarifiwa
kwahiyo unahisi itafanikiwa kwa makonda na dar peke yake bila saport ya police na waziri mwenye dhamani na jamii kwa ujumla kama sasa tunaingia vitani kama kitu kimoja?
 
Hapo Jana Askofu Mkuu wa makanisa ya Ufufuo na Uzima Duniani, Dr Josephat Gwajima aliitikia wito wa polisi, baada ya mahojiano polisi waliamua kwenda kukagua nyumbani kwake, Salasala Dar es Salaam.

Upekuzi ulianza na kumalizika kukiwa na police wa upelelezi zaidi ya sita na ushahidi wa majirani wawili. Mara baada ya upekuzi walisainiana ripoti ya ukaguzi Mbele ya mashahidi hao kukiwa hakuna kitu chochote kilichopatikana kinachohusishwa na dawa za kulevya au bangi.

Baada ya ukaguzi huo polisi waliondoka na Askofu Mkuu Dr Josephat Gwajima na kurudi naye central police majira ya saa nne usiku kwa mahojiano zaidi ambapo hadi muda huu bado wamemshikilia.

Nitawaletea Updates zaidi.
safii
 
kwahiyo unahisi itafanikiwa kwa makonda na dar peke yake bila saport ya police na waziri mwenye dhamani na jamii kwa ujumla kama sasa tunaingia vitani kama kitu kimoja?
Yeye mwenyewe haoneshi dalili ya kuhitaji hiyo sapoti. Usije siku moja ukajichanganya kujiunga na mtu anayekimbia alfajiri mtaani ukadhani anafanya mazoezi, kumbe mwenzako anakimbizwa na ng'ombe.
 
Kosa alilofanya makonda ni kuruka media,hata kama gwajima ni druglord,alikuwa na mda mwingi tu wa kuhamisha ushahidi,
hii inaitwa kutwanga maji kwenye kinu
Ni kweli,kama hakuliona hilo mapema na baadhi inawezekana wamesepa nje ya nchi.
 
Kesi kivipi wakati hawana ushaidi?
i mean gwajima na wote waliodhalilishwa kuwafungulia!!!! kesi kwanini wamewatangaza publicly kwa mambo ambayo hawana uhakika nayo?
impact yake ni kubwa sana kwa jamii kwenye shughuli zao mfano leo nimekatisha mitaani wakati nakuja kazini nasikia mashabiki wa simba wanawaita mashabiki wa yanga timu ya sembe, what about quality group,na kina wema kwanini wasingwavamia wakawasachi wakawahoji kisha ndo wakaja hadharani kutangaza kuwa fulani anauza sembe?
kwa kuwaarifu tu kuwa wao ni watuhumiwa wa sembe huoni kuwa kama walikuwa na maunga yao wangeyaficha na kuyapoteza kabisa ? umpe mtu masaa hata mawili ya kuripoti kituoni kwa kosa fulani unadhani hatapoteza ushahidi?
hivi makonda ana vita ya unga .......... ? like seriously?
ninaclip hapa unga umefichwa kwenye vitunguu maji ........ hii sio vita ya unga ni vita wanavyojua jina hao wanaovifanya ...na si vya unga kama wanavyotuaminisha....
unga is something else, inahitaji umoja ,ushirikiano, dhamira ya dhati na ukweli.. ili kudhibiti unga
,
huu utoto unaoendelea wa kuitana central ni upotezaji wa wakati na kudhalilisha watu na kupoteza kodi zetu ifike mahali serikali ya ccm iache kucheza na akili za watanzania wawe na mikakati madhubuti ya kupambana na umasikini, rushwa ,ufisadi,madawa ya kulevya
tupate elimu bora ,miundo mbinu nk
sio kila siku kutafuta attention ya uma bila sababu za msingi....... kunasiku tutawadai!!!
huku kutuhangaisha kote kutuambia tufanyekazi ni kama tunawafanyia ccm tu maana tunalipishwa kodi lakini hazitumiki ipasavyo kutupatia mahitaji yetu zaidi inatumika kukimbizana na wapinzani

my friend tunahtaji, viwanda /ajira ,shule zenye waalimu wa kukidhi haja miundombinu nk na sio matangazo ya clouds tv ambayo couvarage yake ni dar tu wala kijijini kwetu haifiki wala hawajui kinachoendlea:(:(:(:cool::cool::cool::cool::cool::cool:

mimi nimeichoka ccm inatuumiza sana watz
 
Nawashangaa mnaosema approach anayotumia makonda sio nzuri...approach gani nzuri iliyoleta mafanikio kwenye hui vita?acheni blah blah
Uko sawa mkuu,
Approach wanayoi_support ni ile ya kukaa na list tu.

Bora hata hii ya ku_shake the transparent bottle ili kujua kama kuna kimiminika, na kama hakuna hiyo chupa weka pale pale ilipokuwa.
Kekweli kabisa mkuu
 
Hakuna anayepingana na makonda kwwnye hii vita ila aproach anayotumia ndio haiwezi kuzaa matunda

Approach yake inajustify dhamira yake. Heka heka hizii hazimaanishi ana uchungu na taifa. anajenga jina kwa waamuzi wa hatma yake ambao ameshawajua wanaamua kwa emotions. Usisahau alikuwa akikaa kwa Mwembe. Kumbuka alivyomdhalilisha Warioba na kutengeneza sababu ya kuzuia mjadala wa katiba inayoliliwa na Watz hadi leo na namna alivyopewa cheo. Kumbuka uhusiano wake na aliyemfunga viatu na familia ile. Oanisha uhusiano wa kaya ile kaya ya yanayosumbua nchi kwa sasa.

Watanzania fungueni macho. Nchi haiwezi kwenda kwa sarakasi zenye nia ya kuptosha kweli na kulilnda uovu.

Makonda!!!!!!!!
 
Nimegundua Makonda kachemka sana kwa hii approach yake, hakuna mtu mwenye akili atampata na ushahidi so ni wazi hii ishu imefeli, ajipange tena baada ya mwaka mmoja wakijisahau then awasake kimyakimya (ziara ya kustukiza) la sivyo ataambulia kuwapata mateja tu
 
Back
Top Bottom