Asiyoyajua Yericko Nyerere katika utafiti wa historia ya Mapinduzi ya Zanzibar

Mjadala wa mapinduzi ya Zanzibar kwa muktadha wa Mohamed Said unaacha maswali

Kwa muda mrefu nimemuuliza Mohamed, maandiko yake yanaonyesha mapinduzi kuchagizwa kutoka nje ya Zanzibar na si kwa ridhaa ya Wazanzibar. Kwa mantiki hiyo mapinduzi yana 'Uharamu'

Januari 12 Wznz wanasherehekea Mapinduzi wanayotaita 'matukufu'
Kwa jicho la Mohamed hayakuwa na 'uhalali' achilia mbali damu iliyomwagika

Je, Mohamed anawaeleza nini Wazanzibar inapofika Januari 12?
Wanasherehekea 'haramu' au 'halali' yenye Uharamu?
Nafikiria naweza kumsaidia mzee Mohamed Said kwa ili ni zaidi ya mara 1000 amekuwa akilisemea ili khs mapinduzi hakika yale yalikuwa mavamizi kutoka njee ya Zanzibar...
 
Mzee wangu Mohamed Said kwanza Shikamooo!

Kabla hatujaendelea na mjadala huu, naomba kujua, umekisoma kitabu cha Ujasusi wa Kidol na Kiuchumi chenye sura 6, kurasa 715, vielelezo 368, nyaraka siri 88, nyaraka huru 20????

Je umeelewa dhima ya kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi?

Naomba kujua hilo ili nianzie hapo kukujibu hoja zako zote
3c76fab69f297d7a1053e3c760e87c70.jpg
yericko nyerere sijui unakumbuka ulikuja kuniuzia hicho kitabu ilala amana ofisini kwangu na nikampigia mzee Mohamed Said ukaongee nae nia yngu kubwa nilikuwa nataka uende kuongeza elimu hakika unaitaji kuivishwa zaidi na magwiji km mzee Mohamed Said sio kukalia ubishi km ndugu zetu wa lumumba jaribu kumsoma vizuri mzee wetu utamuelewa nia yke kujaribu kutaka kkujenga zaidi kijana wake lkn naona unataka kuleta ushindani sio na sababu hakika ww ni Kichochi uwezi kuingia kwenye kundi la ninga jaribu kkubari kukoselewa...
 
Yericko,
Marhaba.
Si suala la kusoma kitabu ila yale ulioandika ndiyo ninayozungumza ambayo nimesoma na kutoa maoni yangu.
 
Atakapo kujibu ukiweza ni-tag mkuu nataka kujifunza kitu hapo.
Titi usitumie lugha zisizopendeza utachafua mjadala.

Unaweza tu ukanikumbusha kwa kueleza kuwa umenipa maswali nami sijakujibu.

Hii lugha ya kuwa "nimeruka," "napiga soga" kwangu si mahali pake.

Hapana haja ya wewe kunitusi huu ni mjadala tu tunabadilishana fikra na si lazima tukubaliane.

Nadhani kuanzia hapa utaandika kwa adabu na staha.

Sikumbuki maswali yako tafadhali niulize upya na nakuomba radhi kwa kutokujibu.
 
Mjadala wa mapinduzi ya Zanzibar kwa muktadha wa Mohamed Said unaacha maswali

Kwa muda mrefu nimemuuliza Mohamed, maandiko yake yanaonyesha mapinduzi kuchagizwa kutoka nje ya Zanzibar na si kwa ridhaa ya Wazanzibar. Kwa mantiki hiyo mapinduzi yana 'Uharamu'

Januari 12 Wznz wanasherehekea Mapinduzi wanayotaita 'matukufu'
Kwa jicho la Mohamed hayakuwa na 'uhalali' achilia mbali damu iliyomwagika

Je, Mohamed anawaeleza nini Wazanzibar inapofika Januari 12?
Wanasherehekea 'haramu' au 'halali' yenye Uharamu?
Nguruvi3,
Mimi nitajibu swali lako kwa kukupa kazi kidogo.

Chunguza matokeo ya uchaguzi mkuu Zanzibar toka 1995 angalia vipi Wazanzibari wanapiga kura na nini inakuwa matokeo yake.

Jibu lako liko hapo.
 
Mkuu, huyu Mzee ameandika vitabu kadhaa, na nilishasoma vitabu vyake viwili...cha mwisho ni kile cha Ukweli uliofichwa kuhusu wapigania uhuru wa Tanganyika, akieleza mengi sana na % kubwa ni ya kweli.

Lakini lengo kubwa ni kuujuza umma kuwa TANU ilianzishwa na wazee wa kiislam na waislam ndio Khasaa waliopigania uhuru wa nchi hii ila hawakuthaminika na hawatajwi katika historia. Ukimsoma zaidi atakuletea habari za Nyerere na mfumo Kristo.

Kifupi Mzee Mohammed ni Mdini sana na ni wazi kuwa Mapinduzi ya Zanzibar kwa sehemu kubwa yaliongozwa na mganda John Okell[/] lakini kwakuwa ni Mgalatia huwezi kusikia akizungumzwa sana...lakini Wakristo wala hawajali vitu vidogo hivyo.
Azareli,
Sijui kwa nini unaleta suala la dini katika mjadala huu.

Mimi sijaandika kitabu kuhusu mapinduzi lakini nimeandika makala nyingi na nina audio na video kuhusu historia ya Zanzibar.

Naangia Maktaba nitakuwekea links kadhaa:

Mohamed Said: AZAM TV KIPINDI MAALUM CHA MASHUJAA WA UHURU WA TANGANYIKA
Mohamed Said: WASIFU WA ABEID AMANI KARUME AZAM TV 2015
Mohamed Said: KIPINDI AZAM TV KUMBUKUMBU YA MAPINDUZI ZANZIBAR 2016
Mohamed Said: AZAM TV: MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUTOKA KUMBUKUMBU ZILIZOZIKWA
Mohamed Said: Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere -Azam TV
Mohamed Said: KUMBU KUMBU YA MIAKA 54 YA UHURU - AZAM TV 02
Mohamed Said: AZAM TV KIPINDI MAALUM CHA SABASABA KUASISIWA KWA TANU 1954
Mohamed Said: AZAM TV KARUME DAY: ABEID AMANI KARUME - "THE MASTERMIND" MAHOJIANO NA IRENE KILENGA
 
Azareli,
Sijui kwa nini unaleta suala la dini katika mjadala huu.

Mimi sijaandika kitabu kuhusu mapinduzi lakini nimeandika makala nyingi na nina audio na video kuhusu historia ya Zanzibar.

Naangia Maktaba nitakuwekea links kadhaa.
Mzee, mimi nimeanza kukusoma kitabuni mwaka 2009-2010, na tulishajadiliana mengi hapa na pasco kabla sijaondoka jamvini na kurudi.

Una karama ya utunzi na uandishi wa vitabu, mimi nimesoma vitabu viwili na kurudia zaidi cha historia na harakati za wapigania uhuru wa nchi hii, sikuwafahamu akina Abdulwahid Sykes, Dossa Aziz na wengine wengi kabla, kwani tangu naanza nursery school mpaka nafika kidato cha sita tulimsoma zaidi J.K Nyerere na si hao.

Nilinunua kitabu chako katika msikiti uliopo Magomeni mwaka 2011 na kukusoma kiundani.

Baadae nilikuja kwazika kiasi baada ya wewe kwa kusapotiwa na akina bandubandu na FF kugeuza mjadala humu kuwa kidini badala ya kuelimisha...hasa mwaka 2014 nikiwa humu 24/7.

Yawezekana wewe haikuwa target yako ila mjadala ulionekana kidini na kiitikadi zaidi kuliko kutoa elimu ya historia kwa wengi wasiojua.
 
Kwa sababu hiyo Yericko Nyerere atakuwa kakosea wapi,kucopy makala au kuandika ambayo tayari yameandikwa au kutumia dokezo ?
Idd,
Kwa kawaida ili kitabu kiwe kitabu na ''publisher,'' akichape ni lazima
na hili ni muhimu, hicho kitabu kiwe kina elimu mpya ambayo haipo
mahali pengine.

Hili ni muhimu kwa sababu hapo kwenye elimu mpya ndipo kitabu
kitapata soko na kununuliwa na taasisi za elimu na maktaba.

Ndiyo maana publisher akipokea mswada kutoka kwa mwandishi ni
lazima mswada ule ampe mtaalamu wa somo hilo lililoandikwa kwenye
huo mswada.

Ikiwa ''publisher,'' atapokea mswada na akagundua kuwa mwandishi
hana lake katika aliyoandika hatakubali kuchapa kitabu hiki kwa
sababu kadhaa na kubwa kwa woga wa kushtakiwa kwa kunakili
kazi za waandishi wengine.

Msomaji hawezi kununua kitabu ili asome kile tayari kesha kisoma
kwenye vitabu vilivyotangulia.

Naamini nimeeleweka.

Haya mambo nayajua vyema kwa kuwa mimi ni mwandishi, mhariri na
pia ni ''publisher.''
 
Mzee, mimi nimeanza kukusoma kitabuni mwaka 2009-2010, na tulishajadiliana mengi hapa na pasco kabla sijaondoka jamvini na kurudi.

Una karama ya utunzi na uandishi wa vitabu, mimi nimesoma vitabu viwili na kurudia zaidi cha historia na harakati za wapigania uhuru wa nchi hii, sikuwafahamu akina Abdulwahid Sykes, Dossa Aziz na wengine wengi kabla, kwani tangu naanza nursery school mpaka nafika kidato cha sita tulimsoma zaidi J.K Nyerere na si hao.

Nilinunua kitabu chako katika msikiti uliopo Magomeni mwaka 2011 na kukusoma kiundani.

Baadae nilikuja kwazika kiasi baada ya wewe kwa kusapotiwa na akina bandubandu na FF kugeuza mjadala humu kuwa kidini badala ya kuelimisha...hasa mwaka 2014 nikiwa humu 24/7.

Yawezekana wewe haikuwa target yako ila mjadala ulionekana kidini na kiitikadi zaidi kuliko kutoa elimu ya historia kwa wengi wasiojua.
Azarel,
Tatizo la historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika nimelieleza ndani ya
kitabu chenyewe.

Kwa kifupi ni kuwa wale ambao waliandika historia ya TANU walitishika
na ule Uislam uliokuwa ndani ya TANU na harakati za kudai uhuru na
wakadhani wanaweza kuufuta kwa kubadilisha historia ile.

Angalia hiyo picha hapo chini:

EyrzdVG4GMUBn5aCtqMniFfBptnu6sAkOopZcfM3SIfXns68k4T_hxHoWcSC3OgAFPWWKZUEE7CmcaOnFO2qoEzMl3kzCM1O7gwkwx8iWJXOqH33JGzdX0IDbzwEkB4T6QtKeNBuJqnH5IJIn6S5bgYydMHfhdKIBbRBRjRJvT7ctddHyyWJTblJqm6dn4cte9urPX_bwMJpHGqzwG1ViZDxHSG7Q8JFngJjvGbXtVRZ1r9wfjfIPyVku9Rd6guUKMncTz0kTkH13N8uwKikh3KNaNgKq-I4QXW5h7dryVzldTstnU1r7k38ZxFo0TziQ55djYVo9oQnoq6cVeJJnAgjnXtWfMVQMwEEWsqVRlUqqo_wbeQUs4qfTLVed7UY3jHKWD7ybmFIZxDcRkkVWT1Yj9LTZBBlJ9QPUo5ldnKVtbiue33xL_uURavb9V6LpOspB0GINMEDmPMfZUjt7b1w7CZyidr53SOJnP47kEY4-a4GnS4ABJunpIwO5JMn3VyfdhvggagplU2AHFFBmcCkPeKIMD8oRU-Tp57X2SwKjnCk36lj44vJFTmKCKybH0YN1Ecgj7sfCxr-dBVdbeq3rcdGc-se6v9CocvC=w281-h220-no

Kulia ni Mshume Kiyate, Julius Nyerere, Max Mbwana na Mwinjuma
Mwinyikambi, 1962
 
Mzee Mohamed Said naomba ujibu maswali yangu hapo nyuma ili niweze kukujibu, naona unaruka na kuendelea na soga ukiacha maswali yangu
Yericko,
Ukianza na lugha za ghadabu utauua mjadala.
Mimi sipigi ''soga,'' wala ''siruki.''

Ukinambia hivyo tayari unaingiza kejeli.

Nimekujibu nimesema suala hapa ni yale uliyoandika kuhusu
historia ya mapinduzi hayo ndiyo niliyoyazungumza.
 
Titi usitumie lugha zisizopendeza utachafua mjadala.

Unaweza tu ukanikumbusha kwa kueleza kuwa umenipa maswali nami sijakujibu.

Hii lugha ya kuwa "nimeruka," "napiga soga" kwangu si mahali pake.

Hapana haja ya wewe kunitusi huu ni mjadala tu tunabadilishana fikra na si lazima tukubaliane.

Nadhani kuanzia hapa utaandika kwa adabu na staha.

Sikumbuki maswali yako tafadhali niulize upya na nakuomba radhi kwa kutokujibu.
Nadhani mzee wangu umekosea kunielekeza mimi ushauri huo wa lugha yenye staha.

Aliye andika hivyo ni Yericko Nyerere kisha mimi nikamuomba utakapomjibu aniwekee alama ya kunikumbusha (tag) ili niweze kuona majibu yako nijifunze kitu.

Najua umekosea kunijibu mimi kwa bahati mbaya.
 
... makala ile ''In Praise of Ancestors,'' iliwashughulisha kwa kuwataja Waislam katika historia ya kweli ya TANU na historia ya uhuru wa Tanganyika. Tatizo lilikuwa historia rasmi ilikuwa haitaji mchango wa Waislam katika kupigania uhuru. Historia rasmi ilikuwa inasema kuwa TANU iliasisiwa na Julius Nyerere peke yake. Mimi nikaja na historia ninayoijua kwani waasisi wa TANU ni wazee wangu na nikaandika makala ya kistaarabu tu nikaeleza ilivyokuwa hadi TANU ikaundwa mwaka wa 1954. Jamaa hawakuweza kustahamili kuona ukweli unaelezwa kwa hiyo gazeti lote toleo lile likakusanywa. Abdul Sykes alikuwa kafariki miaka 20 imepita lakini kwa namna nilivyoeleza historia yake nikawa kama vile nimemfufua na nimekuja na kitu kipya katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika. Sasa na hii historia ya Mapinduzi ndivyo ilivyo. Dr. Ghassany amekuja na historia ya kweli na ndiyo hii ndugu yangu inakupa shida kuamini ukweli kama ilivyokuwa hapo mwanzo tabu kuamini kuwa historia ya TANU kama nilivyoiandika katika kitabu cha maisha ya Abdul Sykes ndiyo historia ya kweli. Sasa ikawa lazima Mlamali Adam aondolewe Africa Events na Mohamed Said makala zake zipigwe marufuku. Nadhani unaanza kuelewa sheria za mchezo huu.
 
Hayo hapo nimemwandikia rafiki yangu mmoja...nimeona na Majlis niilete...
 
Titi usitumie lugha zisizopendeza utachafua mjadala.

Unaweza tu ukanikumbusha kwa kueleza kuwa umenipa maswali nami sijakujibu.

Hii lugha ya kuwa "nimeruka," "napiga soga" kwangu si mahali pake.

Hapana haja ya wewe kunitusi huu ni mjadala tu tunabadilishana fikra na si lazima tukubaliane.

Nadhani kuanzia hapa utaandika kwa adabu na staha.

Sikumbuki maswali yako tafadhali niulize upya na nakuomba radhi kwa kutokujibu.
Mimi ni kati ya watu wanao kuheshimu sana Mohamed Said siwezi kukujibu hivyo.

Na pia shabiki wako mkubwa wa mijadala yako hapa JF. Hata ile mijadala ambayo kiimani ipo tofauti na mimi bado nakuja kujifunza kitu toka kwako.
 
3c76fab69f297d7a1053e3c760e87c70.jpg
yericko nyerere sijui unakumbuka ulikuja kuniuzia hicho kitabu ilala amana ofisini kwangu na nikampigia mzee Mohamed Said ukaongee nae nia yngu kubwa nilikuwa nataka uende kuongeza elimu hakika unaitaji kuivishwa zaidi na magwiji km mzee Mohamed Said sio kukalia ubishi km ndugu zetu wa lumumba jaribu kumsoma vizuri mzee wetu utamuelewa nia yke kujaribu kutaka kkujenga zaidi kijana wake lkn naona unataka kuleta ushindani sio na sababu hakika ww ni Kichochi uwezi kuingia kwenye kundi la ninga jaribu kkubari kukoselewa...
Nikushukuru sana mzee wangu kwakunikumbusha vema,

Mohamed Said ni mmoja ya watu muhimu walionifundisha historia, nitakuwa mjinga sana nisipomshukuru na kumheshimu mzee huyu, na katika kitabu changu nimemtaja kama mmoja ya watu muhimu ambao vitabu vyao nimevirejea....

Kitabu tunachokabidhiana hapo kwenye picha ni kitabu cha majaribio tu kikiwa na sura 4 na kurasa 200 tu, lengo la kukichapa ilikuwa ni ushauri wa vyombo vya dola kuona mapokeo ya umma, baada ya mapokeo kuwa mazuri kilihaririwa upya na kuchapwa upya kikiwa na sura 6, kurasa 715, vilelezo 366, vielelezo siri 88, vielelezo huru 34, nyaraka 18 nk....

Kitabu hiki toleo la pili kimechimba historia ya mapinduzi kwa undani wake, hata yale Mzee Mohamed Said na wengine hawakuyajua yamo...

Kimechimba juu ya Abeid Karume, mauaji yake na mapito ya Zanzibar hadi leo hii.

Nje ya hapo kitabu kimebadili kabisa ngano za Mohamed Said juu ya historia ya Uhuru wa Tanganyika, Yale asiyoyapenda Mohamed yote yameletwa pamoja, hasa hasa uratibu na ushiriki wa Kanisa katoliki kupitia shirika lake la kijasusi la Jeisuti juu ya Uhuru wa Tanganyika...

Mambo haya ni mapya kwa Mohamed Said na wengine....ni lazima alipuke kwa hofu...


Mwaka 2013 tulikutana hapa jamvini katika mjadala uliochukua mwaka mzima hapa mimi nikikosoa ngano za Mzee Mohamed juu ya Uhuru akiunasibisha na uislamu wa Dar na kuwatenga waamini wengine kabisa... Nilimuonya kuwa mimi nitazifuta ngano zake na kusimama kwenye mlengo mwingine kabisa... Naam nimefanya hivyo... Leo watu wamejua nani alikuwa nyuma ya uhuru, nani alikuwa nyuma ya Julius Nyerere, nani alikuwa kiungo muhimu mpaka uhuru....

Haya ni mageni kwa Mohamed, mlipuko wake niliutaraji, hapa analipuka huku bado kabisa hata kitabu hajakisoma kabisa, ila anaona hizi dondoo tu ameanza kuja na kejeli na matusi lukuki dhidi yangu...

Kitabu kimeshapata sifa ya kitaifa na kimataifa, yeye amesema hakinunuliki, sijui anataka aje niwe namuonyesha kuwa huyu kanunua na yule kanunua....

Wataalamu na wasomi leo wanapendekeza nitunukiwe shahada mbili za uzamivu kwa kuandika kitabu kimoja tu, na wamefurahishwa sana katika historia na ujasusi.... Leo mzee wa ngano za kariakoo anakuja na matusi juu...

Katika madai ya Mzee Mohamed anasema kwamba nimenakili yaliyoandikwa, ukweli nikuwa wa wale waliobahatika kukisoma kitabu changu wataona maandishi yote yakunakili yanamarejeo na nyaraka mwishoni nyuma ya kitabu... Labda uwe mvivu na mwenye wivu uliovuka mipaka kama wa mzee Mohamed Said.


Nikushauri kama ulivyotushauri sisi kipindi kile 2013 kwamba historia yako tuipinge kwa kuandika kitabu, nawe ni wakati wakupinga kitabu cha Ujasusi wa Kidola naKiuchumi kwakuandika kitabu, nje ya hapo ni porojo tu mzee.... Na zaidi unanisaidia sana kunadi kitabu... Weekend nitakutafuta tupate sharubati na vibansi pamoja
 
Mjadala wa mapinduzi ya Zanzibar kwa muktadha wa Mohamed Said unaacha maswali

Kwa muda mrefu nimemuuliza Mohamed, maandiko yake yanaonyesha mapinduzi kuchagizwa kutoka nje ya Zanzibar na si kwa ridhaa ya Wazanzibar. Kwa mantiki hiyo mapinduzi yana 'Uharamu'

Januari 12 Wznz wanasherehekea Mapinduzi wanayotaita 'matukufu'
Kwa jicho la Mohamed hayakuwa na 'uhalali' achilia mbali damu iliyomwagika

Je, Mohamed anawaeleza nini Wazanzibar inapofika Januari 12?
Wanasherehekea 'haramu' au 'halali' yenye Uharamu?

Wazanzibari hawasherekei mapinduzi. Ila CCM ndio wanaosherekea mapinduzi.
 
Back
Top Bottom