SMG ya nini tena jamani?Bastola ya nini tena jamani!?
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
magufuli anaweza kushinda 99% na ccm yake kwa mbinu chafu kama hizi, lakini asitegemee maendeleo.UKAWA wanaongoza sehemu mbalimbali za kiutawala hapa Tanzania yakiwemo majiji kama ya Dar es Salaam na Arusha. Watanzania, kupitia uchaguzi mkuu wa 2015, waliwaamini Wabunge na Madiwani wa UKAWA na kuwachagua. UKAWA ni CHADEMA, CUF, NCCR na NLD.
Baada ya ushindi, kikaandaliwa na kuwekwa kibano. Vyanzo vya mapato vilivyokuwa vya Halmashauri vimepokwa na Serikali Kuu. Ndiyo kusema, kodi nyingi sasa zinakusanywa na Serikali Kuu na hivyo kuzibana mbavu Halmashauri kama za Majiji kupanga na kutekeleza mikakati yao. Bajeti zao ni finyu.
Kama hiyo haitoshi wala kutisha, wakuu wa Serikali wa sehemu hizo wamekuwa wakiingilia utendaji wa Halmashauri husika. Imeshakuwa sasa fasheni kwa Mkuu wa Mkoa au Wilaya kufuta au kuzuia hata posho za Madiwani. Ni kinyume na taratibu za Halmashauri ambapo Mkurugenzi huwajibika kwa Madiwani (Wakiwemo Wabunge wa Halmashauri husika).
Wakuu wa kiserikali sasa wanapuuza waziwazi Halmashauri ambapo wapo na kupoka kazi na majukumu ya Mkurugenzi wa Halmashauri. Hata Madiwani, ambao ni kama Bunge kwenye Halmashauri yao, wanaonwa si lolote. Hapo wapo pia Mameya na Manaibu Meya. Kila jambo linaamuliwa na viongozi wa kiserikali sasa.
Katika hali hiyo, amini nawaambia, UKAWA hawatobozi. Hawatafanikiwa katika walivyoviahidi. Wanabanwa kwelikweli na barabara. Lakini, UKAWA wana ngozi ngumu. Wanaendelea kupambana hivyohivyo pamoja na kubezwa, kumezwa na kutwezwa. Wanakukuruka kutimiza walichoahidi mwaka 2015.
Ni mwendo wa kudhibiti ili kuwafilisi UKAWA na wasiwe na cha kusema mwaka 2020!
Bastola ya nini tena jamani!?
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Ni mwendo wa pini t
Mzee Tupatupa
magufuli anaweza kushinda 99% na ccm yake kwa mbinu chafu kama hizi, lakini asitegemee maendeleo.
Ameingia kwa hasira kwa kumsimanga JK, katupa miradi yote ya JK ambayo tayari ilikua imesha anza kama bandari ya bagamoyo ambayo Kenya iliwatisha etc na kuanzisha ya kwake kama kununua ndege, kuhamia Dodoma, chato airport, barabara ya kwenda kwa mzee wa upako, etc.
Namba hazidanganyi, hali imekua mbaya, wahisani wameacha kutoa fedha, tanroad imejaza tenda zilizo tangazwa wakati pesa hakuna, tanroad wanabomoa nyumba za watu wakati fedha za kujengea Barbara hakuna, basi tuu waonekane awamu hii wanafanya kitu.
Ametapanya fedha kwa miradi ambayo sio msingi wa uchumi wakati Kenya Leo wamesha maliza reli na bandari kubwa huko lamu.
Ninacho kiona magufuli atamaliza vibaya, kuliko Rais yoyote kama asipo kubali ushindani wa fikra na mawazo mbadala.
Hata ccm wakishinda 99% au 100% kitakacho fuata ni kifo cha uchumi wa nchi na kuzuka kwa kundi moja la wapiga dili ambao watakua hawaguswi.
Mwulize yule mgonjwa alichokikuta Moshi!!Ni mwendo wa pini tu
Mzee Tupatupa
mkuu tupatupa labda wewe unaweza kujua hizi milion 50 kila kijiji zitatolewa lini? au ni 2020 ili wapewe kura?
hatari tupuKundi la akina Bashite aka Makonda.Watu wa Magufuli ndicho anachokupigania.Wanapiga kila mahali bila hata aibu.