Hicho anachoita kitabu wala hakina publisher wala mswada haukusomwa na mhariri yeyote aijuae historia ya mapinduzi ni sawa na mtu aliyejifungia chumbani kwake anaandika katika mtandao wa kijamii.
Yericko hana moja alijualo katika historia ya mapinduzi. Ili kitabu kiwe ni kitabu kinatakiwa kiwe na habari mpya zisizo fahamika.
Huwezi kuungaunga habari walizoandika waandishi wengie ukasema umeandika kitabu.
Anachofanya
Yericko ni kunakili yaliyoandikwa na wengine na kisha akayaleta kama fikra zake.
Hicho kichwa chake cha habari kwa haya aliyoandika ameyanakili kutoka kwangu kayabadilisha kidogo tu.
Mwenye maneno hayo ambayo mimi ndipo nilipoyachukua ni Prof.
Mohamed Bakari nimemsikia akiyasema kwenye kongamano Kampala mwaka wa 2003 akisema, ‘’Ikiwa sisi hatutoandika historia yetu watakuja watu kutuandikia na huenda tusipendezewe na hayo waliyoandika.’’
Mimi ninapofanya rejea ya maneno hayo humtaja
Prof. Mohamed Bakari.
Prof. Mohamed Bakari ofisini kwake Fatih University Istanbul 2015
Yericko angekuwa mjuzi kweli wa historia ya mapinduzi angemtaja kwanza
Ali Mwinyi Tambwe aliyetumikia ''Intelligence.'' toka ukoloni hadi uhuru unapatikana 1961 tena akisafiri kueneza TANU na
Nyerere bila ya
Baba wa Taifa kujua kuwa taarifa zake zote zinafika kwa
Gavana.
Yericko anamwaga majina ya kina
Mzena ambao wakijulikana sana si mara moja katajwa katika mikasa ya akina
Hashil Seif na
John Okello.
Ali Mwinyi ndiye kiongozi wa Kambi ya Kipumbwi na ndiye aliyemtia
Mohamed
Omari Mkwawa katika njama ya mapinduzi na kumpa kazi ya kuvusha askari mamluki akifanyakazi chini ya
Victor Mkello.
Victor Mkello akiwa nyumbani kwake Nguvumali, Tanga
Vitabu vyote vya historia ya mapinduzi hakuna mwandishi aliyelijua hili.
Yeye
Yericko kazi ni yake kukopi tu.
Ghassany kazungumza na
Victor Mkello si mara moja au mbili ilikuwa kazi ya kwenda Tanga na kurudi Muscat,
Mkello hakufungua kinywa chake hadi nadhani alipohisi hana siku nyingi za kuishi na hapo alikuwa tayari mguu mmoja ushakatwa.
Mimi nilikuwapo kwenye vikao vyote isipokuwa cha mwisho
Mkello alipoamua kueleza ukweli mbele ya mkewe kikao hiki mimi nilitoka nje kuwapa faragha na kumtoa
Mkello wasiwasi kwa kuwa
Dr. Ghassany yeye mgeni mimi naishi na yeye mji mmoja.
Yericko hana moja alijualo.
Na Dr. Ghassany nyumbani kwake Muscat 1999 alipomfahamisha Mwandishi mradi wa kutafiti historia ya mapinduzi ya Zanzibar ya 1964
Dr. Ghassany na Mzee Mkwawa, Tanga 2003