Arsenal (The Gunners) | Special Thread

View attachment 3110425
Hua nasema Arteta ni tapeli mnabisha. Haya huenda Kalafiori makaliza msimu
Hamstring injury...wiki 4 nje maximum....Tomiyasu mjapani kasharudi🤠🤠🤠...tabu Iko palepale tu...mmetupita point 1 na hatuna viungo wachezeshaji wetu odegaard. Na merino.....TAfuteni viungo waziri siku tukikutana msije mkamtukana mzee Slot ndugu zetu
 
Arsenal imepiga hatua kubwa kwenye mentality lakini bado kuna hali ya kuridhika na kuruhusu makosa yanayoweza kuigharimu timu.

Sitashangaa timu yangu hii ikibeba epl mwaka huu japo bado sina ujasiri wa kutamba kwamba ubingwa utapatikana maana safari bado ni ndefu sana kuelekea May 2025.

Mwaka jana tulipoteza kwa fulham na aston villa kwahiyo hata ushindi dhidi ya city, liverpool na united haukuwa na maana ikiwa tuliacha point kwa timu ndogo.

Kama msimu huu timu itachukua point kwa timu zote ndogo na kupata wastani wa point 4 kwenye timu zote kubwa basi ubingwa utapatikana mapema.

Apatikane kiungo mkabaji anayeeleweka ili tuachane na Jorginho na Partey, huku mbele tupate striker wa kueleweka na pale nyuma beki mbadala wa Saliba.

Kila la heri kwa msimu huu.
 
Yaani nyie viazi mnapenda kulialia, Calafior alitakiwa kupewa second yellow kwa kumkwatua mtu ila hakuna aliyeongea. Nyie mpk kocha nae amekua mduanzi ona anavyonyosha mikono. Kwan hapo kosa ni nn! Amembashia au?
Tuliza mshono dogo.... asubuhiasubuhi ushaamkia huku jukwaani....Rudi kule kwenu mkajadiliane namna ya kupunguza hamsa nyingine tukikutana maana kipigo kipo palepale
 
Mbona umeshindwa wewe kuongoza Kwa point Moja😂
Marefa walochezesha mechi zetu walitubetia....yule Michael Oliver sijui na yule mpumbavu alochezesha mechi yetu na Brighton yaani walifanya Kila namna tusiondoke na point 3....vinginevyo saahii tungekuwa kileleni na point 18 zetu....Livakuku ya Klopp ndo ilikuwa walau inatisha ila hii ya kipara Slott inaacha matobo nyuma hivi....hakyanani ni suala la muda kitawaramba...mzee midevu wa nott forest kashatoa mchoro namna ya kuwadunda
 
Back
Top Bottom