Anataka niweke status: 'Nakupenda mume wangu' kwenye WhatsApp, kuna maana yoyote ktk hili?

Hana lolote sema tu wivu unamsumbua.. hapo ukiweka ataanza kukuambia uweke picha.. mwisho atataka kila jioni umwachie laini...!
mpotezeee tu!
 
Bila shaka wote muwazima wa afya.

Leo imekuwa Siku trick sana kwangu mpenzi wangu ambaye tunaitana mke na mme kwa miaka mitatu sasa. Anataka niweke neno nakupenda mume wangu katika status yangu WhatsApp jambo ambalo limezua mzozo kati yetu.

Mimi sitaki kuweka kwa kuwa yeye so mume wangu bado hatujafunga ndoa wala hatuishi pamoja ila ameniahidi kunioa kama mke wa pili.

Nimekuwa nikimtii na kuwa mwaminifu kwake na kumpa heshima zote kama mume wangu, naenda kwake anakuja kwangu.

Mwezi uliopita tulipanga kufunga ndoa ya bomani nilipogundua hajamwambia mkewe nikaghairi nikitegemea atafanya chochote katika mipango ya ndoa, lakini mpaka sasa hajafanya lolote. Mimi nimetulia namsubili yeye, ila kuweka neno la nakupenda mume wangu ndo nimegoma.

Sijui kama nimekosea ila nimeona itazua maswali kwa ndugu na jamaa zangu huyo mume wake ni yupi? Ingawa ni maisha yangu naweza fanya chochote.
kwahiyo kabla ya whatsapp walikuwa wanaweka status wapi?au kwenye paji la uso?mwambie aache ushamba nae huyo...na wewe na ubwege wako umekubali kutaka kuolewa kuwa mke wa pili,yet still mnapiga kelele mnataka usawa,hakika hiki ni kizungumkuti!
 
Itakua keshajua ww ni kiazi (huna msimamo) ndo anakufanya anavyotaka!!!
 
kamankula, kwa ufupi tu, husiweke hiyo status, huyo anakupotezea muda wako dada yangu. Sisi wanaume wakati mwingine tunawafanya dada zetu kama vile hawana akili. Kwanza huyo "mumeo " kama sio mwaminifu vile!
 
Bila shaka wote muwazima wa afya.

Leo imekuwa Siku trick sana kwangu mpenzi wangu ambaye tunaitana mke na mme kwa miaka mitatu sasa. Anataka niweke neno nakupenda mume wangu katika status yangu WhatsApp jambo ambalo limezua mzozo kati yetu.

Mimi sitaki kuweka kwa kuwa yeye so mume wangu bado hatujafunga ndoa wala hatuishi pamoja ila ameniahidi kunioa kama mke wa pili.

Nimekuwa nikimtii na kuwa mwaminifu kwake na kumpa heshima zote kama mume wangu, naenda kwake anakuja kwangu.

Mwezi uliopita tulipanga kufunga ndoa ya bomani nilipogundua hajamwambia mkewe nikaghairi nikitegemea atafanya chochote katika mipango ya ndoa, lakini mpaka sasa hajafanya lolote. Mimi nimetulia namsubili yeye, ila kuweka neno la nakupenda mume wangu ndo nimegoma.

Sijui kama nimekosea ila nimeona itazua maswali kwa ndugu na jamaa zangu huyo mume wake ni yupi? Ingawa ni maisha yangu naweza fanya chochote.
hakuna namna, hayo ndio matokeo ya DINI,
 
Weka tu halafu hutaji jina. DP unaweka alama ya love. Jambo dogo sana hilo
 
mwambie akuweke wewe kwenye status picha.alafu status aseme jamani ndugu na marafiki huyo ndiye mke wangu wa pili.akifanya hivyo na wewe mtii
 
Kama huna michepuko muweke japo sio rahisi ukakosa hata kamchepuko kamoja
 
Sasa kuna shida gani hapo? Kama ni mimi naweka, kwani mtu akisoma anajua ni mume yupi? mbona watu tunaweka dp kwenye whatsapp "I love You" alafu naweka na kale kaua kazuuuuuri. Kama nina michepuko yangu kila mchepuko atajua ni yeye. Kalaga bao
 
Mwambie naomba tupige picha ya pamoja kisha niiweke whatsap profile pic kisha niandike ujumbe ulioniambia ktk status yangu. Yeye hataki kukuoa na anataka kukufukuzia ndege wako.
 
bado ana mambo ya kitoto..
na asipobadilika, tegemea kuachana nae siku za karibuni
na msipoachana, tegemea kukosa furaha siku zote zilizobakia endapo hatoacha hizo mambo..

Childish
Umenikumbusha msela mmoja anaitwa Childish Gambino ngoja nitafute hata movie yake
 
Amekuona mjinga na hakuoi huyo anacheza na akili yako! Je kwa nini hakuoi anataka kuwa mume wa status??akuoe kisha adai hiyonhaki yake
 
Kuna watu bwana waajabu sana yaani mapenzi kwenu ndio kipaumbele yanini ujibebeshe mzigo , ooh mara sijui kimepanda kimeshuka, ndio mana hatuendelei watz tumekalia tu story za mapenzi, halafu uje ulalamike njaa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom