Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 1,110
- 2,657
Leo Novemba 29, 2024 kwenye mkutano wake na Waandishi wa Habari, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM, Amos Makalla amesema: Tunakemea na kulaani matukio ya mauaji yaliyotokea kwa vyama vyote katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Na mimi niungane na viongozi wa dini kukemea matukio haya yaliyotokea. Niliseme tu, tusiongelee kwamba tunakemea jambo hili kwa sababu vyama vya upinzani vina watu ambao wamepatwa na matukio haya halafu tukasahau na Chama cha Mapinduzi (CCM) kama nacho kimefanyiwa matukio haya.
Naomba niliweke wazi hili, tunapokemea tukemee wote kwa pamoja. Tunapoeleza kasoro hizi ni kwa wote. Haiwezi ikatokea mtu akakaa akaandika tamko lake kwamba kumetokea mauaji, na kueleza tu ya wafuasi wao. Tunakemea kwa nchi nzima, kwa maana mauaji, kujeruhiwa kwa watu, kupigwa kwa watu ni kwa vyama vyote.
Kwa taarifa nilizo nazo, CCM ina makada sita waliofanyiwa vitendo vya kupigwa na kuuawa. Mimi niko hapa kwa ajili ya vyama vyote.