Angalia Rais Magufuli anakoomba misaada na mikopo utaelewa kwanini hatofanikiwa

Mataifa yote aliyoomba misaada hawatufikii kua na rasilimali , anakimbiza wafanyabiashara na wawekezaji kwa kuongeza mikodi isiyo ya msingi, mazingira ya biashara tanzania ni magumu kuliko sudani kusini.
Wewe ni mfanyabiashara? Au unaongoea tu kama cherehanii...Tatizo la kodi Tanznaia ni la kimfumo. Magu anakusanya tu kodi kwa mujibu wa sheria ambazo hakutunga yeye sema huko nyuma hazikuwa zikikusanywa. Tatizo la makodi mengi ndo pengine nalo limechangia wafanyabiashara kujaribu kukwepa kodi huko nyuma. Badala ya kupambana na Magu pambana na mfumo wa kodi kandamizi ambao umekuwepo miaka nenda miaka rudi
 
BUBb7FngX3c.jpg
 
Unaonesha una uelewa hafifu kwenye masuala ya dunia.Uelewa wako umeishia mkuranga kwenye majambazi yanayoua polisi.
Rwanda wapo mbele sana kwenye IT,sio kosa wakileta wataalam wao kuja kufunza vijana wetu,mbona sie tunapeleka watu kufundisha kiswahili?
Ethipia wanataka kutumia bandari yetu,tuwakatalie?
Afrika ya kusini,kuna nchi za ulaya haziwafikii kiuchumi,na hatukuomba msaada kwa afrika ya kusini,tumeomba kwa jumuia yao inaitwa BRICS=BRAZIL,RUSSIA,INDONESIA,CHINA NA SOUTH AFRICA,wana benki lao la uwekezaji lina nguvu kubwa sana,alichoomba magufuli kupitia Afrika kusini kama nchi mwanachama,atupigie chapuo tupate hizo pesa.ni diplomasia ya uchumi inachezwa hapo.
Morocco wako mbali sana hatuwafikii hata robo,ni sahihi kuomba msaada hata mkopo
BRICS wanataratibu zao za kukopeshana si kumsaidia kumjenga mtu wa nje naimani si mambo ya kupeana tunakofanya mitaani tukaweka huko kule wanalinda maslahi yao na wako makini kutoyajenga makundi hasidi
 
Alidhanii mambo ni marahisii tuu..!! Sasa endeshe nchi bila mikopo rasilimalii si hizoo... Wakukurupukaa... Na badoo tutaomba msaada mpaka kwa MSUMBIJII...
 
Hakuna nchi inayojitosheleza mkuu kuomba ni lazima hata marekani akitaka kupigana na mtu utasikia anaomba msaada nchi fulani kumuunga mkono....kuomba ni kuomba tu mkuu.
Hoja si kukataa kuomba bali kuponda wenzako ambao walikuwepo na waliomba kwa staa hatukuona wakiomba kwa wagonjwa wenzetu Leo dangote angepatikana wapi
 
BRICS wanataratibu zao za kukopeshana si kumsaidia kumjenga mtu wa nje naimani si mambo ya kupeana tunakofanya mitaani tukaweka huko kule wanalinda maslahi yao na wako makini kutoyajenga makundi hasidi
Majibu yako yamejaa chuki na usongombwingo.Ziweke basi hizo taratibu za kukopa BRICS acha blah blah.
Nchi zote za BRICS zina mkataba wa ushirikiano wa uchumi,ilikuwa imebaki South Africa peke yake na wamemalizana juzi.
Tunasubiri ofa na masharti yao tu kwa sasa
 
Wanabodi.
Nakutajia nchi ambazo Rais Magufuli alizoomba misaada Rwanda aliwaomba wataalam wa IT, Ethiopia sijui akawaomba nini, Afrika Kusini amewaomba msaada,Morroco kawaomba. Nchi zote anazowaomba nao bado wanasaidiwa kwa kiasi fulani na wafadhili, ina maana kila mgeni anayekuja Tanzania ajiandae kuombwa kitu tena wengine ni maskini wenzetu tu.

Tujadili.
Mtegemea cha nduguye hufa masikini,sisi tuendelee kuikumpatia ccm tu maana umasikini,unyonge kwetu ni sifa
 
Rwanda ni nchi inayoongoza Kwa kufanya Ujasusi dhidi ya mataifa mengine ya Africa tangu kagame awe rais, sasa kuwaomba wataalamu wa IT kutoka Rwanda ni kwamba alipewa majasusi watupu.
yetu macho, siye tuliona mbali kabisa kuwa, viatu vya urais havimwenei kabisa huyu mh, siyo kila mtu anaweza kuwa rais, urais ni taasisi inayohitaji hekima na busara za hali ya juu, zaidi ya yote ni utulivu, na umakini uliopindukia.
Sasa jamani, hivi kweli Morocco ni nchi ya kuiomba msaada? tukubali tukatae Tanzania ina laana.
tanzania haina laana ni viongoz wetu tu wanatuharibia..tulipaswa tuwe na viongoz kama akina bashe..lissu watu wenye uzalendo wa kweli sio hawa tulionao uongo mwingiii
Kwa mimi nahisi lazima uchague wa kumuomba unaomba nchi ambazo nazo zinaomba na zinasaidiwa kama tanzania maana yake, you are diminishing to them, tunajifedhehesha zaidi kumuomba msaidiwa na kuifanya Tanzania kupungua hadhi yake ki-mataifa
 
Huyu jamaa aliingia kwa mbwembwe sana kwa kumponda JK, eti kwanini anaenda kuomba kwa wazungu wakati nchi ni tajiri, leo amesahau anaanza kuomba omba kwa kila anayemtembelea, aibu! nacheka kwa dharaaaau, hahahahahahahahahahahh!
hta mkwere aliko anacheeeeeeeka..kwa dharau. inabidi msukuma huyu amtake radhi mkwere wa watu
 
Unaonesha una uelewa hafifu kwenye masuala ya dunia.Uelewa wako umeishia mkuranga kwenye majambazi yanayoua polisi.
Rwanda wapo mbele sana kwenye IT,sio kosa wakileta wataalam wao kuja kufunza vijana wetu,mbona sie tunapeleka watu kufundisha kiswahili?
Ethipia wanataka kutumia bandari yetu,tuwakatalie?
Afrika ya kusini,kuna nchi za ulaya haziwafikii kiuchumi,na hatukuomba msaada kwa afrika ya kusini,tumeomba kwa jumuia yao inaitwa BRICS=BRAZIL,RUSSIA,INDONESIA,CHINA NA SOUTH AFRICA,wana benki lao la uwekezaji lina nguvu kubwa sana,alichoomba magufuli kupitia Afrika kusini kama nchi mwanachama,atupigie chapuo tupate hizo pesa.ni diplomasia ya uchumi inachezwa hapo.
Morocco wako mbali sana hatuwafikii hata robo,ni sahihi kuomba msaada hata mkopo
ww bila shaka kama sio mgogo bas ni bashte..kwa hio umeidhinisha swala la kuwa nchi omba omba kisa waliotutembelea wametuzidi uwezo?? shabashi...wapi yale majigambo ya mkuu kwamba sisi si omba omba? ccm mmetuharabia nchi ni heri mngepotelea mbali.
 
Back
Top Bottom